Wakati huo huo, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa Redds Miss Ilala 2009 Jackson Kalikumtima amesema wana mikakati mbalimbali iliyopangwa ili kuhakikisha kanda hiyo inatoa Vodaco Miss Tanzania 2009.
Shindano la Redds Miss Ilala linatarajiwa kufanyika Agosti 7 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijjini Dar. Kabla ya kufanyika kwa shindano hilo warembo watakuwa na ziara ya kutembelea mbuga za Ngorongoro mkoani arusha kuazia kesho Julai 22 mpaka 26 na watakaporudi watashiriki kwenye onyesho la vipaji litakalofanyika Lamada Hotel Julai 28.
Warembo wanaoshiriki kwenye shindano hilo ni Fatma Bongi, Everline Gamasa, Julieth Lugembe, Magreth Motau, Lilian Nyamizi Mihayo, Irene Karugaba, Neema Doreen Kasunga, Winnfrida Mmari na Husna Ahmed.
Wengine ni Doris Luis, Groly Mwandani, Pendo Lema, Anne Mkandawile, Khadija Mhecha, Sylivia Shally, Gladness Shao na Zena Mbasha pamoja na mwalimu wao Regina Joseph na matron Nelly Kamwelu aliyekuwa Miss Ilala namba mbili mwaka jana.
http://missilala.com/gallery.php
ReplyDeleteNataka ku vote for Gladys Shao lakini wame weka picha yake nakusema yeye ni Doris. Na sikujua kwamba tulikuwa na ma miss mwaka 1988. Jamani wa fix web site ili watu tu vote.