Godfrey(shoto) Donald Malunda(kulia). walipokula nondozzz zao IMF dar. hwa wadau wamefanya kila kitu pamoja, hata kumeremeta walimeremeta pamoja na ni waimbaji wazuri sana wa kwaya kanisani na kuna wakati walikuwa na Carolla Kinasha na Shada band

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Ni IMF au IFM? Vipi saumu hiyo au...

    ReplyDelete
  2. Nafikiri ni Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na sio Shirika la Fedha Duniani (IMF). Pole sana.

    ReplyDelete
  3. Asante binamu ulietangulia hapo juu,ni IFM(Institute of Finance Management)Bila shaka naniii saumu ilikuwa kali kidogo.All in all hongereni nyie mapacha mmefanana kama mayai bwana.Vizuri sanaa.Simika J.

    ReplyDelete
  4. cku hizi dar kuna chuo kipya cha IMF??

    ReplyDelete
  5. Nwawakumbuka hawa jamaa nilisoma nao Tuition kwa Njowoka pale ilala that was in Primary school.Congraturation you guys big up and God Bless.

    ReplyDelete
  6. nadhani hatuna chuo cha IMF tanzania kote hii itakuwa IFM kabisaa!!!

    ReplyDelete
  7. Hongera zao. Kilichobaki sana wakatafute kazi shirika moja wafanye pamoja.

    ReplyDelete
  8. KWELI, kuna tofauti:-

    IMF-International Monetary Fund (Shirika la Fedha duniani).


    IFM - Institute of Finance Management (CHUO, DAR).

    ReplyDelete
  9. International Monetary Fund=IMF address 700 19th Street, N.W., Washington, D.C. 20431.U.S.A. (www.imf.org)
    Institute of Financial Management=IFM address Shaaban Robert Street,P.O.Box 3918, Dar es Salaam, Tanzania. (www.ifm.ac.tz)

    ReplyDelete
  10. hv we michuzi mbona unapenda kutuvuruga jamaniii? hapo ni IFM bwama sio IMF acha mbo yako broo bwana halafu naomba utafute habari za wale ndugu waliokufa jana saa 11 alfajiri pale palm beach story yao inasikitisha sana maana kati ya hao marehemu kuna mtu na mchumba wake.naomba utuhabarishe vizuri plz

    ReplyDelete
  11. Siku hizi kuna nondo za IMF?

    Au unamaanisha IFM! Michuzi usituchanganye hapa. Hamna Kozi ya IMF dunia hii!

    Guys nawapeni hongera na mzidi kumtumikia bwana yesu!
    Mungu awazidishie maisha marefu mema.

    ReplyDelete
  12. Nadhani "mouce" imeteleza wakati wa kuandika, kwa sababu amesema IMF DAR atakuwa na maana IFM DAR ambayo ni Institute of Financial Management (IFM) ambacho kiko Dar es Salaam.

    ReplyDelete
  13. Bwana Misupi kweli unazeeka,au saumu kali. Is it IMF or IFM?

    ReplyDelete
  14. Wazazi wenu lazima watakuwa wenye furaha sana juu yenu. Nna mapacha waliofanana kama chupa za fanta. NAWATAKIENI KHERI nanyi mniombee hawa wangu wafikie hatua mlofikia. MAY GOD BLESS YOU BOTH.

    Baba B na B-kijitonyama

    ReplyDelete
  15. kichwa kinauma mimi ona huku nako IFM x IMF kule WALINZI x WAPAMBE, kwingineko WAALIMU x WALIMU x SAALAMU + SALAMU...hivi huu u hovyo hovyo wa kiswahili ni kwa nini wadau wapenzi...kwi kwi kwi siyo siri mnafurahisha, kuliwaza na kuburudisha, Michu kaka blogu hii IDUMUUUUUUUUUUU.........

    ReplyDelete
  16. Wazee congrats!!

    ReplyDelete
  17. Hawa jamaa nimemaliza nao IMF, ohh soorryy IFM hiyo picha hapo ilikuwa mwaka 2005 siku ya graduation.
    Hawa jamaa kweli ni mapacha manake;
    1. Hawajawahi kutengana tangu vidudu hadi chuo, na walikuwa wanasoma darasa moja.

    2. Chuoni wamesoma kozi moja(IT) darasa moja na wamemaliza pamoja. Na matokeo yao yanafanana, hata O -level na A-Level matokeo yao yalifanana.

    3. Wameoa siku moja na wake zao majina yao yanafanana lakini sio mapacha. Mmoja anaitwa Neema na mwingine anaitwa Grace.

    4. Wanafanya kazi kwenye mashirika yanayofanana, mmoja yuko National Health Insurance Fund na mwingine Public Service Pension Fund

    5. Wana magari yanayofanana maumbo(Body Type) mmoja ana Toyota Ipsum na mwingine ana Toyota Gaia

    Duh!! hawa jamaa ni mapacha haswaaaaa!!!!

    ReplyDelete
  18. haya! hongereni but hawajafanana kiivyo!!!!!! maana hofu inakuwaga ni wale wadau wao kuwachanganya tehe tehe.

    ReplyDelete
  19. - wadau, baada ya kurekebisha mengine meengi mmeshindwa kuona 'kwikwi' ya wazi ya mkuu wa nanihii..kiswahili sanifu ni 'pacha'..'mapacha' ni muhali!..

    ReplyDelete
  20. hata GPA zao zi sawa?

    ReplyDelete
  21. nawajua hao jamaa, ni wajukuu wa nkoma kama sikosei

    ReplyDelete
  22. mdau aliyetoa historia yao kwa kifupi hapo juu amenifurahisha, i believe mama yao yuko so proud na wao. may God bless them kwakweli.

    ReplyDelete
  23. Godfrey and Donald,

    Congrats to hear that you guys are married.

    I remember these guys since Shabaan Robert Sec. School - they loved to sing - they would sing on assembly days - food evening, Talent nights and whenever they get a chance. Their bass was Lewis - my classmate.

    And we hanged out on samora road alot - they were living there not sure if it is still the same. I hope just from my writing they would guess who wrote it. Hey Ronald and Godfrey we use to talk like Mr. Tendewa. Remember.

    Guys - give me your emails.

    Mdau - Wichita, Kansas.

    ReplyDelete
  24. MDAU ULIYETOA HISTORIA HAPO JUU ITAKUWAJE MAJINA YA WAKE ZAO YAFANANE HALAFU MMOJA AITWE GRACE NA MWINGINE AITWE NEEMA. SEMA MAANA ZA MAJINA YAO NI SAWA. TENA ACHA KUSEMA MAMBO YA WATU KIHIVYO HUKO NI KUJIPENDEKEZA NA SOMETIMES WATU WENGINE HAWAPENDI. KWANI KUWAJUA HAO NI SIFA SANA AU. kuna mengine mengi bado huyajui kwa taarifa yako. na ungeandika jina lako uone kama wangekusifia.

    ReplyDelete
  25. Wewe Anonymous wa Tarehe Thu Aug 27, 09:31:00 AM,ACHA DONGE!! Mdau aliyetoa historia mbona kaelezea mambo ya kawaida sana!!!hivi wewe mtu kutaja jina la mkeo ni siri?? mtu kutaja unafanya kazi kamouni flani ni siri??tena kampuni halali au serikali inayohudumia wananchi!!Hebu niambie katika vyote alivyotaja mdau ni kipi unaona ni siri??Watu wengine bwana sijui wakoje, "MIGUBU" tu inawasumbua

    KT Wa Gongo La Mboto

    ReplyDelete
  26. WANAICHI WA MTAANI HATA KAMA HUJUI KUOSOMA NA UNA UWEZO WA KUFIKISHA UJUMBE WAKO AU MAONI YATAKAYOWEZA KUBADILI MAISHA YA MWANADAMU KWA NJIA YEYOTE UNIVERSAL VIRTUE UNIVERSITY( THE WORLD SUPER SOLVENT UNIVERSITY) ITAKUPATIA DEGREE KWA MCHANGO WAKO MAMBO YAMESHAISHA KAENI MIKAO YA KULA HASA WALE WANAVIJJI AMBAO KAMA BILA KUHAKKIKISHA INTERNET IN EVERY 10 HOUSEHOLD PROGRAM BY 2065 UNAFANIKIWA KWA NCHI NZIMA NDIYO MAMBO YATAENDA VIZURI. BAHATI MBA YA WENYE UJUMBE HUU HAWATAWEZA KUUPATA.ILA WAZEE WA MISSION TOWN NA WANYONYA NCHI WALIO MIJI MIKUU KAMA DODOMA NA MINGINE NDIO WATASOMA NA HAWATAKI WANANCHI WAPATE HII HUDUMA BURE KWA KUJIFANYA NI WAJASIRAMALI.
    TUMAINI GEOFREY TEMU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...