Mzee wa Libeneke,
kaka michuzi,
pole na shughuli za kujenga taifa pamoja na pilika pilika za kumtafuta mlimbwende. Mimi nina maswali mawili ya kizushi tu, ambayo ningependa wadau wanisaidie kutafuta majibu yake. Ila Michuzi, ukilibania swali langu pia hakuna shida Mungu akubariki tu, usinibague kwa kuwa mimi ni mdada.
Swali la kwanza, nashangaa sana kuona kwamba, watanzania tunashabikia vitu kama harusi na tunatoa michango lukuku. Mashindano ya umiss, mpira na kujiachia hasa anapokuja msanii toka nje, unakuta mara nyingi yanapata wadhamini wengi wanaojikita na hela za kumwaga ilhali inapokuja kwenye maswala ya kijamii utendaji Zero.
Tunajaribu kubomoa kila chema wenzetu wanachojitahidi kujenga ilhali tuna ushabiki mkubwa kwenye upuuzi Maalbino wanauwawa, na badhi yao hapa mjini hawana hata chakula, kwani hawawezi kufanya kazi vizuri wakihofia maisha yao lakini hakuna kabisa wa kuwasaidia. Haya makampuni ya kinafiki yanayotoa udhamini, mbona yasidhamini vya maana? Mashuleni kuna vijana wanakosa hata karo, lakini hakuna hata kampuni inayoweza kujitolea kuwalipia hata karo ya mwaka.
Hapa kwenye blogu ya jamii, kuna vijana wenye uwezo sana wanaotuelemisha kwa kima cha juu sana; hususan Dr. Shayo na Jonh Mashaka ambao wanaandika vitu vya maana kweli kweli, lakini mara nyingi waosha vinywa kazi zao ni kuwaponda.
Ni kwa nini tusiungane na vijana kama hawa ili kulijenga taifa letu au kutafuta namna ya kusuluhisha matatizo yetu? Swali langu watanzania wenzangu akili zetu ziko wapi, kwa nini chetu kikubwa ni kuona wengine wanashindwa maishani badala ya kuwa sapoti?
Mdau Mla vumbi
UDSM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Hey mdau,Una swali zuri japo nilifikiri ni maswali.Kumbuka kuwa waTanzania ni watu walio na uwezo na upeo wa kufanya mambo mengi sana lakini nchini hakuna ukweli bali ni unafiki mtupu.
    Mfano watu wengi huibuka na mambo mengi ya maendeleo yanapofika serekalini huwa ni swala la serikali na kuwekewafungu ambalo halito elekezwa katika maombi.
    Sasa basi imefika wakati watu wamechoka na kuamua kuishi leo si kesho tena,Kwa maana ya kwamba kama kutakuwa na hayo mambo watakayo ona afadhali kuliko kupata story.
    Kulegalega kwingi kunatokana na kizazi cha nyoka kilicho madarakani.Hakuna watu wenye uzalendo na ukiwa mzalendo hupewi nafasi haswa kipindi cha kibonge Ukapa/Mkapa.kiufupi tu ila kuwa uyaone.-D

    ReplyDelete
  2. WAOSHA VINYWA WAPO DUNIANI KOTE, NA ILI KUANIKIWA MALENGO YAKO USITISHIKE NA WANAPOOSHA VINYWA VYAO, NITAKUPA MFANO HAI, HUYU KIONGOZI WA VIRGIN WAKATI ANATAKA KUANZISHA SHIRIKA LA NDEGE LA VIRGIN RAFIKI YAKE AKASEMA AA WAPI HUTAWEZA NDIO UTAKUJA KUFILISIKA TU, LAKINI YEYE AKASEMA NITAANZISHA TU, NDIPO RAFIKI YAKE AKATOA BAADHI YA SHARE ZAKE AKIAMINI MMILIKI WA VIRGIN HATA FANIKIWA. NA ALIPO FANIKIWA ALISHANGAA. NA VIVYO HIVYO MAISHANI HUWEZI KUWAKWEPA WAOSHA VINYWA WATAENDELEA KUOSHA VINYWA VYA KILA SIKU. ILA WEWE WEKA NIA NA UTAFANIKIWA TU HATA KAMA WATASEMA HAIWEZEKANI SI BURE ANA KIZIZI ILA UTAFANIKIWA TU.

    ReplyDelete
  3. Tumekupata dada. Vipi wewe umewahi kufanya nini kuokoa jamii au hata wewe ni wale wale? Usije ukasema mimi ni mwanafunzi na hivyo siwezi kufanya kitu, mbona akina Sarafina wa kwenye movie walifanya makubwa wakati wao walikuwa bado ni wanafunzi?

    ReplyDelete
  4. watanzania tunapenda sifa kwa mambo ya kipumbavu,ulikuwa hulijui?ichi yetu inamambo mengi yanayohitajika kufanyikana pesa si kama hakuna,ILA hatujui nini maana ya PRIORITIES,na kibaya zaidi VASCO DAGAMA anasafiri kila kukicha hata ziara zisizo na kichwa wala mguu.michuzi mwana mi sitoshangaa ukibana comment bt u know what am talking about.thanx

    ReplyDelete
  5. udhamini ni biashara dada watu wanadhamini and they get returns on it. social issues kama hizo unazozungumzia have no returns and hence the incentive to allocate precious resources to them is almost non-existent. wewe kama msomi ningetegemea uwe unaelewa hilo. common sense should override your sentiments....

    ReplyDelete
  6. Ni kweli huu ulimbukeni tusipo angalia tutazikwa nao.Itakuwa aibu kuona wasoma wengi walio na gpa nzuri watashindwa kuchimbia kaburi hili.

    Tunahitaji kutambua kuwa tunaweza kabisa badili jamii hata bila kushirikisaha selikari hii ya silikari. Hata waliofanikisha njia za kupata uhuru walikuwa na mawazao kaa ya huyu mdada na wakaungana na kuokoa wazazi wetu ambao wamesha kata tamaa za maaendeleo.

    Mfano mzuri ujana wangu enzi hizo kulikuwa na camp nzuri za vijana zikaitwa kama mlalakuwa camp, camp hizi sifichi zilikuwa na kujifunza kutanua kuliko camp jirani hazikufikisha kokote vijana. Hata kama makundi mengine yazilsha wasanii waleo lakini bado tu kubwa la kubadilika. Itapendaza sana tukitumia makundi haya kuelimisha jamii kama juu kuatua matatizo yetu bila kusubili serikali. Njia hii itasaidia sana kukukza vijana wanaojituma na watakuwa viongozi bora wa baadae.

    Ona leo taratibu wanakijiji cha fotobaraza wanaonesha mvuto kwa jamii kueleimishana na kutenda yale wanayopata toka kwa wenzao. Wamefikia hata kuwa na foundation yao ili iweze saidia jamii.
    Jamani kubadili nako sio kunasubuli Yesu arudi ni kuamua tu.

    Mungau atusadie tuamua uamuzi uliowa busara.

    ReplyDelete
  7. ulipoweka shayo na mashaka wa trime basi wtu watachafua hewa muda si mrefu wala wewe si mpigwa vumbi nishakudhaminisha saa nyingi wewe ni mbeba mbox na mosha vinywa,usijali sana sijui kaka au dada mtabaki kutafuna kumeza mhawezi nchi yetu ni fisadi kwa warembo,na luxury zote in generaly ili tuonekane lakini haya yote ni mapito tu maana maskini hafilisiki,tajiri.......
    k'zoo concorde michigan

    ReplyDelete
  8. Nakuunga sana mkono mdau wa udsm,ndio maan upo udsm,Mungu akubariki sana,ipo siku utasidia watu.Hata mimi nilikuwa na mawazo kama yako,siku moja nili tazama dvd ya Felix Wazekwa alipokuwa bongo,damn!kuna ma pedejee walimwaga hela sana kwa bendi nzima ni noti za elfu kumi kumi zilikuwa kama karatasi,nikajiuliza huyu jamaa si angepeleka shule ile niliyoina kwenye blog nilisikitika sana.Siwezi kujenga shule lakini nimevisha wengi,tena watu ambao siwafahamu,peleka vitu kwenye donation Mungu atakubariki badala ya kutumia kwa starehe tu.

    ReplyDelete
  9. wewe mla vumbi naomba usuluhishe matatizo ya nyumbani kwenu kwanza ndo ukishamaliza usuluhishe matatizo ya jamii....mtu utalisha vipi wenzio kabla wewe hujala?

    mdau mbeba box original,
    Washington DC

    ReplyDelete
  10. UNAJUA DADA MLA VUMBI UDSM WATANZANIA WAMESHOSHWA NA UNAFIKI NA UFISADI ULIOKUBUHU MIONGONI MWA BAADHI YA WALIOPEWA DHAMANA NA WALIPAKODI KUSIMAMIA NA KUONGOZA NCHI YETU TANZANIA. KUOSHA VINYWA NI NJIA MOJAWAPO INAYOSAIDIA KUPUNGUZA 'STRESS'..

    ReplyDelete
  11. Mgonela FOTO BARAZAAugust 09, 2009

    POLE SANA KWA JINA ULILO JIIITA (mla vumbi)HAKIKA KAMA MICHUZI ANGELIBANIA INGEBIDI AFUNGE MWEZI MTUKUFU NA TOBA YA NGUVU.BINADAMU WAKO TOFAUTI KWA KILA KITU UNAPOKUWA NA JAMBO LAKO WEWE LITEKELEZE TUU NA WENGI HASWA WATANZANIA WAMESHACHOKA KINAFSI KUTOKANA NA MWENENDO MZIMA WA UONGOZI JEMA KWAO OVU OVU KWAO JEMA KWA WA WENYEWE NA HAWA UNAWAONA WANAFADHILI MAMBO FULANI WANA HAKI YAKO NA SI LAZIMA WAFUATE ULICHOKIONA WEWE MUNGU AKIKUBARIKI FATA UTUMBO WAKO NINI UNATAKA UNA HAKI YA KUSHAULI NA KUBALIANA NAWE LAKINI ANGALIA UPANDE WA PILI PAKOJE?

    ReplyDelete
  12. KWELI NDIO MAANA KENYA WANATITA TANZANIA MAGOIGOI! HIVI UNASEMA TANZANIA TUMECHOSHWA NA UNAFIKI WA MAFISADI? MIMI NAFIKIRI WATANZANIA SISI WENYEWE NDIO WANAFIKI NA MAFISADI NAMBA MOJA! WEKA UIANO MZURI WA WABUNGE PALE MJENGONI UONE KAMA WATU HAWATAIKIMBIA NCHI HII!

    ReplyDelete
  13. Umaenza vizuri kuandika; lakini umeharibu baada ya kuwaingiza Mashaka na Shayo. Unapoandika focus na point zaidi zako na si kuwaambia watu wawasikilize Mashaka na Shayo.

    ReplyDelete
  14. Mdogo wangu umeongea vizuri.Hebu jiulize kwanza kwa nini kibaka wa mtaani aliyekamatwa kwa kuiba chakula anachomwa moto wakati fisadi aliyeliingizia taifa hasara ya mabilioni anapeta?Kwanini mtoto wa shule ya msingi akiongea kiingereza kwenye dalala anashambuliwa na watu wazima kwa
    maneno kama "kila mtu anajua kiingereza"kila mtu amesoma"
    "msijifanye wazungu" "brokeni english nk.Matokeo yake watoo hawa
    wanakosa confidence na kuelewa kuwa
    speaking english in public is a
    crime.Wakimaliza kupiga vumbi UDSM
    wanakutana na ushindani katika
    makampuni ya wageni na kukosa kazi
    maana wanaandika good english lakini kuongea ulimi mzito.Hapo akitokea high school graduate toka
    kenya anakuwa bosi wako kwavile
    akitumwa Ulayamerika atafikisha
    ujumbe na kuleta majibu siyo tu kwa
    kuandika bali hata kuongea vizuri.
    Tatizo hili litaeendelea mpaka
    tutakapofiki level ya wajapan au
    Wachina ambao lugha zao zinazungu-
    mzwa na wawekezaji toka nje.Sasa mdogo wangu ukimaliza UDSM na kuamini kuwa education is the
    tranformation from backwardness to
    betterment,wewe na wenzako leteni
    mabadiliko japo kidogo hata kwenye
    familia zenu.Kama mchaga muuza duka mtaani kwenu ambaye hakumaliza
    darasa la saba shuleni Sanya juu
    pato lake ni kubwa kuliko lakwako
    basi kubali kuwa amekuzidi elimu.Kuwa agressive usisubiri kupata kazi ofisini au kuchangiwa ili kubadilisha maisha yako.Weka vyeti vyako kabatini vaa jeans, boots na kofia ya mkeka panda basi
    nenda Singida kalete matenga ya kuku uuze barabarani Dar na siyo kusubiri title za akina Makweta
    waliyokuwa madarakani toka wakati
    sijazaliwa mpaka nilipomaliza masters.Ukiwa icon katika jamii yako wadogozako watafuata na Tanzania ita-move foward.
    Toto tundu, Upper Marlboro

    ReplyDelete
  15. Muswaili iko kama ile debe ambayo hakuna kitu ndani,natoa kisindo kali sana tena nawesa tisa mutu.baadae nakuta hamna kitu.
    Kiswaili murefu kumbe iko nataka ibia kitu.
    hii habari ya kila siku miss ilala, temeke miss shoga hawesi leta maendeleo wala fikisa nyie mbele.wisi toka pande ya juu paka pande ya chini, chapa kasi sio maneno maneno tu.

    ReplyDelete
  16. Ukishiba vumbi utaelewa baada ya dhiki faraja.

    Udhamini ni kazi siyo mgawo.

    ReplyDelete
  17. Hili swali limeulizwa na mwanafunzi wa mwaka wa ngapi?

    ReplyDelete
  18. Dada nakuunga mkono kuhusu umuhimu wa kusaidia ila kumbuka kutoa ni moyo si kulazimishana. Wewe binafsi Mungu akikujalia kupata chochote uwasaidie utakao weza kwa jinsi hio utakuwa umetatua matatizo ya japo mtu mmoja au wawili.. kulingana na uwezo wako. Wapo watu wanasaidia sana watu pale wanapoweza. Ukifanya uchunguzi unaweza kufahamu hilo, mfano kuna watu wanasaidia watoto kielimu na katika mahitaji mengine. Ila ni vitu binafsi kufuatana na moyo wa mtu anavyosikia wito wa kusaidia.

    ReplyDelete
  19. DADA kunawatu wapo huku lakını shuleless kwahıyo usıone mtu anaandıka yupo washgton au ıstanbul ukaona ameendelea kımawazo.kazıyao kukatısha tamaa

    ReplyDelete
  20. Congrats mdada UDSM.Hopefully, you
    will graduate with distinction
    honor and accomplish a significant
    change in our society.Sponsorship
    can sometimes be investiment
    commercialwise where by some money
    could be donated hoping for a big return in a long term to the doner
    but for receipients is up to the air.Whom one to assist and otherwise depends on how much profit earned or expected.I'd like to respond to anonymous of Sunday Aug 09,11:53 who instead of embarking on a contructive debate
    imply attacked uneducated Tanzanians particularly residing in
    DC.Respect people,agree to dessagree.You will never here NBA
    players attacked Kobe Bryant or
    LeBron James simply because they
    never been to college.I specifically cited that example to
    demonstate no matter what level of
    education an individual may have,
    they can be good players to
    accomplishing a positive impact
    that would positively change so many lives in the society.Attacking
    uneducated I dont think is the right stretergy.If you're educated
    be humble,confident with no eagle
    and try to make this world a better
    place to live.Peace
    Izzo Fashizzo(uneducated)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...