Mtafiti katika makao makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Bi.Furaha Chuma akitoa maelezo kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete jinsi ya kudhibiti mionzi waka Rais alipotembelea makao makuu ya Tume ya nguvu za Atomiki huko Njiro,Mjini Arusha leo asubuhi.Wapili kusjoto ni naibu waziri Wizara ya Sayansi na Teknologia Maua Daftari na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Profesa John Kondoro.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Teknolojia ya Nuklia Firmini Banzi akimwonesha Rais Jakaya Kikwete kifaa maalumu cha kutambua mionzi hatari wakati Rais kikwete alipotembelea Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania huko eneo la Njiro,Mjini Arusha leo Asubuhi.Pembeni ni naibu Waziri wa Sayansi na teknolojia Maua Daftari. Picha na Freddy Maro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. jamani hiyo picha ya pili inaeleza nini? mbona mnamchosha jk na mimaelezo mingi?

    ReplyDelete
  2. kama watafiti ndio hao yetu macho hakuna ubunifu...kabisa!

    nadhani maelezo yangekuwa simple ambayo hata mkuu wa nchi angeonyesha kufurahia.

    pili jinsi ya ku-present.
    huwezi weka presentation borad yako huna hata kifaa cha kuonyesha.

    kama huna vya madukani kwa nini usitafute hata fimbo....

    labda mlikatazwa msiche mkaleta dhahama kwa mkuu....

    next time ...muwe wabunifu sio kuweka suti tu

    ReplyDelete
  3. kituko cha mwaka..mkuu wa nchi kaenda simple na vazi la kazi..

    ona mkuu wa kitengo...suti hilo!
    utadhani yeyey ndiye director generali wa Taec...au ndio mkuu wa nchi!

    wajameni kila vazi na mahala pale..

    JK oyeeeeeeeeee!

    Na naibu waziri juuu

    ReplyDelete
  4. WA-TZ hata siku moja hawakosi kukosoa. hata kama hakuna sababu ya kufanya hivyo

    ReplyDelete
  5. UTAFITI SI MCHEZO, HAPO NI CHA MTOTO KUCHEZA MADANGE

    ReplyDelete
  6. ukiangalia kwa makini kwenye picha kuanzia naibu waziri na Rais, walivyo serious, ndio unatambua Presentation yako umetoa maelezo mengi sana kuhusu kifaa hicho kimoja ulichoshikilia mpaka wameboreka.

    ReplyDelete
  7. MBONA HATA HAWAANGALII?

    ReplyDelete
  8. NI KWELI HAKUNA UBUNIFU, UVUMBUZI WA LA UGUNDUZI. UKIONA MTAZANAIA ANAENDA KUONGEZA ELIMU NDANI AU NJE YA NCHI SABABU KUU NI KUPATA NYONGEZA YA MSHAARA NA SIO UFANISI WA KAZI. MUDA AMBAO MTANZANIA ANAKUWA NA BIDII ZOTE NUI WAKATI WA SHULE TUU. IKIISHA BASI ATAKUWA OFISINI ANAFANYA KAZI ILE ILE KILA SIKU KWA MIAKA 30 BAADAYE ANASTAAFU. UKIMUULIZA ANAKWAMBIA SIRIKALI HAIJALI HILI NA LILE KUMBE HAJUI KWAMBA NA YEYE NI SEREKALI. TUMECHOKA UMEME WA MAJI HUU NI WAKATI WA KUWA NA UMEME WA NUCLEA SASA. ELIAS MAHEGERE ENDELEZA HII MAADA

    ReplyDelete
  9. kama wewe ni teacher au mwalimu ukiona wanafunzi wako wa shule au madrasa wamekunja nyuso wakati unafundisha unafanyaje- KWA VILE WAMEBOREKA NA SOMO LAKO LISILO NA TIJA au hueleweki au sio mbunifu wa jinsi ya kutoa material?

    mimi huwa nawaambia waimbe ule mwimbo mzuri.....


    SASA SASA*2
    SAA YA KWENDA NYUMBANI!

    KWA HERI MWALIMU *2
    TUTAONAN !

    KESHOOOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  10. Inasikitisha Tanzania tuna nyanja nyingi za kuzalisha umeme but still eti tunaambiwa umeme wa mgao tanesco kazi kutishia umeme utazimwa tanzania nzima wakati wanatakiwa kuwa innovative na kuangalia nyanja nyengine za umeme. It is the shame tuna maji (Mto Ruvuma na Rufiji, makaa ya mawe, uranium na jua la kutosha, na maeneo mengi ya kuweka shamba la upepo lakini unasikia eti umeme wa mgao. Ikiwa viongozi wetu wanajali watanzania wangeliwekeza katika tukazalisha kwaajili yetu na kuuza nje ya nchi. Uuuzaji wa umeme tu nje ni pato kubwa kwa nchi linaloweza kupunguza utegemezi wa misaada by 10%-20%. Kutuonyesha kama tuna reserve hakusaidii kitu kama madini yenyewe hayana tija kwa mzawa. Tumekuwa na almasi muda mrefu, dhahabu, Tanzanite lakini mtanzania wa kawaida hajafaidi hata thumni. Hili la umeme mtusaidie basi tuwe na umeme angalau na wa bei rahisi ili nasi tuseme tumefaidika na madini

    ReplyDelete
  11. KALAGABAO
    TEH TEH TEHE HE HE HEE HEE

    ReplyDelete
  12. ANON 6:07 UNINIKUMBUSA ,BALI SANA MAMBO YA KWAHERI MWALIMU ASANTE MWALIMU, SIASA ZA UBAGUZI WA RANGI NI UNYAMA SHIKAMOO MWALIMU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...