muonekano wa kiplefti mpya iliyoanza kumea katikati ya barabara ya mtaa azikiwe street jijini dar kuanzia jumatatu ambapo misumeno ya lami, sululu na nyundo zilitembea ili kuweka mambo sawa. redio mbao zinasema hii mchakato ni operesheni ya kutengeneza bomba la maji machafu lililoharibika ila kwa vile bongo ni tambarare kazi hii itapokwisha kiplefti itaendelea kuwepo hadi mwakani. foleni ya magari inayojiri katika kiplefti hii iliyo katika moja ya barabara bize sana jijini si ya mchezo. globu ya jamii itawaletea maendeleo mara kwa mara


kaka majina ya mitaa yamekupitia kiplefti nini? huu sio Azikiwe/ Maktaba?
ReplyDeleteAnonymous unayeuliz kipleft ni nini ni ngumu sana kukueleza kama huwa hufuatilii stori zetu hapa, wacha tuneoelewa tuendelee na libeneke.
ReplyDeleteanko nannhii hiyo kipleft ipo chini ya nani? Nasikia ile karibu na BOT ulialikwa kuizindua ilipokamilika, anko bwana