Waziri wa Habari, Utamaduni
na Michezo Mh. George Mkuchika


WAKUU wa vitengo vya Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wizara, idara, wakala nataasisi Tanzania Bara wametakiwa kutangaza shughuli za wizara zao na utekelezaji wasera za Serikali.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Kpt (mst) George Mkuchika amesema hayo lejanawakati akizungumza na wakuu hao katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) jijini Dares Salaam.
Waziri Mkuchika aliwakumbusha wakuu hao, ambao ni maofisa wa habari wa wizara,idara, wakala na taasisi za serikali kuwa wajibu wao ni pamoja na kulinda amani nautulivu nchini.
Ameutaja wajibu mwingine kuwa ni kutunga sera sahihi za maendeleo ya Taifa nakuzitekeleza na kuzifafanua sera hizo kwa wananchi ili wazielewe, kuzikubali nawashawishike kuwa Serikali yao inawajali wananchi wake.
“Kazi hii inaweza kufanywa vizuri zaidi na maofisa wa habari ambao ndio ninyi.Haiwezekani Ofisa wa Habari wizara akakaa majuma matatu, au mwezi mzima bila yakuwasiliana na Idara ya Habari (MAELEZO),” alisema Waziri Mkuchika.
Katika kulisisitizia suala hilo, Waziri Mkuchika alisema Idara ya Habari ndiyoMsemaji Mkuu wa Serikali, hivyo lazima ijue kila kitu kinachoendelea katika wizarazao.
“Msemaji wa wizara yoyote ile siyo Msemaji Mkuu wa Serikali, bali ni msemaji wawizara husika. Lakini msemaji wa serikali kwa mujibu wa kanuni nambari 16. C yaUtumishi wa Umma. Idara ya Habari ndio msemaji wa serikali,” alisema.
Hata hivyo aliwataka wakuu hao wa vitengo vya mawasiliano wasiwe wavivu kujibu hojana malalamiko mbalimbali ya wananchi yanayotumwa kutipia Tovuti ya Wananchi ilikurahisisha mawasiliano kati ya wananchi na Serikali.
Awali Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bwana Clement Mshana alimweleza Waziri kuwa hadi sasa kuna kero 62,234 zilizotumwa kupitia Tovuti ya Wananchi, lakini kati ya hizo zilizoshughulikiwa ni 32,988.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Sioni haja ya kuwa na Maelezo kwani tuna idara za habari katika ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu - Tukubaliane, mara nyingi hawa ndio wanaoisemea serikali wala si Maelezo

    ReplyDelete
  2. MIMI NI MSIKILIZAJI SANA WA REDIO UHURU HASA KIPINDI CHA MAGAZETI ASUBUHI, KITU KIMOJA NISICHO KIELEWA NI PALE WATANGAZAJI WA REDIO HIYO WANAPOJIWEKA KUWA NAO NI WANASIASA HASA KUVIKEJERI NA KIVIBEZA VYAMA VINGINE KWA MANENA YA DHARAU, SASA SIKU HAWA WAANDISHI WAKIFUKUZWA KWENYE MIKUTANO YA VYAMA HIVYO LITAKUWA KOSA LA NANI? NINAKUMBUKA VYOMBO VYA HABARI VILIWA KUKILAANI CHAMA KIMOJA KWA SHAMBULIO WALILOLIPATA WANAHABARI WA CCM LAKINI SIONI VYOMBO HIVYO KUWALAANI WAANDISHI HAO WA CCM KWA KUJIFANYA WANASIASA.

    ReplyDelete
  3. Swali kwa Mh.Waziri wa Habari:

    1.TBC kurusha matangazo yake yote kwa mfumo wa Digitali mwaka 2012 utawaathiri vipi wananchi wenye TV ambazo siyo Digitali?

    2. Je kama mfumo huo wa digitali utawaathiri wenye TV za analogue, Serikali imejipanga vipi kuwaelewesha wananchi?

    3. Wananchi tujitayarishe vipi? je kutakuwepo na gharama za ziada kwa mwananchi?

    Naomba kuwakilisha
    Mdau
    Bombambili.

    ReplyDelete
  4. mimi nashangaa sana hii serikali, kwa nini haina msimamo? Mara tuko chini ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu mara bila barua wala nini sasa hivi tunaambiwa vile vikao tulivyokuwa tunahudhuria Ikulu sasa tusiende tena tuwe tunaenda Maelezi siku zilezile saa zile zile. Yaani inakuwa kama hivi vitengo mnavigombea kati ya Maelezo na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu. jAMANI TUAMBIENI TUSIPELEKE VITU KIENYEJI. Msikute hivi vitengo mnavifanya miradi inayowanufaisha nyinyi haiwezekani watu wawili wakagombea kila mtu aripoti kwakwe Tufike mahali Tuambiane ukweli

    ReplyDelete
  5. Da kwanza afadhali, tuwe tunaenda Maelezo Rweyemamu kazi imemshinda labda tuangalie na hawa maelezo kama wana jipya la kutuambia!

    ReplyDelete
  6. Big Up Maelezo. Hao ndio wasemaji wakuu wa Serikali na hakuna mwingine. Rweyemamu alianza kubagua kwa kuzitenga Idara za Serikali na kusema eti anahusika na Wizara Pekee. idara ya habari inakutanisha Wizara, taasisi za Serikali na Idara zake na kwa kweli wamefaulu kwa kiasi kikubwa sana. Anayesema tuone kama wana jipya anakosea, kule tunajadiliana na kupeana uzoefu. Period!!!! sisi ndio tuwe na jipya kazi yao ni kutukutanisha. Kuna watu nadhani ni mashabiki tu wakuingia white house. Kazi ya Rweyemamu ni kubwa muacheni ajikite na Mheshimiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...