Wananchi wenzangu wote mnaoishi US na hata nje, na hasa New York City na vitongoji vyake, - Nina furaha kuwafahamisha kwamba kwa niaba ya Balozi wetu wa kudumu katika Umoja wa Mataifa, New York USA, Ofisi ya ubalozi wetu NY, imeniomba kuwafikishia ujumbe huu rasmi kuhusu mnuso wa kuchoma nyama utakalofanyika nyumbani kwa balozi, siku ya tarehe 15/8/2009 yaani Jumamosi ya mwisho wa wiki hii, ikiwa ni kufuatia ahadi iliyotolewa na Balozi mwenyewe kwenye ule mnuso wa mwisho kule Wilson Woods Park.
- Kwa kifupi ratiba ni kwamba:-
1. The bash itafanyika:- Tarehe 15/8/2009, siku ya Jumamosi.
2. Kuanzia Saa Nane Mchana na kuendelea, yaani From 2.00PM.
3. Kutakuwa na nyama za kuchoma, kuku, mpaka nyama ya mbuzi, na pia kutakuwa na vinywaji kwa wingi sana.
4. Wananchi wote mnaalikwa na kukaribishwa na ni kwa wakubwa na watoto, wa umri wowote ule.
5. Baada ya kuchoma nyama kama kawaida kwa kushirikiana na Ma DJ's Mao & Freddy, ninawakaribisha wananchi wote kuelekea Alamo Club, 166 Gramatan Avenue, Mount Vernon NY 10552, - Ambako tutakuwa na muziki wa Disco, mpaka asubuhi na pia kiingilio kitakuwa ni bure kwa kila mwananchi atakayejitokeza.
This time ninategemea tutakuwa na shindano la kutafuta bingwa wa "Ndombolo ya solo", na Bingwa wa "Muziki wa Mduara" yaani Taarabu iliyokwenda shule.
6. Anuani ya kufika Nyumbani kwa Balozi kwenye Bash ni:-
30 Overhill RoadMT. Vernon, NY 10552

Kwa maelezo zaidi wasiliana kwa simu na:-
1. Tanzania Embassy (NY):- 1-212-972-9160,
au
2. Mukulu William Malecela Cell #1-914-473-1033.
Ahsanteni wakuu na See You there

William Malecela - Community Organizer

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ndugu Malecela, si umeshasikia kwamba ni vema tukatumia kiswahili, kichaga, kigogo na au kiingilishi bila kuchanganya lugha? Unajua mimi na Mjomba Mrisho tumeshapanga kuwapata watu kama nyie ili tujaribu kuwaeleza kwamba ni vema tukaupenda utamaduni wetu ikiwa ni pamoja na kukuza lugha yetu ya kiswahili. Kama hutabadilisha mwaliko wako uwe wa kiswahili sanifu MIMI SIJI!. Nafikiri hata balozi wetu akiongea au ingekuwa ni yeye ameandika ujumbe huu asingeweka lugha mbili mbili. Michu mdogo wangu, naomba kutoa hoja (Mtoa hoja ndogo ndogo - MH)

    ReplyDelete
  2. Hapa kweli ndugu yangu naona mwaliko umechemka, kweli leo karibu ni Ijumaa, au tayari kuna watu wamepata mwaliko rasmi nasi wengine ingawa tupo jirani zenu hapa Manhattan tumepitwa pembeni, maana si rahis kubwaga kila kitu na kupaga tena ratiba ya Jumamosi. Tunawatakia Mnusu mwema.
    Mdau
    New York, New York

    ReplyDelete
  3. Mama Kilango MalecelaAugust 14, 2009

    mwanangu mimi nitakuwepo na dada yako hapo nimeona niku surprise na hii blog ya michuzi. Dress code mbona hujaweka? ama tuje na vitenge kama kawa?

    ReplyDelete
  4. Duh, naona balozi wetu ametukumbuka. Mimi nilidhani watu wa NY ni MAYATIMA. Hatuna wawakilishi, kwani wa kawaida ni mpaka wakubwa waje kutoka DAR ndio unasikia matangazo kama haya.

    ReplyDelete
  5. Ninakuja huko. Tafadhali musichome nguruwe.

    ReplyDelete
  6. Richard HillaryAugust 15, 2009

    Sasa William mbona umechelewa sana sana kutoa taarifa ?? Ningekuja ila imekuwa ni ghafla sana.

    Ahsante sana kila la kheri.
    Wasalaaam Richard Hillary. (PA)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...