NANI ANA CONTROLL BIASHARA YA NYUMBA TANZANIA?? NI KILA MTU NA UAMUZI WAKE??
NI AIBU TUPU UKIANGALIA BEI ZA NYUMBA ZA TANZANIA! BEI KUBWA KULIKO HATA NYUMBA ZA ULAYA! BEI KUBWA HAKUNA BARABARA YA KUELEWEKA? UMEME? MAJI?
YAANI SASA TANZANIA KILA MTU ANATAKA KUWA BILIONEA, NYUMBA MBOVU BEI BALAA? HALAFU MSHAHARA WA MTANZANIA NI SH500,000 NANI ATAWEZA AU WANAUZIANA WAO KWA WAO MABEPARI????? AU INTERNET NDIYO IMEHARIBU MAMBO? WATU WANAANGALIA BEI ZA NYUMBA ZA ULAYA HALAFU NA WAO WANAJIWEKEA??
SERIKALI ITAINGILIA LINI KUREKEBISHA HILI TATIZO? THAMANI YA NYUMBA INABIDI IENDANE NA MAZINGIRA YA ENEO ILIPO! SIO MTU ANAJITUNGIA TU BEI YAKE HALAFU HATA SERIKALI HAIFAIDIKI CHOCHOTE!! TUACHE KUIGA WATANZANIA THAMANI YA NYUMBA NA VIWANJA VYETU BADO HAVIJAFIKIA VILE VYA ULAYA HATA KIDOGO!
TUTENGENEZE BARABARA, TULE UMEME NA MAJI, TUPIME VIWANJA KWA KUTUMIA SURVEYORS THEN TUONGEZE BEI! SIO TUNAKURUPUKIA TU FEDHA WAKATI HALI OVYO! WATU AMBAO WANANUNUA HIZO NYUMBA KWA BEI HIYO KALI WANA HATARI KUBWA KWA COLLAPSING YA MARKET KAMA ILIVYOTOKEA USA NA AUSTRALIA SABABU UKWELI WENYE UWEZO WA KULIPA KIASI HICHO CHA PESA NI KAMA 9% YA POPULATION YOTE!
LATER IN FUTURE WAKATI WANATAKA KUUZA NOBODY WILL BUY THOSE PROPERTY FOR THE PRICE THEY ARE ASKING! ITS A VERY RISK BUSINESS
Mdau J. KIONGOLI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. What is wrong with mabeba mabox nowdays? They are loosing temper so fast, it seems like the global recession has severely affected them. Unlike wabeba maboksi place of residence, In Tanzania we do believe in free market economy.

    It is the market that has to decide whether the previously mentioned price is over the top or not. It is not the government job to set houses' prices; in addition, we don't want government intervention in every aspect of our lives; mind you government is not always the solution to our problems.

    ReplyDelete
  2. Nakuunga mkono mdau kwa maada hii iliyokwenda shule. Soko la nyumba Tanzania limefikia hatua ambayo inabidi mamlaka husika ziingilie kati, kwani pamoja na kuwa huria lazima liendane na misingi halisi ya housing market. Kumekuwa na mlipuko wa bei kiajabu ajabu tu watu wanapanga mabei yao bila thamani ya ardhi ya maeneo hayo wala hadhi ya nyumba. Angalia huyo mdau aliyetoa nyumba yake hapo chini na kuinadi kwa shilingi milioni 750...hivi hii inaingia akilini kweli? Hili suala liangaliwe kwa makini sana.

    ReplyDelete
  3. mdau unajua gharama za ujenzi tanzania??? au unallinganisha chungwa na ndizi??/. unakaribishwa ujenge kama unaona kununua ni ghari, hapo ndo utajua kama hizo bei za nyumba zinapangwa ki- holela au la. tatizo haliko kwenye nyumba iliyokwisha jengwa , tatizo serikali imeshindwa kusimamia, mambo mengi, bei za vifaa vya ujenzi, viwanja nk. vyote hivyo hufanya gharama za ujenzi kuwa juu. matokeo ndio haya. wiki chache zilizopita tulishuhudia kiwanja kidogo kabisa cha meta za mraba chni ya 700, kikiuzwa kwamillioni 30,- zaidi ya $20,000 na hicho kiwanja ni kati ya viwanja vya mradi ambavyo viliuzwa miaka mitatu iliyopita kwa shillingimillioni 1.2- sawa na dola mia nane. kwa miaka mitatu, mmiliki amelipa ada ya shillingi 30,000 yaani 10,000 kwa mwaka. leo anauza shillingi millioni 30. hakuna mtu anaeshtuka toka wizara ya ardhi.sasa. tuanze kukemea tangu viwanja, bei za cement, nondo, vigae nk hapo ndiyo tutafanya bei za nyumba zitulie.

    ReplyDelete
  4. Mimi kwa mtazamo wangu mtu yeyote mwenye nyumba anauwezo wakuuza nyumba yake kwa bei yoyote aipendayo isipokuwa ww mnunuz ndio unatakiwa hiyo nyumba kabla hujainunua uifanyie utafiti kwanza kuwa hiyo bei uliyoambiwa je inahathi ya hiyo bei na uangalie vitu uvipendavyo ww muhim kama maji barabara n.k then ndio ununue ila haujalazimishwa ww ukishindwa anatanunua mwenzio ww endelea kutafuta nyumba unayotaka iwe ila sio swala la serikali na wala usilinganishe na nyumba za ulaya kwani nyumba za ulaya hata kama umeinunua hutakiwi kuifanya chochote mpka upate kibali toka council kama kuongezea chumba au kuitanua zaid ss bongo tambalale ukinunua nyumba yako ni yako tayari unauwezo wakuifanya chochote bila wasiwasi wote
    ndio maana bei ni tofauti sana

    ReplyDelete
  5. jamaani mnasahau mambo ya free market. Hii ndio free market yetu hapa bongo unafanya unavyotaka sababu kubwa serikali bado imepiga mbonji

    ReplyDelete
  6. Bwn Kinyogoli hizo theory hazifanyi kazi kwenye developing countries. Kwasababu the market itself has never been efficiency. Kuanzia currency, stocks, bonds etc hakuna efficiency. Tanzania tatizo ni information assymetry hakuna anayeweza kupata reliable inf. Kwahiyo kuna mwingine analiwa hapo lakini mwingine anawin upande mwingine. Hii si kwenye kuuza hata kupanga. Nenda maeneo ya sinza, kijitonyama ambapo huduma muhim hakuna lakini nyumba ni bei ya ajabu kabisa.
    Hapo hapahitajiki interventions, kubwa ni kutengeneza miundo mbinu ya sehem nyingi hata nje ya mji, kuweka na public transport za uhakika, hakuna foleni, maji, afya, shule nk. Ndio hiyo bubble itabust otherwise bei hazitabadilika. Shortly maeneo ambayo yapo overpriced ni yale ambayo yanaangalau huduma muhim na ni potential kwa investments.

    ReplyDelete
  7. Zat isi truu ,praisi is 2 hai.

    ReplyDelete
  8. mbwegelembwegeleAugust 15, 2009

    mtoa maoni wa kwanza mpumbavu. toa hoja kusaidi jamii ambayo asilimia kubwa wanaishi ktk huts.

    housing ni moja ya mahitaji muhimu kwa binadamu.
    serikali inayojali inazingatia hilo, either itajenga nyumba na kuwauzia wananchi kwa bei nafuu au itasimamia suala zima la mortgate.

    Huwezi kuachia wenye capital wawaibie wananchi kwa kisingizio chochote. Riba na thamani halisi ya nyumba vinahitaji usimamizi .

    Pia, kama property zao zina thamani hiyo , walikuwa wanalipa property tax ktk kiwango hicho.
    Kumbuka serikali inajukumu la kukusanya income na sales tax.

    kama una upeo kidogo, fanya research kwa nini housing in botswana(BHC) inayumba, ili NHC isiingie ktk mkumbo huohuo.

    ReplyDelete
  9. ni sawa bei ni kubwa, lakini msifananishe nyumba na maboksi ya ughaibuni. haya ni maboya tunaishi hizo za bongo ndio nyumba, za cement sio hizi za makaratas hata mtu akitembea unasikia nyumba inatikisika. nakubali bei ni kubwa but msisifie sana nyumba za ulaya ulaya tumechoka! Tchao!!!

    ReplyDelete
  10. msaada tena kwa mtoa maoni wa kwanza na wahusika wote wasiotaka kufanya tafiti kusaidi jamii.

    link below ni ya sweden housing.

    --Nearly all of Sweden's housing stock was modernised during a mass housing improvement program in the 1980s. Most houses are built by private contractors, but more than half of new housing is designed, planned, and financed by nonprofit organizations and cooperatives. NPOs and cooperatives provide dwellings for members who are designated as tenant-owners of their dwellings. In 1998, there were 4.3 million dwellings nationwide. Of these, about 2.3 million were multi-family dwellings and the remainder were one- or two-family homes. In 1998, about 20% of all dwellings were tenant-owned, 40% were rental units, and 20% were owner occupied. There were about 4.2 million households that year, with an average of 2.1 people per household. In 1999, 15,000 new dwellings were started.

    The government subsidizes new construction and reconditioning, helps various groups to obtain better housing, and extends credit at interest rates lower than those obtainable in the open market. A system of rent controls, introduced in 1942 and designed to freeze rents at the existing rate, was abolished in 1975. It has been replaced by a policy known as a utility-value provision, through which the rent of a flat may not be higher than that of a similar flat in the same area which is of the same general value to the occupant. Many tenant organizations negotiate rental agreements with landlords and rent increases can be reviewed by a tribunal. The National Board of Housing, Building, and Planning estimates that 250,000 new dwellings will be built from 2000–2010. About 30,000 dwellings per year will be renovated/rebuilt during the same period.

    http://www.nationsencyclopedia.com/Europe/Sweden-HOUSING.html

    ReplyDelete
  11. mimi nafikiri serekali haina haja ya kuingilia suala ni kuwaacha soko litaamua demand and supply kama mtu ameweka bei ya juu sana hata pata mnunuzi,atabaki na nyumba yake,akiona haiuziki atapunguza tu bei kama kweli ni serious saler,ila mdau anayesema kuhusu wamebaba mabox mbona imemuuma sana kila mtu anaweza kutoa mawazo yake, bila kujali yeye ni mbeba mabox au ombaomba etc

    ReplyDelete
  12. Napinga swala hili kuingiliwa na Serekali. Ni sie wenyewe tupendao sana kuishi Dar na miji mingine mikubwea ndio tunaongeza bei za nyumba. Demand na supply "tunazikontrol" wenyewe. Kila mmoja anadai ni born here here na wote tunataka kujenga hapa Dar. Ukibeba box, ukizungusha unataka uje kutesa halafu hiyo nyumba ukodishe watasha. Naelewa kujenga porini kusiko na maji, barabarana na muhimu kusipo na employment ni taabu. Shauri: Tujenge maghorofa sasa, yatafanya wengi kushare bei za viwanja..
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  13. mtoa maoni wa mwanzo na ngeli yako ya ugoko hio unakurupuka tu na matongotongo yako kutoka kwenye kitanda chako cha telemka tukaze vitafunio kipande cha muhogo mchana ugali na papa wa kuchoma,kisha unakandia wabeba boksi kiwanja chako kikali kuliko vyote ulichowahi kukanyaga Nairobi,Dsm na Zenji labda,mtu wako mashuhuri kuliko wote uliewahi kukutana nae ni Juma Nature,ndio maana unaona hizo nyumba kali kweeeeli kweeeeeli na zinastahili hata hizo bei pia ziongezwe shame on you!!tembea utoe tongotongo hizo kisha ndio utaweza kuona kinachoongelewa hapa kwa nyumba gani basi?!nashangaa kiwanja sinza kuuzwa zaidi ya milioni50,sinza ilitakiwa kiwanja hata kiweje kisizidi milioni10 na nyumba isizidi milioni50.Na ndio maana ndugu zetu wakituambia turudi tununue nyumba bongo tunaona nafuu ya kubakia hukuhuku tu,kwavile huwezi kuuza nyumba milioni100 wakati tofali mchanga mwingi kuliko cement na choo kikijaa unaita nyonya mavi huna hata chemba.
    MDAU MLA BATA UBATANI KAMA UNA JEURI NIFATE KAMA HAWATAKUTIA VIRUNGU AIRPORT HAPO HAPO BONGO.

    ReplyDelete
  14. wee anoni wa aug 15, 07:11pm. Maada ziliozoenda shule unazijua wewe au unakurupuka tuu. Una muunga mkono huyo mwana boksi kwani umekatika. SOKO HURIA MAANA YAKE NINI. KILA MTU NA MALI YAKE KAMA HAMNA VIJISENTI FADHALI MDHAMAZE KUA DEKI KAZENI MSULI...

    ReplyDelete
  15. Nadhani mdau wa 6:51 P.M ana uwezo mdogo wa kufikiri.Free market economy haina maana ya kujipangia bei ambazo hazilingani na thamani ya biashara yenyewe.Kunatakiwa kuwe na mamlaka za udhibiti kama vile ilivyo EWURA na kadhalika.Ndio maana katika nchi zilizoendelea thamani ya nyumba au biashara hazipishani sana na ukweli ulivyo, ni ajabu leo bei za nyumba huko Tanzania ni kubwa kuliko USA,Japan,UK,France au hata Australia wakati kuna miundo mbinu dhaifu kuanzia barabara,umeme,maji(untreated kwa sehemu zenye maji)na mipangilio mibovu ya nyumba zenyewe(squatters).Mara nyingi naposoma hayo matangazo naona kama vile ni michezo ya maigizo vile.TUWE WAKWELI KATIKA KUTHAMINISHA.

    ReplyDelete
  16. Nami naungana na mdau kuhusu suala la nyumba! Nyumba ya dola 350,000 mpaka dola milioni 2... it's ridiculous. Mdau wa kwanza mchele wangeuuza $500 kwa kilo ungekuja juu vile vile usingezema ni soko huria. bei za dala dala zikianda wanacnhi wakilalama serikali iingilie unafikiri wajinga? it has nothing to do na reccession ni simple economics.

    ReplyDelete
  17. Huyo anayeuza nyumba chafu kama hiyo yenye ma crack kila kona kwa mil 750shs ni mwehu labda amuulizie yule alumni wa muzumbe university mologolo bwana peter nalitolela inaendana na hadhi yake. Mdau anaedai ana believe in free market inabidi arudi shule ya econ 100, What real determines the market price of such a crap house? with the same money i will be buying big-o house in Miami with good landscape around the house and not that piece of shiit seating in desert condition like, inakera sana Bongo sasa hivi kila mtu anaibuka na bei zao ambazo haziendani na hali halisi ya uchumi utafikiri wanakunya vile...ovyo kabisa acha niendelee kulipia morgage yangu hapa Virginia na siyo kununua uchafu kama huo hata kwa dollar elfu hamsini.pumbaff

    ReplyDelete
  18. KIBAYA ZAIDI HUYO JAMAA ATAWAAMBIA tra KUWA NYUMBA AMEUZA 75M ALAFU ATALIPA CAPITAL GAIN TAX KIDOGO

    HII NI FREE MARKET
    KWA HIYO MARKET ITAAMUA NA SIO SERIKALI
    WANANCHI WATZ INATAKIWA WASIKUBALI KULANGULIWA NA KUINGIA MKENGE KWENYE MABANDA MABOVU KWA BEI MBAYA
    TZ KILA KITU WATU WANALANGULIWA, WENYEWE WANAONA UFAHARI, WAKIAMBIWA UKWELI WANASEMA WABEBA MABOX.

    ReplyDelete
  19. Mtoa maoni wa Sat Aug 15, 06:51:00pm
    Sijui unaishi dunia ipi kwa sababu hiyo free market unaisema ndio iliyopelekea kuanguka kwa uchumi wa USA na washirika wake.
    Ikiwa hakuna udhibiti wa bei katika nchi kama hii Tanzania basi umasikini utawagubika raia wake kama hivi tunavyoona sasa.
    Kuna mgawanyiko mkubwa hivi sasa wa wenye nacho na wasiokuwa nacho.

    ReplyDelete
  20. Nashukuru kwa umakini wa mtoa mada hii. Mimi nadhani hili suala la soko la nyumba tungelijadili kwa undani hasa kwenye hii blog ya jamii. Unajua housing market isiposimamiwa vizuri inaweza kuleta matatizo kwenye mfumuko wa bei. Marekani ingawa ni uchumi mkubwa wameona hilo tatizo na wanalifanyia kazi kwa kuweka financial regulations. Ningependa ndugu Michuzi ukaribishe mjadala makini wenye wataalamu wa uchumi na mambo ya fedha pamoja na wadau wa kawaida.

    ReplyDelete
  21. Kiongoli unaishi dunia gani?
    Hivi unafikiri kuwa serikali ipange bei za nyumba?
    unachekesha sana kwani huelewi free market maana yake ni nini?
    Kama wapo wanunuzi wa kununua nyumba kwa bilioni moja, maana yake biashara inafanyika na wapo wenye uwezo wa kununua.
    Soko ndiyo linalopanga bei, ninakushauri uende shule kidogo uongeze maarifa.
    Halafu hii mambo ya kutoa mada halafu baadae unakuja kujiwekea comments zako, haipendezi.

    ReplyDelete
  22. Akili KumkichwaAugust 16, 2009

    Kiongoli , tuliza mpira. Usiwe na jazba kiasi hicho kwa nchi kama TZ. Watu wamesoma kabla yako huko nje na wakarudi , wakayaona ya kuyaona TZ, wakaiga na na wakatulia.
    Nimesoma article yko ya kwanza , wiki tatu zimepita, bdo unaonekana hata kiingereza chako hakijatulia kabisa , pamoja na kusoma huko nje. Una-copy hotuba ya Obama na kuitumia kuandika article. Pia huna point za kujazia au ukweli wa kutosha , bali unalaumu, bila kujua baba yako mzazi pia amehusika sana kuifanya TZ kuwa hivi ilivyo sasa.
    Wewe una jazba, kwa kuwa nyumba yenu ya Sinza, sio tena nyumba nzuri na ni msumbiji syle ya zamani.
    Tulia na uelewe kwamba matatizo ya TZ, hayataisha leo au kesho , kwa kuwa wewe umesoma nje na unaona jinsi nje wanavyofanya mambo kwa usahihi, basi TZ pia tufanye hivyo hivyo .
    Walio-imaliza TZ ni watu kama baba yako mzazi, waliofilisi RTC huko mikoani.Sasa wewe una jazba kwa kuwa umefikia umri wa kununua nyumba baada ya kumaliza masomo yako nje, ili ulingane na sisi uliotuaacha hapa TZ au tuliorudi.
    Kumbuka hawa na mimi ni kuiba tu na ni wezi watupu.
    Nyumba zinauzwa na kunuliwa na wezi. Huko uliko nje watu wananunua nyumba kwa Credit,wanalipa kidogo kidogo kulingana na kipato chao, hapa TZ watu tuna-corrupt nchi na kununua kwa cash.Mishahara yetu hailingani na nyumba tunazonunua au kujenga hapa nyumbani, ni wizi tupu kama alivyofanya baba yako huko mikoani miaka hiyo.Sio kwamba najisifia kwa huu wizi, bali kila mtu anaiba, na hata wewe ukija hapa na ukapewa mwanya utaiba tu, ili ufanane na sisi tu.
    Unaweza kuwa na point, lakini point zako ni za watu kama nyinyi wenye miaka 30 na kuendelea walio nje na waliomaliza masomo yao na wanao-ona ugumu kurudi nyumbani, pia ugumu wa maisha yao walipokuwa wakisoma nje.Point ambazo nilikuwa nazo mimi pia miaka mitano niliporudi hapa nyumbani.
    Elewa, au kumbuka sio kwa sababu umesoma na kumaliza nje basi ni wewe tu ndio unastahili kuihoji serikali kila siku. Nilirudi hapa TZ miaka mitano iliyopita nikiwa na umri kama wewe, baada ya kusoma nje, nilichanganyikiwa kabisa. Niliomba nirudi tena UK, maana maisha yalikuwa sio, lakini nilihonga hadi nikapata kazi TRA na sasa , mambo powa kabisaaaaaaaa.
    Wewe tuliza jazba na uwe na subira, usiwe na jazba hata kama unasema ukweli, kumbuka sio TZndo yenye matatizo ni Africa yote chini ya sahara iko hivyo hivyo. Leo hii Wewe unazungumzia nyumba, wala hugusii kabisa, wakulima wa Singida, kijijini kwenu au kwa bibi yako kwamba hawana hata fedha ya kula milo mitatu kwa siku au nyama kila siku.
    Zungumzia hao, then sisi wezi tunaonunua nyumba za milioni 200 Boko na kawe, uta-deal na sisi baadaye.Au njoo uonje joto ya jiwe ili uibe kama sisi na kuwa na nyumba Masaki.
    Au baki huko huko na uachane na hii nchi ambayo tuliita bongo, au akili kumkichwa.
    najua wewe na wenzako mtahoji, lakini mambo ndo hivyo. Tuliza jazba.

    ReplyDelete
  23. Stop complaining, and let the Market decide the price. Bei za nyumba zinategemea demand, kama demand ya nyumba ipo juu basi price za nyumba zitapanda vile vile. Serikali haina mamlaka ya kucontrol price za nyumba, ni demand ndiyo yenye uwezo huo. You have to believe, FREE MARKET CAPITALISM IS THE BEST PATH TO THE PROSPERITY.

    ReplyDelete
  24. KUNGEKUA NA KAMPUNI ZA KUUZA REAL ESTATE KAMA ZILE ZA NCHI NYINGI KAMA KENYA HAYA YOTE YASINGETOKEA. JAMANI NINASEMA TENA JIFUNZENI KUTOKA MAJIRANI ZETU WA KENYA. HAINA HAJA YA KWENDA MBALI MFANO HUKO HAPA HAPA KARIBU KWA JIRANI ZETU. MAMBO MENGI HAPA TANZANIA YANAFANYWA KIHOLELA.

    ReplyDelete
  25. Nadhani shule inahitajika hapa wewe mdau Mike John wa 12:51 Am nadhani umekosea sana unapoangalia upande mmoja tu wa DEMAND je vipi kuhusu SUPPLY? Je hujui kama kuna supply kubwa bei itakuwa ime-'stabilize".Ukiongelea Tanzania ni wazi hakuna mortage company na hilo ni tatizo kwa sababu mahitaji ya nyumba ni makubwa sana na hakuna uwezo wa kutosheleza market hivyo wananchi wanalazimishwa kununua kwa bei kubwa wanayotaka hao wanaouza nyumba.Upande mwingine wa shilingi ni kuwa iwapo kungekuwa na nyumba nyingi zilizojengwa iwe na serikali au mortage companies bei ingekuwa nafuu kwa wananchi wanunuzi hata bei ya building materials kama cements na nondo ingepungua.

    ReplyDelete
  26. Mdau, kiongoli, kweli data zako umezipata wapi kwamba 9% ndio wenye uwezo wa kununua nyumba za M750 na kuendelea.
    unajua 9% ya watanzania wote ni karibu milioni mbili na laki saba.Ndio maana unaonekana ni mtu wa kuandika andika tu bila data kamili, bali ubababaishaji.
    TZ wafanyakazi wa mashirika binafsi, ya serikali na serikali yenyewe na mashirika ya umoja wa mataifa , ukiweka na wafanyabiashara sawa sawa hawafiki hata milioni mbili.
    Ukijumlisha watu milioni mbili n kuwapa kil mtu uwezo wa milioni 500-700, basi nchi ya TZ isengukuwa maskini tena.
    Angalia, data vizuri na fanya research, kbla ya kuandika ili jina litokee katika michuzi.
    Serikali haiwezi ingilia kila kitu. Ikiiingilia juu ya hili swala, maana yake ni kwamba ianze kuhoji uhalali wa wtu kuwa na nyumba za milioni 100 na kuendelea mbele, wamepata wapi hizo fedha.
    kuingilia ni kuanza kutaifisha nyumba zote kwa kuwa watu wamezijenga bila mikopo, au fedha halali na hivyo ni wahujumu uchumi.
    Kuacha kutokuingilia maana yake ni kuifanya serikli ikubali hii hali na kuruhusu maendeleo ya mafisadi, kwa jina la soko huria au free market.
    Kumbuka watu waliuziwa nyumba Oyersterbay sio kwa kupenda, bali wale wazee waliitumikia serikali na mashirika yetu vyema kwa miaka 25 na hawakuwhi kuuuibia kisawasawa kama hawa vijana wa sasa wanavyofanya sasa hivi. Miaka mitatu kazini , tayari bonge la nyumba na magari ya kifahari.
    Hili swala ni kulianza kama uhujumu uchumi au kuliacha liwe soko huria kwa mafisadi kuendelea kujiibi na kutuibia.

    ReplyDelete
  27. wadau mnajitahidi kuelezea matatizo ya nchi yetu.

    Tatizo si elimu hasa, bali upumbavu.

    unaweza ukawa msomi mpumbavu, ndo maana nchi zingine zinapata mawaziri au hata raisi pumbavu.

    elimu inaweza kufuta ujinga ,si upumbavu.

    ReplyDelete
  28. Watanzania sisi ni majitu mabwege. Ukienda Nairobi unapata nyumba ya dola laki 2 hadi 3 ambayo ni bora kuliko hii. Hata kupangisha nyumba Nairobi ni gharama nafuu kuliko Dar es Salaam. Mji wetu hauna huduma yoyote, sasa hiyo bei ya juu ya kazi? Uchumi huria si uchumi holela, huwezi kupanga bei bila ile kitu Kimombo inaita "rationality." Huku majuu watu wanapanga bei kwa kuangalia vigezo vingi. Sasa hilo jumba ambalo hata ramani yake ndani ukiingia labda utachoka mwenywe, la nini kununua kwa milioni 750? Mimi hata kwa milioni 100 sinunui.

    ReplyDelete
  29. KWA KIFUPI MBEBA BOX US ANAKAA KWENYE NYUMBA AMBAYO KUANZIA UBORA MANDHARI NA KILA KITU UNACHOWEZA KUFIKIRIA NYUMBA YAHITAJI INAZIDI NYUMBA YA MILIONI 1 HADI NA NUSU YA HAPO BONGO AMBAYO WANAMHITAJI MBONGO HUYO WA TZ ALIPE NA AKAE KWA MWEZI....MPAKA HAPO INATOSHA KUONYESHA HOJA ALIYOLETA MWENZETU HAPO JUU INA UBORA NA UZITO WA HALI YA JUU.

    ReplyDelete
  30. jamani kwanza mmesahau kitu kikubwa kinachopandisha nyumba dar ni mafisadi,wenye pesa za wizi. unadhani wote tungekua tunategemea mishahara yetu mambo yangekua hivi.nyumba zimeanza kupanda miaka 2 iliyopita wakati w2 wamekazana kuiba,hela za wizi ndo zinatufikisha hapa. imagine mi mwaka 2005 hadi 7 nilikaa sinza nililipa nyumba self contained 90,000 ina vyumba vinne,mara mwenye nyumba akasema anapandisha hadi laki tano,imagine,ila nyumba ilikaa sana hadi kuja kupata mnunuzi. siku rushwa na wzizi wa wachache ukiisha nyumba zitarudi chini, angalieni tangu misukosuko ya ufisadi sahizi nyumba tena kidogo zimeshuka na w2 wengi waliama sinza na kwenda kimara na tabata. ch ukweli hapa ni kwamba serikali inatakiwa iangalie kwanza mishahara yetu wote ndo ipange minimum na maximum price.najua kujenga kazi lakini this is too much.kwani dar tu ndo w2 wanajenga mbona mwanza bei si hivi?arusha nyumba zilipanda kutokana na w2 wa UN na EAC sasa wanaondoka zitashuka tu, pale w2 watakapokosa wapangaji. ila jamani rais ivi kafanya nini tangu aingie.ua naimagine angetoka mwinyi akaingi huyu sijui tungekua wapi.

    ReplyDelete
  31. Naona watanzania sasa tumefulia kimawazo. Hata kama tuna free market bado gharama za nyumba, bidhaa na maisha kwa ujumla lazima zilingane na hali halisi ya maisha. Hata kama kuna wajanja wachache wanaoweza kuafford bado tusisahau kwamba walio wengi wanashindwa hata kuweka mlo wa maan mezani. Mimi nafikiri huyo jamma aliyetangaza hiyo nyumba alikuwa anapima watu joto. Watanzania wenzangu, fungueni macho!!!! Tukiendekeza huu mfumo wa free market tutashindwa hata kuwanunulia wake zetu sidiria!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  32. Nasikitika sana kwa mdau hapo juu aliyewaita watanzania waishio nje "wabeba maboksi" kwa taarifa tu wapo wengi wenzetu huku ulaya wana makazi au makampuni ya ajabu yenye mitaji ya mamilioni ya madola. Namshukuru sana bloga mkuu wa nanihii kwani blogu hii inaunganisha jamii ya kila ngazi kiumri,kimapesa nk.
    Nikizungumzia sasa hizo bei za nyumba Tanzania inasikitisha sana kwa nchi kama Tanzania ambako mtu wa kawaida anaishi kwa dola moja kwa siku bei za vitu ni juu kiasi hicho.Swali langu ni kama lifuatalo je ni akina nani wanaonunua mijiibanda hayo? mtu na akili zake sidhani atathubutu. Hebu oneni haya mashida mimbu,shida ya maji,shida ya umeme,shida ya mawasiliana,byurokresia nk. nk. nk.
    KILI
    BG

    ReplyDelete
  33. NAKUUNGA MKONO KABISA ANONY HAPO JUU WATZ HAPA NYUMBANI WAMEZIDI MBEBA MABOX MBEBA MABOX...MBONA HAMUONGELEEI PHAMACIST,FINANCIAL ANALYST,COMP ENGINEER,MD'S ETC ETC WAPO NA WENGINE WANAKUJA,HII INAONYESHA JINSI GANI TULIVYO KTK 'DENIAL STATE" MIMI NILIKUWA US MIAKA MIWILI ILIYOPITA KWA KUBEBA MABOX KWANGU NILIFANIKIWA KUPATA MSHAHARA WA $4000 IN A MONTH...BILLS SIKUWA NAZO NYINGI APT: $840,GARI PAID OFF...STANDARD YA KATI,OTHER BILLS TOTAL 1000 SAVING YANGU KWA MWEZI WAS MORE THAN 2000,NILIKUWA SHULE NA NIMEMALIZA BILA TATIZO LOLOTE NIMERUDI NYUMBANI NIMEFANIKIWA PATA KAZI YA KUNILIPA DOLA 2500 (Gross) SI WENGI WALIPWAO HIYO JAMANI NINALIPA APT 750 ILI ANGALAU NISIBADILISHE SANA MAISHA NILIYOISHI KWA MUDA MREFU KIDOGO NA OTHER COST KWA MWEZI NI KAMA 800, JUMLA 1600 BADO VIHELA NAVYOTOA VYA HAPA NA PALE NABAKIA NA KIASI CHA SANA SANA DOLA 550-600 KAMA SAVING SINA FURAHA KWA SABABU HAIINITOSHI.NAAMINI NINGEVUMILIA KULE US NINGEPATA KAZI AMBAYO INANILIPA MTZ HAPA ANAIFIKIRIA KUIPATA BAADA YA MIAKA 10 NA ZAIDI AKIIBA BASI MITATU AU MINNE SASA NASHINDWA KURUDI US SABABU NIMESHAHARIBU STATUS YANGU LAKINI NATAKA KUWAFUNGUA WATZ WENZANGU KUHUSU SUALA ZIMA LA KUSEMA OHH WATZ WA ULAYA WANABEBA MABOX TO BE HONEST WITH YOU IN ONE WAY OR ANOTHER BOX LAZIMA UBEBE KUPATA GREAT FUTURE NA MABOX WANAFUNZI WENGI WANABEBA SABABU NDIO KAZI AMBAZO UNAWEZA UKAFANYA USIKU HUKU MCHANA UKIENDA SHULE,MF MAREKANI NI NCHI AMBAYO UNAWEZA TAFUTA KAZI YOYOTE UKAPATA SIYO LAZIMA UBEBE BOX KAZI NYINGI SANA ZA KUKAA TU NA KUINGIZA HELA NZURI NA SI PROFESSIONAL JOB SEMA TU ZIKO MCHANA.

    ReplyDelete
  34. Haya bwana hiyo ndo free market, ndo maana tunaibiwa airpot na bandarini ushuru mkubwa, rushwa nyingi ili wanunue hayo majuma.Tanzania ufisadi mtupu., bei inashinda hata ya ulaya ni kitu gani hasa wanachouza, huduma ya maji mgao, umeme, mbali na barabara. Nawahurumia sana watanzania wasio na uwezo wa kupata viwanja je tutafika???? au undo tunaelekea kwenye ubebapari na ubwana mkubwa?????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...