Ilikuwa ndani ya kanisa la Saloam huko mbezi beach jijini dar,ndipo bro Daudi Boniface Magesa amefungua ukurasa mpya wa maisha kwa kufunga pingu za maisha na dada Anitha Masika kama uwaonavyo pichani wakiwa wamepozi ndani ya kanisa hilo mwishoni mwa wikend
Mwishoni mwa Wikiendi katika kanisa la Saloam huko Mbezi Beach ndiko Bro. Daudi Boniface Magesa alipofungua ukurasa mpya wa maisha baada ya kufunga ndoa na dada Anitha Masika na kufuatiwa na hafla ya kukata na shoka iliyofanyika Sinza Lion Hotel jijini Dar es Salaam kama unavyowaona wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Kaka hongera sana sana ila yaelekea ipo shughuli coz mamaa anaonyesha mkali kinoma.

    ReplyDelete
  2. Pongezi zako kuoa ila kuwa makini na mkeo usimletee mzaha anaweza kukukunja huyo.

    ReplyDelete
  3. Duh kama una watoto uliowazaa nje kaka kuwa makini, yaelekea mke yuko moto.

    ReplyDelete
  4. Ndugu yangu Boniface (RADEBE) Hongera sana kwa kupata mke. Tunakutakia maisha mema na yenye furaha.

    Matai family - Beijing

    ReplyDelete
  5. Jamani huyu ni Boni wa Kazima Secondary Tabora? Hongera sana kaka, nakutakia maisha mema wewe na kipenzi chako, Mungu awajalie yaliyo ya kheri ndoa yenu iwe baraka na kwa wengine!

    ReplyDelete
  6. hongereni mmependeza dada anita mtunze mmeo na umpende mwenzangu ndoa ni bidhaa adimu
    mdau canada

    ReplyDelete
  7. Sorry, hivi ni mwisho wa wiki au mwishoni mwa wikiendi?

    ReplyDelete
  8. BAVO aka BONI na leo nimepata Jipya DAUDI. Hongera sana ndugu yangu kwa kuamua kuachana na ukapera. Karibu sana kwenye chama letu japo umechelewa sana. Naona mama yupo serious sana, ila ninakuaminia kuwa hawa watu unaujuzi mkubwa sana wa kuwaweka katika mstari unaoutaka wewe si kwa kipigo bali kwa kuwabembeleza.

    Hongera sana BAVO.

    Rafiki yako, wa kuanzia Uhuru Primary (Tabora), then nikakuacha ila ukanikuta Kazima Secondary (Tabora) nikakuacha then ukanikuta UDSM, nikakuacha then nikakujoin tukamaliza pamoja UDSM. Japo tulikorofishana kidogo kuhusu madesa yako ila ninaamini kuwa bado ni marafiki wazuri tu na tumesameheana bwana BAVO.

    Wa Scotland

    ReplyDelete
  9. Hongera BAVO

    Kitu ambacho I will always remember from you is that, you are such a kind guy who always devoted to helping others when you have the capacity to do so.

    Some said you do that because you seek attention and want people judge you as pedejzee, but I judge you as a real anthropist and devoted man.

    Remember darasa letu la Tution pale kwako na product zake, was really good tution and produced good results, hahahah! just havin fun nimechoka na haya makaratasi.

    All the best in your new life.

    ReplyDelete
  10. Boni,

    Hongera sana kwa kufunga ndoa. MUNGU wa mbinguni akubariki wewe na mke wako na kuwajalia maisha marefu na yenye mafanikio.

    -- Rafiki yako - Magabe 'mura' Kibiti.

    ReplyDelete
  11. Magessa. What a nice name. Here is a great present for you to enjoy over your honeymoon...

    http://www.youtube.com/watch?v=i_N-pDIItYM

    ReplyDelete
  12. Anon: Tue Sep 22, 05:32:00 PM

    Umeenikumbusha mbali sana katika kurekebisha statements, unajua mtu anaweza jikuta amesahau halafu katika kurekebisha ndiyo ikawa kuvuruga.

    Nikiwa secondary school, head prefect alikuwa akitanga mgawanyo wa kufanya usafi kwa kiingereza Assembly. mwisho ikabidi aweke msisitizo kuwa "MAKE SURE THAT YOU DO THIS EXERCISE", akaona watu wanamuangalia sijui akafikiri kakosea basi within four seconds akamalizia na neno "BOOK" wanafunzi wote tukaangusha kicheko kuwa sasa ndiyo kachemka kweli yaani

    "MAKE SURE THAT YOU DO THIS EXERCISE...BOOK"

    ReplyDelete
  13. huyo wa exercise___book kanionngezea siku zangu hapa duniani

    ReplyDelete
  14. hongera boniphace daudi mwenge magesa na mkeo ,mungu awabariki sana


    chocha magesa wa tabora boys

    ReplyDelete
  15. kweli annon wa exercise book me niko hoi apa...

    mamaaa kanona km parachichi safi saanaaa..afu nyie watu ku-judge wezenu kisa eti sura yako apo mna akili kweli???

    ReplyDelete
  16. Inapendeza sana......Mungu awajalie heri sana na zaidi amani na furaha...Usitumie sera ya kwenu kaka ya kupiga ngumi mke kuwa ndio show love...
    Big up bro!!
    Krom

    ReplyDelete
  17. Hongera sana rafiki yangu Bonifas magessa. Mmependeza sana. Nawatakia maisha mema na yenye mafanikio makubwa. Mungu awabariki sana. Amen. Ni mimi rafiki yako wa siku nyingi Deo Raballa

    ReplyDelete
  18. pesa ya album ushalipwa na kuwatoa maharusi kwenye blg umelipwa sh ngapi? kuna tetesi lazima watu watoe michongo ili picha zao zitoke kwenye blog yako mjomba ... kanusha...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...