Na Innocent Ng’oko
WAANDISHI wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoani Mbeya wamesusia ziara ya Waziri mkuu Mizengo Pinda kutoka na na uongozi wa mkoa wa mbeya kushindwa kuaanda gari maalum kwajili ya ziara hiyo.
Wakiwa katika kikundi waandishi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Nico Mwaibale kutoka shirika la utangazaji Tanzania TBC walisema kuwa hawawezi kudandia magari pasipo na utaratibu maalum. ‘
’Hatuwezi kudandia gari kama wapiga debe ikilinganishwa na umuhimu wetu katika ujio wa ziara ya waziri mkuu’’walisema waandishi hao kwa nyakati tofauti.
Akizungumzia sakata hilo mwenyekiti wa klabu ya waandishi MBPC Nico Mwaibale alisema kuwa haiwezekati waandishi wa habari tuburuzwe kama watoto na ni razima viongozi mbalimbali watambue umhimu wetu.
‘’Hakuna mwaandishi yeyote kwenda kwenye msafara wa waziri mkuu ambaye anaelekea kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe kwa lengo la kujionea hali ya ujenzi wa uwanja huo’’alisema Mwaibale.
Hata hivyo taarifa za uhakika zinadai kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa mkoa huo walikuwa wakihaha kuona uwezekanano wa kuwatafutia gari ambapo katika juhudi za awali walifanikiwa kupata gari aina ya pick up lenye uwezo wa kubeba wandishi watatu hali iliyiopelekea wandishi hao kuligomea.
‘’Tumeamua kufanya hivyo ili kulinda na kutunza heshima na utu wetu na tunawataka waandishi kote hapa nchini kuhakikisha wanafuata nyayo hizo’’walisema waandishi hao.
Waziri mkuu aliwasiri jana majira ya saa 11 jioni badala ya saa 7 mchana hali iliyowafanya wengi wa viongozi waandamizi wa serikali na waananchi kutoweka uwanjani hapo kwa muda kutokana na kukaa kwa muda mrefu wakimsubiri waziri huyo.
Hata hivyo waziri huyo aliondoka saa 11 30 kwenda katika uwanja wa ndege wa Songwe kwa lengo la kukagua uwanja huo ambao unadaiwa kuwa ujenzi wake umekuwa ukisua sua .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. BIGUP PAPARAZI
    GJK

    ReplyDelete
  2. hamna freelance reporter? Hapo ndio ulaji kama mtu anaweza kudandia debe akachukue habari na picha akija kuziuza kwenye vyombo vya habari si ulaji kabisa hapo.

    Nshi zilizoendelea zinakwenpa sana kuajiri waandishi wa habari ili kupunguza gharama za kuwa na mfanyakazi permentnt hivyo freelancer ndio wanategewa sana.

    ReplyDelete
  3. mwandishi na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mbeya wote ni sifuri. hapo kilichotakiwa toka kwa serikali ni kutambuliwa kwamba wapo na si usafiri, nk. vinginevyo, mwandishi wa habari wa waziri mkuu alitosha kufanya hiyo kazi waliyoikataa, yaani 'kupiga debe'. wa kulaumiwa ni wamiliki wa vyombo vya habari na si watengeneza habari.
    hivi mwaibale, hiyo ina tofauti gani na kwenda polisi ukaambiwa ugharamie usafiri wa kumkamata mtuhumiwa?

    ReplyDelete
  4. ndipo uduni wa mentality za mbongo unapoanzia!
    ikiwa hata mwandishi wa habari hana mentality pamoja na kupatiwa elimu kuhusu kazi yake, mi mwenyewe nachoka hata sijui nisemeje!
    baadhi ya waandishi wa habari wa kitanzania mnajiona sana nyinyi, eti UMUHIMU WENU!!
    hivi ni umuhimu wenu au majukumu yenu? uandishi unamzalishia nini mtanzania wa kawaida?
    hivi mimi nisipojua kuwa eti huko sijui mbeya, sijui singida, ujenzi wa uwanja wa ndege umekwama, faida gani nitapata?
    mmepewa gari, eti mnaringa, eti nyinyi ni watu muhimu, KULALADEKI!!!
    shombo tupu watu wengine.
    fanyeji kazi wajameni, acheni ubishoo. wenzenu waandishi wa jazeera , bbc, cnn na wengineo wanadandia mpaka madaladala na matatu katika juhudi zao za kueneza habari, nyinyi eti mnataka mtengewe mabenzi.
    ndoo maana mimi nahisi kuwa miongoni mwa sababu za kuzorota kwa maendeleo ya mtanzania ni ubovu wa mentality za waandishi, japo si wote. naamini kabisa kuna waandishi wanaungana nami katika kupinga fikra hizi mbovu za hawa waandishi wachache kujiona eti wao ni MUHIMU. mimi naamini wananchi na uzalendo ni muhimu zaidi, kwa hali yoyote ni wajibu wa kila aliyepewa jukumu kufanya kila mbinu kuwatumikia wananchi na kuwa mzalendo.
    ningekuwa na kajinafasi ka kutia fitna hawa wote kesho tu wangenyang'anywa na hivo vileseni vyao vya uandishi wa habari, kisha tukaona ulipo huo umuhimu wao!
    Mchapa boksi, Ukerewe.

    ReplyDelete
  5. hapa nakupinga wewe anoni wa hapo juu unasema wangedandia hata madala dala. inakuwa hivi, iwapo habari zinazotakiwa kufikishwa kwa wananchi ni za kuipamba serikali ni lazima serikali ihakikishe kwamba inapata waandishi wengi wa kusambaza habari hiyo inaitwa ni 'PR'. mfono kama kiongozi anataka mambo mazuri aliyoyafanya watu wayajue ni lazima alete wanahabari wengi sana ili kutawanya habari zake. lakini kama kiongozi ana habari mbaya juu yake mfano kakamatwa anakula rushwa hawezi kughalamikia wanahabari kuandika habari zake. waziri mkuu kwenda mbaya kuangalia kusua sua kwa uwanja wa ndege ni habari ya kuonyesha kuwajibika kwa serikali kwa wananchi, hivyo serikali inapaswa kuhakikisha kwamba habari inawafikia wananchi. offisa habari wa waziri mkuu peke yake hatoshi kutoa habari kwa wananchi wote na si hivyo tu ni kwamba magazeti mengine inawezekana yasiandike kwa sababu waadishi wake wamepuuzwa.

    ReplyDelete
  6. kweli hao wandishi wahabari ni zero, Je kweli sisi wananchi tutaweza kuamini habari zenu kweli, kama mnataka kupatiwa gari na serikali kweli hizo habari mnazoendenda kuripoti zitakuwa fair and balance kweli? imagine.. unawezaje kuripoti negative news ya serikali kama wao ndio waliokupeleka kuripoti. if they will give you ride they will control what you are going to report and whatever you report won't have independent source/mind into it

    ReplyDelete
  7. Nashukuru kuwa taswira ya Waandishi wetu wa habari imewekwa bayana. Siku zote nimekua nikiongozana na waandishi wa habari kwenye ziara mbali mbali za viongozi, kwakweli vijitabia vyao vya kutaka kunyenyekewa na kupewa uzito kwenye mambo ya posho,usafiri,chakula nk mara vimekua vikinipa mashaka kama kweli wanaweza kweli kufanya kazi zao kwa uhuru na ufanisi. Hata kama vitu hivyo huwa vinatolewa hakika havitolewi kwa nia njema bali katika hali ya kutaka kuwashawishi kwenye kuandika habari zenu, nanyi mmebwetekeka kwenye hilo mpaka mnaona halali yenu! Mmmmh njaa haina adabu kweli.

    ReplyDelete
  8. OBAMA sikubaliani nawe. umezungumzia upande ule ule wa kutumia waandishi kama chombo cha PR. kwahiyo umezungumzia jukumu moja tu la mwandishi na kusahau yale mengine ya kukemea, kufundisha, kukosoa, nk.
    kwahiyo unasikitika waziri mkuu wetu kukosa kipaza sauti cha maigizo ya kufoka na kutoa siku 30?
    narudia tena, kazi ya PR ya waziri mkuu ni ya ofisa habari wake. ila waandishi wa vyombo vingine, hawawajibiki kumfagilia waziri mkuu ila kuweka ukweli hadharani. haijalishi kama ukweli huo ni mzuri au mbaya.
    hapo wa kuwajibishwa ni muajiri yaani mmiliki wa chombo cha habari na sio mtoa/mtengeneza habari. kwa kifupi, nimefanya uandishi katika vyombo mbalimbali vya binafsi na ukiachilia ipp, waajiri wengine wamekuwa wakijikausha kugharamia usafiri hata wa daladala.

    ReplyDelete
  9. Anoni wa hapo juu je unakumbuka kuna kipindi fulani wakati wa kashifa kashifa za Mengi na Rostam waandishi walikuwa wanapewa pesa za taksi na kupikiwa pilao ili kusafisha jina la kiongozi mmoja na kupaka matope la mwingine? hivyo narudia tena ni kwamba inategemeana na habari yenyewe. kama ni habari za udaku ambazo gazeti litauza copy nyingi, hutasikia hata mwandishi yoyote anangoja usafiri wa serikali hata kidogo. wewe unataka kusema kwamba habari zao wanazo ona hii ni biashara wanangoja pick up la serikali?, hapana wanakwenda wenywe kwa sababu ni habari nzuri kwao kwa kibiashara. mfano kaka yangu Obama ndege yake huwa ina beba waandishi wa magazeti na tv wala si Ikulu peke yake, kwa nini kwa sababu wanataka kaka yangu asikike kwa watu wengi jinsi anavyo tenda kazi..

    ReplyDelete
  10. OBAMA, kwa mwandishi kutumia usafiri wa mtoa/mtengeneza habari ni kosa. ndio maana narudisha mpira kwa vyombo vya habari. kwa namna yoyote anabanwa kwenye kazi yake ikiwa ni pamoja na kunyimwa lifti na posho endapo ataandika wasivyotaka hao wanaoandikwa. iwe habari nzuri au mbaya, wa kugharamia usafiri, kula na kulala ni chombo cha habari. habari ya mengi na rostam ni uhaini wa habari kwa sababu waandishi hawalipwi inavyostahili.

    ReplyDelete
  11. AH!WEWE ANONI SIKUWEZI, BASI BWANA UMESHINDA.
    OBAMA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...