Vodacom Tanzania inapenda kuwakumbusha wateja wake wote kuwa zoezi la uandikishaji wa namba za simu lililoanza Julai Mosi mwaka huu bado unaendelea. Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia.
1. Swali: Ni kwa nini nisajili namba yangu ya Vodacom?
Jibu: Ni ili niweze kujilinda na kuilinda namba yangu kutoka kwa wale wanaotumia vibaya huduma za mawasiliano.
2. Swali: Ni wapi ninapoweza kuisajili namba yangu ya Vodacom?
Jibu: Fika kwenye Vodashop au wakala wa M-PESA yoyote yule aliye karibu na wewe ukiwa na kopi (kivuli) ya moja ya vitambulisho vifuatavyo;
I. Kitambulisho cha kupigia kura
I. Kitambulisho cha kupigia kura
II. Pasi ya Kusafiria
III. Kitambulisho cha Pensheni (NSSF, PPF, LAPF, PSPF)
IV. Leseni ya Udereva
V. Kitambulisho cha kazi pamoja na barua ya Mwajiri
VI. Kitambulisho cha Shule au Chuo
VII. Barua iliyopigwa muhuri kutoka kwa Mtendaji Kata pamoja na picha ndogo
3. Swali: Je kuna gharama yoyote ya kusajili namba yangu ya Vodacom?
Jibu: Hapana, usajili ni BURE
4. Swali: Je zoezi hili la kusajili namba za mitandao ya simu limeanza lini na litakwisha lini? Jibu: Zoezi hili limeanza Julai mosi mwaka huu na litakwisha Disemba 31 mwaka huu.
5. Swali: Je ni nini kitatokea iwapo nitakuwa sijasajili namba yangu ya Vodacom baada ya Disemba 31 mwaka huu?
Jibu: Kulingana na maelezo kutoka Tume ya Mawasiliano, mteja husika atajulishwa na kisha namba yake itafutwa kutoka kwenye orodha ya namba za simu.
6. Swali: Je ninaweza nikasajili namba ya mteja mwingine?
Jibu: Ndiyo, unaweza kusajili namba ya mteja mwingine iwapo tu unayo maelezo yote yanayotakiwa na Tume ya Mawasiliano.
7. Swali: Je ninatakiwa niisajili tena namba yangu ya Vodacom hata kama nimeshajisajili na huduma ya M-PESA?
Jibu: Hapana, huhitaji kuisajili tena namba yako iwapo umeshajisajili na huduma ya M-PESA na umeacha nakala ya kitambulisho chako. Iwapo haukuacha nakala ya kitambulisho basi itakubidi uache nakala ya kitambulisho chako chenye picha.
8. Swali: Je ni idadi ya namba ngapi za Vodacom ninazoweza kuzisajili?
Jibu: Hakuna idadi ya namba unazotakiwa kuzisajili. Unaweza kusajili namba nyingi kadri uwezevyo.
9. Swali: Je kuna usiri wa kiasi gani kwa habari nitakazozitoa wakati wa kusajili namba yangu?
Jibu: Makapuni yote ya simu yanatakiwa kwa mujibu wa sheria kutunza kwa usiri mkubwa habari zote zitakazotolewa na wateja wake.
Ahsante kwa taarifa, hebu jaribu tafadhali kututafutia na mitandao mingine, wao wanasemaje?
ReplyDeleteje kama uko nje ya nchi na itakuaje?
ReplyDeleteMkubwa naomba niulize swali,
ReplyDeleteMimi ni mteja wa Vodacom kwa sana tu, tangu mwezi wa nne mwaka huu sipo tanzania na sitarajii kurudi hadi mwakani mwezi wa nne, kwa maana hiyo, usajili wa namba utanipita. Je kuna uwezekano wowote wa mimi kuisajiri namba yangu ya voda? maana licha ya kuwa sipo Tanzania, bado napatikana na mtu akinitumia sms naipata huku nilipo (mauritius). Ningependa kuendelea kupatikana kupitia namba yangu hii kwani inarahisha upatikanaji wangu, si unajua tena mambo ya kupunguza gharama na kutokupoteza marafiki!!
Peter Sakila
+255 754 22 94 07
+230 9474847
Mauritius.
annon "palex" una akili sana
ReplyDeleteswali la maana sana ata me nilitaka kuuliza iwapo mtu uko nje ya nchi yaweje...
maana namba zetu tutataka kuzitumia ati...nisomazo apo juu "waweza kuandikiwa na mtu ila awe na details zako zozote asa zile atazouliwa apo ambazo hatuzijui" "namba itafungwa" khaaa
tufanyeje sasa?
nyie voda msituzingue na watu walioko nje itakuwaje mbona hapo hamjasema ishu hii itakuwaje?? naona mna wateja wengi sana nitaama mtandao na namba yangu ileile watu tumedumu na namba zetu miaka sita tunasafiri tukirudi tunaendelea nazo leo hii sijui itakuwaje au tuwatumieni email na namba zetu mtajua jinsi ya kufanya na mtuarifu humuhumu kwa michuzi jinsi ya kufanya sio mkurupuke tu bila kujali wateja wenu wa kudumu
ReplyDeletemdau safari north america
Huu ndio ule ushenzi wa kuingiliana na kutaka kujua nani anaongea na nani na anafanya nini.Kwa sababu sisi bado hatujaendelea kwa hiyo suala la private Au serikali ndio inataka kujua wapinzani wanaongelea kitu gani na malengo yao ni nini?Kwa sababu kwa nini hawa kampuni ya simu hawakuwa na mpango huu toka mwanzo?Pia wale wenye biashara za haraka haraka siri haipo customer service atakuwa na uwezo wa kusikiliza simu yako kuanzia mwanzo hadi mwisho na kumtonya mshikaji wake.Poleni sana ndugu zangu.
ReplyDelete