juu na chini JK akisalimiana na baadhi ya wazee wa kabila la Wamasai katika kijiji cha Engarenaibor, wilaya ya Longido ambapo alikwenda kukagua hali ya ukame na upatikanaji wa chakula cha msaada katika wilaya hiyo iliyoathirika vibaya kwa ukame.Katika ziara hiyo Rais alitembelea pia kijiji cha Mundarara ambapo aliongea na wananchi baada ya kupata taarifa ya hali ya ukame katika makao makuu ya wilaya mpya ya Longido.
JK akiamkia wazee longido

JK akitoa zawadi kwa baadhi ya wageni walioshiriki katika futari aliyoiandaa ikulu ndogo mjini Arusha jana jioni baada ya kurejea toka Longido

Mama Salma Kikwete akiagana na baadhi ya wageni walioshiriki katika futari waliyoiandaa ikulu ndogo mjini Arusha jana jioni.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mama Kikwete waonaje uendelee kuvaa hivyohivyo hata baada ya kuisha kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani? Umependeza sana!!

    ReplyDelete
  2. Mwacheni First Lady wetu,wewe anon huna la kusema nn?

    ReplyDelete
  3. jk hivyo hivyo 2010 unapata 90% ya kura zote jamaa watakuchagua tu ila sasa hivi kuna longo longo kibao,mara ooh sisi tunaisubiri ccm mwaka 2010,mtu mzima hatishiwi nyau!MUNGU AKUBARIKI SANA RAISI WETU ENDELEA KUTUONGOZA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI ITIKADI KWANI WOTE TUMEKUCHAGUA PIA

    ReplyDelete
  4. mbinguni hatuendi kwa mavazi BALI WALE WASAFI WA MIOYO OK,

    ReplyDelete
  5. jk big up endelea hivyo hivyo kushirikiana na watanzania wote katika kila mikusanyiko bila kujali dini,itikadi au kabila ur a man of people ingawa ukienda kwingine jamaa hawachelewi kupaza sauti eti unawapendelea mmh

    ReplyDelete
  6. CCM NINAVYOKUPENDA NITAKUNYWA SUMU JUU YAKO HAHAHAHA CCM NI NAMBARI ONE.CCM ITACHUKUA ,ITAWEKA ,ITABWAGA WAPINZANI MWAKA 2010. CCM OYEEEEEEEE
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.HATUOGOPI WARAKA HATA IJE HAMSINI.JK ATAENDELEA KUWA RAISI MZURI MILELE.TZ HE IS A SOURCE OF REALY DEMOCRACY WITHIN AND OUT CCM

    ReplyDelete
  7. Kuvaa hijabu kwa mwanamke ni suala la lazima. Ukienda kinyume cha hapo ni dhambi. Kuna ubaya gani Mama Salma akiendelea kuvaa hijabu au kujitanda kama alivyofanya hapo kwenye picha? Havai hijabu kwa ajili ya mtu ila ni kutimiza amri za Mwenyezi Mungu SWT. Ukiamua kuacha kuvaa rukhsa ila ujie utaulizwa hiyo siku ya masiku. Chagua lipi bora. Dunia kuwafurahisha walimwengu au Akhera kumlidhisha Mola wako. Na kumbuka kuvaa hijabu si udini.

    ReplyDelete
  8. Mijitu mingine bwanaa aagh. Oh JK jana alikuwa Monduli kwenye birthday ya mbunge wa
    Monduli kumbe majungu tu. Kwanza jana ni Ramadhani kwa hiyo kuenda is out of question. Kumbe mzee alikuwa Longido. Nchi hii maneno memngine yanakera haswa.

    ReplyDelete
  9. wale wanaoongelea kuhusu nguo.Tusiangalie yanayoonekana nje tu, yale yasiyoonekana nayo ni muhimu jamani. Unaweza kuonekana saafi kwa nje lakini ndani kunatibua kila kitu na siku ya mwisho utaulizwa pia haijalishi ulikuwa unavaa nini.

    ReplyDelete
  10. uwezo wa mwanadamu ni kuona kwa macho ila Mungu ndiye anayeona hadi mawazo ya mwanadamu yoyote yule anafikiria nini?yawezekana mtu akawa nadhifu kwa mavazi kumbe roho yake imejaa uuaji au mawazo ya zinaa,mama jk waa! kila vazi linakupendeza waa! first lady wetu,ila usimshauri vibaya mzee kama yule the former one te te te!
    mdau nawasilisha ngoja niwahi kubeba box zangu nipate walau usd

    ReplyDelete
  11. Kusafisha moyo ni imani na kusafisha mavazi ni matendo. Ukikosa mojawapo haumo katika wa mbinguni. (imani bila matendo ni.....)

    Nyoyo hatuwezi kuzikagua (wala si kazi yetu), ili mradi twaona matendo yao ni mema basi na nyoyo zao pia.

    Kuna mlokole (mwenye fikra) aliwahi kunieleza kuwa "MATENDO NI ISHARA YA YALIYO MOYONI"

    ReplyDelete
  12. Kuna watu wanaumizwa na hijabu na wameshindwa kuvumilia na kuanza kuleta mashambulizi ya nyoyo.

    Ukiwa na moyo safi na mikono michafu ujue pia haisaidii.

    ReplyDelete
  13. Ok, nyoyo safi lakini fikra na mdomo vibaya, mnasemaje?

    Kwa nini watu wanafikiria kuwa wavaa hivyo wana nyoyo siyo safi? hiyo siyo moyo mchafu?

    ReplyDelete
  14. Yaani watu wanafuata dini yao wewe unasema nyoyo chafu? Nini maana ya kufuata dini?

    Mfano, dini gani inahimiza kuiba, zinaa, uongo, dhuluma, kutu?

    ReplyDelete
  15. Hii dini ya waislamu ni ya kati na kati. Matendo kiasi na spirit kiasi. Haina extrema katika matendo wala spirit.

    Wakristo wao huwa na spirit (extrem) kubwa mno hamna mtu duniani anawafikia lakini kwenye matendo pana kidogo.....

    Wayahudi nao kwenye matendo hakuna mtu anawafikia lakini spirit, ...so so. walishindwa hata kumwamini Yesu.

    Lakini kuna watu wanosema
    "MATENDO NI DALILI YA KUWEPO IMANI"

    ReplyDelete
  16. Chonde chonde, uhuru wa dini, na uhuru wa mavazi (hijabu ruksa, kimin ruksa.

    kama hujisikii si ukawahubirie huko misikitini kwao sio hapa buloguni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...