naibu waziri wa habari na michezo mh. joel bendera (shoto) akikabidhi hundi kwa katibu mkuu wa tff frederick mwakalebela ambazo zitasaidia kuendesha ligi kuu ya vodacom inayoanza hivi karibuni kwenye sherehe za kukabidhi fedha na vifaa iliyofanyika hoteli ya giraffe motel jijini dar leo. wengine katika picha ni mama yasoda naibu mkurugenzi wa michezo, bosi wa mssoko wa vodacom ephraim mafuru, na meneja wa udhamini wa vodacom
mh. bendera akikabidhi kifaa cha kubadilishia wachezaji kwa makalebela
gebo peter ambaye ni kiongozi wa manyema fc akipokea vifaa
afande akipokea vifaa kwa ajili ya JKT Ruvu

Kiongozi wa Lyon akipokea uzi wao
Azam FC nao wakabidhiwa vyao
simba ya yuda mwina kaduguda akipokea vifaa kwa niaba ya simba

abdul masmaki apokea vifaa kwa niaba ya kagera sugar na mtibwa
lucas kisasa wa yanga akipokea vifaa vayo


Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imekabidhi vifaa vya michezo kwa Vilabu vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, alikabidhi vifaa hivyo kwa wawakilishi wa vilabu na kuipongeza Vodacom kwa udhamini wake huo.Vifaa hivyo ni kwa msimu wa mwaka huu.

Naye Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza alisema udhamini wa Kampuni yake kwa Ligi kuu ya Vodacom umekuwa ukiboreshwa mwaka hadi mwaka.

Alisema msimu uliopita udhamini wa Vodacom kwa TFF ulikuwa ni karibu shilingi milioni 600, udhamini wa vifaa kwa timu ulikuwa shilingi milioni 230 wakati promosheni ya soka kwa mikoa isiyo na timu kwenye Ligi Kuu ya Vodacom ilikuwa ni shilingi milioni 150, jumla ilikuwa ni shilingi milioni 850.

Alisema mwaka huu, udhamini kwa TFF ni shilingi milioni 613, vifaa milioni 260, promosheni ni shilingi milioni 200.

“Bado tuna kusudia kuboresha udhamini wetu mwaka hadi mwaka,” alisema
Alisema mkataba huo wa udhamini unahusisha gharama za vifaa michezo pamoja na usafiri kwa vilabu vyote, gharama za uendeshaji za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), posho za Waamuzi na Makamisaa pamoja na usafiri kutoka kituo kimoja kwenda kingine ikiwa ni jumla ya shilingi Bilioni moja na Milioni mia moja.

Alisema mbali na mchezo wa Soka kwa timu za wakubwa, Vodacom Tanzania imekuwa ikishiriki katika soka la vijana.

“Tuna programu za kusaka na kuviendeleza vipaji vya soka kwa vijana maarufu kama Vodacom Global Soccer Star (VGSS) na pia tunadhamini kituo cha kuendeleza soka kwa Vijana yaani Tanzania Soccer Academy (TSA,” alisema






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. mambo mswano, vifaa na pamba za uhakika. kazi kwa vijana wetu sasa kucheza mpira wa kiwango.

    ReplyDelete
  2. sasa ule uzi wa simba tulionyeshwa jumamosi iliyopita watachezea mechi gani au mchangani?

    ReplyDelete
  3. jamani Kaduguda anahitaji ushauri wa dressing, yeye ni kiongozi wa timu kubwa, na muonekano wake akiwa nadhifu ni kitu cha muhimu.

    ReplyDelete
  4. haya haya haya haya vifaaa hivyo kazi kwao.Halafu viongozi wa soka wajue mavazi ya aina gani ya kuvaa sehemu ya aina gani kama kadu anatia aibu halafu nasikia katibu wa kuteuliwa simba aibu tupu kama sio msomi bwana.

    ReplyDelete
  5. Huyu ni Gebo Peter yule aliyekuwa mchezaji au jina tu?

    ReplyDelete
  6. Katika hao wote naona kiongozi wa Azam ndiye amevaa kama mwanamichezo!!!

    ReplyDelete
  7. Mie yanga lakini huwa namzimia sana kaduguda, kwa mambo yake tu.

    Naam mambo ya kutumia chaki kubadilisha mchezaji ama kuonyesha mda tunayaweka kwenye kapu la 'enzi za mwalimu'

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...