mdau nambari wani wa cesena, italy, baraka wa chibiriti ndio ameshamaliza vekesheni yake hapa bongo na ameongea na globu ya jamii katika kuaga wadau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. blog ya jamii celeb.


    No way hata wazungu wanataka pc mpya.

    Kuna vitu vya zamani navinatakiwa kutunzwa lakini sio screen ya pc

    ReplyDelete
  2. i was one of wadau waliokupiga madongo but now i realize that you a such a good guy with charisma.
    big up chibi

    ReplyDelete
  3. chibiriti vp?mbona haujui kujieleza?mimi hua ninakufuatilia sana ktk blog hii ya jamii,lakini sijawahi kukusikia ukiongea,kumbe haujui kujieleza,noma chibiriti,kukaa kote mtoni haujui ukuhojiwa ujibu nini!!inaonyesha wazi kua wewe ni mpiga box tu,halafu wewe chibiriti ni mtu wa Kigoma?maana kiswahili chako kinanikumbusha kigoma,kama nimekosea basi nisamehe.

    ReplyDelete
  4. mzee mbona shallow sana,nilitegemea utajibu maswali ya bwana michuzi logically na intelligently kwani tunajua nyie watu mlio nje ya nchi mko exposed vilivyo kwani mmeona maendeleo ya wenzetu live.Jifunze kujibu maswali mzee,sio eti matatito mengi tuuu......sikumbuki,alah maana yake nini hapo?unalokumbuka tu ni congestion na sababu ni daladala,jibu sio timilifu kabisa,na maoni yako ya kutatua tatizo hili ni hewa hamna substance.Jonalists kama Mr michuzi wamesomea kuuliza maswali,sasa nyie watu wa nje mnatuangusha,saa nyingine eti mnaingiza vijimisamiati vya kiingereza ambavyo havileti maana.msikonde,mimi ni mdau ninayecheki mienendo ya watu wanaojifanya wanajua.
    poa baadae.

    ReplyDelete
  5. jamani we chibiriti una aibu kweli any way safari njema
    miss michuzi

    ReplyDelete
  6. Ngoja mie nimsaidie chibiriti.
    MATATIZO:
    1. FOLENI ZISIO TEMBEA
    : Barabara ziongezwe na miji ijitegemee,sio kila kitu mpaka mtu aende mjini au kazi zote zinakuwepo mjini.
    -USAFIRI WA DALADALA(public transport) uboreshwe ili watu waache kutumia magari yao kujazana mjini,sisemi wasiwe na magari.
    -Abiria waelemishwe umuhimu wa DEODRANTS kwani mtu akishika bomba yaani natamani kufa.
    -VUMBI nalo ni tatizo lazima watu wa city angalau wawe wanamwaga maji alfajiri kwani uwezo wa kupiga rami haupo.
    -FORENI KATIKA MABENKI,Haiwezekani mtu unatumia siku nzima uko Benki hapa lazima mabenki yaongeze mashine za pesa ktk kila Kitongoji na ku promote technologia hasa internet banking, telephone banking
    na kuanzisha self service cash/cheque deposit machines.Siongelei mabahasha hapa.
    -HUDUMA MBOVU kwa wateja kwenye sekta zote!Wafanyakazi wana lugha chafu kwa wateja,nyodo,na bado wanatoa huduma huku Mobile iko sikioni!! Sisemi wafukuzwe ila wapewe Customer service trainings!Pia hawa wafanyakzi wa serikali inabidi watambue kwamba hizo huduma wanazotupa sio za Bure,hasa mahospitalini na polisi wasitupe lugha chafu kwani tunalipia hizo huduma kupitia KODI na hiyo ndio mishahara yao.
    MAJI NA UMEME hapa hata sihitaji kujadili chochote kwani nikero kubwa sana.
    ROBBERY/UKABAJI mchanamchana utadhani tuko somalia ambako hakuna serikali hasa mwananyamala na jangwani, hili ni tatizo inabidi polisi wa dolia kuwepo hapo muda mwingi.
    MASHIMO BARABARNI NA MA BUMPER: Yaani unaingia kwenye shimo ukitoka unakutana na Bumper ukilivuka Bumper unakutana na shimo.Mashimo pekee yanatosha MABAMPA YA NINI TENA!!
    ELIMU: Sikuhizi shule zinafundisha wanafunzi ku solve ma papers tu nasio kufuata syllubus!watu wanaingia chuo wakiwa na uwezo mdogo wa kumudu masomo.Sawa wana AAA lakini kichwani hawana kitu,walikaririshwa papers toka form one mpaka six.Sijui serikali iko aware na hili jambo.Hii inapelekea hata foreign inverstors kuajili overseas graduates tu.
    URASIMU ULIOPITILIZA: Kila idara ukienda lazima uwekwe tu,hakuna hata sababu yeyote lakini mtu anataka akuonyeshe kwamba yeye ndio Mshika Rungu au anataka chochote lakini bila kukwambia.
    BIDHAA FAKE: kuanzia mavazi mpaka mikate.
    USALAMA WA MAISHA: Masupermarkets makubwa lakini hayana EMERGENCY DOORS(fire exits).sijui wahusika hawapo au wapo lakini hawaoni.Ni hatari ikitokea dharula watu wote watakufa.Hii inanifanya hata niogope kwenda kufanya shopping huko.Na haya masupermakets yamejaza mavyakula ya watu weupe,ni bidhaa chache sana za wakulima wetu na ambazo ni Bora kwa afya na sijui huyu mkulima atainuka vipi km Bidhaa zake hazipewi kipaumbele(promoted).
    Watu wanaona fashion kula kemikali!!

    Kwakweli naweza nikakesha hapa ila matatizo ni mengi sana labda wadau tusaidiane!
    Thanks.

    ReplyDelete
  7. Mkuu wa nanii!! Kwaheshima yako naomba upost hayo maoni ya mchangiaji hapo juu(MZAWA) kama topic ili tuweze kutoa dukuduku letu,kwani nchi ni ya kwetu wote na inajengwa au kubolewa na sisi wenyewe.
    Mfungo mwema!

    Mdau.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...