Uncle, vipi za siku, pole na mfungo.
Sasa nilikuwa naomba uniwekee hizo link hapo chini, ili angalau Kanumba naye apumzike kha!
Ahsante sana kwa kazi nzuri unayoifanya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Duh A.Y bora kanumba yaani ngeli hakuna kabisaaa

    ReplyDelete
  2. Twende mbele kurudi nyumba mwana FA anaongea poa ila AY bado kidogo...MR BLUE Hahaha ha aibuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  3. Ndio yale yale, tukisema mnatuita waosha vinywa, haya bwana, ndio mastaa wetu hao wa bongo!

    ReplyDelete
  4. Mange KimambiSeptember 17, 2009

    Kaka mithupu ni vipi watu Kama John Mashaka, shayo na wengineo wenye ufundi Mkubwa wa lugha wanaweza kutoa tuisheni Kwetu sisi mastaa wanaounganisha unganisha kiingereza? Tunaweza kutumia pia jamii blog kupokea mafundisho yao. Hii inatia aibu sana hasa Mr. Bluu

    ReplyDelete
  5. I is not bud, just ggod and enough for just communication as they are not speaking for an exam, anyone could understand who knows English. Even that of KANUMBA was not kanumbaring, it was just perfect English with Tanzanian vibes, we call it Bongo accent as the London one called COCKNEY, the working class dialect, but it is like posh speaking for Londoners .

    ReplyDelete
  6. ahahahahahahaha....sina mbavu miye..aibu tupu

    ReplyDelete
  7. Well watanzania wenzangu tusichukue nafasi hii kuwabeza watanzania wenzetu wasioijua lugha ya kiingereza. Labda tumlaumu Mwalimu Nyerere aliyesisitiza kuongea kiswahili kama lugha ya taifa tulipopata uhuru. Nchi zingine zilichagua lugha ya kiingereza na sasa wanajifunza kiswahili kwa nguvu zote na wanatamani kuongea kiswahili kama watanzania tunavyozungumza lakini hawataweza kutufikia.
    Kwa watanzania kutoongera fluent english si makosa yetu bali ni misingi tuliyojengewa tangu tulipozaliwa na kukua. Ndo maana wazazi wengi kabla ya tanzania kuanzisha english Medium schools walikuwa wanapeleka watoto wao nje ya nchi kusoma kama Kenya na Uganda ili kuwajengea watoto wao misingi mizuri ya kuongea kiingereza. Thanks God sasa tunashule zenye kufundisha kingereza kwa watoto wetu kuanzia kindergaten. Kuanzia 2020 watanzania karibu wote watakuwa wanaongea fluent English cha kufanya sasa hivi ni kila mtu kujitahidi kuongea katika kazi, mashuleni na vyuoni wanafunzi wanatakiwa kuongeza bidii ya kuwasiliana kwa kiingereza kuliko kiswahili kwani unakijua kiswahili already.
    Tatizo letu watanzania mtu akijaribu kuongea kingereza unaanza kumbeza oooh anajifanya mzungu, ooh kingereza gani cha ze ze, na mambo kibao tunakatishana tamaa wenyewe na huu ni ujinga uliotutawala watanzania!
    Nitaanzisha chuo cha kiingereza kwa maselebriti ili wajifunze kuongea kiingereza chenye maana. Misamiati tunayo ila tatizo ni jinsi ya kuipangilia. Na tatizo lingine kubwa watanzania tunaongea kiingereza cha kwenye dictionary zaidi ndo maana tunachemsha kwenye interviews nyingi.
    Mungu ibariki Tanzania
    Mdau USA

    ReplyDelete
  8. Baada ya kuziangalia hizo clip zilizotumwa na mdau, nimebaini yafuatayo;-
    -Mr Blue, inabidi urudi shule, chukua hata short course ya ung'eng'e kama unataka kutema yai, la sivyo utaendelea kuwa Mr White kwenye sekta ya NGELI.
    -AY unahitaji kupiga msasa ung'eng'e wako, kwani hauko fluent, maswali karibu yote ulikuwa unamwachia FA ajibu.
    -FA ung'eng'e wako unaridhisha sana tu, inadhihisha kuwa pamoja na kwenda kidato pia unajituma katika falsafa nzima ya lugha. Big up kwako Binamu.

    Ni haayo tu.
    Mdau
    Groningen, NL.

    ReplyDelete
  9. Mnaleta ligi tena jamani? Mbona mtamgombanisha Kanumba na wengi? Mara Ze Komendy mara aangalie dogo wa hip hop. Mmemnanga vya kutosha, hakusikia na bado anaendeleza ligi na ze komedy tena sasa ni maandamano kabisa. Hafunziki huyu, labda Michuzi akimwambia ndio ataelewa

    ReplyDelete
  10. AISEEEEEE NI MAMBO YA AIBU SANA SANA SANA ILA HONGERA KWA SERIKALI KWA KUANZA KUWAFUNDISHA ENGLISH WATOTO WA SASA ILI AIBU KAMA HIZI ZISIENDELEE,DUUUUU I CANT BELIEVE THIS, CAN U?

    ReplyDelete
  11. nakweli acha kanumba apumzike.kwani huyo sijuwiwi ndo mwnamziki anaulizwa swali kwa kijruo anajibu kwa kihaya.mamboooo hayooo means kanumba babu kubwa.

    ReplyDelete
  12. we uliyetuma hizi video pumba kabisa
    nani sasa hapo utamlinganisha na kayumba? Mr Blue mtoto wa mjini kaona kwa kizungu hatatoa point zake vizuri kaongea kiswahili and kanumba should have done the same, mwana FA: don't even go there the guy is well educated, very articulate and goes beyond yes and no..
    what did you want to show us that i didn't see on the video?
    Michuzi please stop this kayumba thing.. kama ujumbe haujamfikia nobody is here to babysit

    ReplyDelete
  13. haya jamani kazi kwelikweli!! mwana FA&AY quote "music and school DOESN'T go in different way"))))people doesn't.....)))))!!!
    mr.blue.....)))))
    wow! hongereni vijana mko juu masuper stars wa tz na EA. msimcheke bw.kanumba ila sogeeni mbele.hii ni lugha tu,mambo mengine mswano kama kawa kamueni tu na muendeleze vipaji.sisi waosha vinywa tunaburudika siku zinakwenda.
    SIJUI TUANZISHE MTINDO WA KUTUMIA POMBE MASHULENI WAKATI WA KUFUNDISHA KIMOMBO))) Maana mtanzania utamfahamu akiutwika ulabu,hapo kimombo kwenda mbele kama kawa yaani ulimi unakuwa kama mercedes benz kwenye barabara ya lami))))

    ReplyDelete
  14. Kwanza kabisa namfagilia sana Mr. Blue...he understood what he was asked and responded it into swahili...Big up blue. Kiswahili kitakuwa kwa style hii.

    Mwana FA has tried, he is doing great. he got confidence...congrats...bt he ddnt talk abt himself, he jst introduced himself same as AY...And Ay ddnt talk much.

    Kanumba alichemka kdg, bt he is smart...very smart. language is a big issue. waswahili wangapi wanachapia kiswahili? wazungu wangapi wanachapia kizungu? Lugha ni ngumu, uzungumzajia wa mtu ktk lugha fulani unajengwa na sehemu aliyozaliwa na kukulia. Ndio mana mswahili wa Dar-es-salaam atasema nimekabwa na chakula, bt mswahili wa Tabora atasema nimenigwa na chakula, wakati mswahili wa Zanzibar atasema vingine.

    Sama as english, people frm England will say dust bin but people from America will call it trash.
    America will call choo huita restroom, while UK wataita toilet...so language is complicated inabidi tubadilike.

    Kuna watu wachache wamebalikiwa kujua lugha kama Mheshimiwa mstaafu Rais Mkapa...Jamaa anatisha kwa English, he is well known world wide.

    Mungu ibariki Tanzania...Asante kwa hizi clip. Wote tuanze kuwa confident in ourselves esp ikija upande wa kujielezea.

    ReplyDelete
  15. Hongera kwa MwanaFA kutumia muda wako vizuri, yaani kazi, muziki, elimu na burudani.

    Mdau
    BwanaKaka

    ReplyDelete
  16. CASE YA MR BLUE INAJULIKANA.HATUWEZI HATA KUPOTEZA MUDA KUMJADILI. LAKINI AFADHALI YAKE YEYE KAELEWA HATA SWALI NA KAJIBU KWA KISWAHILI.KATUMIA UMJINI ZAIDI KUMYEYUSHA HUYO MDADA.
    KANUMBA NI DIFFERENT STORY!!!!

    ReplyDelete
  17. kazi kweli kweli ukiwaona wasepe men nyingi kumbe du.. anyway shall shalln`t they guud day

    ReplyDelete
  18. Mr BLuu Umeona sasa Kama Shule Muhimu?

    AY- Kiengereza Unaonekana Unaelewa Unachoambiwa, Kujibu Unakuwa Tabu sababu muoga unaogopa watakufikiria Vipi wewe Tema tu Ndio mwanza wakulainisha Kinywa, Baadae utaweza kuongea vizuri.

    Mwana Fa kweli nimekuaminia unajuwa nini unachokiongea na Unajibu bila kuogopa nini kitakuja mbele.

    AY Zidi kuongea Kwenye Muziki upo juu.

    Mwana FA mchukue Mdogo wako umuweke na Watoto Wanaotema Kiengereza. Atabaki Yoyoooo tu shaurizake.

    ReplyDelete
  19. If u have money & u dont know Luzungu a.k.a Ung`eng`e a.k.a English, no 1 will say any Nonsense.
    But if u dont have money or vijisent & u dont know ung`eng`e, in short ur in trouble in this world!

    ReplyDelete
  20. Anyway ukweli wala hawaKUKANUMBARING,walikuwa wanaelewa maswali waliokuwa wanaulizwa wala hakuna ambae hakuelewa swali,wameongea vizuri tu wala hakuna tatizo,na ungana na mdau mmoja hapo,tatizo la sisi watanzania tunataka kuongea kingereza cha kwenye Dictionary plus gramma ndani yake,hilo haliwzekani.kwani hata kiswahili bado hatukijui kabisa,ukienda na kiswahili chako mbele ya Mzee Ruksa(rais mstaafu Mwinyi)atakuona kama huzungumzi inavyotakikana.Mfano hapo tutaanza kumumchambua Ay au FA kama kuna gramma au nini,ukija kuelewa lugha ni kuwasiliana baina ya watu wawili,hilo ndio la msingi.
    Nakuja kwa yule dada mwingine alikuwa anauliza kuimba kiswahili au kingereza inakuaje,kwanza ujue kuwa mziki ni unaburudisha,tulianza kucheza MAYENU bongo wala hatukuwa tunajua wanaimba nini,mpaka hata kuimba LINGALA watu wanaimba lakini ukija kuangalia hajui maana.
    Watu tulikuwa tunaangalia filamu za KIHINDI na unakutana na watu wanakuhadidhia kuanzia mwanzo mpaka mwisho na nikweli anachokuadidhia.
    Huyo dada alikuwa anasema Haya mambo ya mziki kupeleka ujumbe,hayo mambo ya kupeleka ujumbe tena yanachukua nafasi ndogo katika mziki wa sasa,ukiangalia au kusikiliza mziki wa hao waliokuwa juu hakuna la maana tofauti na kutumia "F" language kwa sana,sasa hapo kuna ujumbe gani????au MITUNGI!!MIKASI!!cha msingi ni wewe kuufeel mziki na watu tunapenda na kuenjoy kama FA na AY Walivyosema,
    Kwa issue ya Mr Blue mimi nampa BIG UP!! sana,kwanza kaelewa swali wala haKUKANUMBARING kuuliza amesemaje na pia kaona kwake Kiswahili ndio yuko poa.
    Lingine ni kuwa wamependeza sana!!ni hayo tu,

    am log off!!

    Muheshimiwa nanihii usinibanie basi na wewe!!
    mfungo mwema.

    ReplyDelete
  21. Hivi nyie mnaosema Jony masha na Dr. Hibread Shayo ndo waje kutoa twisheni ya kimombo, jee mmewahi kuwasikia hatu watu wawili wakizungumza kimombo? Au mmesoma maandishi yao tuu mkaamua kuwa lazima wawe wazungumzaji wazuri wa lugha hiyo? Kimombo ni lugha ya ajabu, kuandika kimombo ni kitu kimoja na kukizungumza ni kitu kingine kabisa.

    You will be surprised.

    All in all big up Mr. Blue, I personally am profoundly proud of you for being swift and extremely decisive in knowing which language you should use to communicate. There ain't no shame in not being capable of speaking the language of the criminal, cruel, and colonial imperialistic slavers who have no regard what so ever in the existence of other cultures never mind other languages.

    ReplyDelete
  22. AY/KANUMBA Baba moja Mama moja, ngoja tutafute wasanii wengine tutapa jina la inglish mbovu kwa kutumia herufi za kwanza za majina yao...hadi sasa inglish mbovu inaitwa KAY...k for kanumba ,,,ay,,,for ambwene.

    mr blue dd well ukizingatia shule alikimbia .

    ReplyDelete
  23. MWANAFA kajitahidi sana kuzingatia kazaliwa kasomea huko Tanga badae IFM so seriously ni mwenyewe kajitahidi kujifunza lugha...AY sina mameno maana hawezi kujiexpress kabisa japo anaelewa kizungumzwacho anabidi apractice zaidi maana kupata interview kama hivi za kimataifa alafu ung`eng`e inakuwa shida ni noma kiasi, mr BLU nimefurahia aliongea kwa kiswahili hakutaka kujiaibisha. Kaishia form 2 ,Kisomo sio ufunguo wa mafanikio maana hata hao matajiri wakina BIll gates, Ford na wengineo are not college graduates so wmacheni mtoto wa watu kama anaingiza bingo zake..

    ReplyDelete
  24. mwanafa anafaa kuwa mfano kwa ndugu zetu wasanii,what an insipiration!go baba,endelea kupiga shule,na Mungu atakuongoza

    ReplyDelete
  25. huyu mtangazaji anaonekana kama alikuwa anavutiwa na ay zaidi ya fa akawa anaelekeza maswali yake kwa ay zaidi,na ilikuwa inabidi fa aokoe jahazi mara kwa mara,angalau angekuwa na uwiano.ay rudi shule kaka,utasoma namba za mwenzio huyo usipoamka.mr blu mjanja sana,kakimbilia kujiepusha na aibu mapema

    ReplyDelete
  26. Mr.Blue mtotot wa mjini kaona ung'eng'e kimeo kachomekia kiswahili. Ay inabidi practice, mdomo mzito. Mwana Fa upo powa lakini inabidi upate tuition ya grammer ( people doesn't...) hell No.

    In general Mwana Fa did well. Ay needs too much work. Mr. Blue... Rudi shule.

    ReplyDelete
  27. FA ni graduate lkn bado ana gramatical errors kibao...ndo anaenda kusoma master huyu! labda aende vyuo uchwara vya uchochoroni,huyu ndio wa kumlaumu na si AY na Blue

    Blue mtaani utafikiri hajui kuongea kiswahili jamani..! yeye awe mwanamke/mwanaume wote ni man.!Alivyo jibu swali mimi hoi maana aligues ameulizwa unagirlfriend?

    ReplyDelete
  28. WALA SI AIBU KAMA KUNA MTU ANAANGALIA HAYA MASHINDANO YA PROJECT FAME WANYARWANDA WANAHARIBU SANA ENGLISH BUT KENYANS BECAUSE AKILI ZAO ZIKO SAWASAWA NA WANAELEWA MORE THAN US TANZANIAN THEY DONT CARE KWAKUKUBALI KWAMBA KIINGEREZA SIO LUGHA YA KWANZA KWAO THEY ARE FRENCH SPEAKERS KAMA SISI NA KISWAHILI SO WHAT IS THE BIG DEAL HERE DONT YOU HAVE ANYTHING TO DO PLEASE STOP MNABORE SASA TUNAOMBA MAMBO YA MSINGI TAFADHANI HAKUNA AIBU YOYOTE KWA MTANZANIA KUTOJUA KIINGEREZA NONSENSE

    ReplyDelete
  29. kumbe ka-fa kako komfotabo na kiinglishi chake jamani?sikujua,kanajitahidi.ay na blue,mhh.kaka mithupu tutaftie na ya profesa jei na ledi jeidii basi

    ReplyDelete
  30. Mimi nadhani kwa mtanzania ambae shughuli zake hazimlazimishi kukutana na watu wa mataifa mengine kiingereza hakina umuhimu kwahiyo tusimtupie lawama baba wa taifa kwa uamuzi wake wa kukifanya kiswahili kiwe lugha ya Taifa lakini kwa upande mwingine ndugu zangu wasanii na wafanyakazi wa kuajiriwa katika sekta mbalimbali iwe tukubali tusikubali tunatakiwa tujue kuzungumza kiingereza kilichonyooka maana ndio tutaweza kutengeneza mtandao wa kutusaidia maishani na watu mbalimbali duniani.

    Inasikitisha kuona watu kama wasanii wa filamu wanaanzisha bifu na wasanii wenzao wa comedy kisa tu wamekosolewa kupitia maigizo hii ni aibu kwani mbali na upungufu ambao umeshajidhiirisha kwamba ngeli haipandi lakini pia inaonyesha hawajui hata majukumu ya kazi zao mfano mchekeshaji jukumu lake nini na mcheza filamu jukumu lake nini.Mwisho ni lazima wasanii wetu wakubali kwamba wao ni mabalozi wa Taifa hili hivyo kuzungumza kiingereza kinachooeleweka ni wajibu wao kwani Taifa letu lina lugha kuu mbili nazo ni kiswahili lugha ya Taifa na kiingereza lugha ya kibiashara na mawasiliano ya kimataifa

    ReplyDelete
  31. Naungana na Anon 09:30:00 hapo juu, What is Kiingereza anyway? It is a language just like any other. Sisi watanzania lugha yetu ya mawasiliano ni Kiswahili period. Sio issue kwamba watanzania hawajui Kiingereza. Watanzania wenzetu baadhi wamekuwa ni limbukeni wa lugha. Kama mnaangalia Big Brother jana kuna Mshiriki mmoja msichana anatoka Angola, (Angola wanaongea kireno)hajui kabisa kiingereza yaani mnasema Kanumba lakini Kanumba alikuwa afadhali mara mia. Lakini sidhani kama wananchi wa Angola watambeza mwananchi mwenzao eti kwa sababu alishindwa kuongea Kiingereza. Sisi tu watanzania tumekazana kuwabeza watanzania wenzetu kwamba hawajui kuongea lugha ya Kiingereza. LUGHA YETU YA MAWASILIANO NI KISWAHILI, We should be proud of our Language. Big Up Mr Bluu

    ReplyDelete
  32. Mi nimependa strategy aliyotumia Mwana FA kuokoa jahazi la AY. Unaajua hiyo nayo ni strategy mradi AY naye kaonekana hapo. Sasa kanumba hakuwa na okoa jahazi, Ila MR Blu naye dah hata kama ameelewa swali alitakiwa ajibu vizuri so frankly frankly.... wat. Ubishoo umewazidi wasanii Bongo lakini kichwani hakuna kitu mradi maisha. Inabidi wajifunze nchi nyingine watu wanakwenda shule proffesionalised in Music.. na kwenda chuo kikuu sio lazima uajiriwe unaweza ukasoma kwa ajili ya kujiajiri. sasa bongo watu wanakimbia shule eti kisa hela wanayo ya kuwafanya waishi.... kwenda shule si kwa ajili ya kutafuta hela ni kuelimika jamani.

    ReplyDelete
  33. nina wasiwasi na ALLY KIBA!!!!!!!!

    ReplyDelete
  34. Sifa ya Watanzania walio wengi ndio hiyo, kuwajadili watu udhaifu wao, hata kama wao wanao.
    Niliwahi kuuliza mbona WADHUNGU hawakijui Kiswahili, ina maana wao hawajasoma? au mnataka kusema nini,kuwa Kiinglish ndio kusoma. Kama ni hivyo Wajapan, Wajeruman wataitwa hawajasoma maaana wengi wao hawajui Kiingereza,Vijana wetu hawo wamejitahidi, ila ningewashauri wangeongea Kiswahili ili watafutiwe mkalimani,na hapo inakuwa chanzo cha kukiingiza Kiswahili chetu kwenye mtandao wao wa kimataifa
    Jamani tujaribu kutafuta mbinu ya kukikweza Kiswahili chetu, kama wao wamesoma sana MBONA HAWAJUI KISWAHILI,manake kwamantiki hiyo kusoma ni kujua Lugha, AU?

    ReplyDelete
  35. KUJUA KIINGEREZA SIO LAZIMA, MASTAA WA NCHI NYINGI TU HAWAJUI KIINGEREZA NA WENGINE WANAOJUA WAKIHIJIWA WANAJİBU KWA LUGHA ZAO, KOSA ALOFANYA MR BLUE NI KWAMBA HAJATAFUTA MKALIMANI, ONGEA KISWAHILI MR BLUE, NDO LUGHA YAKO WASIKUZINGUE HAWA JAMAA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...