Anko nanihii,
naomba wajuzi wa lugha yetu mwanana ya kimatumbi wanisaidie maana hili linalinitatizaga sana kila nikipita ilala na kuona jengo hili ambalo limeandikwa "Chama Cha Walimu". Swali langu ni je lugha sahihi hapo ni ipi "Walimu" ama "Waalimu??"
Mdau Martin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. Waalim ndiyo sahihi na ni neno ambalo limetoka kwenye Kiarabu, na siyo Walimu ... dRU

    ReplyDelete
  2. hata mie kila siku nikipita hapo naona kichefuchefu,ni Waalimu si walimu,hicho ni kiswahili cha kusema zaidi si kuandika

    ReplyDelete
  3. ni walimu..kutoka ktk kiarabu siyo tatizo kwani neno lililokopwa hubadilishika..

    mifano:
    Kiarabu ni Salaam.
    Kiswahili salamu.


    Kiarabu ni asubhi()wataalamu waweza kosoa
    Kiswahili ni asubuhi.

    ReplyDelete
  4. Anonymous wa kwanza na wa pili nyote ni ma-Idiot inaonekana hata somo la kiswahili hamkulisoma pamoja na huyo mtoa mada mwenyewe.
    Hiki ni kiswahili na siyo kiarabu kumbukeni hata kama maneno mengine yatakuwa yametoholewa kutoka katika kiarabu siyo lazima yatamkwe au kuandikwa kama kiarabu(original).maneno ya kiswahili yanatamkwa ka sauti za kibantu ambazo mizizi yake ni tofauti na kiarabu.
    ikiwa WALIMU mnaona ina makosa basi NGE na MBU pia yana makosa!!!kwanini isiwe N'NGE badala ya NGE na kwanini isiwe M'MBU baadala ya MBU?????

    ReplyDelete
  5. What don't you understand? As long you understand, it's not an issue...

    ReplyDelete
  6. kweli hao wajamaa wasituzingue kiswahili sahihi ni WALIMU,SALAMU, mambo ya AAAAA ni huko nchi nyingine mkifika, huku TZ ni mkato mkato tu single A period....mpo? waharibifu wa kiswahili mwanana nyie ebo! sorry kumbe tuko class..mdau mleta mada tusamehe unajua inauma sana kiswahili kupinduliwa pinduliwa...

    ReplyDelete
  7. Wed Aug 26, 11:50:00 AM umeanza kwa mbwembwe kumbe wewe ndo sifuri kabisaaa,msaada wako uko wapi sasa bora hao wengine wametoa msaada? kumbukumbu zangu zinaonesha waalimu(sahihi) ni wingi na umoja ni mwalimu,walimu sidhanikama ni sahihi. ndo mawazo yangu

    ReplyDelete
  8. - mdau uliyeleta mada, unakumbuka mfano wa 'boriti'?..kazi kukosoa wenzako..na wewe 'linanitizaga' ndo nini?..

    -wadau mlong'aka, ile 'kiarabu'ndo imewatia kichefuchefu ama?..mbona dRU amesema sawa tu? - "na ni neno ambalo limetoka kwenye Kiarabu"..asili yake kweli ni kiarabu (ilm/alm). Linaloipa ubantu ni 'w' ('ua'='wa') na ile u ya mwisho: m-W-alim-U..

    -ukichukua mfano wa nomino zingine hasa za 'taaluma' za kiswahili zinazoanza na 'a-xxx' na kuleta jina 'mu-a' (= mwa), neno sahihi hapa ni 'waalim-u'..angalia: mwandishi = wa-a-ndishi; mwashi = wa-a-shi;mwasi = wa-asi; mwasisi = wa-asisi; mwandazi = wa-andazi (hii siyo ya mahamri, lol!!!)..walioandika hapo jengoni wamechemsha, warekebishe!..naomba kuwasilisha..

    ReplyDelete
  9. Mie naonaga(bad swahili) kuna wadau wagomvi sana ni wakorofi na ni dhahiri kuwa watafuta sababu wapigane ndondi
    If you remove all arabic words from swahili there would be left a bare skeleton, you cant remove all latin words from english
    Mwalimu maalim ,salam saalam zote sawa
    You say potatoes i say pota"toes you say either and i say.....
    Ramadhani karim
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  10. lugha yetu ya kiswahili imetoka kwa waarabu halina ubishi hili kwiii kwiiiiiiii. Sio tu kukopa ni tumechukia kila kitu

    ReplyDelete
  11. waalimu ni wale wanaopenda kukaa mbele kwenye shughuli zinazohusiana na pilau mfano hitma,maulid,vilio,harusi nk lkn hawa ni WALIMU na akiwa mmoja kamwe hatoitwa mwaalimu bali ataitwa MWALIMU kwahio wakiwa zaidi ya mmoja wanaitwa "WALIMU

    ReplyDelete
  12. Umoja wa neno 'Walimu' ni 'Mwalimu'. Kwa hiyo, kifungu cha maneno 'Chama cha Walimu' ni Kiswahili sanifu kabisa. Tukumbuke kuwa Kiswahili na Kiarabu ni lugha mbili tofauti na kuazima neno kutoka lugha fulani hakukuzuii kulifanyia mofification mf. progamme na programu, compyuta na computer, n.k

    ReplyDelete
  13. Blog ya jamii idumu. Kwa maswali na majibu namna hii, blog yetu si tu kwamba itakuwa inaburudisha, inafariji, inachekesha n.k. lakini vilevile itakuwa inaelimisha yake ili mradi tu majibu yatolewe kwa ustaarabu na si kwa kukejeli!! Blog ya jamii idumuuuuuu.

    ReplyDelete
  14. johannes uko sawa kabisa. mchangiaji wa kwanza umesema sawa.

    ReplyDelete
  15. IDUMUUUUUUUU NA WADAU WAKE WADUMISHE USTAAARABU MILELE TUWE TUWE TUNACHEKELEA NA KUONGEZA SIKU NA KUJIFUNZA KWA RAHA ZETU, WITO KILA MTU SHANGILIA SEMA IDUMUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU.........

    ReplyDelete
  16. Pamoja na kutokana na Kiarabu, lugha za Kibantu, Kiajemi, Kihindi, Kijerumani na lugha nyinginezo, Kiswahili ni lugha inayojitegemea. Umoja wa neno Mwalimu ni Walimu na kamwe si Waalimu. Ni makosa kujaribu kushabihisha lugha kwa namna anayofanya mchangiaji wa mwanzo na wengineo. Yapo maneno mbalimbali kwa mfano gorofa, safina, tarehe, shahwa na kadhalika ambayo yamekubalika katika lugha ya Kiswahili kwa maana kidogo tofauti na yalivyo katika Kiarabu. Kwa hiyo jengo lile ni la chama wa walimu.

    ReplyDelete
  17. Mzee Kifimbo ChezaAugust 26, 2009

    Here we go..

    Mwanafunzi = Wanafunzi
    Mbeba box = Wabeba mabox
    Mla vumbi = Wala vumbi
    Fisadi = Mafisadi
    Mwalimu = Walimu
    Mmachinga = machinga
    MWARABU = WAARABU

    Need I say more?

    ReplyDelete
  18. Hakuna lugha isiyo na maneno ya mkopo (loan words). Kiswahili si hakijatokana na Kiarabu bali kina maneno kiliyotohowa toka katika Kiarabu. Kiswahili mzizi wake ni Kibantu. Tunaposema Kibantu tuna maana ya zile lugha zinazofanana fanana za kuanzia nchi za Afrika ya kati, Mashariki hadi kusini. Kwa mfano,katika lugha nyingi za nchi hizo wanapohesabu kuanzia moja, mbili, tatu hadi nne huwa matamshi ya namba hizo yanafanana. Pia maneno kama Mtu, Mwana, Mama/Mawe/Nyoko, Baba, Shangazi/Sengi, Mungu/Mulungu, Soni/Aibu, Munyu/Chumvi, Maji/Mazi, lia/lela/lila, Kufa/Afwile, Kula/Kulia.

    Tofauti moja kubwa kati ya iswahili na Kiarabu ni kwamba Kiswahili kinanyambulika wakati Kiarabu hakinyambuliki. Kunayambulika ni jinsi neno linavyoweza kupanuka mafano, Shambulia, shambulieni, shambuliana, shambulianeni nk.

    ReplyDelete
  19. kweli wote saumu. mpaka leo hii jumla ya mwalimu hamjui, siamini lakini ukweli ni walimu,

    ReplyDelete
  20. Hilo jengo nilifikiri linaitwa MWALIMU BUILDING kumbe ni Chama Cha Walimu wa??????

    ReplyDelete
  21. Kweli nimecheka sana kwa maoni ya wadau.
    Ila baada ya kicheko kwisha ndo nika anza kutafakari, je, kwa maoni ya wadau waliopita tunahitimisha kuwa tunajua kiswahili? Nimeishia kwenye maumivu ya kugundua kuwa kumbe wabongo hatujui kiswahili, lugha inayoaminika kutumika Bongo kwa ufasahaha. TUMENYANG'ANYWA TULICHOKUWA NACHO!

    GJK

    ReplyDelete
  22. Katika wadau mliotoa maoni hapa kuna aliyeangalia Kamusi ya Kiswahili Sanifu, toleo la pili kama ilivyotolewa na TUKI inasemaje?

    ReplyDelete
  23. Maandishi yanatakiwa kurekebiswa. Neno sahihi hapo ni WAALIMU period.
    Hii mambo ya kusema si umeelewa ni upuuzi mtupu. Elimu muhimu sana jamani achane kuzugazuga tu wabongo, hadi lini?
    Mnatia hasira ninyi

    ReplyDelete
  24. Hatusemi walimu wetu bali waalimu wetu, ninyi vipi?

    ReplyDelete
  25. Unajua hii inakuwaje? Mkurugenzi kiswahili hajui, bali kwa kuwa ni bosi huamua yote yeye. Watu wanaacha kupeleka kazi hizi kwa wataalu wa lugha hasa wanawaachia mabosi wabishi waamue.

    Wabongo kwa ubishi,sina hamu. Yaani hiyo walimu hata haikai sikioni.

    ReplyDelete
  26. lugha sahihi ni matumizi ambayo wazungumzaji wengi wa lugha wanaelekea kukubaliana kutokana na mazoea ya matumizi. neno 'walimu' ni sahihi zaidi ya 'waalimu'.

    ReplyDelete
  27. Wacha watu wabishane maana hakuna reputable source online ya kuhakikisha lipi ni neno sahihi.
    Labda tuwaombe Taasisi ya uchunguzi wa kiswahili (TUKI) nao waamke usingizini watuwekee an online version ya kamusi yao.

    Halafu hawa jamaa wanapigania shule za bongo zitumie kiswahili kufundishia wakati hata muda tu wa kuweka hiyo kamusi yao mtandaoni hawana, au ndo wanataka wageuze mradi wa kiuchumi?

    Hivi wabongo kweli tutaacha kubishana?

    Mzee wa nanihii fikisha hili kwa huyo bosi wa TUKI, tuamshie huyo mtu. Kama wanataka kukuza kiswahili duniani inawabidi waamke na kuutumia mtandao kukinadi kwa kuweka official site ya kamusi ya TUKI. Mwambie aache uzembe.
    Kwa nini waingereza hawabishani kama ni teachers au tichazi

    ReplyDelete
  28. Nimeingia website ya University of Dar es Salaam nika search "TUKI" kutoka kwenye search field yao, nilichokipata baada ya hapo kinafuata.

    Search Results


    Warning: fopen(/home/ududsm/public_html/modules/search/dgssearch.cache) [function.fopen]: failed to open stream: Permission denied in /home/ududsm/public_html/modules/search/libs/utils.php on line 206

    Warning: set_file_buffer(): supplied argument is not a valid stream resource in /home/ududsm/public_html/modules/search/libs/utils.php on line 209

    Warning: fwrite(): supplied argument is not a valid stream resource in /home/ududsm/public_html/modules/search/libs/utils.php on line 213

    Warning: fclose(): supplied argument is not a valid stream resource in /home/ududsm/public_html/modules/search/libs/utils.php on line 214
    Search for query 'tuki' found no results. Search took 0.2 sec.


    Nikafungua link inaitwa dictionary services nikakumbana na ERROR http://rdu.udsm.ac.tz:50000/dist/download

    Sasa nimechemsha wacha watu wabishane tu.

    ReplyDelete
  29. Woote mumekosea, ile iilitakiwa iitwe Maalim.

    ReplyDelete
  30. Mwalimu - Walimu

    Mifano zaidi....
    Mwanafunzi - Wanafunzi
    Mwanajeshi - Wanajeshi
    Mwanasiasa - Wanasiasa
    Mwanakamati - Wanakamati

    ReplyDelete
  31. Kwani wewe MWAALIMU wako wa kiswahili nani? lol.

    ReplyDelete
  32. hakika tatizo watanzania kila mara ni masihara na ndio tatizo hata penye kuhitaji kupata nuru nyie ni masihara kibao.

    navyokijuwa kiswahili ni hivi:

    walimu hutumika katika shule hivyo ukisema MWALIMU ni mmoja na wengi WALIMU hivyo sawa.

    ukija katika dini ya kiislam mwalimu huitwa MAALIMU NA WENGI PIA MAALIMU MFANO MAALIMU WOTE NJOONI HUKU INA BINDI SENTENCE NDIYO IJIELEZE NI KAMA MANENO MENGINE YA KISWAHILI UTALIJUA KUTOKANA NA SENTENSI MAANA HUWA LIN MAANA MBILI MFANO HIKI CHUNGU NI KUZURI KWA KUPIKIA MAHARAGE NA WAKATI HUO HUO HILI CHUNGWA LADHA YAKE CHUNGU KAMA SHUBIRI

    ReplyDelete
  33. Jamani ehh! kulikuwa na kipidi cha kiswahili enzi za Mwalimu radio Tanzania hivi bado kipo huko bongo ? haya yote yasingetokea ...mkishindwa kabisa mkamuone mzee ruksa awasaidie fasta ! hapo jibu ni Waalimu fullu stopu !Chief

    ReplyDelete
  34. Umoja wa 'walimu' ni 'mlimu', kama ilivyo watu (mtu), wahindi (mhindi), wabishi (mbishi), wajinga (mjinga) nk.

    Wingi wa nomino yoyote unazingatia mzizi wa neno hilo, kwa hiyo huwa inatangulizwa 'wa' nyuma ya mzizi wa neno, na kama ni umoja inatangulia 'm' iwapo mzizi wa neno unaanza na konsonanti au 'mw' iwapo mzizi wa neno unaanza na irabu(vowel).
    Mifano:
    -vivu: m-vivu, wa-vivu
    -janja: m-janja, wa-janja
    -athirika: mw-athirika, wa-athirika
    -ajiri: mw-ajiri, wa-ajiri
    -alimu: mw-alimu, wa-alimu.

    Natumaini imeeleweka sasa kuwa kwa usahihi, wingi wa 'mwalimu' ni 'waalimu'.

    ReplyDelete
  35. kweli we kifimbo cheza umenichekesha na hiyo mifano hai yako sina hamu, tukirudi kwenye mada sahihi hapo ni waalimu, walimu iko veri rafu

    ReplyDelete
  36. Nyote mliotoa maoni ni vichaa,mnataka kuwafundisha lugha "WALIOWAFUNDISHENI" nyie mpaka mkapata hekima za kuwahoji tena?Anae sema kiswahili ni kiarabu huyo bado ni mtumwa wa Waarabu,kiswahili ni kibantu bwana.Vipo vijineno vichache vya vilivyokopwa uarabuni kama Mwalimu,Hamsini,Mtihani na Mushkeli. Vijineno vingine vimetoka ufaransa kama safari na Nanasi,na vijineno vingine toka kiiengereza kama Shati,soksi na mengineyo,sasa utasemaje kiswahili ni Kiarabu?mshamba weeee rudi darasani,wenzio walipokuwa wakisoma ulikuwa ukiruka madirishani kwenda kupiga chabo!!!!

    Anaesema Maalim ni sahihi hachelewi kukuambia 3 x 3 = 33 au wingi Umoja wa Chipsi ni Kipsi,umoja wa Vietnam ni Kietinam au wingi wa karakana ni Vyarakana(Wizi Mtupu!)

    ReplyDelete
  37. Nyote mliotoa maoni ni vichaa,mnataka kuwafundisha lugha "WALIOWAFUNDISHENI" nyie mpaka mkapata hekima za kuwahoji tena?Anae sema kiswahili ni kiarabu huyo bado ni mtumwa wa Waarabu,kiswahili ni kibantu bwana.Vipo vijineno vichache vya vilivyokopwa uarabuni kama Mwalimu,Hamsini,Mtihani na Mushkeli. Vijineno vingine vimetoka ufaransa kama safari na Nanasi,na vijineno vingine toka kiiengereza kama Shati,soksi na mengineyo,sasa utasemaje kiswahili ni Kiarabu?mshamba weeee rudi darasani,wenzio walipokuwa wakisoma ulikuwa ukiruka madirishani kwenda kupiga chabo!!!!

    Anaesema Maalim ni sahihi hachelewi kukuambia 3 x 3 = 33 au wingi Umoja wa Chipsi ni Kipsi,umoja wa Vietnam ni Kietinam au wingi wa karakana ni Vyarakana(Wizi Mtupu!)

    ReplyDelete
  38. Mwalimu Julius K Nyerere
    au
    Maalim Julius K Nyerere.

    ReplyDelete
  39. MAALIM NI KAMA SEIF SHARIFF HAMAD KWAVILE HAJAWAHI KUFUNDISHA JAPO CHECHEKEA ILA MWALIM OFCOURSE NI JULIUS.K.NYERERE MAANA ALISHIKASHIKA CHAKI YLE MZEE

    ReplyDelete
  40. Utawajuwa tu watu ambao vichwa vyao vibovu Mwalimu=Kiswahili na Maalim =kiarabu Nyerere kafundisha Seif Shariff Hamad pia Kafundisha Chuo vyote nia mafundisho hata wewe ukiwafundisha Watu wawili au Mmoja kitu chochote unaweza kuwa Mwalimu au Maalim kwa hao watu Wawili au Mmoja sio Lazima mpaka Wakubatize hilo jina kila siku.

    Anayesema kubishana hakuna aliyebishana Humu ni kufahamishana pengine mwengine atanikosoa mie pia kukosea. Ndio Critic zenyewe sio hahaha. Tunajaribu kufahamishana sio kubishana. Ila mie Maoni yangu binafsi ni Mwalimu ni Mmoja Wengi Walimu au sawa na kusema sehemu Chuo Cha Uwalimu au Ualimu? Pwani Mnajuwa kwamba Mwalimu pia ni Jina tu? Msije Kusikia Mwalimu Mkafikiri Ni Wa Chuo au Madrasa au Chekechea wengine wanapewa majina tu Bagamoyo,Kisarawe,Tanga,Mafia,Rufiji Mwalimu ni jina tu. James.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...