Michu eeeeehh...
Habari za swaumu yakhe!!
Wakati mwingine uchokozi unauanza weye na sisi waoshavinywa tupo gado tutavisuuza tu vinywa japo mfungo .. nimiona hili niliseme kuhusu "tovuti ya wananchi"
Nimeona Libeneke la tovuti ya wananchi – “kila mwananchi aweze kutuma maoni yake” .. Hakika hii ni hatua kubwa sana ya mendeleo ki-mtandao!!! … Lakini haya ni ya kweli? Hivi ni watanzania wangapi sasa wanapata mtandao ambao unawawezesha kutumuia tovuti hii? Ni wakati gani palifanywa uchunguzi (research) na tukapata japo taarifa ambayo imetusaidia “serikali” kuanzisha tovuti kama swala mbadala wa wahesimiwa wetu watukufu sana – WABUNGE -?
Maana inaonyesha kwamba labda palikuwa ama pana ka-uzembe fulani hivi mpaka ikaonekana kwamba labda njia ya tovuti italeta masikio ya serikali karibu na wananchi!
Hakika mimi siyapingi asilani maendeleo haya ya utumiaji wa mtandao ila badala ya kupata uvumbuzi wa swala zima ni vipi tumekwenda na kufikia hapa ninapata maswali mengi tuu ambayo majibu yake labda yanaweza kupatikana kutoka kwa wadau wengine – Nilitaraji kwamba kabla hatujafika huko basi pangelikuwepo na mkakati mkubwa wa makusudi kabisa wa kuelimisha watanzania wote wa ngazi zote ndani ya jamii kuhusu mawasiliano ya mtandao na vile vile serikali kujenga vituo vingi vya kufundisha na kutoa huduma za mtandao.
Hakika mimi siyapingi asilani maendeleo haya ya utumiaji wa mtandao ila badala ya kupata uvumbuzi wa swala zima ni vipi tumekwenda na kufikia hapa ninapata maswali mengi tuu ambayo majibu yake labda yanaweza kupatikana kutoka kwa wadau wengine – Nilitaraji kwamba kabla hatujafika huko basi pangelikuwepo na mkakati mkubwa wa makusudi kabisa wa kuelimisha watanzania wote wa ngazi zote ndani ya jamii kuhusu mawasiliano ya mtandao na vile vile serikali kujenga vituo vingi vya kufundisha na kutoa huduma za mtandao.
Ninafahamu wapo watu watasema kwamba kwa namna moja ama nyingine serikali imejaribu kufanya hivyo na kutoa mfano kama vile wa kille kituo cha mawasiliano cha Sengerema.!! Swadakta, lakini kituo hiki kwa upande mkubwa ni kutoa huduma (kwa malipo) an siyo kutoa mafunzo ambayo yangetegemewa kuwa ya bure maana serikali inawajibika kuwa –empower – watu wake na –knowledge – ya kutumia mtandao –
Mifano hai ipo - Jumuiya ya Ulaya (EU) wao walikuwa na mkakati kabammbe ambao ulitengewa muda na fungu maalum kwa ajili ya kuwafundisha na kuwahamasisha watu wa jumuiya hiyo kuhusu matumizi ya mtandao na mkakati huu ulitambua mgawanyo wa mafungu kadhaa ya ufundishaji yaani palikuwa na watoto, watu wazima na wazee.
Makundi yote haya yalifanyiwa – research – ili kuweza kupata dondoo ambazo zitaonyesha mahitaji na matatizo ya walengwa – Ni kweli kwamba uelewa na mahitaji ya kutumia mtandao kwa vijana ukilinganisha na mtu mzima ama mzee (senior citizen) kuna tofauti kubwa tu.
Sasa sisi tulifanya wapi hata kwa mfano kufahamu kwamba yule mganga wa kienyeji na familia yake uliyekwenda watembelea hivi karibuni kule ROCKCITY - Mwanza naye anaweza kutumia mtandao, ama hata wazee wa Bagamaoyo wanawezaje kutumia mtandao kutoa kero za wingi wa mahoteli ya kitalii Ama ni namna gani huduma zingeboreshwa basi hata wao na mamsapu wao wakaenda kusheherekea miaka 50 ya ndoa zao?
Haya na mengine mengi bado ni kitendawili na bado tovuti yetu hii ya wananchi ina kazi kubwa ya kutuelimisha kabla ya hata hatujatoa maoni kwamba inafaa ama haifai ama imetuongezea mzigo zaidi na kutufanya tuwe mbali na wawakilishi wetu waheshimiwa sana – WABUNGE - !! Vile vile kwa nafasi ninaomab kusikia mchango wa waheshimiwa - WABUNGE – kwamba vipi hii tovuti imewaongezea ufanisi wa kazi yao ya uwakilishi ama imepunguza kasi zao za kuchangia hoja Bungeni?
Tukimaliza kuelimishwa kuhusu utumiaji wa mtandao basi sasa tutakuja ngwe ya pile ya kutizama kama kweli tovuti ina – CONTENTS – ambazo zitatufanya tuitumie kikamilifu. Maana sasa hivi ukienda kwenye tovuti hii kuna mambo mengi tu ya kuyaangalia na kujadili ili kuiboresha.
Hivi sasa tovuti bado haijalenga mtazamo wa kundi kubwa la wananchi ambao wangekuwa wachangiaji muhimu, nina hakika blogspot za Tanzania kama vile hii ya mkuu wa nanihii zimeipuku kwa mbali sana hii tovuti ya wananchi - Kila la kheri ninawakilisha – Mdau - dRU


Nichokoze mada kwa upande wa pili wa shilingi.
ReplyDeleteMwanzo siku zote huwa mgumu. Kwa sasa hivi matatizo yetu mengi yako bayana. Hatuna hospitali, shule, barabara, matabibu, walimu, wauguzi nk nk. Hatuhitaji teknohama au tovuti ya wananchi kutambua kero hizo. Kupanga ni kuchagua. Je, tununue vitanda kwa ajili ya wodi ya wazazi au kufundisha wananchi jinsi ya kutumia tovuti mpya?
Jamani Mimi hata sikielewi kilicho andikwa
ReplyDeleteGet to the point. Swaumu kali au ni jua kali?
ReplyDeletemie mwenyewe sielewi panga ,mawazo yako vizuri muosha kinywa nielewe hasa wasema nini!!!!
ReplyDelete