Mzee wa Libeneke,
kaka michuzi,
pole na shughuli za kujenga taifa pamoja na pilika pilika za kumtafuta mlimbwende. Mimi nina maswali mawili ya kizushi tu, ambayo ningependa wadau wanisaidie kutafuta majibu yake. Ila Michuzi, ukilibania swali langu pia hakuna shida Mungu akubariki tu, usinibague kwa kuwa mimi ni mdada.
Swali la kwanza, nashangaa sana kuona kwamba, watanzania tunashabikia vitu kama harusi na tunatoa michango lukuku. Mashindano ya umiss, mpira na kujiachia hasa anapokuja msanii toka nje, unakuta mara nyingi yanapata wadhamini wengi wanaojikita na hela za kumwaga ilhali inapokuja kwenye maswala ya kijamii utendaji Zero.
Tunajaribu kubomoa kila chema wenzetu wanachojitahidi kujenga ilhali tuna ushabiki mkubwa kwenye upuuzi Maalbino wanauwawa, na badhi yao hapa mjini hawana hata chakula, kwani hawawezi kufanya kazi vizuri wakihofia maisha yao lakini hakuna kabisa wa kuwasaidia. Haya makampuni ya kinafiki yanayotoa udhamini, mbona yasidhamini vya maana? Mashuleni kuna vijana wanakosa hata karo, lakini hakuna hata kampuni inayoweza kujitolea kuwalipia hata karo ya mwaka.
Hapa kwenye blogu ya jamii, kuna vijana wenye uwezo sana wanaotuelemisha kwa kima cha juu sana; hususan Dr. Shayo na Jonh Mashaka ambao wanaandika vitu vya maana kweli kweli, lakini mara nyingi waosha vinywa kazi zao ni kuwaponda.
Ni kwa nini tusiungane na vijana kama hawa ili kulijenga taifa letu au kutafuta namna ya kusuluhisha matatizo yetu? Swali langu watanzania wenzangu akili zetu ziko wapi, kwa nini chetu kikubwa ni kuona wengine wanashindwa maishani badala ya kuwa sapoti?
Mdau Mla vumbi
UDSM
Hey mdau,Una swali zuri japo nilifikiri ni maswali.Kumbuka kuwa waTanzania ni watu walio na uwezo na upeo wa kufanya mambo mengi sana lakini nchini hakuna ukweli bali ni unafiki mtupu.
ReplyDeleteMfano watu wengi huibuka na mambo mengi ya maendeleo yanapofika serekalini huwa ni swala la serikali na kuwekewafungu ambalo halito elekezwa katika maombi.
Sasa basi imefika wakati watu wamechoka na kuamua kuishi leo si kesho tena,Kwa maana ya kwamba kama kutakuwa na hayo mambo watakayo ona afadhali kuliko kupata story.
Kulegalega kwingi kunatokana na kizazi cha nyoka kilicho madarakani.Hakuna watu wenye uzalendo na ukiwa mzalendo hupewi nafasi haswa kipindi cha kibonge Ukapa/Mkapa.kiufupi tu ila kuwa uyaone.-D
WAOSHA VINYWA WAPO DUNIANI KOTE, NA ILI KUANIKIWA MALENGO YAKO USITISHIKE NA WANAPOOSHA VINYWA VYAO, NITAKUPA MFANO HAI, HUYU KIONGOZI WA VIRGIN WAKATI ANATAKA KUANZISHA SHIRIKA LA NDEGE LA VIRGIN RAFIKI YAKE AKASEMA AA WAPI HUTAWEZA NDIO UTAKUJA KUFILISIKA TU, LAKINI YEYE AKASEMA NITAANZISHA TU, NDIPO RAFIKI YAKE AKATOA BAADHI YA SHARE ZAKE AKIAMINI MMILIKI WA VIRGIN HATA FANIKIWA. NA ALIPO FANIKIWA ALISHANGAA. NA VIVYO HIVYO MAISHANI HUWEZI KUWAKWEPA WAOSHA VINYWA WATAENDELEA KUOSHA VINYWA VYA KILA SIKU. ILA WEWE WEKA NIA NA UTAFANIKIWA TU HATA KAMA WATASEMA HAIWEZEKANI SI BURE ANA KIZIZI ILA UTAFANIKIWA TU.
ReplyDeleteTumekupata dada. Vipi wewe umewahi kufanya nini kuokoa jamii au hata wewe ni wale wale? Usije ukasema mimi ni mwanafunzi na hivyo siwezi kufanya kitu, mbona akina Sarafina wa kwenye movie walifanya makubwa wakati wao walikuwa bado ni wanafunzi?
ReplyDeletewatanzania tunapenda sifa kwa mambo ya kipumbavu,ulikuwa hulijui?ichi yetu inamambo mengi yanayohitajika kufanyikana pesa si kama hakuna,ILA hatujui nini maana ya PRIORITIES,na kibaya zaidi VASCO DAGAMA anasafiri kila kukicha hata ziara zisizo na kichwa wala mguu.michuzi mwana mi sitoshangaa ukibana comment bt u know what am talking about.thanx
ReplyDeleteudhamini ni biashara dada watu wanadhamini and they get returns on it. social issues kama hizo unazozungumzia have no returns and hence the incentive to allocate precious resources to them is almost non-existent. wewe kama msomi ningetegemea uwe unaelewa hilo. common sense should override your sentiments....
ReplyDeleteNi kweli huu ulimbukeni tusipo angalia tutazikwa nao.Itakuwa aibu kuona wasoma wengi walio na gpa nzuri watashindwa kuchimbia kaburi hili.
ReplyDeleteTunahitaji kutambua kuwa tunaweza kabisa badili jamii hata bila kushirikisaha selikari hii ya silikari. Hata waliofanikisha njia za kupata uhuru walikuwa na mawazao kaa ya huyu mdada na wakaungana na kuokoa wazazi wetu ambao wamesha kata tamaa za maaendeleo.
Mfano mzuri ujana wangu enzi hizo kulikuwa na camp nzuri za vijana zikaitwa kama mlalakuwa camp, camp hizi sifichi zilikuwa na kujifunza kutanua kuliko camp jirani hazikufikisha kokote vijana. Hata kama makundi mengine yazilsha wasanii waleo lakini bado tu kubwa la kubadilika. Itapendaza sana tukitumia makundi haya kuelimisha jamii kama juu kuatua matatizo yetu bila kusubili serikali. Njia hii itasaidia sana kukukza vijana wanaojituma na watakuwa viongozi bora wa baadae.
Ona leo taratibu wanakijiji cha fotobaraza wanaonesha mvuto kwa jamii kueleimishana na kutenda yale wanayopata toka kwa wenzao. Wamefikia hata kuwa na foundation yao ili iweze saidia jamii.
Jamani kubadili nako sio kunasubuli Yesu arudi ni kuamua tu.
Mungau atusadie tuamua uamuzi uliowa busara.
ulipoweka shayo na mashaka wa trime basi wtu watachafua hewa muda si mrefu wala wewe si mpigwa vumbi nishakudhaminisha saa nyingi wewe ni mbeba mbox na mosha vinywa,usijali sana sijui kaka au dada mtabaki kutafuna kumeza mhawezi nchi yetu ni fisadi kwa warembo,na luxury zote in generaly ili tuonekane lakini haya yote ni mapito tu maana maskini hafilisiki,tajiri.......
ReplyDeletek'zoo concorde michigan
Nakuunga sana mkono mdau wa udsm,ndio maan upo udsm,Mungu akubariki sana,ipo siku utasidia watu.Hata mimi nilikuwa na mawazo kama yako,siku moja nili tazama dvd ya Felix Wazekwa alipokuwa bongo,damn!kuna ma pedejee walimwaga hela sana kwa bendi nzima ni noti za elfu kumi kumi zilikuwa kama karatasi,nikajiuliza huyu jamaa si angepeleka shule ile niliyoina kwenye blog nilisikitika sana.Siwezi kujenga shule lakini nimevisha wengi,tena watu ambao siwafahamu,peleka vitu kwenye donation Mungu atakubariki badala ya kutumia kwa starehe tu.
ReplyDeletewewe mla vumbi naomba usuluhishe matatizo ya nyumbani kwenu kwanza ndo ukishamaliza usuluhishe matatizo ya jamii....mtu utalisha vipi wenzio kabla wewe hujala?
ReplyDeletemdau mbeba box original,
Washington DC
UNAJUA DADA MLA VUMBI UDSM WATANZANIA WAMESHOSHWA NA UNAFIKI NA UFISADI ULIOKUBUHU MIONGONI MWA BAADHI YA WALIOPEWA DHAMANA NA WALIPAKODI KUSIMAMIA NA KUONGOZA NCHI YETU TANZANIA. KUOSHA VINYWA NI NJIA MOJAWAPO INAYOSAIDIA KUPUNGUZA 'STRESS'..
ReplyDeletePOLE SANA KWA JINA ULILO JIIITA (mla vumbi)HAKIKA KAMA MICHUZI ANGELIBANIA INGEBIDI AFUNGE MWEZI MTUKUFU NA TOBA YA NGUVU.BINADAMU WAKO TOFAUTI KWA KILA KITU UNAPOKUWA NA JAMBO LAKO WEWE LITEKELEZE TUU NA WENGI HASWA WATANZANIA WAMESHACHOKA KINAFSI KUTOKANA NA MWENENDO MZIMA WA UONGOZI JEMA KWAO OVU OVU KWAO JEMA KWA WA WENYEWE NA HAWA UNAWAONA WANAFADHILI MAMBO FULANI WANA HAKI YAKO NA SI LAZIMA WAFUATE ULICHOKIONA WEWE MUNGU AKIKUBARIKI FATA UTUMBO WAKO NINI UNATAKA UNA HAKI YA KUSHAULI NA KUBALIANA NAWE LAKINI ANGALIA UPANDE WA PILI PAKOJE?
ReplyDeleteKWELI NDIO MAANA KENYA WANATITA TANZANIA MAGOIGOI! HIVI UNASEMA TANZANIA TUMECHOSHWA NA UNAFIKI WA MAFISADI? MIMI NAFIKIRI WATANZANIA SISI WENYEWE NDIO WANAFIKI NA MAFISADI NAMBA MOJA! WEKA UIANO MZURI WA WABUNGE PALE MJENGONI UONE KAMA WATU HAWATAIKIMBIA NCHI HII!
ReplyDeleteUmaenza vizuri kuandika; lakini umeharibu baada ya kuwaingiza Mashaka na Shayo. Unapoandika focus na point zaidi zako na si kuwaambia watu wawasikilize Mashaka na Shayo.
ReplyDeleteMdogo wangu umeongea vizuri.Hebu jiulize kwanza kwa nini kibaka wa mtaani aliyekamatwa kwa kuiba chakula anachomwa moto wakati fisadi aliyeliingizia taifa hasara ya mabilioni anapeta?Kwanini mtoto wa shule ya msingi akiongea kiingereza kwenye dalala anashambuliwa na watu wazima kwa
ReplyDeletemaneno kama "kila mtu anajua kiingereza"kila mtu amesoma"
"msijifanye wazungu" "brokeni english nk.Matokeo yake watoo hawa
wanakosa confidence na kuelewa kuwa
speaking english in public is a
crime.Wakimaliza kupiga vumbi UDSM
wanakutana na ushindani katika
makampuni ya wageni na kukosa kazi
maana wanaandika good english lakini kuongea ulimi mzito.Hapo akitokea high school graduate toka
kenya anakuwa bosi wako kwavile
akitumwa Ulayamerika atafikisha
ujumbe na kuleta majibu siyo tu kwa
kuandika bali hata kuongea vizuri.
Tatizo hili litaeendelea mpaka
tutakapofiki level ya wajapan au
Wachina ambao lugha zao zinazungu-
mzwa na wawekezaji toka nje.Sasa mdogo wangu ukimaliza UDSM na kuamini kuwa education is the
tranformation from backwardness to
betterment,wewe na wenzako leteni
mabadiliko japo kidogo hata kwenye
familia zenu.Kama mchaga muuza duka mtaani kwenu ambaye hakumaliza
darasa la saba shuleni Sanya juu
pato lake ni kubwa kuliko lakwako
basi kubali kuwa amekuzidi elimu.Kuwa agressive usisubiri kupata kazi ofisini au kuchangiwa ili kubadilisha maisha yako.Weka vyeti vyako kabatini vaa jeans, boots na kofia ya mkeka panda basi
nenda Singida kalete matenga ya kuku uuze barabarani Dar na siyo kusubiri title za akina Makweta
waliyokuwa madarakani toka wakati
sijazaliwa mpaka nilipomaliza masters.Ukiwa icon katika jamii yako wadogozako watafuata na Tanzania ita-move foward.
Toto tundu, Upper Marlboro
Muswaili iko kama ile debe ambayo hakuna kitu ndani,natoa kisindo kali sana tena nawesa tisa mutu.baadae nakuta hamna kitu.
ReplyDeleteKiswaili murefu kumbe iko nataka ibia kitu.
hii habari ya kila siku miss ilala, temeke miss shoga hawesi leta maendeleo wala fikisa nyie mbele.wisi toka pande ya juu paka pande ya chini, chapa kasi sio maneno maneno tu.
Ukishiba vumbi utaelewa baada ya dhiki faraja.
ReplyDeleteUdhamini ni kazi siyo mgawo.
Hili swali limeulizwa na mwanafunzi wa mwaka wa ngapi?
ReplyDeleteDada nakuunga mkono kuhusu umuhimu wa kusaidia ila kumbuka kutoa ni moyo si kulazimishana. Wewe binafsi Mungu akikujalia kupata chochote uwasaidie utakao weza kwa jinsi hio utakuwa umetatua matatizo ya japo mtu mmoja au wawili.. kulingana na uwezo wako. Wapo watu wanasaidia sana watu pale wanapoweza. Ukifanya uchunguzi unaweza kufahamu hilo, mfano kuna watu wanasaidia watoto kielimu na katika mahitaji mengine. Ila ni vitu binafsi kufuatana na moyo wa mtu anavyosikia wito wa kusaidia.
ReplyDeleteDADA kunawatu wapo huku lakını shuleless kwahıyo usıone mtu anaandıka yupo washgton au ıstanbul ukaona ameendelea kımawazo.kazıyao kukatısha tamaa
ReplyDeleteCongrats mdada UDSM.Hopefully, you
ReplyDeletewill graduate with distinction
honor and accomplish a significant
change in our society.Sponsorship
can sometimes be investiment
commercialwise where by some money
could be donated hoping for a big return in a long term to the doner
but for receipients is up to the air.Whom one to assist and otherwise depends on how much profit earned or expected.I'd like to respond to anonymous of Sunday Aug 09,11:53 who instead of embarking on a contructive debate
imply attacked uneducated Tanzanians particularly residing in
DC.Respect people,agree to dessagree.You will never here NBA
players attacked Kobe Bryant or
LeBron James simply because they
never been to college.I specifically cited that example to
demonstate no matter what level of
education an individual may have,
they can be good players to
accomplishing a positive impact
that would positively change so many lives in the society.Attacking
uneducated I dont think is the right stretergy.If you're educated
be humble,confident with no eagle
and try to make this world a better
place to live.Peace
Izzo Fashizzo(uneducated)