JK akimkabidhi hati ya kumiliki ardhi kimila Mzee Swedi Maulid wa kijiji cha Msindo,wilaya ya Namtumbo jana.Pembeni anayeshuhudia ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi john Chiligati.Ardhi yote ya kijiji cha Msindo imepimwa kwa matumizi ya makazi,malisho ya mifugo na kilimo na wananchi wamepewa hati za umiliki wa ardhi yao.
JK akikagua masjala hati za kumiliki ya ardhi kimila katika kijiji cha Msindo, wilayani Namtumbo jana muda mfupi kabla ya Rais kugawa hati miliki za kimila kwa wanakijiji wa Msindo.Kushoto ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi John Chiligati,Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bi.Salome Sijaona na Mbunge wa jimbo la Namtumbo Mhe.Vita Kawawa.

JK akimpongeza motto Zabiuna Kasim anayesoma katika darasa la awali katika Shule ya Msingi Msindo, katika wilaya ya Namtumbo, m koani Ruvuma baada ya kucheza kwa umahiri ngoma ya Mganda wakati wa sherehe ya kukabidhi hati za kumiliki ardhi kimila zilizofanyika katika kijiji cha Msindo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwa jambo hili tu, JK umepata KURA yangu ili uongoze nji yetu miezi mingine 60! Mungu akubariki wewe pamoja na mama watoto SalmaJK! Naomba pia uende kule Moshi kijijini ili watu wapate maji, angalau iwapunguzie muda wa kwenda kuyatafuta mbali hivyo.
    Mheshimiwa (sijui kama ulikataa usiitwe mheshimiwa au la, lakini ninaomba nikupe heshima ya ofisi yako), ninakuomba utumbushe tena ile namba yako uliyotoa ile miaka ya "ari mpya" nguvu mpya na kasi mpya" kwani ninakutafutia msemo wa kutumia mwakani! Mabadiliko yanakuja? Hapana, hiyo imeshatumiwa na BHO huko majuu! Ukinipatia tu hiyo namba ya kiselula nitaku"""beep""" halafu, utanipigia halafu nitakupatia mwelekeo wa mwakani!! Ni mimi mwanaCCM damuuuuuuu.
    Michu mdogo wangu naomba kuwasilisha hii hoja (MH)

    ReplyDelete
  2. JK, hongera hii ni programme nzuri, pia katika ofisi ninayofanya kazi ni NGO ina support hii programme kwa sehemu tofauti ni kitu kizuri sana, inapunguza unyanyasaji wa wakina mama.
    hongera serikali kwa kuikubali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...