breakdown ikijiandaa kuondoa moja ya magari yaliyohusika na mzinga huo ambao chanzo chake hakijajulikana
kila mtu anashangaa maajabu ya jinsi abiria na madereva walivyoweza kunusurika
magari haya yaligongana uso kwa uso usiku wa kuamkia leo maeneo ya namanga jijini dar. ishukuriwe yote yana mifuko ya hewa ambapo abiria na madereva walinusurika kifo kimaajabu
breakdown za dar huwa hazilali
mataa mengi ya kuongozea magari yameharibiwa na ajali kama hizi





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hiyo Subaru Bluu ni ya "Wadosi" fulani ambao wana vurugu sana mitaa ya Posta..
    Wakisha kolea "Majani" wao ni speed 120.. shaaah !!! wakifukuzana na wadosi wenzao,
    basi hapo "walavumbi" inatubidi tupishe njia mbaaali kabisa tusije vunjwa viusafiri vyetu tulivyozaliwa navyo "miguu",
    huku tukiziba masikio dhidi ya sauti nzito ya makelele ya hilo gari lao ambapo wakipita hamsikilizani.

    Sijui ni "kulewa" mapesa ya ufisadi au vp!!!
    aah! "walala hoi" yetu macho tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2009

    Hao jamaa wanao husika taa za barabarani wasilale wajitahidi warudishie hizo taa haraka iwezekanavyo maana hapo mahali bila taa ni hatari ya denger.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2009

    Wee acha tuu, maji ya mende yana raha zake bwana au sio wadau?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 19, 2009

    Hizi towing trucker za bongo ni za karne ya nuhu lol

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 19, 2009

    Hizo towing trucks ni kampuni ya inspector so and so...huwezi kuweka kampuni yako ndani ya hii business....ni ngumu sana!! Au nimekosea?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 19, 2009

    Hivi Breakdown ina maana gani?

    ReplyDelete
  7. pombe,
    kutosimama kwenye taa nyekundu
    spidi
    kuna jingine??

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 20, 2009

    Breakdown ni "kuharibika" kwa mfumo wa kitu fulani....mfano, car breakdown ni kuharibika kwa mfumo wa gari, iwe tairi la gari au engen.
    Ila, naona hili neno linatumika interchangably na towing truckers kimakosa, kwa anayeongea lugha ya kiswahili na mswahili mwenzie wanaweza wakaelewana, ila ukiongea na mtu asiyejua kiswahili, ukalitamka wakati unaongea lugha ya kiingereza kamwe hutaeleweka

    ReplyDelete
  9. Ndugu Karl hapo juu...

    Huyo Michuzi aliyetumia neno "break down" nae ni mchovu wa lugha. Wabongo wana viingereza-swahili vyao wanaelewana wenyewe.

    Mtu akienda kufanya admission test kuingia kidato cha kwanza atakwambia anaenda kwenye "interview," utafikiri anatafuta kazi vile...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...