Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu ((kushoto), akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Uchangiaji wa Mfuko wa Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Tumaini, jijini Dar es Salaam, Mhandisi Harold Temu, mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 25 mchango wa TBL kusaidia ujenzi huo. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika, Dar es Salaam jana, ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Geoffrey Mmari (wa pili kulia) na Japhet Minja ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho upande wa taaluma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Naona hiki chuo hakina tumaini kabisaa, kama ninavyofahamu itikadi za kanisa la kilutheri, wasingekubali vijisenti vya kilevya. Ni kama mfano TBL wafuturishe waisilamu, nafikiri hii haiwezekani.

    Mkulima Kisarawe

    ReplyDelete
  2. Tumaini kulikoni majina ya Temu, Minja, Mmari bila shaka bursar atakuwa Masawe n.k!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. MUNGU WANGU,YESUUUUUUUUUUUUUUU!!!!!!!!!!!!!!!!!!! NI NINI HIKI, SASA TUTAPONEA WAPI? KAMA WALUTHERI YALE YA ROSTAM MLIPIGA KELELE ETI FISADI HAWEZI KUSHIRIKI NA NYIE BIBLIA INAKATAZA, JE KILEVI MUNGU ANARUHUHUSU, HII HELA YA TBL YA NINI MNAPOKEA? KWANI ILI CHUO CHA KANISA KIENDELEE LAZIMA MPOKEE HIYO HELA?
    SASA VIONGOZI WA DINI MNATUPELEKA SIPO?

    ReplyDelete
  4. Mkulima Kisarawe alishasema, pls rudisheni hiyo hela, hatuitaki humu kanisani. Eeehe ni nii hiii ..!!???, semeni wakulima tuwachangie vijana wetu waende shule

    ReplyDelete
  5. Acheni itikadi zenu mbovu nyie wakati mnalalamika kilevi legue ya Znzibar inazidi kudidimia ebu jaribu kufikiria chuo cha Kiislam pale Morogoro kingekuwa kinapokea misaada kama hii kingekuwa wapi? Wale wanaopinga shule ya Kikristo kupokea misaada ya TBL nathani ni wenzangu nami Walokole wanaosoma biblia wakati wameigeuza! Yesu mwenyewe aliongeza mikate, divai (Wine) na samaki watu wakanywa mpaka wakasaza! sasa tatizo liko wapi? Solder on Prof.(s) na wala msiwasikilize hao wanaopiga makelele eti mbona majina yenu yakina Masawe nauhakika vyeti vyenu vilikuwa bora zaidi wakati wa Interview ya kuomba kazi Tumaini! Mbona hamuulizi siku hizi CCM kila baba aliye madarakani na mtoto anafuata hata kama baba bado yupo madarakani? haohao wachaga mnaowasema ndo haohao wako ready kufanya kazi na mtu yeyote awe Mkenya (KCB,Precissionair, ITV/EATV, Athi River)? awe M-South Africa(TBL, Mnet, Kwanza Bottlers,Tanga Cement, Vodacom, Zain) kama Wahaya walivyo makatibu wakuu wa Sirikali ya Mafisadi! ina maana hawaogopi kunyang'anywa kazi au biashara zao kufa? Jibu ni hapana ni watu wanaopenda kujaribu ukiwapa nafasi na kila Mtanzania anapaswa kuwa hivyo! Acheni kelele nyingi kuweni washindani!

    ReplyDelete
  6. wachagga bwana, wako kila mahali, TBL wamejazana kibao wao ndiyo mameneja, wao ndiyo mamiss kote huko wapi, nawapa hongera kwa hilo

    ReplyDelete
  7. TBL wanashindana na VODA nani mwenye pesa zaidi na kutoa msaada zaidi, nyie tu hamjui

    ReplyDelete
  8. wachagabwana hata kule kijijini kwetu malangali mufindi kijiji cha itengule wapo tele,kwa kugombania ardhi ndo wenyewe, ukipakana nao kwenye ardhi imekula kwako bora uuzie mchaga mwenzie wapambane wao kwa wao.siwapendi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...