Nakubaliana na wadau wengi waliochangia, ni kweli nyumba, vifaa vya ujenzi na vitu kama magari tanzania vinakuwa over priced. Ila sioni kama kuna ulazima wa serikali kuingilia kati juu ya bei za nyumba. Muhimu ni kudhibiti bei za vifaa vya ujenzi na bidhaa nyengine ikiwezekana kufanya tahafifu ya kodi ili watu wengi waweze kujenga.
Aidha, nakubali sio sawa kulinganisha bei za nyumba tanzania na ulaya au marekani, ila pia lazima tukumbuke katika ujenzi, ni vifaa vichache sana ndio vinazalishwa tanzania vingine vyote ni kutoka nje na huko vinauzwa kwa dollar na ukweli bei zake zinakaribiana na hizo za ulaya kabla kutiwa kodi, hasa kwa zile bidhaa zenye quality nzuri.

Niliatangulia kutoa maoni kwenye posti ya mdau alitetangaza kuuza nyumba kwa milioni 750. That property is highly over priced, ila napingana na baadhi ya wadau waliosuggest ilikuwa ni typo error na ad eti ilipaswa kuonesha milioni 75 tu. Sijui ile nyumba kwenye lile tangazo imejengwa vizuri kiasi gani, ila naamin ina worth more than that ukizingatia na ukubwa wa eneo.
Kwa mtazamo wangu, naamini serikali inapaswa kusimamia swala la uzwaji wa viwanja na kudhibiti bei za vifaa hio tu ndio itasaidia properties kuwa affordable, mimi natokea zanzibar, kule kwetu ukipewa hati ya kiwanja inasema,"HATI YA MATUMIZI YA ARDHI" sio umiliki na hairuhusiwi kuuza ndio maana ukuninunua ardhi kule, wanacheat na kuandika umeuziwa msingi wa nyumba. Ughali wa nyumba, unaanzia kwenye bei mbaya za plots na mifumuko mibaya ya bei za hardwares.

Mimi, nilianza kusimamia ujenzi wa nyumbani, mwaka 2002 na ndio umekamilika mwaka huu, tulianza kujenga wakati bei ya cement ilikuwa Tshs. 4000 kwa paketi na sasa cement imefikia elfu 16, tulinunua harvey tiles zile za south africa kwa 7500 kwa moja na sasa sina hakika ila about 3 years ago nilinunua za nyoongeza tayari bei ilifikia elfu 12.
Tunilinunua plot 1000sq m. kutoka kwa mtu binafsi mwaka 2000 kwa Tshs. milioni 5, november mwaka jana plot ya opposite na sisi ukubwa sawa, tena undeveloped iliuzwa kwa shs milioni 45. Tulitumia matofali 6" close to 8000, kipindi tunaanza kujenga tofali moja grade B lilikuwa linauzwa shs. 380 last year nilinunua tofali kama hilo kwa shs. 950. Hatujatumia hardboards kwa ceiling ila just for refference kipindi hicho moja liliuzwa shs. 4000 na sasa moja wanauzwa elfu 12.
Tumekwenda dubai mara tatu kununua hardwares na ujenzi wetu ni 2-story, 600 sq metres, hadi kukamilika tumetumia a little above milioni 250 ila kwa kutumia hizo bei wakati tunaanza kujenga, sasa wadau hapo ukinzingatia huo mfumuko wa bei hatupo tayari kuuza nyumba yetu hata kwa milioni 500 ukizingatia exchange rate ya dollar hajabadilika kiasi hicho.

Haya, naomba nitumie fursa hii kujaribu kutoa muongozo kwa wananunuzi, nini wanatakiwa kuzingatia katika kupatana bei wanapofikiria kununua nyumba.Awali sishauri mtu mwenye muda wa kutosha na upeo kununua nyumba iliokamilika, badala yake ni vizuri kutafuta plot na kuanza kujenga kuanzia msingi, hiyo itapelekea kupata nyumba kulingana na matakwa yako, utaweza kujachagua plans nzuri unayoipenda na hali kadhalika utakuwa na uwezo wa kuchagua vitu kama rangi za tiles na fixtures nyengine.

Kwa wasiokuwa na muda, kabla kununua nyumba unatakiwa kuikagua vya kutosha, nyumba ina tegemea sana imejengwa vipi na ina nini na nini, sio kuangalia floor imeweka tiles na kuna masterbedroom tu. Unatakiwa kutathmini nyumba imejengwa vizuri kiasi gani, kuna tiles za kila aina, kuna za india/ china cheapest baada ya maika miwili zinakuwa scratched hazifai, na kuna za spain, hata hizo za spain zina grades zake kuna grade A nzuri then kuna commercial grades rahisi ila sio nzuri sana kwa hiyo usiwe excited ukitajiwa hizi spain au kuona imeandikwa made in spain. Vile vile kuna natural marble and granite na pia kuna cultured yani atificial wanatengenezwa kwa kutumia resin na unga wa marble.
Ukija kwenye matofali kuna matofali mchanga mtupu, muhimu kuzingatia sana ubora wa nyumba kama plaster, nyengine ukigusa ina mung'unyuka! Wanaweza kuja majambazi kwa kutumia kidoletu, wanapukuchua motor baina ya matofali na kuyatoa wanaingia ndani kiulaini kama kwao. Kama ni nyumba ya roshani inabidi udadisi ni nyuma (nondo) aina kani vimetumika, napenda sana kuwa mzalendo ila hapa inabidi niseme ukweli, nondo za tanzania ni mbovu na hazifai even though ni cheap, nzuri ni wanatoa uarabuni, bila kujua kwanini unauliza muuzaji anaweza kukueleza alitumia nondo gani.
Pia sio tu nondo gani imetumika ila kuna ujenzi wa uswahilini beam inakuwa reinforced na nondo mmoja au mbili badala ya vyuma vinne kama inavyotakiwa, inapaswa hilo pia ulidadisi! kwa kweli ni kununua mbuzi kwenye gunia, huwezi kujua hadi nyumba ikianza kufanya nyufa ila ujaribu kudadisi huenda ukapata ukweli. Tukija kwenye ceiling, thamani ya nyumba pia inategemea katumia nin, hardboards, mbao, plaster board chips board kila kimoja kina bei yake hapo.

Kwa kuongezea, unatakiwa uangalie fixtures kama za umeme, vitu kama water heaters ni aina gani zimeweka, au mafeni, kama kuna air conditioner, hivo vitu ni muhimu sana dont be carried away ukapuuza kwa kutegemea utabadilisha kirahisi ukishanunua, hivo vitu ni ghali, vitu kama sockets, switches, "kuna za kichana na kuna za england", hizo za england pia kuna imitations so unahitaji mtalaam kukusaidia kujua, hali kadhalika wires kuna nyengine mbaya kiasi cha kuwa fire hazard kabisa, vile vile muhimu sana kukagua na kutathmini wiring ilivyofanywa, wengine sebule nzima anaweka socket mbili tu na chumbali unawekewa mmoja tu, au jiko zima unakuta kuna socket ya cooker na moja ya friji kwisha!
Mara nyengine mtu anauzwa nyumba ya vyumba 4 kwa milioni 300 kaweka fuse box ya kichina tena 4 ways tu, matokeo yake taa za nyumba nzima zinatumia fuse moja! yote hayo ni mambo ya kuzingatia sana. Fixtures za vyooni, kuna vyoo vya kichina una flush mara kumi vitu bado vinakutizama tu, yote ni mambo unatakiwa kuzingatia na hii ni hata kwa wale wanaojenga wenyewe lazima wawe makini. Katika nyumba yetu ya mwanzo tulijenga, trust me, yalitukuta tuliishia kureplace vyoo viwili kwa kadhia hiyo, una maliza maji tank zima na bado choo kina goma na wala hii haimaanishi vitu vyetu vizito sana, kawaida tu.

Pia muhimu kuzingatia vitu kama faucets( mabomba sisi zanzibar tunaita mifereji), kuna ya china/ india unapata kwa chini elfu 30 na unafunguka kwa mbwembe tele! na pia kuna vitu vya uhakika vya italy vinaanzaia laki na elfu 50, vya kichina baada ya siku mbili crome finish inatoka, na mingine unafunga bado unakuta una endelea ku drip, vifaa vya maji vizuri ni kutoka Italy au Germany.
Pia usisahau kupeleleza water pressure, nyumba nyingi zinakosewa kwenye hili, yani unakuta ukifungua maji jikoni mtu wa chumbani hawezi kuoga, jambo kama hilo ni ghali kurebisha, inaweza kukubidi kuongeza lines za ziadi au kutumia water pump, kwa hivo uzingatie kwenye hiyo bei kabla kununua, kwenye hili la pressure ya maji ni muhimu sana hasa kama kuna water heaters, hizi zinategemea sana mskumo wa maji, hivo muhimu kuzingatiwa, hasa kama kuna bathrooms zinashare heater moja, hali kadhalika angalia ni heaters aina gani(instant au zile za kuweka maji) na ni kabila gani, kuna vitu vya kichina binafsi naogopa hata kutumia kwa kuogopa electric shock, aina maarufu nzuri kwa tanzania inaitwa ariston( sina hisa na hiyo kampuni), though siku hizi wanatengeneza china.
Vitu kama vitasa vya milangoni vyote ni vitu muhimu sana kukagua, utapeleleza asilimia kubwa ya nyumba zetu hata milango ya vyumbani haifungi vizuri au mara kwa mara unaishia kujikomelea ndani kwa ndani, vitasa vizuri vinatoka Italy ila kumbuka kuna imitations kibao. Ninachokusudia kustress hapa, usidharau kitu hata kimoja kwa kufikiria utareplace kirahisi, vifaa vya ujenzi na gharama za mafundi ziko juu sana, isotoshe nyumba ilijengwa kimaskini haiwezi kustand kuvunjwa vunjwa kuanza kurekebisha vitu kama hivo ni kutia ubovu zaidi.

Wadau waosha vinywa samahanini sana kwa kuwachosha, lengo hapa ni kuwasaidia watanzania wenzangu, naamini sio kila mtu anaelewa yote hayo when it comes to nyumba. Kama sijakuwa wazi vya kutosha hapo juu, ninachokusudia kusema bei ya nyumba inategemea itafaulu kiasi gani baada ya kuipa a thorough scrutiny, yani chunguza kila kitu then ndo ujaribu kutia thamani.
Kama nilivosema awali kwa wenye nafasi na muda nashauri wajenge, kwani kwa kufanya hivo watasaidia wengi badala ya kutoa hicho kitita kumpa mtu mmoja aende kuzilia kiti moto na bia au kuzipeleka nyumba ndogoz, basi ni vizuri kujenga na hiyo pesa itanufaisha familia nyingi za mafundi, engineers na vibarua, pia utapata kitu roho inapenda (hapa na assume kwamba una taste na macho, otherwise kama nyumba ni nyumba tu basi muda wote huo nilikuwa nampigia mbuzi guitar)! Natania tu, naamini sote tuna macho ya vitu vizuri, kwa vyovyote vile kama hutoibiwa wakati wa ujenzi siku zote kumbuka its cheaper kujenga kuliko kununua nyumba unless muuzaji anauza ili kwenda india kwa matatibabu ya transplant ya figo, in that case itakuwa unfortunate kwa muuzaji na kuna baadhi ya watu wenye utu huwa hawawezi kununua nyumba kama hiyo kwa huruma.
Namalizia na ushauri wa bure, kama utaamua kujenga nyumba basi hakikisha unafikiria uwezekano wa kuja kuuza baadae, kwa hiyo hakikisha hiyo nyumba sio inakuvutia wewe tu bali iwe inavutia in general na usifanye obvious mistakes kwenye ramani kama kujenga nyumba ya vyumba vitano na kuweka choo kimoja tu.
Nawasilisha!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Tunashukuru Mdau kwa Darasa. Binafsi nakupongeza kwa 'kushare' na sisi uzoefu na utaalamu wako katika mambo hayo muhimu sana katika ujenzi. Akijitokeza mwingine aliye na uzoefu na 'process' hiyo ya ujenzi kwa Bara, nae atueleze kuanzia kiwanja alipataje, vifaa, mafundi nk itakuwa murua!

    ReplyDelete
  2. Mdau kwanza asante saaana kwa huu ushauri..yani nimecopy and paste into a word document na kusave. Hivi ni vitu muhimu sana kwa watu tunaozingatia kujenga!! Asante sana..
    Pia ningependa kuongezea kitu kingine kimoja LOCATION!! Mara kibao nimekuwa nikifuatilia nyumba zinazo uzwa dar na za kupangisha..unakuta apartment nzuri upanga, mikocheni, masakai kuanzi $1000-3000. Lakini unaenda kunduchi. tegeta, salasala napo unakuta apartment for the same price. Sehemu zingine kama huna gari kwenda dukani shida, kituo cha polisi kipo mbali, hospitali ipo mbali, maji na umeme unakatika ovyo ovyo na usalama si wa kuaminika. Ingekuwa vyema sehemu hizi bei ishuke kutokana na essential facilities surrounding the area. Nawakilisha!

    ReplyDelete
  3. KWA KWELI MDAU TUNAKUSHUKURU SANA KWA KUTUELIMISHA KWENYE MAMBO MUHIMU KAMA HAYO

    NA NI SAWA KABISA TUNAOMBA WAHUSIKA SERIKALINI WAFATILIE KWA KARIBU UUZAJI WA VIWANJA NA UUZAJI WA VIFAA VYA UJENZI KWA KWELI WANAUWA SANA

    NA HAO WAUZAJI WA VIFAA VYA UJENZI NA WENYEWE WASAIDIWE KWENYE USHURU WA KULIPIA PINDI MIZIGO YAO INAPOFIKA BANDARINI

    KWANI WAO WAKIBANWA SANA NI LAZIMA NA WAO WATAWABANA WANUNUZI KWANI BILA KUFANYA HIVYO HAWAWEZI KUFANIKIWA..mdau uholanzi

    ReplyDelete
  4. Nampongeza huyu mdau kwa kuandika kitu ambacho "practical" kwa mazingira yetu ya Tanzania.

    Wale wengine wanasoma kwenye vitabu vilivyoandikwa kwa mazingira ya Ulaya/USA na kulazimisha Tanzania ifanane.

    Wadau wengine wenye "Ushauri wa Bure" kama huu kwenye sekta nyingine, tafadhali tupeane.

    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  5. NIMEPATA DALASA LA KUTOSHA NASHUKURU.

    ReplyDelete
  6. Thats good article.
    Mzanzibari kweli mahiri kwa ukweli.
    Tunapenda kama una article nyingine kuhusu ujenzi wa nyumba nyumbani, hata kama ni page 20, wewe tuandikie tu.
    Wewe umetupa argument na solution nzuri kabisa, tofauti kabisa hasa ukilinganisha na msomi KIONGOLI , ambaye aliandika kwa hasira.
    Wewe umeweka mambo sawa na ukweli kabisa.

    ReplyDelete
  7. safi sana,asante kwa hili.

    kama wapo ambao hawataelewa somo hili na kung`ang`ania housing market inavyoendeshwa kwa sasa. Basi tuna haki ya kuwa ignore.

    ReplyDelete
  8. Duh! this Zanzibar dude got some useful tips,got to save this stuff coz I thought I know but I´ve realize I didnt know shit about building house in TZ.One thing I´ve notice almost all materials from China and India are crap.Damn this Chinese people.I recommend other experienced people to drop their ideas here in that way the knowledge we are getting will help to stabilze the real estate market.The more we know the better.
    Mdau Helsinki

    ReplyDelete
  9. Mimi pia hakika nime-save haya maelekezo. Asante sana muandishi kwa kuchukua muda wako kutoa mwangaza na uelewa wako (inaonekana we pia ni memba wa familia bora, au mwenyewe una $$ za kutosha) Na we si fisadi -- mafisadi na watoto wao hawanaga muda wa kueleza mambo kama haya. Tunaojenga nyumbani na tuko mbali hakika tumefaidika. Nafurahi kwamba ujenzi naofanya mimi, so far ni kama nilikuwa nimesoma maelekezo haya mapema -- so far so good.

    TIP NZURI ALIYOTOA MWANDISHI, japo haikuwa moja kwa moja, ujenzi wa maana si lazima ukamilike katika miaka miwili tu. JApo wako watu wengi wanaojisifu kwa kukimbiza kimbia nyumba, na ukiangalia kazi "iliyokamilika" haiwi kwenye kiwango.

    Na wenzetu ambao mnafikiria kujenga, hii si article ya kupitia tu -- copy na kusave haya maelekezo mahala yatakuongoza ukiamua kuanza hiyo kazi.

    Asante sana

    ReplyDelete
  10. HONGERA MWANDISHI KWA ELIMU ULIYOTUPA.KWA KUSOMA TU HIYO ARTICLE UTAJUA MWANDISHI NI MTAALAM MAHIRI NA ASIYE NA CHOYO.NAKUPA PONGEZI KWA KUTUELIMISHA NA KWA MSAADA WAKO

    ReplyDelete
  11. Mkuu Hongera kwa Article nzuri namna hiyo.

    Nakubaliana na wewe mia kwa mia. Keep it up!

    ReplyDelete
  12. Yaani wewe ni mwisho huwezi kuamini umenifumbua kiasi gani!! Siku zote nilikuwa nawaza kujipanga kununua nyumba leo nimepata ufumbuzi huko sipo tena,halafu sikuchoka kusoma hata kidogo Asante sana

    ReplyDelete
  13. Tungepata watanzania kama kumi hivi, wenye moyo kama wa kwako mdau!! watanzania tungefika mbali sana. huu ni moyo wa kizalendo kukaa chini na kuwajalia wenzio kile ambacho unakijua vizuri. mungu akubaliki na tuombe watanzania wengine kwenye fani ya magari.kilimo na mazao watuelimishwe wenzao namna bora ya kuchagua bidhaa.

    ReplyDelete
  14. michuzi tunahitaji vichwa kama hivi kwenye hii blogu yetu ya jamii sio wale wanaouliza eti ukijifunika shuka moja na mkeo halafu akajamba utakuwa zezeta,JAMAA ANAJUA ANACHOKIONGEA KWA UKWELI AMENIGUSA SANA ANA MANTIKI

    ReplyDelete
  15. aise this guy is smart...wa tz tulio wengi tunakosa ufahamu/uelewa ktk mambo ya msingi kuhusu nyumba na ujenzi.na vilevile upeo wetu mdogo,utakuta mtu wazo lake ni kujenga nyumba ya vyumba vitatu atamtafuta mchoraji achoree mchoro tu.mradi kuna jiko bafu na sebule..the rest is up to mchoraji..tina sahau vitu muhimu,setting ya nyumba, kuangalia upepo(hewa) Jua lina piga wapi,varanda nk...ni vitu vidogo but vinachangia sana value ya nyumba..kununua nyumba ni headache..sababu ya kukosa test yako.kuepuka kuichukia nyumba baada ya kuhamia...anakaa unawaza hapa pangekua hivi au ingegeukia vile jua lisinge piga sebuleni au chumbani..utakuta nyumba ina joto la hatari..sio kua sehemu hiyo haupo ila setting haikuzingatia hilo.wachoraji nao hawapo profrssional, unampa wazo anakuchorea(au ana copy na kupaste) ramani akiwa ofini kwake au nyumbani anakunja hela yake basi.,site haendi.una tegemea nini hapo.? na mafundi nao wana matatizo yao...kuna mafundi washauri..watakushauri vitu vingi kama utawapa nafasi(ikibidi uliza) ,hata kama vina ongeza gharama za ujenzi..mimi ni mfano halisi..nilijenga nyumba kabla sijaezeka msingi ukapata nyufa zisizo rekebishika...namuliza fundi ana nijibu ..boss tunge weka nondo size kubwa na zege lake gharama ingekua kubwa sana...nilitamani nimmeze..hasara nilio pata haielezeki.
    na vilevile tusichukue mafundi mradi fundi..kuna wengine hawaja wahi kujenga nyumba,ni mafundi repair..umjue na akuonyeshe hata nyumba alizojenga..
    vile vile tuombe ushauri na kutembelea site na nyumba za wenzetu walio maliza au wanaendelea na ujenzi (wazoefu) utapata mawazo mapya.tusiwe wavivu kupoteza muda kuzunguka ina saidia sana kujenga nyumba nzuri yenye taste yako ambayo huta juta au kuichukia.kwani ujenzi ni ghali na time consuming.so take your time fanya tafiti kabla ..usije juta...mimi nilipata fundisho,imenisaidia sana kua mwangalifu na mdadisi.. na matokeo nimeyaona na kuyapata and am Happy and proud with the end product at last....
    =swala la location ni gumu na expensive kuchagua au kuamua kwa dar es salaam unless your rich..but few tips before buying a plot..huduma za jamii(bank,hospital,socialclubs,soko,maduka for groceries nk.)majirani(same class this is very important),usalama,shule kwa watoto (for young couples)...kwa kweli ni mateso and not healthy kwa watoto ku amshwa saa 10 au 11 alfajir ili kuwahi daladala au school bus...NAWAKILISHA BY MDARESELAMA

    ReplyDelete
  16. toka nianze soma hii blogu...sijawai ona comments positive toka ka wadau km apa leo..yan burdani kabisa kila mdau kaandika waaa

    ni kweli uyu mtu katufudisha somo me nimecopy hii article now ntajenga kwa umakini maana nilishawaza duh ntaanzaje?vitu vingi ni wizi mtupu sasa sijui tumwamini nani kununua vifaa na wapi angalau ni genuine?

    tupeni madesa zaidi watu msio na choyo!km uyu mzenji

    ReplyDelete
  17. Asante sana kaka! umetufungua macho sana! ungetupa na majina ya maduka ungetusaidia zaidi!

    ReplyDelete
  18. Habari zenu wakuu,

    Nawashkuruni sana kwa kuipokea makala yangu vizuri, nilikuwa na wasi wasi sana ningewachosha kutokana na kubwa wake, sina uzoefu na skills zozote za uandishi hivi sikujua jinsi nzuri ya kupresent hii mada, ila namshkuru Mungu mmenielewa na kuipokea vyema. Nililenga zaidi kwa wanaotaka kununua vyumba kuliko wale watakao amua kujenga weneyewe. Kwa kweli kiasi fulani nimepata uzoefu wa kutosha kwenye maswala ya ujenzi hadi nimejuta kwanini sikuamua kusomea field hiyo. Hata hivo niliweza kumshawisho mdogo wangu wa kike na mwaka 2007 alijiunga chuo marekani kusoma architecture na baadae walishauri abadilishe na sasa asomea civil engineering, muombeeni dua afanikiwe.

    Sasa ilikuiboresha hii makala ifae kwa wale wanajenga wenyewe, nahisi kidogo nimekwenda overboard na nimeishia kueleweka kila kitu cha kichina ni kibaya. Hapana china pia kuna vifaa vizuri ambavyo kidogo vitakuwa affordable kwa mtanzania wa kawaida. Istoshe hata sisi wa huku ughaibuni, at least huku Canada niliko tunaielewa products nyingi tunatumia huku ukigeuza ni made in china vile vile.

    Sasa ukipata fundi mzuri anaweza kukusaidia kifaa gani ni kizuri kulikana na uzoefu wake, hivo jaribu kujikuna unapojipata, afterall kuna mambo ya msingi na mambo ya mapambo hivo unaweza kujikita ukatumia hela zaidi kwenye mambo structural na kwenye urembo ukabana kidogo.

    Kuna tiles nzuri tu kutoka china au india. Hali kadhalika hata hizo nondo za tanzania nilisema mbaya, kwa nyumba ya chini unaweza kutumia ila usianze ubahili wa kuweka mmoja au badala ya 12mm ukaweka 10. Sisi katika ujenzi wetu tulitoa ramani kwenye vitabu vya ramani kuta customize na kumpa mchoraji aweeke vipimo tu. Then tukaenda nae hadi structure kukamilika tukaachana nae, hawa watu wanaringa na utaalamu wao na unaweza kumaliza hiyo hela yote kwa kulipa engineer asiepita site kabisa, kwa hiyo kama alivosema mchangiaji mmoja ni vizuri uhakikishe unatafuta mfundi mzuri na hakikisha anakuonesha kazi yake iliyomalizika ndio umpe hiyo tenda ya kukujengea.

    Unahitahi kuwa makini sana na walizi wa site na mafundi kwa ujumla uaminifu nyumbani bado tatizo binafsi tumeibiwa sana katika ujenzi vifaa amounting to tshs. milioni 5, vitu kama cement, tiles, nondo, mbao, roofing tiles wanavipenda sana. Jengine baadhi ya sehemu unaweza kufikiria other flooring options kama yale mawe ya urembo yanayotoka Tanga, binafsi katika ujenzi wetu nilienda tanga mara mbili kule kijiji cha Doda kufata hayo mawe, nilinunua mawe karibu milioni 3, enzi hizo niliweza kupata mafuso 3. Nimesikia rumors eti kumepewa mzungu ndio anachimba hivo yamekuwa ghali sana sijui kama kuna ukweli.

    Location, yeah nimehimu sana inabidi uweze kucompromise unaweza kusacrifice nini upate nini, istoshe na mfuko wako, sehemu za karibu na mjini bei za plots ziko juu sana wachache sana wanaweza kumiliki. pia nimekumbuka pointi mmoja kwa wale wanaofikiria kununua nyumba, wengi wetu tuna desturi ya kuweka concrete kwenye compounds zetu, sasa kama mpenzi wa bustani unataka kununua nyumba na 2 thirds ya compound imewekwa cement utapanda majani wapi. Na kwa wanaojenga sasa wazingatie hilo bustari nayo ni muhimu sana.

    Kwa wale, wanafikiria kujenga majiko ya kisasa, yale yenye makabati na counter space, hapa inabidi utafute mtu akusaidia kuna kanuni zake za kuzingatia sio kila fundi mbao anaweza kujenga. Lazima uzingatie vipimo yasiwe marefu sana, na yale ya juu usiweke juu sana mama hatapatia na pia watoto wanaomsaidia jikoni.

    Nimeandika makala nyengine ya uchambuzi wa wizi wa airport na ufisadi mwengine kwa ujumla tayari nimemtumia mkuu kaka michuzi ila nadhani ana posti nyingi huenda ataitoa siku za mbele ukizingatia ni ndefu zaidi ya hii. Nawatakieni kila la heri katika ujenzi. Kuna mdau alichangia akaeleza makala yangu inaashiria natoka familia bora, hapana ni kawaida tu hata hivo namshkuru sana Mungu nasilalamiki, na naweza kujitapa familia yangu si fisadi kwa hiyo hela tumejengea haijatoka serikalini wala sisi si wafanyabiashara. By the way, Ahmed sio jina langu halisi ni alias tu!

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  19. Ahsante sana mdau, ushauri wako umetufumbua macho, hasa sisi walala hoi tunaochanga changa hel zetu za box ili tujenge vibanda baadaye huko home. Mimi kama usingesema, nafikiri ningevamia vifaa vya china kwa urahisi, kumbe changa la mato! ahsante sana na mungu akubariki.

    ReplyDelete
  20. Hata mimi nilisoma yote...then niaakaamua ku copy for future use...nikasema je wenzangu wamaichukuaje...niakfungua maoni...nikiogopa wataku demoralize....thanks god....wote tumeelewa somo sawasawa....god bless yu my friend nad the one who owne this blogg.be blessed.

    ReplyDelete
  21. Asante sana kwa ushauri wako mzuri. Mie pia nimekuwa nikijenga nyumbani.. nimekuwa nikisimamia mwenyewe niendapo 4wks holiday kila mwaka. Na mwaka huu Mungu kanijalia nimemaliza ujenzi. Engineer wangu alinishauri ninunue vitu vya finishing hapa UK.. nimenunua kuanzia mabomba hadi nyaya za umeme toka hapa UK zenye British standard.. Pia tiles hadi grout hapa UK nakusafirisha Tanzania via Mombasa. Kwa hakika nyumba imependeza sana na value yake sio mchezo.
    Tatizo la nyumbani hata hilo kitchen sink wanalosema stainless still ukitafuta gauge/quality yake haijaandikwa nyuma ya sink. Yani kila kitu kipo kipo tu..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...