Mgeni wa heshima Naibu Balozi wa Tanzania katika nchi za Skandinavia Mh. Jacob Msekwa akimkabidhi kombe nahodha wa kilimanjaro Kabrao
habari za saa hizi bwana michuzi. mimi bwana ni mmojawapo wa viongozi wa kilimanjaro na asante sana kwa kutoa taarifa ya mechi baina yetu Kilimanjaro FC ya Tampere na FC Bongo ya Helsinki ambapo tuliwachapa 8-1. Ila naona picha tumebaniwa kidogo. Kwa hiyo nakutumia hizi uzirushe kwenye globu yetu ya jamii ili jamaa wa nanihii waipate freshi....wangeshinda wao naona globu yote wangeinunua hahahaaa..! Yaani kama namuona Ezza alivyonuna. Ndio ukubwa huo kaka. Nasikia kazi yako ya ukocha imeota mbawa. Na bado...
kikosi cha kilimanjaro FC ambacho kiliwachakaza FC Bongo kwa mabao 8-1. Na kinasadikika kwamba ni kikosi bora cha watanzania wote wanaoishi ughaibuni. Kikosi cha FC Bongo ambacho kilisambalatishwa vibaya sana na bila huruma na wana Kili FC.
Picha ya pamoja ya kilimanjaro FC wakiwa pamoja na mgeni rasmi kutoka ubalozi wa Tanzania katika nchi za skandinavia Mh. Jacob Msekwa
Kikosi cha maangamizi cha Kili FC mara tu baada ya kukabidhiwa kikombe chao ambacho wamekichukua mara ya pili mfululizo, na watachukua tena mara ya tatu gemu lijalo na kuliweka kimoja Tampere. Picha na maelezo M/Hazina (Kilimanjaro club)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2009

    Huyu alietoa habari hizi kwa michuzi wala hajatoka kilimanjaro, kama angekuwa ametoka kilimanjaro asingesema kuwa wanatoka norway, huyu ni mshabiki wa TAS tampere na tunamkumbuka alipopiga picha hii.
    Michuzi usiibanie hii komenti kwani jamaa kaongopa hapo wazi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2009

    Mjomba Kablau tuwasiliane kwa e-mail godi80@hotmail.com
    Godi-Bogota

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2009

    kiongozi wa timu ujui uko nchi gani? wizi mtupu ati norway. mdau helsinki

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2009

    Wabongo kuleni dagaa za kigoma tuu.zenu nikubamizwa tuuu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2009

    Hicho kikosi cha Kili kinatisha. Watu wa Norway, Denmark, Holland, Germany na kwingineko mpo? Njooni nanyie mpigwe.

    Mdau Stockholm

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2009

    Hawa tampere wantapatapa kwani wanajua kiama kinawasubiri jumamosi hii vumbi stadium.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2009

    Jameel nakuona hapo pamoja na baby. Salaam.

    ma' mdogo
    dar es salaam

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2009

    Imesemwa mara nyingi rangi ya jezi inaweza kukuharibia watu wakawa wanabisha. Si mnaona wenyewe.

    ReplyDelete
  9. FC Bongo, Jumamosi sio mbali.. subirini kichapo kingine toka kwa TAS!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 02, 2009

    KILI FC LAZIMA WASHINDE, HAMUONI KAMA KUNA WACHEZAJI WA YANGA NA SIMBA NDANI YAKE? NAMUONA MACHUPA HAPO, CREDO MWAIPOPO ALIYEKUWA YANGA NA WADAU FLAN FLAN WANAOJUA KUKIPUTA...HAWA SAIZI YAO TIMU YA VODACOM, JAMANI TUNAOMBA MSAFIRI MJE BONGO HUKU, ACHENI KUONEA WENGINE...NJOONI MPIME UBAVU BONGO NA TIMU KAMA YENU SIO LAZIMA SIMBA AU YANGA AU AZAM, KUNA VODAOM, ZAIN,STANCHART, TIGO ETC...NJOONI KUDADADEKI NA MAJESHI YENU HAYO.

    HUKU NI KICHAPO TU, HUMPHREY ANATUTAMBUA...MUULIZENI.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 02, 2009

    Jumaa habari za miaka mshikaji wangu tumepoteana naona umetulia nyuma hapo wewe ndiye coach nini...??? tuwasiliane bwana
    Bob

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 03, 2009

    nilishauliza

    ivi ao watu wana rangi-rangi wa nchi gani??au wazenji?au chotara wa kibongo

    mana naona sii kawaida

    afu kuvaa "jezi" ambazo bongo ni vazi la watanzania wanaposhangilia timu ya taifa!!!!....!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 03, 2009

    Mbona watu wengine wana maswali yaajabu kwani watanzania wote weusi??? Tanzania ni taifa lenye mchanganyiko wa watu wengi iwe waarabu,wahindi,weusi,machotara,wangazija n.k Acha ubaguziiiiii......Hao warangi rangi pia watanzania na wanatambulisha tanzania ndio maaana wanacheza kwenye timu ya tanzania so simple.....

    ReplyDelete
  14. Nyie FC Bongo msitapetape oh wana wachezaji kutoka yanga simba nk.
    kilimanjaro inatisha sana. na yule mtoto aliyewafunga bao la kwanza jee anatoka wapi Si Simba wala yanga na wengineo tu ambao wanasakata kandada kiukweli sio piga ni kupige na kuhusu rangi huku Skandinavia ni baridi hata wewe ukija utaiva tu. ha ha ha
    Mdau Stockholm

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 03, 2009

    kilimanjaro Club inatisha baadhi ya wachezaji ni Kipa Cabrao zamani kacheza Bandari Mtwara,Machupa kacheza Simba na Taifa Stars,William John kacheza Simba, Shekhan Rashid kacheza Simba, Bwana mdogo Richard(Messi) keshaitwa Barcelona kwenye trial. Huyu bwana mdogo ni nuksi hasa akiwa na boli anaweza kumfaa sana Maximo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...