Balozi na Mkuu wa Nanihii...
Naomba niweke japo pembeni, usinitie kapuni nipate kusema na wadau kidogo kisha kuuliza kajiswali kangu ka kizushi.
Juzi umetutundikia taswirazzz za waheshimiwa wabunge wakiwa katika fasheni shoo kule Dodoma. Baada ya hapo kumekuwepo na mjadala mkali baina ya waliopendezwa na jambo hilo na wasiopendezwa nalo. Swali langu hama maswali yangu ya kizushi ni kama ifuatavyo.
1. Mheshimwia Mbunge ana haki/ hana haki kufanya fasheni shoo? Nauliza hivyo kwa sababu ya niliyoyaeleza kwenye utangulizi, na kwa kuongezea tu wadau wanaopinga watueleze ubaya wa fasheni shoo,na wanaoafiki waeleze uzuri wake....
2. Je, ni nini Mheshimiwa Mbunge anatakiwa kufanya wakati wake wa ziada, hususan katika kushiriki katika aidha michezo ama utamaduni ili wadau wasipige kelele kwa kile wanachokiita kupoteza muda? Nauliza hivyo kwa kuwa nadhani iko haja wadau waweke wazi Waheshimiwa wafanyeje katika muda wao wa ziada baada ya mijadala bungeni??
Ni hayo tu kwa sasa. Chonde chonde nanihii naomba usiniweke kapuni.
Mdau Evans
Magomeni, Dar
Asante sana kwa kutuletea swali hili mimi nafiriki wale wanaowasema vibaya wahesimiwa wabunge kuhusu kushiriki fashion show ni kwamba wanahusisha utendaji wao wa kazi na tukio hili. Nafikiri wanaona kwamba waheshimiwa wabunge bado hawajafanya kitu cha chenye kuonekana machoni mwa wananchi na sasa wanashiriki kwenye matukio kama haya ya fashion show ambayo labda wanaona hayasaidii wananchi na wanaona kama ni upotezaji wa muda badala ya kufanya kazi kubadilisha nchi. Huu ndio mchango wangu. Asanteni
ReplyDeleteThey showed how they are not serious with our business, they just went off road, and are utterly ridiculous, and SHAME ON THEM. In fact they have no free time, they are at work 24/7 and there are so many things to do, for instance they could go and lecture people how to eradict poverty by giving them vivid strategies and examples at root levels, like how to form small groups for businesses and how to get help such as loans from relevant establishments and how to go about it, to talk education, HIV, Volunteering in our communities and stuffs like that.
ReplyDeletenadhani kuondoa umasikini wa wananchi si kipaumbele cha kivitendo! Sijawahi kuona baba mwenye nyumba aliyetimamu kifkra ambaye analia njaa na ufukara wa kaya yake kila siku na huyo huyo tunamkuta anacheza ngoma ya sindimba eti ana muda wa ziada. Hapa kutaleteleza wenye upeo kudadisi utashi wake kivitendo. Nani miongoni mwetu anapata muda wa kufanya vitu vya kisanii visivyo na tija kwa familia yake au hata kwa yeye binafsi huku ana matatizo kibao??
ReplyDeletebaada ya miaka mitano tutawapeleka Rwanda kwa kodi zetu wakajifunze kuleta na kusimamia maendeleo kwa wananchi.
ReplyDeleteNadhani kupumzika ni haki ya kila kiumbe na wao wanahaki ya kuchagua watumieje muda wao wa mapumziko ilimradi hawavunji heshima. Hata hivyo kwa faida ya taifa letu na wananchi wote tungependa sana tuone matunda ya uwakilishi wao kwenye majimbo wanayowakilisha na si maneno tu wakati wa kampeni, sehemu nyingi huduma hakuna kabisa matatizo matupu na hilo ndilo linalo tugusa.
ReplyDeleteSuala la wabunge wanafanya nini kwa wakati wao sio ishu mradi hawavunji sheria.
ReplyDeleteTatizo lipo kwenye wabunge wanafanya nini kwa muda wetu sisi walipa kodi (wao wamejitoa kwenye ulipa kodi). Suala la kupiga mbavu badala ya kujenga hoja za kuleta maendeleo ya nchi yetu halikubaliki.
Kuna wabunge (au ni mbunge mmoja tu) ambao hawajawahi kutoa mchango wa hoja yoyote bungeni. Why? Why?
Mimi naona Waheshiwa Wabunge wanaweza wakafanya chochote wanachotaka katika muda wao wa ziada kama wangekuwa wanafanya kazi za wananchi. Ila tatizo linakuja ni kwamba hamna wanachokifanya katika kuendeleza nchi so from not doing anything up to do fashion show!! please give me a break, this people who are called waheshimiwa are not serious, people are dying with HIV and Poverty but you guys have guts to do shows!! that pathetic and redicoulous. Hata bila aibu mnajibitisha na matumbo yenu!! shame on them!! Viongozi wengi wabinafsi sana wanagombea vyeo kwa manufaa yao na familia zao, that all nothing more that, wananchi go to hell!! Ila Mungu atawaona.
ReplyDeletewao kama wabunge pia wana haki ya kufanya chochote ambacho wamekipangilia katika mikakati yao,pia michezo ni muhimu aijalishi wewe mi rais mpunge au waziri,swala lao la fashion show ni haki yao wala sijaona lolote baya.....
ReplyDeleteWabunge wanapokuwa bungeni Dodoma kimsingi hawana muda wa kupumzika likizo yao ni baada ya bunge kwisha!Jioni wanatakiwa wajisomee na kujiandaa kwa mijadala ya kesho yake[preparation] na sio kwenda kusinzia na kupiga kura kwa kufuata mkumbo kesho yake.Vilevile wanaweza kuwa na vikao informal vya kuelimishana kujadiliana na hata kujisomea mengine yasiyohusu bunge. Wabunge wetu wengi ni mbumbumbu pamoja hizo phd zao uchwara!Kujihusisha na ulevi,uzinzi na burudani wakati wako Dodoma ni kashfa na matusi kwa wananchi!Halafu mtu kama Karamagi[karaha ya maji]ambaye ameshatuliza na TICTS yake bila hata haya eti anapanda jukwaani na kuringa ati ni modo jamani sie wabongo tukoje!!!
ReplyDeleteWaheshimiwa serious wanatakiwa wawe wamelala ifikapo saa nne usiku ( mfululizo Jumatatu mpaka Jumapili), ili wakidamka mapema asubuhi wawe na muda wa kupitia makabrasha na miswada na kujenga hoja au maswali ya hapo kwa hapo.
ReplyDeleteWangefanya hiyo fasheni shoo wakati bunge limemaliza rasmi hicho kikao cha bajeti.
Sio wabunge wa Tz tu ambao sio serious na kazi zao, bali hata vingunge vingine vya Afrika. Wakati wa mikutano Arusha, vingunge vya Afrika hulala saa kumi usiku, wakati wenzao wa Umoja wa Mataifa, World Bank, IMF n.k huwa wameshaingia vitandani mwao saa nne usiku.
Mdau
Aliye Karibu na Vingunge
Arusha.
Tatizo sio kuwa wasifanye mambo mengine zaidi ya kazi zao, tatizo ni kuwa kufanya mambo ambayo hayana faida kwa wao na wala taifa letu. hebu wewe mwenyewe niambie pamepatikana nini hapo zaidi ya kumpa umaarufu zaidi mbunifu wa mitindo aliyefanya maonyesho haya?
ReplyDeletepia nina hakika ni pesa za serikali ndio zilizotumika katika kufanikisha shuhuli hii, ningelipenda kumsikia mhusika yeyeto yule atuhakikishie kuwa katika kufanya hili pesa za serikali hazikutumika.
Wengi kilichotuudhi ni aina ya walichofanya, hutujawahi kupiga kelele walipocheza mpira, walipofanya mashindano ya kuvuta kamba na mengine mengi, ila fashion show? come on this is taking a biscuit.
Mbunge ni mwanadamu kama mwingine, ana haki ya kushiriki michezo na burudani nyingine,ila burudani hizo zisikwaze majukumu yake.
ReplyDeleteKitu kinachowasikitisha wananchi ni kipato chao, yaani `wanapata zaidi ya ziada' ikizingatiwa kuwa hicho wanachokipata kimetoka kwenye jasho la wavuja jasho.
Mfano mzuri raisi Obama, mbona mimi simuoni akiwa `double-man' Well,pengine mimi sijui mengine yake, lakini mbunge kachaguliwa juzi tu, oooh,samahanini sana! Hicho ndicho wananchi wanajiuliza hivi kweli hawa watu wanakesha kufikiria jinsi gani ya kuwasaidia hawa walalahoi.
Nasema hivi kwasababu chukulia mfano wa nyumba ya baba, ina matatizo kibao, njaa, magonjwa nk. kweli baba atakuwa na raha kiasi cha `kuhumuka mwili' . Sidhani, labda huna huruma na familia yako. Sikatai wote hatupo sawa, lakini nikiongelea `kuhumuka' siangalii tu `mwili'!
M3
It's such a shame kumuona kiongozi mwenye kashfa nyingi za ufisadi kuwepo bungeni lakini sio hili la wabunge kufanya fashion show.Inawezekana kabisa wao (wabunge) kutokuweko kwenye fashion show na pia wasifanye lolote la kuwafaidisha wananchi, so waachwe wafanye wanachotaka kufanya kwani wao wana haki zao za kimsingi kama binadamu wengine. Ila kama kuna Mbunge/Waziri ambaye anashutumiwa kwa rushwa halafu aonekane tena anafanya fashion show, thats a shame, Shame upon their face!!
ReplyDelete