Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Amir Kificho akiwa na mgeni wa heshima siku hiyo Mkuu waMkoa wa Arusha Mh. Isidori Shirima
Mwenyekiti wa Arusha Wazee Danford Mpumilwa (mwenye spycoat) akikabizi zawadi ya set mbili za jezi kwa Mweyekiti mwenzake wa Zanzibar. Mhe. HamzaHassan Juma ambaye vilevile ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi.Wanaoangalia ni kutoka kulia, Kingdom Mwanguku, katibu wa Wazee na Bw.Zamberakis, Meneja wa Kanza wa Masoko na Mauzo wa Vodacom waliodhaminimichezo hiyo.

Kamati ya Ufundi ya Wazee wa Arusha ikifuatilia mpambano, kutoka kushotoChief Mirambo, Mzee Mgaya na Mzee Sanda.

Mashabiki walijaaa kuangalia mpambano huo.
Kamati ya Ufundi ya timu ya Wawakilishi ikijishauri, kutoka kushoto,Mhe.Haji Kheri Omar, ambaye vilevile ni Mnadhimu Mkuu wa Baraza la Wawakilishi,Mhe. Machano Othman, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mwasiliano na Usafirina Mhe. Mustafa Mohamed Ibrahim, Mkuu wa Mkoa, Kusini Unguja.

Mambo hayawezi kunoga bila msosi wa nguvu mwisho wa siku.
Bro Michuzi,

Happy Birthday ya Miaka Mitano

Pamoja na kwamba kiwanda cha General Tyre cha Arusha kimefungwa lakiniuwanja wake wa mpira wa miguu bado unawakamoto kwani ndiyo makao makuu yatimu ya Arusha Wazee Club.
Na Jumapili hii mambo yalikuwa makali zaidi paletimu hiyo ya Arusha ilipowakaribisha Wajumbe, karibu mia moja, wa Baraza laWawakilishi la Zanzibar, wakiongozwa na mawaziri wapatao kumi na Spika waBunge Mhe. Idi Pandu Kificho.
Michezo mingi,ya kuvuta kamba, kufukuza kukuna kukimbia ndani ya gunia iliandaliwa na mwisho ndiyo kikapigwa kipute chaboli ambapo ngoma ilikuwa droo kwa kufungana 1-1.
Hii yote ilikuwa baada yaWajumbe hao kutembelea park ya Lake Manyara na maonyesho ya Kilimo ya TASOhapo Nanenane grounds. Safari ya Wawakilishi ilidhaminiwa na VodacomTanzania, AICC, Tanzania Breweries Ltd. Bonite Bottlers Ltd. na Wazee wenyewe.

Mdau wa A-Taun






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mzee wa Libeneke sahihisho Spika wa Zenji anaitwa Pandu Ameir Kificho na sio Juma kama ulivyoeleza.

    ReplyDelete
  2. kaka.. huyo VTL Arusha ni TZAMBURAKIS, na sio ZAMBERAKIZ

    ReplyDelete
  3. sasa ni Juma Ameir Kificho au Iddi Pandu Kificho?? vipi tena mzee wa libeneke!!!!?? Usahihi ni Pandu Ameir Kificho kama alivyoeleza mdau hapo juu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...