Mwanamuzi maarufu wa kitanzania anayeishi na kupiga muziki wake nchini Uholanzi, Henry Galinoma (also known as - a.k.a) akila eid el fitri nyumbani kwa mshikaji wake Aboubakary Liongo mtangazaji wa dw ambapo walisherehekea pamoja na wadau wengine wa dw.Galinoma na Liongo ni watoto Kinondoni Muslim. Toka shoton ni Abou Liongo,Mrs Alma Liongo, Halima Nyanza(DW),Christiana, Galinoma a.k.a Buti Jiwe, Mrs Joyce Kitojo, Sekione Kitojo, na Mdau Imma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Kinondoni muslim ni chama kubwa.Hivi mwalimu OYA na SHARIF wapo wazima?

    ReplyDelete
  2. Michuzi kuwa specific. Liongo na Kitojo tunajua wapo Ujerumani. Sasa sherehe ilifanyika Uholanzi, Ujerumani au Dar? Wee vipi bwana!!

    ReplyDelete
  3. Nyakatakule Unyilisya EchaloSeptember 21, 2009

    Rekebisha:
    Hao hawapo Uholanzi bali Ujerumani!
    Najua kinachowachanganya watu ni pale mtu anasikia kuwa Waholanzi pia wanaitwa 'Wadachi' (Dutch) na wakati huo huo Ujerumani inatambulika kama 'Deutschland' kama vile Dutchland!!

    Ingawa kuna ushabihiyano fulani, Hizi ni nchi mbili tofauti kabisa tena zenye ukinzani wa jadi/kihistoria.

    ReplyDelete
  4. Hii ni issue ndogo, Wabong. Kwani kusafiri (hata kwa treni) kutoka Holland kwenda Germany inachukuwa muda? Ni mdomo na pua ati. Na visa ni hiyo hiyo moja (Schengen). Siyo issue kubwa - whether sherehe ilifanyika Germany or Holland...

    ReplyDelete
  5. ..mdau maelezo yako yanazidi ku-konfyuz!..sina hakika hata siku moja kuwa kuna kiswahili fasaha cha 'mdachi' kuwa ni mholanzi..hasha!, mholanzi ni mholanzi (anatoka uholanzi - netherlands sio holland)..'mdachi' ama jeremani, ni majina ambayo hususan mababu zetu waliwaita hawa ambao leo kwa kiswahili fasaha tunawaita 'wajerumani'..UzenG!

    http://answers.google.com/answers/threadview?id=138376

    ReplyDelete
  6. Unajua wabongo wenngi ndo tuko sampuli hizi za Echalo na huyo mwenzie hapo juu,Michuzi kaweka maelezo ambayo kwa mtu aliemaliza walau standard seven hayawezi kumchanganya.Hakuna kipengele kinachoonesha hapo ni Uholanzi,amesema akila sikukuu nyumbani kwa mshkaji wake.Ila huyo Galinoma ndo anaishi Uholanzi,sasa wabongo kama ilivyo jadi yetu watu wanakurupuka na kuanza kujifanya wanajua saaaana kufafanua Uholanzi na Ujerumani.Ulizani kwakuwa anaishi Uholanzi hatoweza kula sikukuu kwa mshkaji wake Bonn???? mnaboa sometimes, Eid moubarek wadau..........

    ReplyDelete
  7. Idd mubaraka njema Abou&Alma Liongo,
    pamoja na wadau wote wa Huko.

    mdau,
    Lusungo Ipinda Kyela Mbeya

    ReplyDelete
  8. Wabongo mnapenda kuwatoa wenzenu kasoro kwa kweli hata pasipo haja. Wapi hapo pameandikwa wako uholanzi. Aliyetajwa yuko Uholanzi ni Mwanamuziki Galinoma tuu anyeafanya shughuli zake huko. Otherwise hapo ni nyumbani kwa ABUU Liongo, na kichwa cha habari kimeshawataja wote na kina Kitojo ndiyo wadau wa BONN. Sasa BONN iko wapi kama si GERMAN(deutscland)

    ReplyDelete
  9. Jamani inawezekana kutembeleana kutoka nchi tofauti. Lipi la ajabu mtu anayekaa Uholanzi kumtembelea rafikie ujerumani? Hiyo haimaanishi wanaishi pamoja.Sijaona ujumbe unakosema wote wako ujerumani au Uholanzi, tuachekushambulia hata yasiyohitaji kushambuliwa. Tusome habari yote tupate ujumbe halisi kwanza kabla ya kuchoma baadhi ya maneno na kuyapa maana tunazofikiria wasomaji tofauti na ujumbe halisi.

    ReplyDelete
  10. kaka Abu Liongo umezidi kila kitu upo ukiende Bongo upo umefika Bongo je wakina Tido Muhando itakuja??

    ReplyDelete
  11. Eeh Kaka Michu, Inakuwaje leo ni tarehe 21/09/2009 lakini hiyo picha inaonekana ilichukuliwa tarehe 28/09/2009? Au hao wadau wanaishi sehemu ambayo kwao hiyo tarehe ilishafika na kupita? Halafu kama vile wengi wao hapo ni waandishi wa habari kwa hiyo sidhan kama yalikuwa ni makosa kwenye kamera seting!!

    ReplyDelete
  12. Nawatakieni kila la heri, sasa ninakubali kua, Kinondoni Muslim ni shule ya elimu dunia, vijana wanatuwakilisha Ughaibuni katika fani zao,Bwana buti Jiwe unaonekana unapiga nondo sana, naona kifua kimetanuka kama pawa Mabula .
    Mdau

    ReplyDelete
  13. Tunafurahi tukiwaona NDUGU zetu wanakumbukana huko MAMTONI, LAKINI INAKUWAJE WENZETU WAMEKULA IDD TAREHE 28/09/2009? wadau warekebishe TAREHE!!!!

    ReplyDelete
  14. Liongo hiyo suruali vipi, huyo si mkeo, hujamzoea tu?

    ReplyDelete
  15. TAREHE 28/09/2009? isiwashangzaze ndiyo matatizo ya kamera za kichina

    ReplyDelete
  16. jamani msiwashangae hao waramba vumbi waliopo bongo wao wanadhani kama ilivyokuwa mbinde kwao kupata visa basi hadi wengine hawawezi kusafiri kutoka uholanzi kwenda germany wanaona ni miuuuuuuuuujiiizaaaaaaa.kule kwetu bonde watu kama hao tunawaita MLANGO WA NANE

    ReplyDelete
  17. NDIO KUSEMA KULIKUWA HAKUNA MNUSO WA MAHANJUMATI? TUNAONA KUNA GLASS ZA MCDONALDS MEZANI,VIPI? WADAU MMESHINDWA KUMWAGA PILAU NA WESE?????

    ReplyDelete
  18. sasa hii tabia ya wanamziki kukimbilia chakula tabia gani?Michuzi tuwekee picha zao hao wanamziki wapo jukwaani ndio ofisi zao

    ReplyDelete
  19. Sebule utadhani si majuu bali ni Tandale kwa Mtogole!

    ReplyDelete
  20. Hej Alma, jeg kan godt ser du, du se flot ud, hvor du hen i tyskland? Jeg vil gerne besøge dig og din familie. knus sweden

    ReplyDelete
  21. Kaka Abou, tafadhali nitafute.

    Nduguyo, Holland

    ReplyDelete
  22. Mmeanza kunanga waswahili!!Hamuachi?Sebule inakuhusu nini?Weka yako tuone...

    ReplyDelete
  23. hao wanaochonga ni wabongo wachache tu ambao wanaharibu sifa nzuri waliyonayo watanzania. huyo aliyechonga keshapiga kazi mpaka sasa ana miaka 50 na ushee na hajafika popote....na anavyopenda sifa? angepata hiyo nafasi ya abuu pangekuwa hapatoshi...ndiyo maana unalaanika unazidi kutapatapa... vijana wanakuja wanapata michongo maskini ya mungu wanakuacha hapo hapo kila siku na bado utahangaika sana... mwenyezi mungu hapendi kabisa mambo ya mtu kumuonea wivu mwenzako. Iko siku utaumbuka tu, amini usiamini. kila mtu ameshajua kwamba una roho mbaya kwani hutaki wenzako wa shine ...Hongera Abuuu kwa kazi nzuri usimsikize huyo juha kwa vile shule ilimpiga chenga anaishi kiujanja ujana tu! penye mwanzo huwa pana mwisho!

    ReplyDelete
  24. huyo lazima atakuwa anko nanii!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...