Mwenyekiti wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na katibu Mkuu wa CCM Luteni (mst.) Yusuf Makamba wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa ofisi kuu ya CCM Dodoma maarufu kama White House muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo asubuhi.
Baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya CCM wakati wa kikao hicho Dodoma leo




Viongozi waandamizi wa Kamati kuu ya CCM kutoka kushoto Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi,Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Kaqtibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba wakati wa kikao cha kamati kuu kinachofanyika mjini Dodoma.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. CCM MkereketwaAugust 15, 2009

    Je kwenye hivi vikao vya kamati kuu ya CCM waandishi wahabari wanaruhusiwa kuingia? Je wanachama wengine wa CCM wanapataje kujua mambo yaliojadiliwa na viongozi wao kama hayaandikwi au kurushwa hewani kwenye TV? Au sisi wanachama wengine ni wanachama wa kupiga kura tu lakini hatupaswi kujua yanayoongelewa kwenye chama? kunautata sana kujiita mwana CCM wakati huhusiki hata wala kujua lolote ndani ya chama chako. Tunaishia kupokea amri na vitisho kutoka ngazi za juu za chama. tunataka kuanzia sasa vikao vyote vya chama virushwe hewani kwenye TV na redio.

    ReplyDelete
  2. Hapa hakuna chengine zaidi ya kupanga mkakati wa namna ya kudhulmu haki ya wananchi ya kuchagua wanaowataka, mkakati ni ccm kushinda kwa hali yoyote, hata kwa kuiba kura ama kutowaandika wanaostahili katika daftari la wapiga kura.
    ccm oyeeeeeeeee

    ReplyDelete
  3. Mwenyezi Mungu awalinde na muendeshe kikao kwa hekima na busara. kila la kheri

    ReplyDelete
  4. haya bwana wabongo mkoje white house ya dodoma,makubwa.kwanini msiite hata chawino house,nanyie kwa kuiga,mkiita white house dodoma ndiyo pataonekana pamaana au inakuwaje? jaribuni kutokuwa mnaiga,huku ng,ambo hatujawahi kusikia sehem yao waita chamwino au ccm kirumba,mbona mnakuwa mnajishusha kifikra.marlesa mussa wa 22 hapa.uk

    ReplyDelete
  5. ufisadi tu hapo hakuna la maana

    ReplyDelete
  6. Ninaheshinu sana Busara ya Mzee Mwinyi, Mkapa, pia na haoa walio kwenye ulingo sasa Msekwa na Makamba na Mwenyekiti wa Chama chetu, Jakaya Mrisho Kikwete: Lakini Mkijiangalia mnajua wazi kuwa nyinyi karibu ni wapishi wa mwelekeo mmoja. Ingekuwa Busara kwa sasa kumkaribisha kijana mwenye busara, nia ya kujenga Taifa kushiriki kwenye uongozi wa juu wa Chama. Ninawatakia Kikao chema

    ReplyDelete
  7. Misupu unaniangusha hiyo ni State house sio White House au ulimi umeteleza ndani ya Kiswangish?

    ReplyDelete
  8. ili bongo tuendelee lazima CCM ivunjwe, tuanze upya, hapa hakuna demkrasia ila legacy ya nyerere inaendelea tuu, we all know during nyerere tulikuwa sio huru, hii nyumba ya ccm ni ya wananchi sio ya ccm, but nyerere made all stay with ccm ili ujambazi wao uendelee, hapa kwenye kikao hiki kingekuwa cha bunge amabacho wangezungumzia jinsi kwa mfano kuimarisha bandari dar-es-salaam ili tupitize bidhaa za eastern congo,burundi,rwanda,uganda. kenya leo iko vitani, wabongo tungechukua fursa hiyo kuundoa wananchi kwenye ufukara.

    ReplyDelete
  9. Hapo nikujadili jinsi ya kulinda mafisadi tuu wasikamatwe,
    Cha muhimu wananchi tunatakiwa kuwa macho mwaka ujao, tuchague watakao chenji huo uongozi kama wa Mugabe.Eeh!!

    ReplyDelete
  10. Ufisadi ni sawa na Chukua Chako Mapema (kabla hujaumbuka). Baba yangu alifanya kazi sirikalini (sio serikalini) miaka 30 na upuuzi, aliumbulia baiskeli tu. Na tena alikuwa tarishi kwenye idara yenye kukusanya mapato ya sirikali. Walahi, nasema, Chukua Chako Mapema kwa sababu hakuna atakaekupa!

    ReplyDelete
  11. KILA LA KHERI VIKAO VYA KAMATI KUU NA H/MASHAURI KUU TAIFA.

    MAAZIMIO YENU NI MWELEKEO SAHIHI WA KULIJENGA TAIFA,KUPUNGUZA UMASKINI, KUONDOA DHULUMA KWA WANYONGE NA KUINUA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.

    MAPINDUZI DAIMA

    MAINA ANG'IELA OWINO
    CCM UK

    ReplyDelete
  12. SIASA NGUMU BWANA HAPO KILA MTU NA LWAKE MAANA MSEKWA KASEMA YEYE WARAKA WA WA WAKATOLIKI SAFI HAUNA SHIDA MZEE MAKAMBA YEYE HAPANA KWAKE WARAKA UNA WALAKINI LAKINI LEO WAPO MEZA MOJA NA BOSI WAO ...TATIZO LA NCHI MASIKINI VIONGOZI WAKUBWA HASA RAIS ANAPEWA MADARAKA MAKUBWA SANA KARIBU VIONGOZI WOTE SERIKALINI ANACHAUA YEYE MPAKA NGAZI YA WILAYA HAPO NIPO KWENYE TATIOZO.ANGALIA SAMWEL SITAA ANAVYOWAPELEKESHA MAANA YEYE ANAJUA HAKUTEULIWA NA RAIS YEYE AMETEULIWA NA WABUNGE NA RAIS HANA MAMLAKA KIUTENDAJI JUU YAKE .PATAMU HAPO

    ReplyDelete
  13. KUPUNGUZA UMASKINI? SI KUONDOA UMASKINI? KWANINI TUNA MALENGO MABOVU YASIYOANGALIA MBELE? KUPUNGUZA UMASKINI HAITOSHI TUNAWATAKA WAUONDOE UMASKINI NA WALA SI VINGINEVYO ILI HATA KAMA HAWATAFIKIA LENGO LAKINI KWA SEHEMU KUBWA WATAKUWA WAMEFANIKIWA.TUTAENDELEA KUDANGANYWA KWENYE KILA IDARA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...