Mama Salma kikwete akiwasili kwenye eneo la tukio jana mjini Bagamoyo tayari kuzindua kampeni ya Vodacom Foundation ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo pamoja na kufuturisha sehemu mbalimbali nchini misaada kibao hutolewa.
Mbunge wa Viti Maalum Mh. Kweigr akiongea na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare na Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba huko Bagamoyo jana. baadhi ya wanafunzi wa madras katika hafla hiyo
Mama Salma Kikwete akiwakabidhi vyakula watoto yatima ambao wanaishi katika mazingira magumu msaada huo ulitolewa na Vodacom Foundation katika kampeni yao ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,(katikati)Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba(kulia)Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare,Wilayani Bagamoyo jana.

Mama Salma Kikwete akimkabidhi vifaa vya charahani Mwenyekiti wa kikundi cha kina mama wanaolea watoto yatima Bi.Muridhia Bakari msaada huo ulitolewa na Vodacom Foundation katika kampeni yao ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,(katikati)Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare, Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba,Wilayani Bagamoyo jana.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Mwezi mtukufu wa Ramadhani udumu sana kwa sababu umefanya watu wamrudie Mola wao kwa kuvaa kama alivyoagiza, hata kama ni mavazi tu!!

    ReplyDelete
  2. siyapendi hayo mavazi mimi.....jamani

    ReplyDelete
  3. We anony wa pili kama huyapendi hayo mavazi, mpango wako! Na hiyo ndio sitara kwa kweli, I wish tuendelee kuvaa hichi kivazi cha heshima kabisa.

    ReplyDelete
  4. Miye ananimaliza Bint Makamba,Mwezi Mtukufu hijabu na nguo ndefu mpaka miguuni. Ukiisha Mwezi Mtukufu kichwa wazi kama Flavian Matata na mafasheni kwa kwenda mbele kama Naomi Campbell.

    ReplyDelete
  5. Wewe Mdau wa pili hapo juu kama uyapendi hayo mavazi ni kivyako loo! kwani sisi ndio tunaamini kua ndio mavazi mazuri kwa wale wanaofuata Dini kwa Waislamu wote duniani

    ReplyDelete
  6. Anon wa pili hivi huwa ukikutana nao bararani waliovaa hivyo huwa unafanyaje?? maana duniani kote hata uwe wapi utakuna nao tu labda uhamie sayari nyingine

    ReplyDelete
  7. Anon wa pili, angalia na kwenye mazishi ya askofu, utayaona kwa dini zoote.

    ReplyDelete
  8. Ukiona unakereka na mavazi ya watu basi ujuwe una matatizo angalau mawili:
    1. Si mvumilivu wa kidini
    2. Una Udini: Usimchague jamaa 2010 kwa sababu anavaa hivyo.
    3. hujakuwa kimawazo huru (unadhani jamii ni HOMOJINIAZI). demokrasia kwako bado ni kichwa cha habari. Hujui kama kuna uhuru wa kuchagua vivazi chini ya ulinzi wa kisheria.

    ReplyDelete
  9. we anony wa pili una matatizo gani kichwani mwako, kama huyapendi ni wewe ambaye umezoea kukaauchi usiye jistiri, mwanamke stara babuee, sehemu nyingine haziruhusiwi kuonekana na mtu yeyote zaidi ya MR ndio aneruhusiwa nani kwambie mimi mkristo naninalifagilia saaaaana tena kwa saaaaaaana kwa raha na isitoshe ninayo kila rangi nitapiga picha niweke kwenye blog ya jamii. nivazi ambalo nila kiukweli kila mtu analikubali, sijui wewe ajuza. INAHUSUUUUUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  10. Kila siku Mwamvita Makamba...Misupu ndo maandalizi au?

    ReplyDelete
  11. M.k.a.T.O.L.i.K.iAugust 26, 2009

    Ndugu zangu tuache unafiki, kwani vazi ndio linamfanya mtu amrudia muumba wake. Kama inakubidi usubiri mpaka wakati wa mwezi fulani ndio umjue Mungu wako, then wewe ni mnafiki, na wanafiki wanapigwa vita katika dini zote!

    ReplyDelete
  12. Mwanangu MWAMVITA YAANI UMEMFUNIKA
    KABISA KELVIN TWISTER!!He is nowhere near to be seen or felt!!

    Thank you my lovely intelligent Daughter!

    Proud Dad!
    DAD!

    ReplyDelete
  13. michuzi anammmaindi mwamvita...kaolewa jamani haha

    ReplyDelete
  14. Anony wa pili kama huyapendi wewe sisi tunayapenda na tunaona raha kila tunapovaa maana tunaheshimika kuliko tukivaa vimini.

    ReplyDelete
  15. hehe anony wa pili anafuata utmaduni wa kimagharibi.waarabu walieneza sana dini ya kiislamu na wamisionari kutoka magharibi walieneza dini ya kikristo.hapo ndo utajua tofauti ya titamaduni baina ya hizi dini mbili nchini mwetu. ukiendelea kujiumiza kichwa utakuwa na upungufu wa akili.

    ReplyDelete
  16. Haya ndiyo matunda ya free market capitalism. Vodacom endeleeni na mchango wenu kwa jamii. Makampuni mengine yaige mfano huu wa Vodacom.

    ReplyDelete
  17. Kama Mkatoliki alivyosema Mavazi siyo kigezo cha kujionyesha mtakatifu mbele za Mungu. Unatakiwa kumtukuza mungu na kuwa msafi kiroho kila wakati.Sio mwezi mtukufu ndio unajifanya upo karibu na Bwana God au X-MASS na Pasaka ndio uvae nguo za Heshima. Baada ya hayo mapito unarudi kule kule ulikozoea. Hasaidii

    ReplyDelete
  18. Big up wakinamama. Mashallah mmependeza sana. Inshallah Mwenyezi Mungu atatusikiliza na kutusamehe madhambi yetu waislamu wote tunaofunga mwezi huu mtukufu. Big up Vodacom kwa kuongoza...

    ReplyDelete
  19. BintiSheriaAugust 27, 2009

    Jamani nyie mnaomsema huyo anonymous wa pili aliyesema hayapendi hayo mavazi, kama vile mnavyosema mna uhuru wa kuyapenda au kuyavaa hayo mavazi na yeye pia ana uhuru na haki ya kusema kama hayapendi au la. Binafsi kama muislamu sikubaliani na hoja yake ila namchukulia kama alivyo na haki ya kusema anachokipenda au la. Kama mimi leo nikisema sipendi keki, je nimemtukana mpika keki au mlaji wake? La hasha. Watanzania tujifunze kuchukuliana na kuelewa kwamba kila mmoja ana mapenzi yake na ana haki ya kuyajadili popote as long as hajamtusi mtu yeyote.

    Big up to freedom of expression!!!

    Asanteni, ni hayo tu.

    ReplyDelete
  20. JAMANI NINA SWALI...MBONA WATU WAMEPUNGUA KWENYE MABAA NA MADISCO BONGO?

    MDAUZ

    ReplyDelete
  21. Anon wa Thu Aug 27, 10:05:00 AM, mshauri kwanza huyo unayemtetea kwanza akubali kuwa watu wana uhuru wa kuchagua makazi si kumfurahisha yeye bali Mola wao na nafsi zao.

    Labda kama unatushauri tupuuzie uchizi wake.

    ReplyDelete
  22. Anon wa Thu Aug 27, 04:25:00 PM, kwa maoni yangu,

    Dini ya kiislamu inasema watu wataenda mbinguni kwa imani na matendo.

    Imani inahesabiwa kisiri na Mungu. Matendo yanahesabiwa kwa siri na dhahiri. Kanununi ya kwenda mbinguni ni

    Net score = (score za imani na matendo mazuri - score za dhambi ) > 0.

    NB: score ziko weighted. Imani na matendo lazima vyote viwepo pamoja si kimoja tuu.

    Waislamu huhimiza kuifanya figure iwe kubwa. Si lazima kuwa uliwaona baa basi utawaona motoni, hapana.

    Dini tofauti zina kanuni tofauti ya kwenda mbinguni. Wako ambo imani pekee inatosha (wasfisha moyo).

    ReplyDelete
  23. Ufaransa tayari kuvaa mavazi kama hayo ni MARUFUKU.Denmark ndio wanaanza kupiga marufuku nadhani kuanzia mwezi ujao tu mambo yatajipa.watu tunalipa kodi zetu halafu wao wanapita kwenye barabara zetu huku wamejiziba uso na mwili mzima bwana.TUNATAKIWA TUFAIDI JAPO KWA MACHO HATA KAMA WANA WAUME NYUMBANI SIE TWAHITAJI KUONA TU NA SIKUGUSA.INANIKERA SANA UTAKUTA BINT KAUMBIKA HASWA LKN KAJIFICHA MTU HUWEZI HATA KUMUONA I HOPE NA BONGO NAKO WATAPIGA MARUFUKU

    ReplyDelete
  24. Anon wa Fri Aug 28, 08:42:00 AM, kwamba wanawake wa kiislamu ni masikini saana hawawezi kulipa kodi?

    ReplyDelete
  25. Anon wa Fri Aug 28, 08:42:00 AM, hutwo tunchi unataja tudogo na hatuna sauti duniani.

    Sikia mavituz kutoka masteti, mzee Barry alisema inakuja sheria ya kuwakaba wapata kichefuchefu wakiziona.

    Achana na taifa kubwa, uhuru na demokrasia duniani.

    ReplyDelete
  26. Anon wa pili, laa, dini yako inafundisha chuki?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...