mshambuliaji hatari wa yanga hamad ndikumana na mai waifu wake ambaye ni mcheza filamu maarufu irene uwoya wakitoka kumeremeta kanisa la mtakatifu joseph jijini dar wikiendi iliyopita na kuelekea kwenye mnuso kwa sataili ya jangwani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2009

    mzee huyo bwana ndikumana si mchezaji wa yanga bali ni mchezaji wa timu moja ya pale Cyprus, kitaifa ni mnyrwanda. nimeona kuna watu wametoa maoni yao kuwa mshkaji ndikumana alichemsha vilivyo pale kanisani st joseph kwamba alikuwa hafuati taratibu kama vile wakati wa kupokea sakramenti, wakati wa kupiga magoti na mambo kama hayo lakini ningependa kuwaambia watu kuwa hayo tulitakiwa kuyategemea yatokee SABABU huyu bwana HAMAD NDIKUMANA kidini ni muislamu kwa hiyo yale mambo hakuwa akiyajua tangu mwanzoni na bahati mbaya hakupata mafunzo ya kutosha kabla kuingia pale St Joseph. Kinachonishangaza mimi ni je Ekalist na Kipaimala amevipata lini?? au walifoji vyeti??? manake mpaka u-qualify kufunga ndo ya kikatolic inabidi uwe umeshafanya ekalist na kipaimala na uwe na vyeti vyake!!!! na kama unavyo hivi vyote basi ni lazima mambo ya kupiga magoti wakati wa sala na mambo ya kwamba sakramenti inapokewaje ni lazima uyajue!!! hapo ndipo bado mi mwenzenu nabaki kinywa wazi!!! Wale St Joseph nao inakuwaje hawakuwa serious kiasi kile???? manake jamaa alikuwa 100% anakwenda kinyume na taratibu za kazisani!!!. lakini dada yangu Irene mi namjua vizuri anapenda kulazimisha mambo makubwa hata pasipo penyewe!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2009

    makubwa haya!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2009

    Kana Kwamba ni Staili au ni macho yangu????

    ReplyDelete
  4. Mshambuliaji wa Yanga?? Lini wamemsajili? kumbe niko nyuma kwa habari za home?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2009

    Anon namba moja hapo juu....kanisa katoliki pamoja na ungangali wake limepisha policy ya NDOA ZA MSETO...Kama mmoja ni mkatoliki na partner ni muislamu RUKSA.....yaani kwa ufupi ni kwamba kanisa LIMETULIZA MZUKA

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2009

    Anon wa kwanza, nyamaza hujui usemalo...anon wa Jul 14, 10:55:00 sawasawa kabisa, wapashe hao mana wana midomo kama chuchunge..mlitaka kumuoa nyie? mbona mna kelele sana? ndo keshaolewa na kama kuchemsha washachemsha, unatoa macho ya nini sasa? hovyooo!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2009

    Tue Jul 14, 03:51:00 AM
    Asante kwa kutujulisha kuwa ni Mnyarwanda, anacheza sijui Rwanda au Yanga hakuna noma.

    Kuhusu dini. Asante sana anon 10:55 July 14. Ndoa za Mseto kanisa katoliki zinakubaliwa ila huyo mwenza wako anayetoka dini nyingine sharti afuate mambo fulani atakayopaswa kufanya na kanisa. Sio lazima apate sakramenti husika. Irene Hongera dada kwanza kwa kufunga ndoa pili kuweza kumshawishi jamaa afunge kwako ili uzidi kuwa mmoja wa waamini kamili wa kanisa. Hongera

    ReplyDelete
  8. Ama kweli ndoa ndoano na usilolijua niusiku wagiza hivi tuseme tu naukweli kitendo cha Iren kushika kamba yangamia mwanume kuwa juu mmmh kinawalakini kwan unaweza usienjoy ndoa yako fresh ukashikilia tu kamba kama kwenye Ndoa yako Take care Iren.All the best

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2009

    Kwa Waislaam pia, kama mmoja ni muislam na mwingine ni dini nyingine - RUKSA kufunga ndoa lakini kwa utaratibu wa kiislam. Hii yote inaonyesha jinsi dini zinavyotuhamasisha kufunga ndoa ili tuepukane na Zinaa.

    Irene we ni mrembo, hongera. Hamad, hongera kwa kujenga daraja kuliko ukuta

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2009

    heee ivi kumbe ni kweli???ni yeye irene uwoya dadaa wa kumwaga lazii adi unakoma na roho yako

    nimemuona kule blog ya nanihii!!

    dada hongera zako sana na umependeza sana na mumeo,sasa HAMAD tena kaingia kanisani??
    sijaelewa....

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 14, 2009

    wadada wenye majina ya IRENE acheni tu,wako juu,bomba,friendly,wanaSHIKA mwanaume adi unapata khabari yako

    hongera sana dada nguo yako nzuri sana sana na iyo style ya KAMBA inamaana utamshika vizuri mumeo,ndio usukani na hachomoki ng'o labda weye ndo uamue

    asante

    ReplyDelete
  12. mama hanselJuly 14, 2009

    KWAKWELI DADA GAUNI ZURI,ILA HIYO STAILI YA KUINGIA ATI MKE ANASWAGA MIGUU MUME KAKAA KWENYE NGAMIA HAPO MI NAONA WAMECHEMSHA AU WALIKUWA WALIKUWA WANA RECORD FILAMU BASI HATA HUYO MTUNZI ATAKUWA KAJIKANYAGA,KWAKWELI SI KILA KITU CHA KUIGA ,INABIDI JUA MAANA YA JAMBO UNALO TAKA KUIGA KABLA YA KUIGA.ILA HONGERENI KWA KUFUNGA NDOA MDUMU KATIKA UPENDO NA AMANI.

    ReplyDelete
  13. mzee wa bunjuJuly 14, 2009

    Inna Lillahi Wainnna Ilaihi Rajioon, Kwenye uislam hakuna kitu kama hicho cha ndoa ya mseto,tunaruhusiwa kuwaoa manaswara ila wasilim!!! na pia iwe ya kikiristu au ya kiislam kote biblia na qoran imekataza mwaume kuvaa mapambo ya kike hali kadhalika kwa mwanamke kuvaa mapambo ya kike, sasa nashangaa mfungishaji amekubalije mwanaume kuvaa heleni na kusuka nywele kanisani??? ndugu zetu wakiristo mbona mnakua flexible kiasi hicho??? Yesu akirudi akakuta mambo kama haya yanafanyika kanisani hatapata BP, nawaomba sana mrejee kwenye maadiko ya kale dini si swala la kwenda na wakati, hata Yesu alikataa kutengua yodi ya moja ya torati itakua ninyi???

    Aaaaaa ndikumana sikuhukumu ndugu yangu ila kwa mujibu wa imani yangu hapo ndoa bado.

    Mzee wa Bunju

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 14, 2009

    Kwa Mdau MZee wa bunju, Kiislamu inaruhusiwa kuwaoa wanaswara na mayahudi bila shaka, sharti wawe watulivu na wenye kufata dini zao bila kuwa waasherati, rejea Surat Alanaam aya ya nne utapata ufafanuzi kutoka kwenye Qura'n. Kumbuka hutakiwi kusema kitu hakifai au haramu bila ushahidi na hutakiwi kuhalalisha kitu bila ushahidi. Kisheria ya kiislamu ndoa yao haifai kwasababu hawajafunga katika maadili na muongozo wa kiislami ilitakiwa waende kwa Shekhe na si kanisani.
    Pili Si kila anayeitwa HAMAD ni mwislamu na si kila anayeitwa irene ni mkristu, imani zao wanajua wenyewe na Mungu wao, na mafunzo waliyoyapata. Jamani someni na Dini zenu mzielewe, mtapata kunusurika Duniani na Akhera, utakuta mtu anaitwa Muhammad, ana PHd na Degree za dunia kibao, kufunga swala hajui wala kumsujudia Mungu wake hafanyi hivyo mpaka siku ya Iddi! Allahi almustaan.

    Michuzi Usibanie comment ujumbe ufike na watu waelimike.
    Blog ya jamii haifungamani na dini yoyote wala haina upendeleo. Sijatoa maelezo haya ila tu kwasababu kuna mtu kachanganya mambo hapo juu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 14, 2009

    michuzi acha kutuzengua. uwe unachuja mambo ya kuchanganya r na l. hebu tazama 'Ekalist na Kipaimala'. watu wengine kuweni wastaarabu edit unachoandika bw unakua kama mtoto!

    ReplyDelete
  16. HII NI DAR YA WAPI???? KUNA NGAMIA?
    MBONA MNATUDANGANYA


    Kasmka

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 14, 2009

    Mzee wa Bunju akchuali nimependa komentz zako kwako. Naupenda uislamu hata kama ni mkristu na umeonesha mapenzi makubwa na ukristu hata kama sio dini yako.

    U ar da man na keep it up ikiwamo kuhamasisha ungunguli ktk dini.

    Cha kwanza tunadharau mafundisho ya dini then tunadharauliana wenyewe, kufanya maasi, uzinzi na kuuana.

    Teribo bro na inaniogopesha hata mimi
    Ona watu wanavyonengua kwenye miziki ya injili. Nasasa kuipua albamu ni kama Ndanda Kosovo ikiwamo wacheza show wa ajabu

    Rabi tuhurumie wote kwa pamoja wakristu na waislamu-Dunia inakwisha

    ReplyDelete
  18. jamani mambo ya kutaka kujifanya hamrudii mambo mbona mnachemsha hayo ya ngamia yanahusiana nini na ,hilo gauni si ungevaa baibuina bwana kanzu,huku kuchanganya mambo kwa kweli umependeza lakini hiyo staili ya ngamia mie bado,kwahiyo inamaana wewe utakuwa wa kumvuta kila siku mbona kazi na kwa shemeji kusuka mbona noma,wazazi kweli wanasemaje hapo dada simtakuwa mnagombania vibanio,na msusi atamuanza nani mambo ya wenzetu tuwaachi,kwa mila zetu hiyo noma,,kama ulivyomvuta kwa kamba na kanisani kaingia pia kamba peleka kwa kinyozi na herini atoe noma na gari la mbuga noma,unachanganya keki na bia haviendi,

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 15, 2009

    Mimi naona ingekua poa kama yeye ndiye angepanda huyo ngamia na Mumewe ampeleke.

    Dada kushika kamba nakumbeba mume ...mhhhhhh......tukiangalia hii .....

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 15, 2009

    Hongera dada Irene ila hapohapo nakupa pole kwa sababu msichana mzuri kama wewe kuolewa na mcheza mpira tena raia wa kigeni sidhani kama ilikuwa wazo sahihi.
    Nachoweza kusema tusubiri baada ya mwaka mmoja tuone kama ndoa hii bado itakuwepo!!!!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 15, 2009

    watu mna mapepo humu ndani???

    eti tuone ndoa itadumu..
    dini sijui wakristo wako felxibo..
    uislamu unasemaje..
    mara ngamia wako dar..

    nyie vipi

    khaaaa

    samahani lakini

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 15, 2009

    mama yeyote mtanzania,mstaarabu,na anaefuata maagizo ya dini tena niseme tu mkristu asingependa kuona mwanae au bintie anaolewa na mtu wa dini tofauti,tena msuka nywele,na pia mtoboa maskio.
    any-way hongera sana irene
    jk

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 15, 2009

    annonymous wa Tue Jul 14, 06:21:00 PM naomba nikuulize kwa vile umenukuu katika qur-an, sasa basi niambie ni nini tafsiri hasa ya manasara na ahli kitab? kumbuka waislamu wamepewa rukhsa kuoa ahli kitab (watu waliojiwa na vitabu vitatu vya mwanzo), na unajuwa fika kuwa nabii issa hakuletwa kwa ulimwengu wote ila kwa taifa fulani, kwa hivyo watu wa mataifa mengine hawamo katika unasara au ahli kitab.

    Pili sababu hasa ya kuruhusiwa kuoa ahli kitab ni kwa sababu wanafata sheria sawa na za waislamu katika maisha yao ya kila siku toka kuammini kuwa kuna mola mmoja tu, kula vilivyochinjwa, kuoga baada ya jimai, kuoga baada ya siku za mwezi na kadhalika, kujikosha baada ya kwenda haja kubwa na ndogo, mambo ambayo wafataji wa dini ya kikristo hawayafati.

    Kumbuka sio wakristo wote wa sasa ni ahli kitab, kwani kitabu alichokuja nacho nabii issa hakikuwa kwa kila binaadamu duniani. kumbuka kuwa ni nabii muhammd pekee ndie alieletwa kwa ulimwengu wote.

    Michuzi comment yangu ya mwanzo kam hii sikuiona hapa naomba hii uiweke ni kuelimishana hapa kidogo

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 15, 2009

    Mwenzenu anawaambia watu kaolewa na staa[UJIKO],iga vinavyoigika,huyo ngamia wanini really? wote wamekutana washamba tu.CONGRATULATIONS ON YOUR UNION.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 16, 2009

    anonymous 01:25 pm, ni kweli unayosema, lakini kuna 'kupenda', na kuna 'reality'. Unaweza ku-wish kitu fulani, lakini reality isiwe hivyo. Hivi umeshawahi kufikiria, kama kuna 'mama yoyote mtanzania na mstaarabu' ambaye asingependa akae na mwanae au bintie mpaka miaka 40 bila kuolewa...?!!!! Ataolewa na nani hayo mengine sasa... mzazi anapaswa kushauri tu, mwanae kashakua ana maamuzi yake...
    Pia utu wa mtu haupimwi kwa kuwa huyu ni mtu wa dini gani... that is why watu wa dini tofauti wanapendana kila kukicha. Yote ni majaribu ya dunia tu, hakuna aliyefika huko chini akajua kukoje. Unaweza kuona mwenzio anaenda jahanam kwa kuolewa na mtu wa dini tofauti, lakini wewe na uislam au ukristo wako na upo na spouse wa dini sawa na yako msiende peponi pia.... Let us not be judgemental, na tumuombe Mungu atunusuru na adhabu zake

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 16, 2009

    Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote ulimwenguni...PERIOD

    ni weli annon,utang'ang'ania dini na mbingu usiingie...patamu apo

    ni hayo tu

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 16, 2009

    Jamani maneno mengi ya nini kama kuolewa kashaolewa waacheni waendeleena maisha yao msianze tu kuwatabiria eti tuone kama ndoa itadumu blabla kibao kilichopo ni kuwaombea Mungu ili waishi kwa amani na upendo na ndoa yao idumu tusipende kuwa judgemental maana hata sisi hatupendi watu watujudge its only God knows khaaaaaaa!!! give them breack

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...