bango la 'village pastor' filamu mpya ambayo
stelingi ni kanumba na hadithi ya kweli imetokea
hizi ni baadhi ya picha za matukio ya filamu mpya
ya kanumba iitwayo 'Village pastor' ambayo
inaibuka madukani mwisho wa mwezi huu.
sehemu ya filamu hiyo mpya

kanumba akiingia kijijini katika filamu yake mpya
ambayo kaiambia globu ya jamii kwamba ni moto
wa kuotea mbali kwa vile ni hadithi ya kweli




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Msaada tutani. Niko nje ya nchi, na mara nyingi filamu za Bongo zinapotangazwa ninaona zimebatizwa majina ya kizungu kama hii 'village pastor'. Je hadithi yenyewe iko katika kiingereza au Kiswahili? Na kama ni hadithi ya Kiswahili kuna haja gani ya kuibatiza Kiingereza!

    ReplyDelete
  2. Go Kanumba go, your trying even sisi tuliopo Ughaibuni tuna enjoy movie zako, keep it up the good job.

    ReplyDelete
  3. Tafadhali wacheza sinema wa kitanzania msipaze sana sauti,yaani msipayuke wakati mnazungumza kama sinema za ndugu zetu wa Nigeria.Ni ustaarabu wetu sisi watanzania kuzungumza kwa utulivu.
    rhoda

    ReplyDelete
  4. Safi sana Kanumba nakuamiania kwa maburdani yako mtu wangu lete vitus

    ReplyDelete
  5. Safi sana Kanumba,wewe ni msanii hasa na nadhani Tanzania hii unaongoza kwa mauzo ya movie zako.Mimi binafsi kama movie haina Kanumba siangalii au nitaingalia kwa mashaka.Big up na tunaisubiri village pastor.By mpenda movie za kanumba

    ReplyDelete
  6. Huyu kaka napenda anavyoigiza kwa kweli anajitahidi, tatizo langu moja tu pale unapokuna nae amejiremba na angel face aghhh anabore kwa kweli. michuzi usiibane kwani hata watoto wetu wanaompenda wataanza kumuiga kwa kweli abadlike asijipodei na kupaka makrimu

    ReplyDelete
  7. Kanumba anajitahidi lakini kibongo bongo. Mi nasubiri kwa hamu hiyo movie yake aliyoigiza uingereza! I can not wait

    ReplyDelete
  8. Kanumba anakubalika sana kwa filamu za kitanzania kwa kweli yeye na wenzake akina Kigosi wanajitahidi sana, ila bado wanahitaji kupandisha soski juu. Kama baadhi ya waliotangulia kuchangia walivyosema, ni wazi filamu zao na nyengine nyingi za kitanzania zinamapungufu mengi. Sio tu kama wanaongea kwa kupayuka tu na kwa makelele mengi kama alivyohusisha mdau Rhoda kuwahusisha na wanaijeria, bali kutatizo sugu zaidi la uhalisi wa dialogue, yani katika filamu nyingi sana utakuwa hakuna uhalisia kabisa katika maongezi kati ya waigizaji, kuna mifano ya wazi wazi utakuwa mtu anaongea na mke wake kwa lugha kama anaongea na dada yake, mwengine anaongea na mwanawe kwa lugha isioashiria authority yeyote kama mzazi. Natoa wito hapo kuna hitaji kuboreshwa.

    Nikiendelea hapo hapo kwenye uandishi wa scripts za hizo filamu kuna kuwa na mlolongo wa factual errors, yani ule uhalisi ya mtiriko wa hadithi kwenye filamu unakuwa unapingana sana na ukweli wa maisha katika jamii zetu. Hili nadhani pia linachangiwa na nature ya utengenezaji filamu huko nyumbani, yani utakuta mtu mmoja huyo huyo, hasa Kanumba, atakuwa ameandika script mwenyewe, yeye ni director, producer na hali kadhalika ana appear kwenye screen, hebu niambie mtu mmoja huyo anaumahiri wa kiasi gani kuweza kumudu yote hayo? waingereza wanasema, "Jack of all trades, master of none" yeah, I know wadau wataanza kutoa mifano sijui Clint Eastwood na wengine wa hollywood wana direct na kuigiza katika filamu zao! Hili linazidishwa na hii tabia ya kutoa filamu mpya kila week, hivo kuna kusekana muda wa kukaa na kuedit film vizuri na kurekebisha kasoro ikibidi kurudia baadhi ya scenes.

    Haya tukija kwenye utengezaji wenyewe wa hizo filamu utakuta kuna kasoro nyingi vile vile, nilisoma interview moja ya Kanumba kule Bongocelebrity kama sikosei, analalamikia ugumu wanaokutana nao kutokana na kukosa vifaa na msaada kutoka serikalini sijui wanahitaji uniform za police na vitu kama hivo, kweli nakubaliana nao upatikanaji wa vifaa vya filamu ni issue ukizingatia vitu kama professional camera ni ghali mno, yani entry level equipments vina cost zaidi ya milioni 10 za kitanzania, ila sasa hiyo ni hali halisi kwenye kila sector na kwa kwawaida kila mtu hujikuna pale ajipatapo.

    Huwezi kabisa kulinganisha filamu za kimarekani na za kwetu, wao wanakuwa na budget kubwa sana, kwa mfano filamu zinazotengenezwa studio za hollywood zinagharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 200. Kule zile filamu za chini wanaziita low-budget hizo huwa zina gharimu kama dola elfu 50. Hatari wakati bwana Kanumba sijui kama revenue inayotokana na filamu yake moja inafikia shs. milioni 50 za kitanzania. Hata hivo kwa kutumia hiyo budget finyu, kama ntengenezaji wa filamu atakuwa makini ana nafasi ya kutengeneza filamu nzuri tu kwa gharama nafuu, hii zaidi inawezekana kwa kuandika scripts rahisi.

    Binafsi nimebahatika kuona filamu nyingi za kimarekani na chache sana za huko nyumbani, kwa mfano kutoka kwa Kanumba nimepata kuona The stolen will, Family Tears, Johari na kadhalika, pia nimeona filamu kadhaa za Musa Banzi kama vile Veronica. Utakuta katika filamu zetu kuna makosa hayo kwa hayo yanajirudia, kwa mfano wapiga picha wanaonesha bado hawamudu kutumia manual settings za kwenye camera zao vizuri, picha nyingi zinapigwa zikitwa hazina focus, au una kuta video iko overexposed yani hadi inaumiza macho kuangalia, basic principles za kucompose kama ile rule of thirds haizingatiwi, utakuta wanapiga picha sehemu za public watu wanawanawazunguka waingizaji hivo inaondosha ladha ya filamu. Kadhalika kuna tatizo nimeliona linajirudia katika filamu nyingi sana, yani ni katika uaandishi wa credits, yani nani katengeneza filamu na vitu kama hivo, hapa pia wanapenda kuchanganya kiswahili na english, utakuta wanaandika "a so and so film" wanakuletea.. licha ya obvious kasoro ya grammar ila pia ina kuwa confusing sana haijuilikani nani hasa kafanya nini katika filamu husika.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  9. Kwa wale wadau walio ughaibuni ambao wanatamani kuona filamu za kitanzania, wanaweza kutembelea site hii http://movies.greatlakesmix.com/category_home.php?cid=Tanzania%20Movies

    Hapo kuna filamu kadhaa pamoja na bongo fleva hata hivo nashauri kununue filamu au kwa walionyumbani angalau kukodi kutoka kwenye maduka ya filamu ili tuwaunge mkono.

    Asante

    ReplyDelete
  10. KIJANA ANAJITAHIDI KWA USHAURI WANGU NAOMBA AACHE KUJIPODOA NA KUWAIGIZIA WA POPO ATAPOTEZA WAPENZI WAKE ASIPOJIREKEBISHA

    ReplyDelete
  11. Wee mtoa maoni wapili hapo juu, huko ughaibuni unakodai una-enjoy movies za Kanumba na hicho kingereza chako hicho sidhani kama utakuwa na makaratasi wewe"your trying even sisi...."!!!siuongee kindengereko tuu shida gani utokwe majasho kaka?

    ReplyDelete
  12. Jamani check buddy nae wamo tena yuko natural kabisa, napenda unavyoigiza ila nna wasiwasi vp mashekh hawatakujia juu na kua pastor japo wa uongo?
    Hongera unajitahidi kaka.

    ReplyDelete
  13. Ila single mtambalike anakuwaga na picha zenye uhalisia zaidi kuliko Kanumba. Hivi yule Bishanga yeye ndo aliachanaga kabisa na uigizaji?
    Nawaombeaga nyie waigizajimuendelee kuongeza juhudi ili kufikia mafanikio siku moja tuwe juu ya hata hao wanaijeria.

    ReplyDelete
  14. This looks interesting! Keep it up Steven Kanumba!

    ReplyDelete
  15. naomba websites ambazo naweza kuona filamu za kibongo hiyo greatlakes ina movies chache sana , nyingi hazinivutii na ni za zamani.

    ReplyDelete
  16. Jaribu kutembelea http://nahoza.ning.com wao wanauza matoleo ya karibuni, pia unaweza kuona trailers ila nyingi ndio hivyo hivyo stori za kukuunga unga tu, hakuna jipya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...