Kamanda Ebrahim Makunja akiwajibika

Radio Voice of America idhaa ya kiswahili inayorusha matangazo yake kutoka mjini Washington DC inawaletea mahojiano maalumu na kiongozi wa The Ngoma Africa band,Ebrahim Makunja aka Ras Makunja "Bw.Kichwa Ngumu".

Mahojiano hayo yatasikika wakati wowote leo hii jumatano 8-07-2009 kwa wasikilizaji wa Afrika mashariki na kati, wakati Mtangazaji wa radio VOA Bw. Abdushakur anamuhoji Ras Makunja kuhusu nafasi ya mziki wa dansi katika soko la kimataifa?

Pia Misukosuko na mitihani gani? iliyokumbana na bendi hiyo hadi kufikia mafaniko ya kuburudisha mziki wa dansi kwa kasi kubwa katika himaya ya jamii na washabiki wa ulaya ambako mziki huo wa dansi kwa sasa unatamba!

mtangazaji wa VOA Bw.Abdushakur ambaye pia bingwa wa maswali alimuhoji mengi Ras Makunja kuhusu mziki na nyimbo za ngoma africa ambazo mara nyingi zimekuwa na ujumbe au ushauri muhimu kwa jamii,pia miziki wa dansi kwa nini umeelekeza kasi kubwa ulaya?

Ili kusikiliza mahojiano hayo na majibu ya Ras Makunja tembelea mtandao wa radio VOA

ingia katika 'muziki kutoka Afrika'
utapata kitu na boksi lake...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2009

    kamanda naona kasi kubwa,sio ya kawaida,umekuwa hazina mpya katika box la dansi

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2009

    Kamanda hapumziki,kila kukicha mzigoni,kaza buti ukubwa jiwe mkuu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2009

    Hi! inaelekea kajamaa ketu kanafanya kweli na mwendo wa kasi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2009

    interview yake inaujumbe wa maana,nimemsikiliza kajitahidi sana kuongelea swala la ulevi katika jamii,pia mzungumzaji mzuri.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2009

    Unajua Ras kuna kitu kimoja kanigusa katika mazungumzo yake na VOA,kuhusu takwimu na vigezo vilivyotumika shiliaka la WHO na kuiweka bongo kuwa nchi 20 katika orodha ya nchi zinazoongoza kwa walevi! Mimi nakubalina na ras,kuwa takwimu hizo sio sahii kwani bongo haina viwanda vingi vya vinyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...