Anko nanihii ambaye ni mkuu wa
wilaya ya nanihiino na balozi wa nanihii,
Bila kukupoteza muda, naomba unisaidie kupata maoni ya wadau kuhusu swala hili ambalo kwa muda sasa linanisumbua saaaaaaaaana kichwa. Ni kuhusu wizi wa mizigo eapoti ya uwanja wa ndege Dar.

Sijui mimi nina gundu, sijui ndo utaratibu? ila nimechoka.
Mwaka jana June nilienda home kutoka Japan nilikuwa na digital Camera nne,laptop moja, simu za mkononi tatu na vifaa vingine vidogo vya electronics. Hizi zilikuwa ni zawadi kwa ajili ya ndugu zangu kwani ilikuwa ni siku
nyingi sijaenda nyumbani..

Tulivyotua eapoti ya uwanja wa ndege wa Dar, nilishangaa kuona masanduku yangu hayajafungwa. Na ile kufungua nikakuta vitu vyangu vyote havimo! Nikalalamika sana mpaka kwa mkuu wa kitengo cha mizigo nikaambiwa wala hawajaona kitu.
Nikabwaga manyanga...vekesheni yangu yote sikuwa na raha.
Sasa la kusikitisha zaidi, juzi nilikutana na mzungu mmoja raia wa Norway, yeye ni mhadhiri wa wa Chuo. Katika maongezi yetu nikamwambia natokea Tanzania, akasema alikuwa Tanzania mwezi wa tano ila akasema hatasahau safari hiyo, kisa? Akasema aliibiwa vifaa vyake vyote vya electronics alivyofika Eapoti.
Anasema aliumia sana kwani aliibiwa laptop iliyokuwa na information muhimu sana alizotakiwa kupresent kwenye mkutano Tanzania, kidogo achanganyikiwe.

Sasa hapa ndo mambo yananichanganya zaidi, kabla ya kwenda nyumbani nilituma laptop mbili kupitia Express mail, nilitrack mzigo mpaka Dar. Ila zilivyofika Dar. Posta wakasema kwamba hawajapata mzigo wowote na wala hawana information zozote, niliongea na Postal manager Dar. akasema wala wao hawausiki kabisa na kupotea kwa mizigo kwani hawaiwafikii.

Naomba wadau mnipe mawazo, tukisafiri na vitu vyetu wenyewe vinaibiwa na tukisema tuvitume bado vinaibiwa! Besides insurance, nini cha kufanya kuhakikisha unapata mizigo yako kamili?

Na nimefuatilia na watu wa ndege wanasema mizigo haifunguliwa tena mpaka final destination. Tafadhali nimechooka na hii kitu.

Mungu azidi kutubariki
Libeneke lidumu
Mdau Mwenye Usongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 66 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2009

    vitu muhimu kama laptop, camera etc kuwa navyo kama hand laggage. Usiweke kwenye mabegi. Pole sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2009

    Pole sana na matatizo yaliyokupata. Kwa kweli imefika wakati watanzania tubadilike. Tunatia aibu nchi.... Halafu pale waziri akisema hatupewi kazi kwa sababu si waaminifu tunakuja juu.

    Uwajibikaji wa udokozi unatakiwa uanzie kwenye menejimenti ya Posta na DIA/DAHACO, kwani wao ndio tumewapa mamlaka ya kusimamia vyombo hivyo. Kama wizi unakithiri, inabidi tuanze kuwawajibisha viongozi wao.

    Fikiria huyo Mnorway atakavyoenda kwao, ataitangaza vipi Tanzania?? Tujirudi jamani...it is too much !!

    ReplyDelete
  3. beba kama hand luggage,au tumia DHL....

    tutafanyaje na sisi wenyewe watanzania tushakuwa mbumbumbu na kuamua kiujinga kabisa kuibiana wenyewe, na hapo hapo tunataka uchumi ukue???

    yote maisha...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2009

    Nchi ya Tanzania ni nchi ya wezi sijawahi kuona kabisa,,,yaani mpaka vitu vilivyopitia njia ya post vinaibiwa!!! ah,,,ama kweli wezi duniani ,Tanzania mnajiaibisha kabisaa.Ndio maana nyinyi tu ndo mnazidi kuchukua dola 20 kwa visa kwa wananchi wa inchi zinazopakana na Tanzania,,,ni nchi yenye uroho tuu wa hela...Ama kweli mafisadi,wezi,watoa hongo,wababe,wanyonya watu, woooote wako hapo Tanzania.nikumbukapo kuja Tz roho inanitoka puuuu!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2009

    Pole sana Mdau. Mimi nimekuwa na kawaida ya kupiga debe hawa jamaa wawe wanakuja Tz kwa jili ya utalii, kwa kuwaelezea vivutio vingi tulivyonavyo. Katika harakati zangu hizo, nilipiga debe kwa Sister mmoja aliyekuwa akipanga kwenda Namia kwa mara ya pili, ili aende Tanzania badala yake. Nilichoka aliponielezea yaliyo mkuta rafiki yake ambaye alikwenda Tanzania, na wakaibiwa at GUN POINT kambini kwao! Aibu Loh!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2009

    Ebwana umenichekesha!Ila nakuonea huruma at the same time.Pole sana kwa mkasa huu.

    Bilasha,huyo raia wa Norway akiflash back memory juu ya TZ anakumbuka hiyo experience rather than kindness and warm welcome ya watanzania.

    Ni aibu rafki yangu na I would like to suggest solutions,

    I am not sure of this that there is proposed plan to build/extend/refabrish or complete overhaul of the DIA.If it is true then the following will occur i guess

    New modern control mechanisms such as CCTV,swipe cards,proper personnel recruitment with attitide towards risk such as that of theft as they will be risk aware

    customer services will improve and could even be automated or outsoursed to servicing organization who in turn will provide value for money services(efficiency,effectiveness and economy).

    Therefore,directors should ensure compliance with procedures,policies that minimize this risks and take a lead in stressing the importances to safeguard properties to all empoyees.Stringent actions have to be taken for any breach of control activities.

    The complete value chain should as well be monitored by independent person with objective mind with regard to the achievement of complete system.Ie that ensure customer like you be satisfied.

    Moreover,one could think of theft risks to be prone to violation and stuffs will still be susceptible to be stolen regardless of proper of the above controls since Tanzanians are clever people when it comes to take/rukia opportunities.

    In this case I could write about cognitive moral reasoning behind their action but I think at this time,it will not serve a purpose.

    So,ndugu yangu,currently,for things of material value and scarce such as digital equipments that would defenetly tempt someone to take, i would use trustwoth mechanisms of tranfer such as a person to person.eg someone you know is going home for a vacation.

    I would seek feedback from customers everytime on adequacy of this system as you current do ,so as to get altenatives of this issue.Niko UK na ninaundergo same sort of thoughts especially on insurance on properties held at home whether insurance firms are credible as these in UK

    There is a lot to write about Tanzania.At the moment lets read about others opinions

    Mdau (John) UK

    ReplyDelete
  7. Babau hiyo noma mimi mwenyewe nilimpa jamaa Begi na full electronics ,dogo kapata begi bongo halijafunguliwa kufuli ipo pale ,halijakatwa .Kufika home anafungua Begi kuna vitu vitatu tu ,Power Amp 45Lb na taa ya Dj.Kwa ushauri wangu naomba watu wafungue mabegi pale Airport nje kabla hawajaenda nyumbani ,Washenzi wale hawana maana hata kidogo.
    Sijui lini tutaendelea maana nilipeleka Technolgy bongo jaribu kubadilisha sitasahau Camera kama 7 ,camcorder,Hard drive and DVD kama kumi hivi vyote vimeondoka.
    Itabidi siku niwashukie tu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2009

    Sio siri hivi vitendo vinasikitisha sana,Hebu fikiri laptop yako imesheheni document zako. Mimi naifahamu setting ya pale Airport. Eneo ambalo wizi unafanyika ni wakati wale wapakua mizigo wanapotoa mizigo kuleta kwenye mkanda! Hapo!!!!!!! Cha kushangaza ni kwamba SwissPort ambao ndio wanahusika na ground handling ya mizigo wana full CCTV Camera ambazo zinamlika tangu mzigo unapopakuliwa mpaka abiria anapochukua mzigo wake kwenge belt. Kama hao mamanager wanasema hawajui aliyechukua basi wanashirikiana na hao wadokozi!!! Hakuna sehemu nyingine pale airport udokozi unaweza fanyika! Ni hao hao!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2009

    yamekukuta yaliyonikuta kaka. mwaka jana nilikuwa njia kuja sweden, walichonifanyia hao jamaa wa uwanja wa ndege sio. walichukua laptop, speaker fulani, na vyakula vya kibongo. unga wa mahinhi, karanga, dagaa na kitiomoto iliyokaangwa. juzi pia nimetuma barua moja muhimu sana bongo. hadi sasa ni wiki ya pili, haijafika katika box husika, japo huku inaoneka kuwa ilifikaposta tanzania tarehe 4/7. nimepanga nikirudi lazima sh isimame.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 22, 2009

    Hizi njaa zetu zinaharibu mambo mengi sana.Tatizo ni kwamba wizi umeanzia Huko kwenye ngazi za juu serikalini na ndo maana kila mtu amejichokea saiv na hakuna utu tena.Mbaya zaidi ni kwamba Hata ma-bosi wa hao wezi hawachukui hatua yoyote saa sijui wanafanya kazi gani huko ofisini. NA kikwete pia am sure anayaona yote haya lakini sijawahi kumsikia akimchimba mkwara bosi yoyote, nalo ni tatizo la kua na rais anae-smile all times. Inaboa sana.Ren-Mich!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 22, 2009

    Pole sana Mdau,uwizi ni kitu cha kawaida sana pale Airport,jirani yangu ambaye anafanya kazi pale alikuwa akinielezea jinsi gani kulivyokuwa na uzembe katika usimamizi unaosababisha watu waibe wanavyotaka,iliniuma sana aliponiambia kuwa wakubwa wanafahamu fika hilo tatizo ila hawataki kuwajibika,sasa nyie wapuuzi vigogo wa Airport munashindwa hata kufunga camera moja tu inayoweza kurecord shughuli zinazofanyika pale ndani ili panapotekea uwizi mujue kufuatilia?ni lini mutapata akili ya kuacha kufikiria matumbo yenu na kuwa na ubinadamu wa kujali wale wanaoibiwa?ni Aibu ngapi tungeweza kuzizuia kwa ajili just ya kukubali jukumu kama mfanyakazi adili wa serikali?Au ni hivi viburi vya kuwa na mtu wako serikali anayekulinda siyo?Serikali nayo sehemu sensitive kama hizi ifuatilie ufanyaji kazi zake

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 22, 2009

    Pole sana bwana! Nami nilituma kitabu cha dini, kimefika posta Tanzania - recorded delivery, halafu ndugu yangu hakukipata, sasa jamani nikajiuliza hivi kweli mtu anaiba kitabu hata cha dini?

    Nikatuma pesa kwa njia ya Western Union, basi walimzungusha ndugu yangu mpaka inakatisha tamaa. Ati mtu unasimama foleni siku nzima kumsubiria bosi anayehusika na Western Union wakati wafanyakazi wengine wapo na wanaendelea kutoa huduma kama kawaida.

    Namwonea huruma huyu ndugu aliyeibiwa hizo laptop, kwani ni ngumu sana. Unajua ikishakupata basi unajua uchungu ulivyo.

    Pole sana mdau!
    sayonara!
    Mkulima

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 22, 2009

    mdau pole lakini mimi hii story haijanikalia sawa kuna kitu kinamiss hapa imetiwa chumvikidogo hasa kwenye tracking ya express mail.. kawaida mzigo ukifika kampuni iliyotuma inakupa taarifa kupitia tracking number yako kuhusu muda, mahali na jina la mpokeaji.kama ni kweli ulipaswa ufe na kampuni uliyoikabidhi mzigo ili wao wakabane koo na posta

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 23, 2009

    Pole sana mdau mwenye usongo. Yaliyokupata na Posta yameshanipata mara mbili. Zote mbili zimeishia kwa wafanyakazi wasiofahamika wa Posta kupata laana maana mizigo yenyewe ilikuwa zawadi kwa watu waliokuwa wanaihitaji kuliko wafanyakazi wa Posta.
    Ushauri wangu kwako mdau ni huu: Kama unasafiri na vitu vya elektroniki usipakie kwenye mizigo ya kucheck in. Beba kwenye mzigo wako wa carry on. Kuna wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa eapoti watakuangalia kwa jicho la usongo lakini utakuwa umewapiga bao.
    Kama unataka kutuma mzigo wenye thamani kubali kubeba hasara lakini uutume mzigo huo kwa njia ya Fedex/UPS/DHL. Wafanyakazi wa shirika la posta wako tayari kurisk vibarua vyao kuliko kuachia mzigo hata kama umekuwa registered.
    Mwisho kwa wafanyakazi wooote mnaoshughulikia mizigo ya watu iwe bandarini, eapoti, posta nk. Mnaitia aibu nchi yetu. Fanyeni kazi yenu kwa uaminifu. Wanaijeria waliletaleta utapeli sasa hivi mtu ukimwambia tu wewe ni Mnigeria anakuona tapeli. Mnavyoendeleza udokozi ndio mnalijengea taifa sifa mbaya. Itafika kipindi mtaenda vekesheni ughaibuni na hela za vitu mlivyoiba halafu mtaona vinavyowatokea puani. Ukimwambia tu mtu umetokea nchi gani unakuta anashika pochi yake vizuri. Mbaya sana!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 23, 2009

    Pole sana mdau kwa masahibu yaliyokukuta. Ni uungungwana tu kutoa pole mtu anapopata matatizo lakini kuna mambo mawili naomba nichagie. Mosi si sahihi sana kusema mizigo hiyo imepotelea Tanzania japo inawezekana. Kabla ya mizigo yako kufika Tanzania ni nahakika imepakiwa mara mbili au zaidi kwenye ndege tofauti kwa ni usidhani imepotelea huko?
    Pili kama alivyosema mdau wa kwanza hapo juu huo ni uzembe wako vitu vyote ulivyotaja vinawezekana kabisa kuingia kwenye "carry on luggage" kwa nini uviweke kwenye mizigo ya kucheck-in? Mbali yakuwa kuna hatari ya kuibiwa vilevile kunauwezekano wakufikisha vitu hivyo vikiwa vipandevipande

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 23, 2009

    Inasikitisha sana,hapa tatizo ni nini? mshahara mdogo au tabia ya udokozi posta wanaiba vifurushi,eapoti wanaiba mizigo ya watu watanzania tumerogwa jamani?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 23, 2009

    Kwa mtanzania yeyote aliekulia tanzania na kuijua tanzania kama bongo daima akirudi nyumbani na laptop, camera huvibeba katika hand laggage kwa kuepuka kuibiwa. sisemi huwezi kuibiwa namna hiyo lakini una chance nzuri ya kusalimika. Na ukiibiwa airport huna hata haja ya kulalamika kwa mkuu wa nini au nini pale airport kwani wote wanajuana na naamini wanagawana kila wakipatacho. TANZANIA TAMBARARE!!!!

    ReplyDelete
  18. Hili naona Raisi aliingile maana hii inatia aibu sana.Itabidi nipege simu nyumbani kuona kama mama amepata dawa nilizomtumia kwa posta. Njia nyingine ya kutuma ni kwa DHL ambaye ni ya uhakika. Haya mambo ya wizi yanatakiwa yatiliwe mkazo mashuleni kwamba kuiba in vibaya, kusema uwongo ni vibaya n.k. mambo mengi haya yanatokana kwa sababu ya umaskini na tamaa wakati mwingine. Nafikiri Raisi ana kazi kubwa sana ya kupungunza unemployment rate nchini. Ukipunguza unemployment na crimes pia zinapungua. Nafikiri serikali inapokuwa madarakani hayo ni mambo mojawapo ya kuipima serikali kimaendeleo la sivyo uchaguzi mwingine unapokuja ichaguliwe serikali nyingine ambayo inasaidia kutatua matatizo ya unemployment nchini.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 23, 2009

    pole ndugu , huo mchezo mchafu sana hapo dar airport wameshajua kua watu kutoka nje ya nchi mara nyingi wankuja na electronics hasa laptop,simu camera, so kuna kamchezo kachafu kafungua na kuchukua..MKASA kam HUO umekuta my AUNT last month WAMECHUKUA PSP GAME zawadi yA mtoto(siunajutena mtoto ukimuahidi kitu) af bila AIBU wakasema may b uliibiwa Nairobi.bahati nzuri laptop alikua nayo ktk hand luggage.MICHUZI please tunaomba uwasilishe(print km yalivyo) malalamiko kwa mkuu wa kitengo cha mizigo dar airport hii ni AIBU, km halijakupata linakuja basi.. be careful...

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 23, 2009

    Rais jk alitembelea bandari ya dar nakuwahambia wafanyakazi kua anajua wanachokifanya(yani wizi), kama Rais anaongea hivyo badala ya kuwawajibisha sidhani kama tutapunguza wizi.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 23, 2009

    Mtoa maoni Tarehe Wed Jul 22, 10:28:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous na Mtoa maoni Tarehe Wed Jul 22, 10:35:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
    MAONI YENU ninayaafiki kwa kiasi kikubwa sana. Uzembe unafanyika sehemu ya kuhamisha mzigo toka kwenye ndege kupeleka kwenye mkanda. Hata utilie kufuli kubwa kiasi gani, haiwashindi kuiba ikiwa sanduku lina zipu, unatakiwa kutumia sanduku lisilokuwa na zipu.

    Mtoa maoni Tarehe Thu Jul 23, 12:00:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
    PENDEKEZO lako naliafiki kwa kiasi kikubwa mno kwa kuwa tangu nimelizwa kwa laptop kuibwa kwa kuwa nilijaribu kutuma bila warranty, tangu siku hiyo natumia Registered Mail na vifurushi vinafika salama u salmin. Walioko Marekani tumieni USPS International REGISTERED MAIL, ni nafuu sana ukilinganisha na FedEx/UPS/DHL. Mfano, laptoop kwa FedEx ni USD$ 280 wakati USPS ni USD $ 100 tu! USPS registered mail hiyo inaandikisha kila kitu na kila step inakofikia anayeandika lazima atie jina na sahihi, sasa ole wake kutoka kwake isifike inakotakikana ataeleza alimpa nani na sahihi ya huyo aliyepewa ipo wapi, akishindwa maelezo anatoa fidia na adhabu atapewa na ofisi yake.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 23, 2009

    Mpwa pole sana. Tutaanza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, mpaka tarishi. Watu wanaendekeza sana njaa! Shortcut haitakuja kuwatoa maisha!!! Wezi wote wanajulikana,hakuna siri Airport! Na kibaya zaidi wanalizana wenyewe kwa wenyewe! Mkuu wa Wilaya ya nanihii, kwa heshima na tahadhima, tunaomba utuwekee picha za wafanyakazi wa nanihii, lifanyike gwaride la utambulisho online!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 23, 2009

    Pole sana mdau kwa hasara uliyoipata. Kwa kifupi eapoti,posta,bandarini,hospitali kote kumeoza. Mabosi na wakuu wa idara wanajua na wanashiriki kwa njia moja au nyingine katika wizi unaoendelea kukua siku hadi siku. Wenyewe wanajiona watoto wa mjini kumbe ujinga na kuharibu jina la nchi. Mdau Ally....employment unayozungumzia katika comment zako hapo juu haina msingi. Wale wanaoiba ni wafanyakazi halali wa posta,eapoti n.k. Tanzania inakatisha tamaa. Wizi na rushwa vimekua tatizo sugu. Aibu tupu.

    ReplyDelete
  24. Solution ni kubinafsisha polisi,dahaco,DIA,posta na bandari ili chain yote ya mizigo iingiayo isiwe na wabongo.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 23, 2009

    Poleni, huu ndio mfumo wetu nchi za dunia ya tatu. Pale Kenyatta Airport usiseme begi linafunguliwa mbele ya macho yako na ukija juu wanakuzushia balaaa ambayo utajuta kuzaliwa. Umaskini Umaskini Umaskini!!1

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 23, 2009

    oh pole sana ndugu yangu!! kukupa pole ni wajibu kwa sababu umepoteza vitu vyako. Naungana na mdau mmoja aliyecomment kuwa fikra zetu hasa sisi tunaoishi nje tu haka kakasumba ka kuwa kila wizi unafanyika hapa bongo,.KWA KWELI BONGO KUMEBADILIKA SANA KUHUSU MAMBO HAYO!!Nasemea DAR airport. jaribu sana kutumia flight zinazotoka ulaya direct to DAR uone kama hayo yanafanyika bongo. kumbukeni hasa wale wanaopitia flight za ghuba kumbukeni pale wafanyakazi wa mizigo wengi wao ni wahindi ambao wametoka kwao kwenda huko kutafuta maisha tena kwa mikataba ya muda fulani hao je hawawezi kuiba? kufanya kazi.kuna kisa kiliwahi kutokea dar eapoti na kilirushwa na vyombo vingivya habari vya bongo hata mitandaoni! Kuna kina mama wawili walisafiri na Ethiopian airline nao walikuta mabegi yao yako wazi na baadhi ya vitu vimeibwa basi walikomaa kiasi cha kuita waandishi wa habari na vyombo vingine vya usalama. Meneja wa Ethiopian airways alikuwa mama mmoja ambaye pia aliungana na wale abiria. Kuanzia hapo vyombo vya usalama vyote vilihusishwa kufuatilia kia ndege inayofika kutoka nje. ilikua kila flight kuna kamera inayo chukua picha mara mlango wa mizigo unapofunguliw .AIBU ilioje kwa Ethiopian airlines kila flight yao ilikutwa mabegi yamevunjwa na kufuli zimezagaa ndani ya ndege.Matokeo yake yule mama meneja aliondoka kimya kimya.
    HALAFU KUMBUKENI KUWA TICKET NI MKATABA HALALI JARIBUNI KUSOMA KILA KILICHOANDIKWA MANBO YOTE HAYO YA KUWEKA VITU VYA THAMANI YAMEELEZWA VIZURI SANA INAKUWAJE WE UNAWEKA ELECTRONICS KWENYE CHECKED BAGGAGE? HUO NI UZEMBE WAKO MWENYEWE INGAWA SIO LESENI KWA WAFANYAKAZI KUIBA. PIA NAWAPA TAHADHARI KUTRANSIT KWENYE BAADHI YA VIWANJA HASA CAIRO,NAIROBI,JOHANNESBURG, ADDISS HAPO UKITRANSIT KWA MUDA WA MASAA YANAYOZIDI MATATU BASI UJUE UWEZEKANO WA KUPOTEZA VITU AU MZIGO MZIMA NI ASILIMIA KUBWA.
    JAMANI TUWE WAZALENDO.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 23, 2009

    HILI SUALA KAMA LILIVYO LIWASILISHWE KWA WAHUSIKA, YAANI KITENGO CHA MIZIGO AIRPORT, MKURUGENZI AIRPORT, WIZARA YA MAWASILIANO, NA KITENGO KIHUSIKACHO NA USAFIRI WA ANGA. MICHUZI TAFADHALI TAFADHALI NAOMBA HII HABARI/EMAIL UI-FOWARD KWA HIZI SEHEMU, HATA MTU AKIHITAJI EMAIL TUNAWEZA KUZITAFUTA KWA KU-GOOGLE AU WEBSITE YA TAIFA-TANZANIA. HALAFU TUONE KAMA KUNA LITAKALOENDELEA AU LAH THEN WANANCHI WAJUA PA KUANZIA.ASANTE

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 23, 2009

    Michuzi tafadhali waprintie hii na umpelekee juyu sijui General manager au la, kama ameshindwa kazi bora aachie ngazi, au naye anapata mgao nini. They are not serious at all with their business. Naamini kabisa uizi huu unatokea ndani wakati wakipeleka mizigo kweny conyer, kama yupo sarious kwa nini wasiweke kamera?sehemu zote za mizigo kuwanasa wezi? Hana hela apishie harambee tutachangia.Kwanini hili jambo halimkeri hata kidogo maana limekuwepo kwa muda mrefu. Posta ndio uozo mtupu kwanini nao wasiweke camera? Aibu tupu.TANZANIA NCHI YANGU NAKULILIA WAPI UNAKWENDA?

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 23, 2009

    hapo ni kufukuza tu na kuajili upya.

    ReplyDelete
  30. Duhh!!! Jamani wadau hii post kidogo inipite.Jamani posta posta posta Tanzania mtaiba hata MAVI jamani.Ni JANA TU JIONI NIMEPOKEA PARCEL YANGU IKITOKA ENGLAND NA HIYO BAADA YA KUKAA SIJUWI WAPI ZAIDI YA MWEZI KWANI IME FLIGHT TOKA HUKO TAREHE 26/06/2009 INAFIKA HAPA TAREHE 22/7.IKIWA IMEKATWA UPANDE MMOJA WA BAHASHA NA BAHASHA YAKE ILIKUWA YA SEALED ETI POSTA TANZANIA KWA KUJIBARAGUZA NDUGU WADAU,WAKACHUKUA BAHASHA HIYO NA KUIWEKA NDANI YA MFUKO WA NYLON KWA KUAPOLOGISE "SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LINASIKITIKA KUKUJULISHA KWAMBA BARUA YAKO IMEPOKELEWA KATIKA POSTA HII IKIWA IMECHANIKA.BARUA HYO IMEHIFADHIWA KTK MFUKO HUU WA PLASTIC ILI ISIATHIRIKE ZAIDI" HAYA POSTA NASHUKURU LAKINI, JE KUNA UKWELI HAPO JAMANII!!! Cjuwi kama tutafika kwa mwendo huo.

    ReplyDelete
  31. Pole mdau, mi huwa narudi home kila baada ya 2 months, na nimeshajifunza maana wale hawachagui, walishafungua langu wakakuta hamna cha maana wakaishia kuiba perfume iliyokwishatumika!
    Ila huyo mzungu atawekaje laptop kwenye mzigo, hiyo hubebwa popote pale uendapo!

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 23, 2009

    NI SIFA MBAYA SANA KWA TANZANIA TENA SANA,HII NI MIAKA MINGI SANA HAKUNA KINACHOFANYIKA KUKOMESHA HALI HII NI AIBU,UNAJUA MIZIGO INAIBIWA NA WAFANYAKAZI WANAOINGIA KUSHUSHA TOKA KWENYE NDEGE,MAANA HAPO HAKUNA CCTV,KILAMTU ANALALAMIKIA AIRPORT YA DAR ES SALAAM,NA MIMI BINAFSI HAKUNA KITU KINGINE KINACHONIUDHI NA KUNISIKITISHA KUWEKA VIJANA WA KUSAIDIA KUBEBA MIZIGO(PORTER) HII NI AIBU TUPU YA WATU ILIWAPEWE ASANTE ETI WAMESAIDIA KUKUPA TOROLI,NIMESAFIRI SANA KWENYE VIWANJA VIKUBWA HAKUNA HII ILA TZ TU,HAWA WANAKIMBILIA KUCHUKUA MATOROLI ILI WEWE UWAPE CHOCHOTE NA KUJIFANYA WANAKUSAIDIA TANZANIA INAKWENDA WAPI????

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 23, 2009

    Pole sana mdau uliyeibiwa.Hivyo ndivyo Tanzania ilivyoingia karne ya 21.
    Solutions:
    1.Ukituma mzigo tumia UPS,DHL,FEDEX
    or any other reliable carriers kutegemea uko wapi.All must be insured ili ikipotea ulipwe.
    2.Put all your electronic equipments in your CARRY ON and never put them in your CHECK IN BAGS
    3.Unapokaribia kutua omba dua/muombe Mungu kulingana na imani
    yako.
    Nafikiri wadau wengine wataongezea
    kutokana na uzoefu waliokutana nao
    wa sayansi na teknologia karne ya
    21 Dar Airport.
    Mdau DC

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 23, 2009

    Jamani nahisi pia Hand laggage pia zina limitations zake, nakumbuka isiziki zaidi 7kgs. sasa sijui kama huyo jamaa mwenye lapotop 2 au tatu na vitu vingine vidogo vidogo angeviweka kwenye hand laggage. Tatizo wizi umezidi sana.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 23, 2009

    tanzania tunaanza kua kama naigeria wizi wizi usiokua na maana!
    Jamani mbona wenzetu hata begi libaki siku nzima kwenye mkanda unalikuta salama kesho yake?mfano heathrow-uk au kwasababu kuna camera uwanjani?kwanini bongo zisifungwe?

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 23, 2009

    HILI NI JAMBO MOJA LILIOMTOA LOWASSA KAZINI.ALIFUTILIA HAKI WATU WAKA AMUA KUMTOA.SIO SIASA HII,NINACHO SEMA KWAMBA SWISS PORT NDO WANA USIKA NA MIZIGO KUTOA KWENYE NDEGE.MIMI BEGI NILIPOTEZA KWENYE NDEGE SASA BEGI LITAPOTEAJE KWENYE NDEGE?NIKAAMBIWA LABDA LIMEIBIWA KENYA KUFUATILIA BEGI LIPOKELEWA DAR KUFUATILIA ZAIDI MARA NIKAPEWA BEGI LANGU NIKA AMBIWA LILICHANGANYWA KWENYE MIZIGO YA DOMESTICK.KWA KUWA NILIKUWA NIMEPATA BEGI LANGU SIKUTAKA MAMBO MENGI. SWALI NI JE VINATOKOJA PALE?UKISHIRIKIANO NA WAKUBWA

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 23, 2009

    Ushauri wangu kwenu ni kwamba, muwe mnapitia Nairobi kwenye uwanja wa Jommo Kenyata maana kule ndio kuna usalama zaidi. Huwa mara nyingi nafanya hivyo, kwani wabongo hata muongee vipi hawawizi kulitatua tatio hili ambalo kwa uzoefu lilianza mwaka 1990. Inauma sana kuibiwa vizawadi vyako ambavyo kwa mapenzi mema tu umeamua kuwabebea ndugu zako waliokumiss.

    Mdau
    Kimara Bongo.

    ReplyDelete
  38. AnonymousJuly 23, 2009

    Hii ishu utaielewa zaidi kama kwa namna mmoja au nyingine upepo umekupitia..Inauma sana wadau.

    Mimi kuna mizigo ilitumwa na Brother USA-Wichita, laptops mpya 2,na simu Blackberry mpya 2, na kila step muhimu kazifuata na tracking number(Sender USPS) kujua mzigo unatoka wapi unaenda wapi, na tatizo ni pale ambapo inakuwa ni international dispatch hapo ndipo ugiza unaanza.
    Jamaa wa posta huu mchezo ni wa kawaida sana, nimejua hali ya pale baada ya ya UPEPO wa kuibiwa kunikuta, jamaa wanatakiwa kurudisha respond to sender kwamba mzigo umefika,na tamaa inaanza pale ambapo wakisoma details za mzigo na mchezo mchafu ndio unaanza,jamaa wa posta wanauwezo wa kuutoa mzigo so easy kwa nyuma ya posta(nenda utaona pale posta mpya kwa nyuma kabla ya kuingia packing ya magari,papo so easy).Pia mchezo huu wa kutoa mizigo ya wateja nahisi umewezeshwa zaidi na wakwepa kodi za TRA(nimejua yote haya kwa kujua ukweli wa mizigo yangu,wapi kuna bleach?)so jamaa wanauweza wa hata kuinyima serikali kodi,so tamaa ya receiver kukwepa kodi kwa kujaribu kutoa mzigo kabla jamaa wa TRA kuugagua(kufungua na wewe kuwepo hapo hapo)ndio mianya na kuharalisha mchezo mzima, ni deal ya mkuu wa kupokea mizigo na msuka deal(messengers), so simple logic yangu ni kwamba kama wataweza kumkwepesha mtu na kodi je kuiiba mizigo mingine si humo humo maana kwa wasioelewa ni kuwa mizigo inakuwa kwenye dispatches(Mizigo mingi kwenye limfuko limoja,say from Chicago to tanzania)na iwapo mkwepa kodi yupo kwenye dispatch say dispatch 78 na jamaa X ambaye si mkwepa kodi na katuma nice SONY camcoder na jamaa wameiona basi ajue kaumia jamaa wataichukua kama yao tu(Wataiba)...
    Na ukifuatilia mzigo wako watakwambia either in between mzigo umeenda wrong address(kuna maneno kama destination Darrusallam-brumei,not Dar es salaam-Tanzania,jamaani ni uongo wa kila siku pale,maana Dar es salaam ipo East Africa,with this 255 code!!! na mwishoni kabisa wanakwambia any loss wao kama reeiver hawawajibiki, posta hao pale ghorofa ya pili)
    INAUMA SANA, JAMAA NI WEZI na WANA MAKESI KILA LEO!!!

    Chakufanya si kufanya marketing kwa DHL/TNT etc bali kwa shirika letu la kitanzania POSTA si wawo kujirekebisha(maana hawawezi maana wanajuana)ni kwa serikali kulitolea macho lile shirika kwa serikali kuwawajibisha management nzima.

    Ni hayo tu, Mdau(The Dreamer)

    ReplyDelete
  39. AnonymousJuly 23, 2009

    Njia mojawapo ni kumuhoji mkuu moja hapo air port aeleze hii nadhani inaweza kuleta mshtuko kwao wakaanza kudhibiti hayo wezi.

    Wezi ni hayo wafanyakazi wadogo wadogo and may be wanashirikiana na baadhi ya mabosi.

    Badala ya kumuhoji Dr LIKI kila siku, au kuweka habari za Sexiest men Bongo, wawahoji wakuu airport kuhusu ili issue.

    ReplyDelete
  40. WIZI umezidi Tz, si kwa ajili ya umaskini, bali kwa sababu ya ukosefu wa imani na maadili.

    ReplyDelete
  41. AnonymousJuly 23, 2009

    mh! ati bongo tambare ni maporomoko ya mlima sekenke!!!

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 23, 2009

    Kaka Michuzi nami sipendi hili swala wizi wa mizigo linalifanyika Posta na Airport zetu lipite bila kulizungumzia. Ili swala linakera sana na pia linatia aibu. Mimi binafsi nilimtumia jamaa yangu ulaya mizigi kama yeye alivyoniagiza nilipaki mizigo posta mpya dar na listi nikamtumia lakini ilivyofika akaniuliza mbona vitu fulani fulani havipo, alafu akasema mbona vingine sio specifications tulizoelezana na kweli mie sikuvipaki ina maana vilibadilishwa vikawekwa vibovu. Sasa swala kama hili mtu unaona AIBU kwamba ina maana jamaa kaniona ni tapeli nimemdanganya nimetuma vitu kumbe uwongo. yaani mtu mzima unakosa raha unafikiri huyu kaniona mimi TAPELI au vipi, hasa ikiwa ni jamaa wetu wa nchi ambayo sio yetu. JAMANI HAWA NDUGU ZETU MAMBO WANAYOFANYA WANATUAIBISHA, WANATUKOSESHA UHAMINIFU WA JAMAA NA RAFIKI ZETU MBALI NA KUTUPA HASARA YA VITU VYETU WANAVYOIBA. NA HII IMEANZA MIAKA MINGI. WAHUSIKA TUSAIDIENI. HII INAUMA SANA.

    ni mengi ya kuandika lakini wacha niishie hapa tu kaka.

    by mdau niliyewahi kuumizwa

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 23, 2009

    Miaka michache iliyopita Johannesburg ndiyo waliokuwa wanasifika kwa kuiba kwenye mizigo ya watu. Inashangaza sana kuona watanzania kuanzia muajiri hadi muajiriwa wanakuwa wezi. Ninaamini uwanja wa ndege ni eneo ambalo limezingirwa na kamera kupita eneo jingine lolote. Sasa kama hizo kamera zinatumika kukagua ugaidi na kushiriki wizi haifai na siyo busara hata kidogo. Kuiba mali za watu wengine ni kujilaani kwani hujui aliteseka kiasi gani hadi kuipata.
    Isitoshe wote hao wanakwamisha jitihada za Raisi JK kuzunguka kutafuta wawekezaji huku akiimba wimbo wa Tanzania ni kisiwa cha amani kumbe ni kisiwa cha wezi! Aibu iliyoje! Na inakasirisha!

    ReplyDelete
  44. AnonymousJuly 23, 2009

    kituko kabisa

    siku JK alipoenda bandarini na kutamka anajua sana yanayofanyika pale(ndivo sivo) na asifanye lolote adi sasa

    nyie mnategemea nini sasa?ya ATCL tu hamjaona?
    apa ni kubeba mzigo wako ndani tu,yalishanikuta ata mie nilikuta begi limechanwa kichini sijui walifikiri nimebeba almasi kumbe maharage na mkunungu wangu

    nachoka kabisa ikifika apa

    ReplyDelete
  45. AnonymousJuly 23, 2009

    mdau (the dreamer)

    umenichekesha sana sana,ofkoz sii mzaha ila duh

    kuna wezi waganga njaa Tz?acha tu

    anyway the best soln.kutumia makampuni ya kigeni tuachane na posta thing...uhsenzy tu

    ReplyDelete
  46. AnonymousJuly 23, 2009

    Jamani laptop 2,Video camera 3,simu,mazawadi zawadi ya mama,dingi,mabro zetu! tena wamekusubilia kwa hamu almost more than 4yrs hawajakutia machoni eti uniambie iyo ni "carry on luggage"
    Iyo ni bora tushauliane kuacha wizi kuliko kukukuruka na mamizigo kibao eti carry on luggage.Mbeki(TZ)

    ReplyDelete
  47. AnonymousJuly 23, 2009

    inatiia hasira

    ReplyDelete
  48. AnonymousJuly 23, 2009

    Eee bwana mi nashindwa kuelewa kitu kimoja tu ina maana mtu aende kwao awe mtumwa kweli?????mi najua mtu akienda kwao hawi mtumwa hata kidogo inakuwaje kwa WATZ??wizi mtuupu yaani lazima iwe inakera hata jamaa awe aliweka electonics ktk hand bag still kwanini aogope kujiwekea vitu vyake katika begi?wizi yes WIZI ni kwamba upo kwa wakubwa na ndo maana wadogo hawaogopi wala hawaoni haya!kumbukeni enyi wezi za mwizi...na viongozi mnawaachia hao mnapandikiza mbegu mbovu ktk jamii maana mtoto umleavyo...
    Mkereketwa Baba Prince
    US.

    ReplyDelete
  49. AnonymousJuly 23, 2009

    JAMANI HIVI HUU WIZI UPO MPAKA LEO!!MIE NILIDHANI WAMEACHA..HIVI JAMANI KWELI UNAMWIBIA MTU VITU VYAKE VYOTE SIJUI HUWA WANAFIKIRIA NINI...NA HIVI HUO UONGOZI WA DAHACO UNAFANYA NINI???DAHACO NI WIZI WA SIKU NYINGI SANA NA SIJUI KWANINI HAWACHUKULIWI UCHUNGUZI..MDAU MWENYE HASIRA NORWAY

    ReplyDelete
  50. AnonymousJuly 23, 2009

    Kwanza nampa pole mdau, this is a tragedy. Yaani kesi kama yako ni very common, my own cousin hapa US alituma laptop mbili kupitia USPS kwenda Arusha by express mail. Lakini alitrack kama wewe mpaka Arusha, then giza likatokea kila mtu anamsema mwenzake.Jamaa alifuatilia mpaka makao makuu bado bila bila.

    Pili nimjibu Nukta 77, registered mail na express mail through USPS zote zina tracking option. Ila ndugu yangu kwa Bongo hata akisign waziri wa posta utaambiwa mzigo wala hatujui ulienda wapi.
    Jamaa alichoelezea ni very common nyumbani, nina mifano mingi sana ya watu wanatuma mizigo express mail of which u track ur package ila ikifika Bongo unaona imekuwa received na watu wa Posta. Then unamtuma ndugu yako kwenda kuchukua mzigo, guess what? wanasema hatujaona mzigo kama huo.
    Ukweli ni kwamba kuna tatizo, na hili ni tatizo kubwa

    ReplyDelete
  51. AnonymousJuly 23, 2009

    Wadau lazima tukubali kuwa watani wa jadi pale Jomo Kenyatta wametuzidi mbali sana.Wana ustaarabu wa hali ya juu katika
    usalama wa mizigo.Nadhani hiyo ni
    moja ya sababu ndege nyingi kutoka
    Nje ya Africa zinatua pale.Wadau kutoka USA mtagundua kuwa hata nauli za kwenda Nairobi na kurudi
    US ni almost half ya nauli za
    kwenda Tanzania na kurudi US.Hata hivyo Mungu hawezi kufungua dirisha na mlango,wasioiba mizigi
    Jomo Kenyetta wanachinjana baada ya
    uchaguzi wakati ndugu zetu wanaoiba
    mizigo Dar airpot wanasherehekea
    amani na utulivu.Taarifa zisizothibitishwa zinasema kuwa
    majizi pale Dar airport wanaigopa
    sana KLM kwasababu imeshatishia
    kusitisha huduma zake Tanzania
    kutokana wa wizi wa mizigo ya
    wateja wake.Hiyo ndege pale Dar
    airport iajulikana kama FBI.Wadau itumieni kwa usalama wa mizigo yenu.Wafanyakazi wengi wa Dar-airport wanalalaka kuwa KLM hailipi
    yaani haina maslahi,Gulfair ndiyo
    inalipa vizuri.
    Naomba mjadala uendelee labda
    itasaidia.

    ReplyDelete
  52. AnonymousJuly 23, 2009

    Pole ndugu...Na mimi nina jamaa alituma mzigo toka February 09 ( laptop 3 and other few things) Mpaka leo Posta wanasema mzigo haujafika wakati tracking # inaonyesha ulifika Tanzania within 10 days. Ni aibu na inaumiza sana! we need a solution!

    ReplyDelete
  53. AnonymousJuly 23, 2009

    BWANA MICHUZI TUNAOMBA TUONE SASA NA WEWE MCHANGO WAKO KATIKA UJENZI WA TAIFA HILI.
    KWA KUWA BLOG YAKO NI CHOMBO CHA HABARI, TUNGEOMBA UCHUKUE PRINTOUT YA LALAMIKO HILI ULIPELEKE MAHALA HUSIKA, NI VIZURI UKILIWASILISHA WIZARA HUSIKA NA NAKALA YAKE NDIO UPELEKE KWA MKURUGENZI WA DIA NA MENEJA WA SWISS PORT. KAMA UTALIPELEKA DIA TU PEKE YAKE LINAWEZA LISICHUKULIWE HATUA AMBAZO SISI SOTE TUNGEPENDA ZICHUKULIWE. HII NI SIFA MBAYA SANA KWA TAIFA LETU. KITENDO ALICHOFANYIWA HUYO LECTURER WA NORWAY NA WAZAWA WENGINE HAKIVUMILIKI. NAKUOMBA KWA NIABA YA WALALAMIKAJI WOTE CHUKUA HATUA TAFADHARI. WIZARANI USISAHAU KAMA KWELI TUNATAKA KUFIKIA POPOTE.
    binafsi niliwahi kupotelewa sanduku zima nikienda Atlanta kwa emirates na kisha kuunganisha kwa delta pale gatwick london kufika atlanta sanduku hakuna, niliamua kulia na ofisi ya delta airlines,nilijua nikianza kufuatilia na bongo nitalost mi nikalia nao haswa nikawaambia hakieleweki bila vitu vyangu walivyo waungwana wakanifungulia faili na wakanipa baggage claim number wakaniambia haya we zama ATL tunashughulikia ishu yako kama baada ya mwezi wakaniandikia email wakadai wameshindwa kabisakabisa kutress lilipo wala lilipopotelea sanduku langu so shirika limeamua kukulipa waliniandikia check ya mahela mengi tu ingawa walidai mzigo wangu haukupanda ndege yao pale london, wakadaai ngoma ni DIA, au Dubai au London, lakini kwa harakaharaka nadhani hii maneno itakuwa ni dar.
    juzi hapa naenda home vekesheni kwa emirates hiyohiyo, mtaalam mmoja kanunua spea expensive ya gari kutoka dubai, kufika dia wakamliza jamaa kidogo azimie, nae walimpa jibu lao hilohilo hatujaiona!!!
    na wanachofanya ni kwamba unaweza subiri kwenye conveyer belt hata saa nzima hujaona mzigo wako na wakati ndege iliyoshuka ni hiyohiyo yenu. ukiona mzigo wako unachelewa basi ujue mzigo umeingizwa kwenye chumba chao maalumu chakufungulia na kusearch mizigo ya watu. mi safari hii niliweka ka-perfume ka gharama sijui hawakukaona!!!
    ila jamani laptop, camera and the like you board the flight with them they so light.
    pia masanduku ya zipu kwa safari za bongo siku hizi hayalipi zaidi ya kukulostisha sababu they can easily be tempered with, nunueni ile mitambo isiyo na zipu ile watalia nayo haifunguki labda uvunje kwa nyundo, sababu siku hizi hata nguo wanaiba!!

    ReplyDelete
  54. AnonymousJuly 23, 2009

    Pole sana ndungu yangu kwa mkasa huo wa kusikitisha,kuhuzunisha na waaibu kwa kwa taifa kijumla,sasa mimi ntakupa njia moja naona ni salama sana mimi nimeisha jaribu (niko uk),njia hii nilielekezwa na dada mmoja tunaishi naye hapa uk,nenda posta ya huko uliko yaani japani waambie hivi unataka kutuma mzigo wako kwenda tanzania lakini kwa huduma moja inaitwa HAND TO HAND, utalipa ghalama si kubwa sana lakini mzigo utafika,na ukipotea unalipwa na wanajua umepotelea wapi ,mimi nimeishatuma simu ,nimetuma laptop tena siyo kwenda dar ,nimetuma viende Tabora na wamevipata vyote,huyo dada anatuma vitu kila siku kwenda mbeya tena siyo mbeya mjini, wilaya ya kyela na havijawahi kupotea hata siku moja,kuhusu uwanja wetu wa ndege usijaribu wala kuthubutu hata siku moja kuweka vitu vyako vya thamani kwenye begi beba mkononi,nikwambie mkasa mmoja wa aibu ulitokea miaka miwili iliyopita mtoto wa Rais Kikwete anayeitwa Ridhiwani Kikwete alikuwa hapa uk anasoma chuo kimoja kiko mji mmoja unaitwa HULL,sasa alipokuwa anarudi nyumbani akanunua simu nzuri sana kwa ajili ya kumpelekea BABA YAKE(yaani Rais Kikwete)kama zawadi kufika BONGO uwanja wa ndege kwanini wasifungue begi lake nakuuiba ,jamaa alilalamika sana mpaka akatoa machozi na ilibidi atoe taarifa kwa polisi wa uwanjani hapo,mpaka mkuu wa uwanja alifahamishwa sasa ikaanza pekua pekua kwa wafanyakazi pale ,sijui aliipata au vipi maaana yeye aliamua kuondoka kwenda nyumbani kwa hasira,sasa wewe ndugu yangu nakushauri usirudie makosa,BONGO kwetu lakini weee acha tu!

    ReplyDelete
  55. Naishi mitaa ya majumba sita ambako wafanyakazi wengi wa uwanja wa ndege wanaishi.Ukikaa nao bar kila siku utawasikia wanavyojisifia jinsi walivyoiba simu au laptops na camera.Na hata ukifatilia maisha yao utagundua kuwa hawadanganyi manake spending yao ni baab kubwa hailingani na mshahara wao.

    Kumaliza wizi airport ni kuhakikisha kuwa SWISSPORT ambao wamepewa kazi ya kupakia na kushusha mizigo kwenye ndege wanabadilisha wafanyakazi wao ambao wengi wameajiriwa kwa ukabila (sitaki kutaja kabila lenyewe).

    Nakumbuka mwaka jana waliiba mzigo wa laptop zaidi ya 20 alafu wakati wa kutafuta soko wakaenda kumuuzia mwenye mali.

    ReplyDelete
  56. CASHMONEY...USAJuly 23, 2009

    WADAU WIZI BONGO SI POSTA AU AIRPORT HAUTOKWISHA....MUHIMU KAMA UTAKI KUTAKE RIZKI NI BORA UTEREMKE NA VITU VYAKO MWENYEWE NA HANDBAG....KWANI WANAOIBA SIO ULAYA AU JAPAN...AU MAREKANI...MAJIZI YAKO BONGO...NA HAYATOACHA WIZI...SITUMI KITU KAMA KITU NAWATUMIA PESA WESTERN UNION WANUNUE BONGO.MDAU CASHMONEY.U.S.A.

    ReplyDelete
  57. AnonymousJuly 23, 2009

    Hao wezi wa hapo air port sasa hawana chao na lazima watalipa kiaina wala msiwe na wasi wasi,kwasababu kuna siku nilienda kumchukua wife pale kazini kwake air port na ilikuwa usiku sana nikakuta jamaa(mafundi)wanaweka hide camera(camera za kujificha)ili kufuatilia wezi wanaofungua mabegi ya watu na kuchukua vitu mbalimbali bila huruma

    ReplyDelete
  58. AnonymousJuly 23, 2009

    Kaka Michuzi tunaomba ulifikishe hili suala kwa wanaohusika hawa jamaa wanatuumiza sana baba,ukisema utume vitu kwa njia ya posta wanaiba ukisema ubebe mwenyewe ukifika air port Dsm wezi wanachukua kama vyao au kama wao ndiyo wameweka kwenye begi,lakini najua ipo siku wataingia mtegoni,na kama mtu unauwezo unawategeshea nyoka tena cobra mtu akifungua begi tu cobra kapofua jicho.

    ReplyDelete
  59. AnonymousJuly 23, 2009

    Aah! Michuzi ndugu yangu! nimetoa maoni yangu hujayaweka bwana! unawaficha nini hao Swissport nakuambia wana cctv camera, I have been there! wanaona kila kitu! Eneo ni moja tu ambapo wizi unaweza fanyika, ni pale wanapopakua Mizigo kuleta kwenye Mikanda (Belt) uthibiti uanzie pale

    ReplyDelete
  60. AnonymousJuly 23, 2009

    Hicho Ki anonmy cha July 22 9:50 PM nI kiazi Kweli! Kinaponda Tz huku kinaandika kiswahili, Tunakuambia hivi wewe ni mtz tu! Huko uliko kwenyewe unabeba box! na kuosha wazee! Halafu kijamaa kinasema kifikiria kuja bongo roho inakutoka! Roho inakutoka kwa sababu huna paper! Toa mawazo ya namna kusaidia tatizo hili!

    ReplyDelete
  61. AnonymousJuly 24, 2009

    ebwanaeeeee....mi nilifikiri mshamba, nakwambia mwaka jana basi nikaenda na video camera mbili.

    Kufika Dar. nikasubiri wee...begi linakuja sikuona kitu, nakwambia kidogo moto uwake. Nikalalamika mpaka kwa mkuu wa mizigo, kesho yake asubuhi nikarudi wakasema moja imepatikana, eti ilidondoka.
    Nikasema basi lete zote kama zimedondoka, sikuwahi kuipata nyingine.
    This is totally sick...mdau hata mimi inanitia sana hasiria.

    ReplyDelete
  62. AnonymousJuly 24, 2009

    mi nilituma mashine ya kupimia diebetic na needle zake imefika salama ila boxi limefunguliwa na kuchanwa nafikiri walidhani sim ya mkononi na inawezekana aliefungua pia hakujua maana yake aliona aniachie tu mwenyewe nilishukuru walikaonea huruma kamzigo kangu, inatia kichefuchefu nchi yako mwenyewe unaogopa kutuma kitu kwa ndugu yako home,sijui lini tutastarabika

    ReplyDelete
  63. AnonymousJuly 24, 2009

    Pole sana mdau kwa yaliyokupata maana hata mimi yalinipata kama hayo, ingawa vilivyoibiwa havukuwa vifaa vya electronics. Nilikuwa narudi Tanzania na nikabeba pea kadhaa za viatu kama zawadi kwa jamaa zangu huko. Nilisafiri na flight ya KLM na nilipofika wakaniambia mabegi yangu hayakufika, hivyo niende kesho yake kuyachukua. Hiyo kesho kwenda nikakuta mabegi yamefika lakini yamefunguliwa na viatu vimechukuliwa. Nilifuatilia kwa watu wa KLM na wakanipa $250 pamoja na gharama za taxi $60. Dar airport ni mbovu sana.

    ReplyDelete
  64. AnonymousJuly 24, 2009

    mdau wa mwisho umesema dar airport hovyo sana. nataka nikwambie hata sehemu zingine kama bandarini ni hovyo zaidi. sie watanzania hatuna uzalendo, ndio tatizo letu la msingi kabisa. maana yake ni kwamba hata sku moja hatutaendelea. mafisadi tunao kibao wanatanua mitaani sasa watu wengine nao wataacha kuiba? Mie airport waliniharibia begi langu samsonite ndo kwanzalilikua jipya, walitaka kufungua wakashindwa majinga yale....

    ReplyDelete
  65. AnonymousJuly 24, 2009

    Duu!!! inauma sana yaani hata mimi nina hasira nao ile mbaya waliniibia simu zangu tatu kwenye begi halafu nilimpa tu mtu anipelekee nyumbani alivyoniambia kaibiwa sikuamini nusu nihisi kanifanyia mchezo lakini sasa ndio nagundua hakuwa yeye ni hao mabwege hapo wana njaa sana lakini jamani ina maana Airport ya Dar haina cctv? kwa nini wasifuatilie kuangalia pale watu wanapolalamika kwamba wameibiwa? bila shaka wanashirikiana na hao mabosi wao aibu tupu bongo ni dhambi kuiba vitu usivyovitokea jasho huwezi jua mtu kapate hivyo vitu we unajichukulia tu serikali nayo iingilie kati jamani tunaaibika.

    ReplyDelete
  66. AnonymousJuly 24, 2009

    Mimi ninausongo naho wa DIA, we aache tu, mimi nisote kubeba box huku wao wale kiuraini,wanatamaa sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...