Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imekabidhi vifaa vya michezo kwa Vilabu vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, alikabidhi vifaa hivyo kwa wawakilishi wa vilabu na kuipongeza Vodacom kwa udhamini wake huo.Vifaa hivyo ni kwa msimu wa mwaka huu.
Naye Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza alisema udhamini wa Kampuni yake kwa Ligi kuu ya Vodacom umekuwa ukiboreshwa mwaka hadi mwaka.
Alisema msimu uliopita udhamini wa Vodacom kwa TFF ulikuwa ni karibu shilingi milioni 600, udhamini wa vifaa kwa timu ulikuwa shilingi milioni 230 wakati promosheni ya soka kwa mikoa isiyo na timu kwenye Ligi Kuu ya Vodacom ilikuwa ni shilingi milioni 150, jumla ilikuwa ni shilingi milioni 850.
Alisema mwaka huu, udhamini kwa TFF ni shilingi milioni 613, vifaa milioni 260, promosheni ni shilingi milioni 200.
“Bado tuna kusudia kuboresha udhamini wetu mwaka hadi mwaka,” alisema
Alisema mkataba huo wa udhamini unahusisha gharama za vifaa michezo pamoja na usafiri kwa vilabu vyote, gharama za uendeshaji za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), posho za Waamuzi na Makamisaa pamoja na usafiri kutoka kituo kimoja kwenda kingine ikiwa ni jumla ya shilingi Bilioni moja na Milioni mia moja.
Alisema mbali na mchezo wa Soka kwa timu za wakubwa, Vodacom Tanzania imekuwa ikishiriki katika soka la vijana.
“Tuna programu za kusaka na kuviendeleza vipaji vya soka kwa vijana maarufu kama Vodacom Global Soccer Star (VGSS) na pia tunadhamini kituo cha kuendeleza soka kwa Vijana yaani Tanzania Soccer Academy (TSA,” alisema
mambo mswano, vifaa na pamba za uhakika. kazi kwa vijana wetu sasa kucheza mpira wa kiwango.
ReplyDeletesasa ule uzi wa simba tulionyeshwa jumamosi iliyopita watachezea mechi gani au mchangani?
ReplyDeletejamani Kaduguda anahitaji ushauri wa dressing, yeye ni kiongozi wa timu kubwa, na muonekano wake akiwa nadhifu ni kitu cha muhimu.
ReplyDeletehaya haya haya haya vifaaa hivyo kazi kwao.Halafu viongozi wa soka wajue mavazi ya aina gani ya kuvaa sehemu ya aina gani kama kadu anatia aibu halafu nasikia katibu wa kuteuliwa simba aibu tupu kama sio msomi bwana.
ReplyDeleteHuyu ni Gebo Peter yule aliyekuwa mchezaji au jina tu?
ReplyDeleteKatika hao wote naona kiongozi wa Azam ndiye amevaa kama mwanamichezo!!!
ReplyDeleteMie yanga lakini huwa namzimia sana kaduguda, kwa mambo yake tu.
ReplyDeleteNaam mambo ya kutumia chaki kubadilisha mchezaji ama kuonyesha mda tunayaweka kwenye kapu la 'enzi za mwalimu'