












Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
naona ilikuwa ni who's who
ReplyDeletePumzika kwa amani, japo ni uchgungu kwa waliobaki, tangulia katika makao ya milele......
ReplyDeleteKelvin, Doncaster
Mmh, naona hapo wenye mi-kanga walisogezwa nyuma kabisa wasiharibu mandhari.
ReplyDeleteIt's HARD to beleive you (Anita) have departed from us. R.I.P.
ReplyDeletePoleni wanadugu kwa kumpoteza mama/ dada/ mtoto wenu. May you find consolation in prayer.
ReplyDeleteVilevile hongera kwa kamati ya mazishi kwa kufanya mazishi ya heshima namna hii. A real officer's funeral.
Mungu wa neema ailaze roho ya marehemu pema peponi...jamani naona mazishi TZ sikuhizi ni babu kubwaaa yaani hakuna tena makanga kanga naona na maglass ya jua watu wameyapigilia si utani!!!!mmmmm..Nimeshangaa kidogo kitu ambacho sikuwahi kukiona BONGO...hayaaa, asanteni sana..
ReplyDeleteKwa kweli inasikitisha sana,pumzika kwa amani dada Mary.Ila jamani hata mkiniita mshamba basi,lakini toka tumeona msiba wa Michael Jackson kwenye tv kila msiba sasa hivi watu wanaacha khanga,wanavaa suti na miwani ya jua.Huku marekani ni culture kuvaa suti nyeusi kwa sisi wabongo wanawake tulikuwa tunavaa khanga.
ReplyDeleteKaka Issa,
ReplyDeleteTeknolojia inabadilisha mambo mengi sana, siku hizi mtu akifa mie naona kama ni sherehe fulani vile kwani hebu angalia ndugu zake na marehemu walivyopendeza. Msiba ukitokea unaanza kuwaza nitavaa nguo gani? huko tunakoelekea sijui, anyhow, Poleni sana wafiwa.
Jamani dada Anita siamini kama umetutoka. Nakumbuka ulivyo tusaidia mimi na rafiki yangu tulivyokuja NEMC kwenye field 2003. Dada mwenye huruma na upendo,wala ubaguzi siamini inabidi nifute namba yako kwenye simu.. haupo nasi tena.!!!!.
ReplyDeleteMungu akupumzishe pema na awajalie wanao amani, upendo , furaha na maisha bora.
Its hard to believe..Anita Ngowi R.I.P.
We anony 09:09:00 usitutie haibu, nani kakwambia tumeiga kwa michael jackson, ni kwamba sio kila msiba unatoka kwenye blog, ninao msiba nilihudhuria hapa dar miaka miwili iliyopita wafiwa walikuwa suti za nguvu na huyu marehemu alikuwa na mtoto mmoja tu wa kike nae alivaa suti moja matata na kofia kali sana na miwani ya jua. hata kabla michael jackson hajawaziwa kufa.
ReplyDeleteNa pili naomba nikufahamishe kwamba msiba ni sherehe ya mwisho, kama uwezo upo unaruhusiwa kufanya vikubwa hata zaidi ya hapo.
Nihayo tu
We Anony wa kwanza hapo, nathani inakuwa si ustaarabu kutotambua mchango wa huyu mama na ukumbuke kwenye mazishi si sehemu ya kuanza kukejeli ati who is who huwatendei haki ndugu wa marehemu walio na uchungu wa kupotelewa na mwenza wao! Mungu amrehemu na apumzike kwa amani amina!
ReplyDeleteMungu amweke mahali pema peponi.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa, wazazi, watoto, ndugu, jamaa na marafiki.
Hivi heshima za mwisho zilitolewa wapi??
Amaa kweli 'MAENDELEO' hivi huyo ni mama mzazi wa marehemu au ni mama wa kambo,pomoja na hao wadogozake?Nadhani mtakua mnanielewa.PILI japo hili Ni TOO PERSONAL, Nilikua nataka nitoe pole zaidi kwa MUME wa marehemu lakini sikuona alipooneshwa katika sherehe hii.
ReplyDeleteNAWAKILISHA
kwani alikuwa anaumwa nini?
ReplyDeletesidhani kama kanga ndiyo kielelezo cha machungu na majonzi katika msiba. mkumbuke kwamba waswahili huvaa kanga katika harusi na ngoma pia.
ReplyDeletepia sidhani kama wale wanaovaa kanga kwenye misiba huchagua zile kuukuu au chafu.
R.I.P MARY NGOWI. POLE KWA WANAFAMILIA, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.
"siku hizi tumeendelea sana bwana, angalia kwenye misiba, no mi-khanga khanga, tunavaa miwani ya jua, jeneza expensive, kama tupo ma_mtoni vile, swaaaaafi sana, na ngoja afe mtu mwingine munione suti yangu mpya, na tai yangu ya ki-french kravat"
ReplyDeleteMdau
Wazungu kwenye mazingira ya jua kali kama haya, wasingevaa hayo masuti meusi.
ReplyDeletePole kwa wafiwa watoto, wazazi ndugu na marafiki wa marehemu. Ni pigo kubwa kwa familia ukichukulia watoto walioachwa na mafanikio ya kimaisha aliyokuwa nayo.
ReplyDeletePia niiopongeze kamati ya mazishi kwa kazi nzuri ya kumuaga. Alikuwa ni kipenzi, ameishi na watu vizuri, na anaagwa kwa heshima zote anazostaili.
Mungu amlaze mahali pema peponi - Amen.
Aliyeuliza huyo ni Mzazi wa marehemu. Sema kwa sababu hii sio msiba wa kiswahili hamna haja ya kuvaa Khanga na vilemba. Mikoa na makabila mengine wanawake wako huru kuvaa wanavyotaka ili mradi kuna heshima. Kanga ni kitambaa cha kujifunikia wakati unapika au kusafisha kitu, kufua nguo ili vazi la ndani lisiharibike. Saa nyingine ni kujaribu kuficha maungo kama vazi ulilovaa unaona halitoshi kufanya hivyo. Lakini sio vazi la kuendea sehemu maalaumu mfano hata kanisani. Tena mama wa heshima sana huyu na watoto wake ni wenye mafanikio. Pole mama Ngowi na msiba
ReplyDeleteKweli we sarcasticumepinda. imawezekan mtu mwingine atakayefuata kufa ni wewe.
ReplyDeletehiyo suti mpya utaivalia wapi?
This was a natural death, R.I.P sis Ngowi.
ReplyDeleteInabidi tujue kuwa hata ukijigaragaza chini bado kifo ni kifo tu.Ni bora ukasheherekea maisha ya mwenzetu aliyetangulia na kusifia yale mema aliyotenda duniani kwa faida ya waliobaki.
Nawapongeza kamati iliyoandaa,huyo dada ni kijana mdogo lakini heshima yake kwa waliobaki imeongezeka.
Wafiwa poleni sana na Muumba mpokee marehemu katika ufalme wako.
ReplyDeleteKuhusu mavazi ya suti za ulaya katika misiba ni mada halali na tunahitaji tuiweke katika mawanda mapana. Mavazi ni sehemu ya utamaduni na utamaduni hubadilika. Kubadilika kwa utamaduni si lazima iwe kuiga kila mtu mwingine afanyacho. Utamaduni unaweza kubadilika ndani kwa ndani kwa kuchanganya miensendo ya ndani na yale ya kutoka nje. Tatizo letu Bongo tumekuwa malimbukeni kwa maana tunaiga bila kuchuja. Utandawazi unatudumaza sana. na hii ninafikiri ni kutokana na kile kipindi cha ujamaa kilichokuwa kinasisitiza ubunifu badala ya kuigaiga. Ni kweli msiba ni sherehe ya mwisho ya binadamu, lakini bado tulikuwa na uwezo wa kubuni mavazi yetu mazuri kwa sherehe kama hiyo kama tusingukuwa tumedumazwa na huyu mdudu utandawazi. Si dhani kama kweli mama wa marehemu ametendewa haki kuvalishwa suti. Kwa mfano, khanga ni vazi linaloheshimika na siku hizi tunaona hata baadhi ya viongozi wa kike wanabeba upande wa khanga mabegani katika halfla rasmi. Ubinifu huo huo ungeweza kuingizwa katika misiba. Kama tungepata vazi la khanga angaa kwa akina mama watu wazima, kwa wale wenzake mfiwa wasiokuwa na uwezo wa kununua suti siku hiyo hiyo ya msiba wataweza kujumuika naye bila kutengwa kwa vile tu wamevaa khanga!!! Ndiyo kuiga sawa, ndiyo uwezo wa pesa sawa, ndiyo kumfanyia ndugu sherehe ya kumwanga sawa na haki, ndiyo kwenda na wakati sawa, LAKINI jamani tutumie zile za kichwani badala ya za miguuni!!! kifo ni kifo na kamwe hakitakuwa harusi!!!
jamani mavazi kama khanga sio kwamba yanaonyesha eti wewe ndo unauchungu sana, hawa wafiwa wanauchungu sana na ndugu yao nao wameamua kusindikiza safari yake ya mwisho kwa heshima zote...wewe unaesema baada ya kifo cha michael jackson watu wamebadilika pole sana, watu kuvaa hivi kumeanza siku nyingi tu mwaka 1999 nilienda kwenye msiba wa mzee nkya, mke wa marehemu na watoto walikuwa wamevaa suti hata sie waombolezaji wengine tulijiona wachafu ila ukweli ulibaki pale pale wao walikuwa na uchungu zaidi yetu...jamani rudini bongo muone maendeleo sio mseme tunaiga toka huko nje!!!
ReplyDeleteEternal rest grant to her, O Lord. And let perpetual light shine upon her. May she rest in Peace. Amen
ReplyDeleteHenry Kapalata
Wichita, KS.
Nilikuwa sitaki kuchangia lakini nimelazimika. kwanza poleni sana wote mlioguswa na msiba wa Dada Mary Anita Peter Ngowi.
ReplyDeleteyangu machache ni kwamba mavazi katika msiba ni uamuzi wa familia au taasisi aliyofanyia kazi marehemu. napenda kusema kwamba marehemu mary alikuwa mwanasheria, na naamini wanasheria mavazi yao ya kazi ni black and white, basi naamini uamuzi wa kuvaa suti ni kutokana na kujaribu kumuenzi marehemu katika wadhifa wake aliokuwa nao na sijawahi kuona eti mwanasheria eti akavaa shabby lazima awe smart na usmart huo ni suti ndo vazi la kuonekana. mbona sijawi kuona mkihoji manesi, askari polisi, jeshi wanapovaa mavazi yao ya kazi wanapokwenda kuzika mwenzao???? ila hili la huyu dada ndo limewaudhi. miwani ni katika kupunguza mwanga yeyote anaruhusiwa.
uchungu wa kufiwa si lazima uonekane kwa kuvaa khanga.napongeza kamati ya maandalizi it was nice job.
ni hayo tu
kuna watu wanajidai wanajua mila na desturi sana humu ndani kwani huo msiba ulikuwa unawahusu? ndio wamevaa suti nyie ndo mnajidai mna uchungu kuliko wao???? ati ooh mama wa marehemu sijui asingevaa suti mlitaka avae kaniki acheni upuuzi wenu hapa ndio walivyoamua kumuaga mpendwa wao kwa heshima zote mlitaka wavae kanga ili iweje??? ...MBONA JUMAA KUU YA PASAKA HAMVAAGI KANGA? SI TUNAPIGA PAMBA ZA BLACK?? AU KIFO CHA YESU HAMNAGA UCHUNGU ACHENI UMBEYAAAAAAAAA
ReplyDeletepoleni saana wafiwa Mungu awape nguvu hasa katika kipindi hiki cha majonzi
miss michuzi
may the Almighty God rest her soul in peace, Amen
ReplyDeleteIla kusema ukweli msiba umependeza, yani kwa haraka haraka huwezi kuamini hapo ni bongo, tena kinondoni makaburini. watu wamelipuka, tena very smart, afu watoto kama wamevaa sare kiaina. Mi nilikuwa naona wazungu, na kiafrica africa, wanigeria, ila kibongo bongo, nilikuwa sijawahi kushuhudia. Tofauti ipo, uki-compare na zamani, this is way different. they look good though wana uzuni.
we anon wa 5:7:00 hayo masharti yako uyapeleke huko kwenye ukoo wenu na usitake kulazimisha watu fikra zako mbovu na ukumbuke pia kwa sisi wakristo tunaamini mwanadamu ana arusi tatu za maisha kuzaliwa, arusi kufa kama hujui utajiju na pia kulia saaana kwenye msiba sio kwamba ndo una uchungu sana siku zooote tunajua vazi jeusi ni la kwenye misiba ni wapi imeandikwa kanga ivaliwe misibani??? mambo yanaenda yakibadilika sio tukangamale na mila za kizamani tuuuuuuuuuuu kama wewe
ReplyDeleteHuyu Sarcastic ni mtu intelligent sana, na wewe uliyesema kwamba Sarcastic amepinda ni wazi hujui maana ya Sarcastic. Mimi nimeuelewa ujumbe wake vizuri sana. Katizame Dictionary maana ya Sarcastic kisha njoo hapa umsome tena ndo utaelewa alichokisema.
ReplyDeletePole sana familia ya Ngowi. Kweli kifo chake kinasikitisha.
ReplyDeleteRest in Eternal Peace Mary Anita.
Poleni sana Familia ya Ngowi,Bamamongo(Birmingham,Alabama) tupo na wewe Gerard,Deo na wengine wote kwenye kipindi hiki cha machonzi.MUNGU AMETOA MUNGU AMETWAA !!
ReplyDeleteREST IN PEACE ANITA MARY NGOWI.
Tuachane na ushamba twendeni na wakati MISIBA ya KILEO tuna furahia maisha ya marehemu nakuongelea MEMA yote aliyoyafanya na legacy alizoacha. ANITA alikuwa msaidizi sana alikuwa mtu wa watu ndiyo maana sisi ndugu jamaa na marafiki tumeamua kumuenzi kwa mema yake.... Na siku ya mazishi yake tulikuwa tuna-celebrate maisha yake na yote mazuri aliyotufanyia..! R.I.P ANITA wewe umetangulia sisi tunakufuata...
ReplyDeleteMdau
Overseas
kwanza itanibidi niseme kwamba inaonekana huyu binti alikua ni mtu hodari sana kwasababu sijawahi kuona msiba wa kibongo ambao umeleta historia sana.kimavazi...chakula...jeneza..mapambo, na hizo miwani ni balaa(mambo yalikua ni ya gucci na versace usisahau dior).alafu huo mziki ulikua wa mzuri sana mpaka makaburini kulikua na mziki.
ReplyDeletekingine ni kwamba watu waliokuwepo ni watu wakubwa wenye wadhifa na vyeo vya nguvu.inaonesha jinsi huyu dada yetu alivyokua anaheshimika.
kusema kweli hii familia ni ya kipekee..yani hotuba za kizungu kwenda mbele...ilibidi uingie shule kidogo na wenyewe wamekaa kizungu kweli.
mmejitahidi sana..mungu ailaze roho ya huyu dada mahali pema peponi..amen.
Anita was beatiful na alikuwa akijipenda haswa, sasa leo kwenye msiba wake mkamvalie makanga yahusu nini???? hata mwenyewe asingefurahi, alipenda kuona mtu umebandiks kisawa sawa, uchungu wa kuondokewa upo pale pale uvae kanga, suti chupi etc. mmefanya vizuri sana wanakamati kuwezesha mazishi. kuhusu makingereza sijui lakini ndugu zake wote wameshuka toka majuu, labda wako more comfortable na kienglish je, kama we hukielewi basi kalagabaho nenda shule bwana utapitwa na mengi, dunia inabadilika, sio kila siku black and white kuna other colours. well done!!
ReplyDeletehuyo ndugu aliyezungumzia suala la ulimbukeni yuko sahihi. mara nyingi limbukeni hajijui. ni nani aliwaambia kuwa vazi rasmi la kanisani, au la uanasheria, au la kumpa heshima marehemu ni lazima liwe suti ya ulaya? tuambizane ukweli ni kwamba wabongo tumelimbuka kweli kweli.
ReplyDeletena je uchungu wa kuondokewa na mpenzi unakuwa umehifadhiwa wapi wakati ndugu zake wanahangaika kwenda saluni kutengeneza nywele na kufanya shopping ya suti ili kujiandaa na 'show business' ya mazishi?
kwa hakika kama ndio kazi ya pesa basi tunaanza kukufuru!!! kweli siku za Yesu kurejea duniani zimekaribia.
maskini dada ANITA!may u rest in peace. Dada Anita alikufa kwa cervical cancer na mdau juu alieuliza kuhusu mume wake jina sitaliachia hawakuweza kudeclare kama ni mumewe kwakuwa yeye alikuwa mke wa pili, Jamaa ameoa kwingine na anawatoto wengine watatu na mke wa kwanza. Tulikupenda zaidi Mary Anita may u rest in peace. CUTE, CLEVER,ila kaburi halichagui
ReplyDeleteWafiwa poleni sana. Mwenyezi Mungu amlaze marehemu mahala pema peponi.. Amen. Hivi huyu Roderick Ngowi ndiye yule tulikuwa naye Ruvu JKT Operation Miaka 30 ya Uhuru? Nilishamsahau lakini jina ni familiar.
ReplyDeleteMdau, Ulaya.
uliyeuliza ati mwili wa marehemu ulikuwa umehifadhiwa wapi wakati ndugu walikuwa saluni ovyo sana kwani mtu akifa anahifadhiwa darini?
ReplyDeleteIna maana ni kweli haya mazishi yalifanyika kwa lugha ya kiingereza? Kama ni kweli basi mimi sitaki tena kujihusisha na huu mjadala wa lugha.
ReplyDeletewe donald huna lolote usidhani kila mtu humu ndani umemzidi elimu ovyo tu wape pole wafiwa na sio ujidai we ndo unajua kiinglish fala wahed... poleni saaana wafiwa ingawa ukurasa huu umegeuka wa malumbano yasokuwa na kichwa wala miguu
ReplyDeletewabongo acheni maneno jamani, kai, Anita Ngowi katika uhai wake tunaomfahamu alikuwa MREMBO, ANAPENDEZA ANAJIPENDA, NA KUJUA KUVAA VIZURI. sasa kulikoni kwenye msiba wake mkavalie makanga inahusu? unayetaka kuvaa kanga vaa, kwani nani amekuzuia?
ReplyDeletePoleni sana familia, ndugu na marafiki.
Nimefurahi kumuona DOREEN NGOWI kalikuwa kembamba naona sasa amenona ana mwili, usijali dada ingawa ulipata matatizi kwa waingereza ukafatwa saa 12 za asubuhi na mtu wa idara ya uhamiaji, na kupewa masaa 24 kurudi bongo. Mungu si asumani umejaaliwa kupata mzungu wa maana akakurusha tena USWISS, hongera tunaona umependeza sana. na Dada huyu hana mchezo, tangu ujana, hataki kubabaishwa na wanaume wa kiswahili, awe mbongo au wa nchi nyingine. yeye ni wazungu tu. SAFI SANA.
HEEEEEEEE DOREEN NAKUONA HAPO, HUYU DADA NI WAZUNGU TUU KAMA KAWA.
ReplyDeletehahaha,nimecheka sana na comment za wajinga wengi.kuna kitu gani cha kubishana hapa.Ila dada ulikuwa mkali yaani hata siamni kama umeondoka.anyways its life.rest in peace.such a diva.
ReplyDeleteKaka Michuzi,
ReplyDeleteMbona huyu anony, Wed Sep 23, 03:14:00 hakujibiwa?
Kama kuna mtu anajua au alikuwepo atusaidie, heshima za mwisho zilitolewa wapi tunaona tu picha lakini hakuna maelezo ya zaidi.
Asanteni sana. Poleni sana wafiwa.
Dada Rose Chambe POLE sana kwa kumpoteza rafiki, shoga na ndugu yako! Pole nyingi kwako na marafiki wengine wa Anitha. Jamani poleni sana!!! Sote tuna natume mlilia sana Anitha. Si rahisi kwa kila mmoja wetu kuelezea anavyojisikia! Wengine hatukujaaliwa kuja mazikoni lakini tuna- na tutamkumbuka Anitha kwa mema yake...!
ReplyDeletePoleni sana wafiwa!
Mdau
heshima za mwisho zilifanyikia kwa wazazi wake umeshajua sasa inkupa raha gani? watu bwana na ukitaka kujua kwao ni wapi usome kuanzia walipoweka tangazo la msiba utajua kwao sio mnatuma ujumbe bila kusoma taarifa kwanza matokeo yake wengine wanauliza ati nini kimemuua? wakati imeandikwa hapo juu msomege kwanza ndo mtoe comment!!!!
ReplyDeleteNdio ni Rocrick Ngowi tuliekuwa naye RUVU JKT OPERATION MIAKA 30 YA UHURU.
ReplyDeleteKaka Michuzi,
ReplyDeleteMbona huyu anony, Wed Sep 23, 03:14:00 hakujibiwa?
JIBU: MAREHEMU ALIAGWA NYUMBANI KWAKE MAWENZI ROAD HOUSE NO.283 OYSTERBAY JIRANI KABISA NA SEHEMU INAYOTUMIWA KUJIFUNZIA MAGARI COCO BEACH Natumai nimekujibu...
Mimi sielewi kwanini watu wanapenda wazungu. Au labda ni katika kujaribu kujitafutia maisha mazuri zaidi. Ukweli ni kwamba Wazungu hawatupendi namna hiyo na nadhani kwa muono wao hawatuoni kama binadamu kamili, ni kama anakufanyia favor.
ReplyDeleteMsiba umekaa poa ila kasoro ni kwamba kama walifanya msiba kwa lugha ya kizungu hapo ndipo walipoharibu.
Acheni mambo ya kishamba nyie watu...na wewe wa mwanachi,haikuhusu kama yule ni mama wa kambo au mzazi...lakini kwa taarifa yako,yeye ndiye mama mzazi mwenyewe na pia hao ni dada zake....hizi ndio sababu kwanini tanzania haiendelei....watu huvaa suti kuonyesha heshima kwa wengine....R.I.P anita....you will always be remembered
ReplyDeleteheshima za mwisho za kumuaga marehemu ANITA NGOWI zilifanyika nyumbani kwa wazazi wake, ambako ndipo alipokulia marehemu tangu udogo wake mpaka alipomaliza masomo na kuanza kujitegemea, na ndipo hapo hapo alipozaa watoto wake wawili wa kwanza, Walter na Miriam. na ni ILALA SHARIFF SHAMBA. Natumaini nimejibu swali la wadau wachace waliokuwa na msisitizo wa swali hili na kutaka kujua kwa makini. Asanteni.
ReplyDeleteHakuna UTU tena Tanzania. Inasikitisha sana. Kukaa, na kuzungumzia appearence ni ufinyu wa akili.
ReplyDeleteSo what!!!
Poleni sana wakina Ngoi.
Nadhani uchungu wa ndugu hao sis wa nje hatuujui. Uchaguzi wa nini kuvaaa pia kwa wavaaji wa kanga na T shirt uko kwanini tunawazogoma wafiwa hawa? Waachiwe waomboleze wajuavo wao uchungu wao hatuujui sisi. Nguo zao sio zinazo omboleza. Poleni sana kwa msiba wenu. Siwafahamu lakini maoni mengine ni kama ya watu ambao hawajapata shida. Tuache hayo jamani. Tuwaliwaze kwa yaliyowafika wenzetu sio kuwazogoma.
ReplyDeleteTafadhalini tuache kumsema mtu ambaye hawezi kujitetea. Kila mtu ana chaguo lake, familia imechagua hivi na imekuwa. Mary shoga yangu pumzika kwa amani, mwenzetu umetutangulia na ulitayarisha njia yako ya kwenda mbinguni, ya kwetu hatuijui. Familia ya Ngowi na Tenga poleni sana. S. Toronto
ReplyDeleteWEWE MICHUZI ACHA USHAMBA WAKO LUSHA MAONI YETU YOTE ULIYOBINYA!!TUINUSURU NCHI IKWENDA PABAYA WATU WANAKUWA NA UMASKINI WA MAWAZO NA KUIGA CULTURE AMBAZO SI ZETU YANI USHAMBA UTATUPELEKA PABAYA.
ReplyDeleteHUO NI USHENZI KUTETEA UPUUZI MICHUZI TAFADHARI LUSHA COMMENT ZOTE ULIZOBINYA
mmmhhh!Alosema khanga vazi letu nani..?Mbona hilo tumeiga toka kwa wa-arab?Vazi ni uamuzi wa mtu mradi havunji heshima.Rest in peace Dada Mary.Tuache wafiwa waomboleze kwa amani.
ReplyDeletenaomba mjue kutofautisha aina za cancer, nenda kwenye kitengo cha cancer utaelimishwa zaidi kabla hujaandika kitu hukijui.kumbuka ni dakari wake tu ndie anaepaswa kutoa taarifa za mgonjwa na kwa idhini ya mgonjwa na sio vinginevyo.huyu aliyeandika cervical cancer you are wrong and you can be prosecuted to lable someone with wrong diagnosis.
ReplyDeleteJamani waswahili hivi education system yetu ndio pua au tumejaa roho za kwanini? yaani watu wanawakejeli wafiwa kisa wamependeza.. na roho dizaini hii tutafika kweli? How about acknowledging the fact that they are entitled to wear whatever the hell they want? Huku tunaita playa hatin' kuwa hupendi mwenzio akiwa nacho badala ya kuelevate your game.
ReplyDeleteTutafika lakini.
Mdau, Boston, US.
nakubaliana na maoni ya muungwana aliyesema UNAWEZA KUCHUKULIWA HATUA KWA KUTOA WRONG DIAGNOSIS YA MTU, ni kweli kabisa anayejua ni Daktari wake, wewe unayeingia hapa kusema alikuwa na CERVICAL CANCER kakwambia nani? sie wengine tulisikia ni CANCER YA MIFUPA aliyokuwa nayo ANITA NGOWI, lakini hatuingii humu kustate that fact. wewe haupishani na watu wengine waliokuwa wakizusha tangu alipoanza kuumwa kuwa alikuwa na AIDS. hata kama ni kweli hakuna mtu yeyote atakayeweza kuhakiki hili jambo, jamani mwacheni dada wa watu apumzike tu kwa amani.
ReplyDeletePoleni familia ya NGOWI. nilikuwa namjua DEO NGOWI, LAKINI HAPA SIJAMUONA KATI YA WANANDUGU, VIPI? TULISIKIA NAYE YUPO MAREKANI, SASA MBONA HAKUJA KWENYE MSIBA WA DADA YAKE?
pole sana MR. TENGA.
ReplyDeletenaona ni watu wachache tu katika blog hii wanaomrecognise mpenzi wa ANITA NGOWI. jamani si vizuri Mr. Tenga ni baba wa watoto wawili wa marehemu Anita. ndio ana mke wa kwanza na ana watoto wengine watatu katika ndoa yake. lakini Anita alikuwa kama mke wa pili na amezaa nae watoto wawili hata mkewe mkubwa hili jambo alilikubali na alikuwa akielewana vizuri na mkemwenzake. Swala Hili tunatakiwa wote tuliheshimu. Na tumsabahi na kumpa pole pia Mr. Tenga kwani ana uchungu sana. Napenda kuwakilisha.
Tutafika tu zamani watu kwenye harusi ilikuwa ni mabuibui na kanzu tu reception chai na maandazi lakini sikuhizi baada ya kuona vitu kama hivi watu wanapiga reception za nguvu suti na limos.
ReplyDeleteHivyo taratibu tu punde utashangaa watu watashusha suti. Pia namuunga mkono Mdau kwamba Kanga na Baibui ni mavazi waarabu, ni masalia ya culture za waarabu.
Mary kama walivyosema wengine alikuwa mtu wa watu. Alikuwa na marafiki wengi na wapenzi wengi pia. Kama sio umbea alikualika harusi yake na Tenga? Aliwaaeleza baba za wanawe? Ukizaa na mwanamke anakuwa mkeo?Unasemaje kwa uhakika kuwa Tenga alizaa naye watoto wawili wakati wengine wa karibu tunajua kuwa sivyo?Muacheni mtoto wa watu apumzike na mumuache Tenga pia na maisha yake kwani hayawahusu katu.Usimsemee mtu hata kama ni marehemu jambo usilopenda hata wewe usemewe, unajitakia laana ya bure.Mwogopeni Mungu. Kwa heshima nawasilisha.
ReplyDeleteNdugu zangu, Watanzania wenzangu, kiwango cha ustaarab hupimwa kulingana na mtu au hata taifa linavyoheshimu haki ya binadamu mwenzake hasa privacy yake. Ndio maana mtu akikuchungulia ukiwa chooni au chumbani uchi utamwona wa ajabu na wa kuonewa huruma kwa jinsi alivyokosa ustaarab. Sasa vipi mnajihusisha na private life ya mtu kiasi cha kuandika hadharani mambo binafsi ya Mary Anita kiasi hicho. Mbaya zaidi mtu huyo ni marehemu. Yaani mmekuwa wajima kiasi hicho? Ndio maana mmebaki mnashangalia miwani ya jua na suti. Jamani marehemu husifiwa tu, na hapigwi vijembe, mipasho wala kejeli kwa sababu hawezi kujitetea. Hivi ndivyo ilivyo duniani kote isipokuwa hapa kwetu kwa wachache wenu. Elimikeni jamani na muonyeshe ustaarab. Mnatutia aibu duniani.Mungu ailaze roho ya Anita mahali pema peponi na aipe moyo wa subra familia yake na hasa watoto wake.
ReplyDelete