James Nhende, jina kubwa katika uandishi wa habari nchini, linalokupeleka kwenye kumbukumbu za enzi za Mwalimu, bado yupo katika libeneke la uandishi na amejibanza jijini mwanza kwa miaka takriban saba toka aondoke gazeti la 'mfanyakazi' lililotamba vilivyo kila jumamosi enzi hizo. Hajakanyaga Dar toka aondoke mwaka 2002. Hivi sasa anaendeleza libeneke kupitia gazeti lake linalohudumia kanda la ziwa liitwalo 'Mzawa' na bado anaheshimika kama mwandishi asiye na mfano nchini.
anko nanihii akiwa na James Nhende barabara ya Posta road jijini Mwanza jioni ya kuamkia leo wakiperuzi gazeti lake la 'Mzawa' linalotamba kanda ya ziwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hii ndio power ya hijab.

    Michuzi hapo hakuweza kupachika mikonozz kama kawaida yake.hahaha

    Dada uliyevaa hijab nakupongeza.Kweli mavazi ni statement!

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  2. Jamaa alikuwa mnazi wa Yanga ile mbaya!! Mpaka MOGELA siku mmoja uzalendo ukamshinda

    ReplyDelete
  3. uncle sam unatoa shavu tuu la sangara sana tuu mnooo

    ReplyDelete
  4. Nafurahi sana ninapowasikia/kuwasoma watu waliokuwa Dar na kurudi walikozaliwa kuendeleza libeneke kama James Nhende. Leo Gazeti la Raia Mwema lina habari ya David Ngonya aliyekuwa boss wa NIC lakini sasa yupo TUKUYU Mbeya na mambo yake Mswano sana. Wapo kina Edwin Mtei (yupo Arusha)Phillip Mang'ula, na wengineo wengi. Naomba baadhi uya vizee vikishastaafu virejee vijijini na kuwapa vijana nafasi ya ajira, badala ya kuendelea kuomba mikataba au kuomba tenda hapa na pale. Utawagundua tuu kwa vibegi vyao waviwekavyo mikwapani. Nawasilisha.

    ReplyDelete
  5. Hey Kaka James! Nafurahi kukona! Wakati ule gazeti la Mfanyakazi ulikuwa gazeti hasa. Watu walikuwa wanaingojea kwa hamu kila jumamosi. Wakati huo magazeti yalikuwa Uhuru na Daily News tu. Keep it up Kaka James!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...