Ngeleja kumshuhudia Redd’s Miss Ilala
Mwandishi wetu
WAZIRI wa Nishati na Madini William Ngeleja anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kinyanganyiro cha kumtafuta mrembo wa Redd’s Miss Ilala katika shindano litakalofanyika Ijumaa hii Agosti 7 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati ya kanda Miss Ilala, Jackson Kalikumtima alisema kuwa tayari waziri huyo amethibitisha kuhudhuria shindano hilo linalotarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Akifafanua Kalikumtima alisema kuwa kwa mujibu wa mwalimu wa warembo hao Regina Mroni na matroni wao Nelly Kamwelu ni kwamba warembo hao wako tayari kwa shindano na kinachosubiriwa sasa ni siku ya mpambano huo wa fani ya ulimbwende.
“Mwalimu wao amenithibitishia kuwa warembo wako tayari kwa kila kitu, kuanzia mavazi, kutembea kwa mikogo yaani ‘catwork’ na kujibu maswali kwa ufasaha kutokana na mafunzo mbalimbali waliyoyapata wakiwa kwenye kambi yao iliyoanza Julai 14 kwenye hoteli ya Lamada & Apartements iliyopo jijini,” alisema Kalikumtima.
Mbali na hayo alisema kuwa jana ilikuwa siku ya warembo hao kufanyiwa uamuzi wa awali ‘pre judgement’ kabla ya siku ya shindano ili kufahamu uwezo na ufahamu wao kiujumla lengo likiwa ni kumpata mlimbwende mwenye sifa za kuiwakilisha kanda hiyo ya Ilala.
Vilevile warembo hao walipata fursa ya kutembelea magazeti ya kampuni ya New Habari Cooperation ambapo leo wanatarajiwa kutembelea kampuni ya The Guardian Limited kujifunza hatua mbalimbali zinazipotiwa katika uchapishaji na uandaaji magazeti.
Kabla ya hapo pia walitembelea maeneo mbalimbali mkoani Arusha, Kampuni ya utengenezaji video ya Sofia, Hifadhi ya Taifa ya ziwa Manyara, Kiwanda cha Banana Investiments Limited, Makumbusho ya elimu ya viumbe ya Arusha, TBL Arusha na maeneo mengine.
Warembo wanaowania taji hilo la Redd’s Miss Ilala kinyang’anyiro kitakachofanyika Agosti 7 kwenye viwanja vya Karimjee ni Glory Mwandwani, Pendo Lema, Nyamizi Mihayo, Irene Karubaga, Husna Omar, Neema Sylivester na Everyline Gamasa.
Wengine ni Fatma Bongi, Khadija Muhecha, Margareth Motau, Julieth Mombury, Sylivia Shally, Glads Shao, Anne Mkandawile, Doris Jimmy, Zena Mbasha na Winfrida Mmari


MICHUZI NIMEKUONA LIVE KWENYE SKY 194 BEN TELEVISION KUMBE UNAJUA KIMOMBO KIASI HIKI? HONGERA SANA UMEKULA NUSU SAA LIVE.
ReplyDelete