Kaka Michuzi,
nashukuru tunajifunza mengi katika blog ya jamii na napenda kushirikiana na jamii kuwaasa ndugu wawe wanahesabu fedha zao wanazochukua kwenye ATMs kwa sababu kuna mchezo mchafu wa kupunguza fedha na mashine kuonesha hesabu kamili.
Yaliyonikuta leo ni pale nilipoenda kwenye ATM na kuchukua fedha kiasi nilichotaka na kuondoka nazo, nilivyofika kwenye kununua nilichotaka nikatoa fedha nikijua nina taslimu kutoka kwenye ATM nikawa na pungufu ya shillingi 40,000/=.
Risiti niliyopata inaonesha hesabu iliyokamilika lakini kiasi kilichotoka kwenye mashine ni pungufu. Nimeongea na jamaa zangu wa karibu kumbe kati ya watu watano, wawili walishakuta pungufu lakini wakajiona labda wao ndio wamekosea kuhesabu kwa sababu mashine haiwezi kukosea.
Nimejiuliza ni mara ngapi nachukua pesa kwenye ATMs na kuanza kuzitumia kidogo kidogo bila kuhesabu si ajabu nilishapoteza maelfu ya fedha kwa namna hii.
Labda niombe wataalamu wanielimishe kama kuna uwezekano wa mafundi wa ATM kuchezesha vyombo humo ndani wakabaki na balance kutokana na kuwakata wateja wao. Hii ni hujuma kabisa.
Mdau
Mhanga wa ATM
njoweni mpige box huku ATM hazikopeshi kama huna kitu inakwambia hakuna kama unahitaji hela nyingi na balance ipo kidogo inakwambia ubadili kiasi unacho hitaji sasa mmekalia kutoa matusi eti bongo tambarare wakati mnajipanga kwenye ATM kwa foreni kibao semeni ukweli msitukane bila kuwa na uhakika. Safi sana hii topic...mtatoa siri zote sisi box mbele kwa mbele lakini maisha ni bora na matamu!
ReplyDeleteYaani elfu 40 ipungue usishtukie? Na kwa nini usihesabu right away? I am sorry huo ni uzembe fulani wa kuamini marobot.
ReplyDeleteMimi hapa nikitoa hela zangu lazima nicount no matter what...Na mashine za huku zinatoa kwa increment ya $20.00 but still saa zingine bill moja inaweza kuwa imeng'ang'ania au kweli kuna some mistakes siku hiyo kwenye hiyo machine. Things happen.
Kwa kuhesabu hapo hapo utaweza kwenda ndani kama Bank iko open, uende kesho yake kama wamefunga au hata ukipiga simu tu kama kulikua na tatizo utaelezwa.
Na kama wakikubishia lazima wataangalia camera tu. Wataona reaction yako ulivyoact at the time umegundua uko short.....
So next time just do yourself a little favor and count the money.
Na kama ni mchezo mchafu basi hautakua peke yako siku hiyo itakua kila aliyetoa hiyo bank siku hiyo aliwe 40,000.
HATA BABA AMELIWA KIASI KAMA HICHO HICHO ALIPOTOKA LUMANDE AMEKWENDA KWA MGANGA WAKE BAADA YA BENKI KUKATAA KUMRUDISHIA MGANGA KAMWAMBIA ATAZIRUDISHA KIMIUJIZA AKIENDA KUTOA TENA BAADA YA WEEK MBILI ILIMRADI IWE NI SAA 8 USIKU. BADO TUNASUBIRI HIYO SIKU IFIKE.
ReplyDeleteBONGO TAMBAAAALAAAAALEEEEEEEE.
ReplyDeleteMatatizo ya hesabu ATM yapo. Wakati mwingine, waweza kupata risiti as if umepokea pesa, lakini mashine haikutoa kitu. Niliuliza Barclays nilipokuwa Bongo, walisema, makosa huwa yanafahamika baadaye kwenye mashine, na huwa wanakurudishia pesa yako kama kawaida. Hivyo, baada ya sh. 40,000 kupungua, angalia salio lako baada ya siku tatu, unaweza kukuta haikutoka/kupotea. Kwa upande wangu, pesa yote ilirudishwa. FirePower, UK
ReplyDeleteWe anony wa kwanza sijui unabiga box wapi mimi ishanitokea hapa ukerewe nimeenda kuchukua pesa kwa ATM haikunipa kitu kucheki balance inaonyesha pesa imetoka bahati nzuri nilichukua risiti, nikaenda kwenye branch yangu (barclays) nikamuona mdada mmoja akadai hawezi kunisaidia niende kwenye bank ya hiyo ATM (bank of scotland) na wenyewe wakasema hawawezi kunisaidia nirudi kwenye bank yangu. Na hapo nilikua nasubiria mshiko huo kwa hamu kama unavyojua kazi za agency malipo fridayz. Anyway baada ya kupata hayo majibu nikadata kidogo nikarudi nyumbani kupumzika after few days nikarudi barclays nikaongea na mdada mwingine nikampa issue kama ilivyo nikampa risiti akawacontact bank of scotland wakaconfirm kua ATM yao ilikua imeishiwa pesa ndio nikarudishiwa pesa zangu. So sio bongo peke yake hata ughaibuni ATM mbovu tu, hamna dili lolote labda uwe kwenye benefit of which is stupidit.
ReplyDeleteyani nikisoma izi mada these days za WIZI wa mabenkini...sina hamu kabisa
ReplyDeleteyan either 2 natumia pesa adi mwisho na kuweka uchagoni zile chache..
mateso matupu izi benki
Hilo lipo sana Tz,mi ilitokea hivyo mwaka jana,mama yangu alikuwa busy nashughuri zake hivyo akanipa card yake na ps nikamchukulie pesa pale NMB Ilala, mi nilipokwenda baada ya kuingiza card nikataka kuchukua kiasi alichoniambia,mashine ikagoma kutoa ile pesa!!ila ikanipa risity ikionesha sijachukua kitu.
ReplyDeleteMi kwa fikra zangu nikasema labda pesa haitoshi,lakini mashine haikujibu hivyo kuwa pesa haitoshi,nakumbuka nikajaribu kuchukua tena nikaomba kutoa elfu 20,machine ikatoa risiti ikiniambia kuwa ombi langu limefeli. Basi nikampigia cm bi mkubwa nikamweleza hari ilivyo hivyo sijafanikiwa,nilichofanya jioni nikampelekea risiti zote mbili nilizopata pale kwenye mashine.
Baada kama ya wiki yeye akaenda kuchukua pesa,akakuta pesa si kama alivyoziacha,akaomba bank statement,pale ikaonesha kuwa tarehe ile ambayo mimi nilikwenda bank na mda ule ule kuwa nilichukua pesa mara mbili.Basi wakamuuliza nani kwa mda ule alikwenda kuchukua pesa ikabdi awaambie kuwa alimtuma kijana wake,wakamwambia kuwa kafanya makosa sana na kijana mie si waaminifu hivyo nimemuubia tayari!!
Bi mkubwa akanipigia simu na kuniambia kuwa imekuaje nimechukua pesa na yeye nikamwambia vingenevyo, wadau najua hapo mnaelewa kuwa kidogo hali na upepo ukawa si wenyewe, mi nakamshawishi sana kuwa anielewe na hizo pesa mimi nafuatilia na watarudisha hakuna pesa mimi niliyochukua.
Basi siku ya pili mimi na bi mkubwa tukaenda pale bank, pale nikaomba kuongea na afisa wa wateja,sasa dada yule tuliyemkuta na kumuomba aniruhusu nikaongee na huyo customer care, akashtuka akaniuliza kuna nini kwanza, mi nikamwambia nina shida naye, akanijibu nimweleze kwanza hiyo shida yeye akishindwa kuitatua ataniruhusu niende kwa customer care.
Basi mi nikamweleza tatizi lililopo, hoja yake yeye pia ikawa mimi nimemuibiwa bi mkubwa wangu, kwa hakika aliniudhi sana yule dada na maneno yake ya kiswahili swahili,mi nikamwambia,kama hiyo ni hoja yako niruhusu niende kwa customer care nahisi na yeye tutaelewana,akagoma!!
Nikamwambia,mara ya kwanza niliandika nataka kuchukua laki 2,mashine ikasema ombi limafail,lakini huku inaonekana ilitoka elfu 60, mara ya pili nikaomba elfu 10,mashine ilifail lakin huku ikaonesha ilitoka elfu 20,nikamwambia kama hiyo program imeandikwa na mtu basi mi nataka kuongea kwanza na customer care wenu pili nitaomba pia kuongea na huyo muhusika wa hizo mashine zenu,wakimishawishi kuelewa kuwa mi pesa nilichukua basi mi na bi mkubwa wangu tutamaliza home, na wao pesa sitawadai. Yule dada akafikiria basi akaniambia nyie nendeni kesho wewe mama njoo uangalie uangalie pesa zako.Basi bi mkubwa yeye akaondoka ila mimi bado nikawa nataka nikaonane na customer care wao kujua nini hasa wanachofanya kwa binafsi niliamini kuna wizi huwa unafanyika,na kama mimi nisingekuwa makini wakupeleka zile risiti ningeweza kupoteza uaminifu kwa mzazi wangu. Nasikitika kuwa sikufanikiwa na yule dada pale alikataa kata kata kuniruhusu kwenda mbele, lakini siku ya pili bi mkubwa alipokwenda kucheck pesa zikawa sawa sawa nikimaanisha zilizoandikwa zimetoka zilirudi.
Kwa kusema hayo, wanaohujumiwa na ATM kwa TZ ni wengi ila hasa usipokuwa makini na kwa kujua kuwa pesa si kitu cha kufanyia mchezo.
Ninachoamini baada ya mkasa ule, kwa pale bongo hasa ATM ni kuwa yawezekana ndani kwenye kile chumba yawezekana huwa kuna mtu anakaa,hasa siku za jumamosi, na huyo mtu ndiye anayesaidia kuzifekisha zile mashine,na yawezekana ni dili la watu kadhaa kwenye hiyo branch husika.
Du sanaa mpaka bank, Bongo si mchezo!!!! Yaani jamaa walitaka kukupeleka jela live bila kosa lolote na hela wawalize. Ukizingatia kuwa bongo hakuna police wa upelelezi, mzee ungenyea debe, shukuru tu kwa kuwa pesa ilikuwa ni ya mzazi wako, ingalikuwa ni jirani alikutuma na mtu wa kuwaka, leo ungelikuwa Segerea.
ReplyDeleteBongo headache tu si tambalale wala nini
After reading about ATM issues and poor customer service tulionayo bongo kwa kweli ina discourage kurudi bongo. Kama unaibiwa macho macho hivi na bank, how about kwenye huduma nyingine. This is ridiculous.
ReplyDelete