rock city ilivyo leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Sasa jamani mbona mambo tunafanya yale yale.... ebu angalia ukubwa wa hiyo barabara yaani baada ya miaka kadhaa tu itakuwa kama mtaa wa Azikiwe(Maktaba) Dar au wengine husema posta mpya.. . jamani hivi tunavyopanga tunaangalia miezi mingapi mbele???!!!
    Inabidi kuangalia miaka 100 au zaidi ijayo. Hili si jiji jipya tunajenga wenyewe??!!

    Ebu jiulize muingereza aliiona hali ya baadae ya usafiri London akaanza kujenga treni ya chini mwaka 1886,(London underground). Mwaka 1939 UK walikuwa kama milioni 40 hivi sasa wanakaribia 70 sasa jiulize hapo 1886 walikuwa wangapi London ikiwa sasa ni kama milioni 10?!! Lakini waliliona tatizo la baadae...si waliona wanavyozaliana??!! Na pia wakaona wanavyoanza kuendelea??!

    Sasa sisi tunavyopanga(kama tunapanga) hatujiulizi hayo?! wala kujiuliza si lazima maana tumeshaona wenzetu wamefanya nini na hali ikoje. Ebu jiulize kwa wale walikwishafika London kama hiyo treni ya chini isingekuwepo hali ingekuwaje sasa hivi??!!
    Tujikomboe jamani katika umasikini huu wa Fikra. Mheshimiwa JMK si unazunguka huku na huko unayoyaona si uwabadilishe basi mawazo watu wako huko wizarani(lakini hata wao safari kila kukicha).
    Si lazima kujenga sasa hivi bali nafasi ya upanuzi ikibidi baadae iwepo.......Aaah nimekumbuka wakubwa wanasubiri muda ukifika Mjapani akitoa msaada walete karandinga..." X X X" .... kwa wasiojua hiyo alama tena nyekundu ikishapigwa kwenye nyumba yako ujue...."BOMOA BOMOA YAJA"

    "TUONDOE UMASIKINI WA FIKRA JAMANI," Naamini itatusaidia kuondoa hii tabia ya "MRADI LIENDE"

    Mzawa

    ReplyDelete
  2. Mza ohh mza, mza nitarudi tena, kaka Michuzi ungeniwekea tu na wimbo wa Remmy. Ohh Mwanza

    ReplyDelete
  3. Naangalia hii picha naona inanichanganya wadau nijulisheni hii round about ni ya wapi? ni pale jirani na fourways bar ya zamani ama?? aisee mbona taswira mpya mpaka nachanganya jiji langu nililokulia miaka kadhaa iliyopita duh

    ReplyDelete
  4. Michuzi naomba ufikishe salamu zangu kwa wana Kawekamo na wana Mza wa Roman C kwa kumpoteza kiongozi wao Askofu Mayalla. M'Mungu amlaze anapostahiki

    ReplyDelete
  5. katika picha kali ulizotoa tangu mwaka huu uanze, hii ya rock city ni baa'b kubwa, ebwana hapa mahali pasafi sio mchezo, vipi makao makuu ya Tanzania yahamie huko?

    ReplyDelete
  6. Anon wa kwanza aka Mzawa
    Mara nyingi tatizo kubwa sio Upana wa barabara bali ni idadi ya barabara.Angalia hapo London ulipo kuna barabara ngapi kubwa?
    Kwetu tunajenga barabara moja kubwa halafu kina Michuzi wanakuja kusifia.Sehemu kubwa ni uswazi na hili sio kosa la serikali tu bali ni la wananchi(sisi) wote tunavamia viwanja pia hao wapima viwanja wanapima sehemu kuuuubwa za kujenga nyumba bila kuacha sehemu za barabara,Park na makaburi.

    ReplyDelete
  7. Michu mdogo wangu huu ni mtihani kwako, ukipata, nitakutumia corolla. Mdau wa mabatini mwanza. Swali ni je ulisimama wapi wakati unapiga picha hii. Nipatie jibu.

    ReplyDelete
  8. Hapo ni Makoroboi

    ReplyDelete
  9. Afahali angalau Mwanza mnajitahidi hasa kwa usafi, angalia "jiji" kama Mbeya, uchafu mtupu sidhani kama hata hadhi ya jiji ilistahili!!

    ReplyDelete
  10. Tuna tatizo kubwa sana la mipango miji, sijui hii inatokea wapi na kwanini itokee,kama wataalamu wapo na wahusika wapo.
    Nazungumzia hivi nikitoa mifano hai ya miji mipya inayojengeka sasa. Serikali ipo kimya, inasubiri wananchi watumie vijisenti vyao walivyo-jilimbikizia kujenga kiholela na baadaye wanaanza kubomolewa.
    Kuna maenea kama Kipunguni, Majohe nk, ujengaji wake hauna mipangilio kwasasa, na nahisi huko baadaye serikali itaanza kugombana na wananchi wake,kwasababu ya hili.
    Kwanini pale mnapoona wananchi wanaanza makazi msiweke ramani wazi,kinachotakiwa kupitia serikali za mitaa wawaelekeze wananchi hao wajenge vipi kwa mipangilio gani. Hili jamani nalolinahitaji wafadhili?
    Basi cha ajabu kwa mfano serikali kama itaamua ifuatilie hili, utaona nguvu ya ziada zitakayotumika, utaona ufisadi fulani utakavyoaanza, lakini toka mwanzo hili lilikuwa linaoanekana, na nahisi ramani zipo, na wengine tuliofika mwanzoni tulikuwa tukiambiwa tuache barabara mita kadhaa,lakini hawa waliokuja baadaye hawajali cha barabara wala nini, na serikali za mitaa zipo!
    Au ndio tunasubiri uchaguzi uishe, kama mnavyosubiri uchaguzi uishe ndipo muanze kuwafukuza wafanyabiashara wanaouza sehemu zisizoruhusiwa jijini, hili hatulioni kweli? AU?

    ReplyDelete
  11. Mbeya mbali, dar kwenyewe tu kuchafu ukipita salender bridge lazima uzibe pua.

    ReplyDelete
  12. anon wa 08:09 umeongea swala la mbeya umenikuna, kweli hata mimi naona mbeya haikustahili city status nafikiri ni viongozi wetu waliamua kuridhishana ni pachafu sana hata ukipalinganisha na dom, dom inaonekana Ulaya, magari ya kuzoa taka hakuna, miundo mbinu yote mibovu sitaki kusema mengi

    ReplyDelete
  13. you can register for the marathon at www.rockcitymarathon.com

    ReplyDelete
  14. binadamu mshaanza kuchafua khali ya hewa stop blaming the goverment blame yourself unapoonglea viwanja kwanini usiwapatie ushauri before they start the plan watanzania kwa kujibeza sisi kwa sisi bwana hatari kwelikweli.John Dotto Ngongoseke Oakland ,CA

    ReplyDelete
  15. Wakati fulani katika kazi yangu ya kubeba maboksi maeneo fulani...nikawa ninauliza maswali kwa nini hivi kwa nini vile...basi mpopo(nnigeria) mmoja akanichoka akasema..." Wewe mtanzania unataka nini haulipwi kufikiria hapa bali kubeba maboksi..."
    Hii inanifanya sasa nione kama watu wa serikali tunawalipa tu ili bora liende na sio wafikirie jinsi ya kuiendeleza nchi....kama anon wa tarehe 20 04.40 anavyosema tuwalipe tu serikali halafu tupange wenyewe...Na ndio kinachofanyika... Tuondoe basi Serikali tufanye tu wenyewe au kwa nini tunawalipa kama hawana kazi??!!
    Ama Kweli
    Mzawa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...