Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na uvivu Mh. John Pombe Magufuli (pichani) leo ametangaza kwamba zile tani 296.32 za samaki zilizokamatwa kwa wavuvi haramu wa kigeni sasa hazitouzwa wala kupigwa mnada bali zitagawiwa bure kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo za elimu.
Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari leo mjini Dodoma Mh. Mafufuli kasema serikali haifanyi biashara hivyo samaki hao wenye thamani ya shilingi 2.07 bilioni watagawiwa bure katika sandakarawe ambalo litafanyika wakati wowote kuanzia wiki ijayo.
Habari zaidi
Ni vizuri kutoa vitoeo hivyo kwa taasisi zilizotajwa kama shule na hospitali. lakini sidhani kwamba ni kwa sababu serikali haifanyi biashara. Mbona nyumba za serikali ziliuzwa na hazikutolewa bure? Hiyo haikuwa biashara?
ReplyDeleteBaada ya miaka michache TAKUKURU wataibuka na kudai jamaa ameisababishia serikali hasara.
ReplyDeleteTanzania, nakupenda kwa moyo wote.
Hao tuna ni dhahabu Japan ambako wanakula samaki wabichi ndio maana hao wavuvi haramu wamekuja kuwasaka Tz. Ila kama serikali imesema haifanyi biashara basi huo uamuzi wa kuwagawa bure ni mzuri sana. Hongera kwa hilo.
ReplyDeletebora watafanya la maana sana tena sana.....
ReplyDeletebro mithupu kigezo gani wametumia kufikia maamuzi hayo sasa na si toka wakati ule? na zile milioni 700 zilizotumika kuwatunza samaki hao hasara ya nani? inaniuma sana maana nakatwa kodi katika kijimshahara changu kila mwezi matumizi yenyewe ndiyo hayo. Haya bwana ipo siku! Bazoka
ReplyDeletehahahahahahaaaaaaaaaaaaaaa......michu
ReplyDeleteumeniacha hoi! mzee john pombe kakukosea nini mpaka ukamuita Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na UVIVU! taratibu lakini, kiongozi wa kitaifa huyo...hivi hivi tutastukia usalama wa taifa wamekuchukua kimya kimya kwa mahojiano ya kina.
mmmhhhhhh maajabu ya musa kwa serikali ya tanzania kutoa kitu bure namna hiyo,au hao samaki wameisha haribika ndio maana mnataka kutupa bure?
ReplyDeleteHao samaki ni wazima lakini wakufaa kuliwa na binadam??
ReplyDeletehao samaki lazima watakua wamepungua viwango vya ubora wa kuuzwa, shule na taasisi mtakao bahatika mkiwapata tu spidi kwenye kikaango mkichelewa tu wanawaozea mikononi. naomba mniamini katika hilo!!
ReplyDeleteThe brain
Matatizo ya socialism ndio haya-mgao mgao.Hivi kwanini hawapigi mnada ili hela watakayoipata wainvest kwenye kitu cha maana cha maendeleo.huyu si waziri wa maendeleo. fikirieni la maana la maendeleo ya nchi..
ReplyDeleteMdau UK
duh, talk about misplaced priorities..... yaani tumewahifadhi kwenye private cold facilities muda wote na sasa tunasema tunawagawa bure??? hapana, wauzwe kisha pesa zinazopatikana zitumike kuli madeni na balance ipelekwe hukohuko kwenye mashule na taasisi nyingine kununulia vitu vingne muhimu jamani, hata mchele etc itakuwa na manaana zaidi!!!!
ReplyDeletejamani, eeeeeeh!!!!
Samaki wagawiwe kwa watumishi (Mkoa mzima au Nchi nzima kama wanatosha) wa idara iliyoibua na kusababisha kukamata wezi kama motisha kwa Watz kuajibika kulinda mali za umma.
ReplyDeleteThe goverment does not do business.Is the reason from the minister behind the idea of auctioning.
ReplyDeleteWhat is the business?different nature of businesses?Not for profit and for profit.why does the goverment borrow money?why issuing gilts?to finance the different ministries budgets?Public sectors eg police,educational institutions,public transport systems,technological infrastuctures?
The issue is obvious NOT FOR PROFIT but for EFFICIENCY,EFFECTIVENESS,ECONOMY.
GVT does have a lot of developmental projects and has to protect front line public services such as health care.....
Anyway,I am trying to ascertain opportunity costs with this decision.2Bil Tsh could help create jobs let say in Fish industries if REINVESTED......
anyway....there are better decisions he could have made.....
THERE ARE NUMBER OF STRATEGIC CHOICES/DECISIONS TO HAVE SUSTAINABLE ECONOMIC DEVELOPMENT
...Have got to invest in future..socialistic views lead to iefficienciess and are not long term but merely social fantasy....Mgaooooo
Mdau ( John ) UK
siamini...after all these months?kwa sababu gani asa/yaani vigezo vilivotumika?
ReplyDeletekwa kweli sijawahi kuona nchi ilio na viongozi wabovu kama tanzania (michuzi usinibanie) yaani serikali imetumia mamilioni ya pesa kuwahifadhi hao samaki katika majokofu, imetumia pesa nyingi kuendesha hiyo kesi, kuwatunza hao mabaharia na kuwalisha wakiwa mahabusu...wananchi walitoa maoni hao samaki wauzwe kwa bei nafuu kwa walalahoi lakini serikali ikajifanya kiziwi na kupanga bei ya juu sana kutaka kuuza hao samaki, wananchi wameona hiyo ni bei kubwa wakashindwa kununua; swali la kujiuliza je kwa nini hawakuamua kugawa bure au kuwauzia wananchi kwa bei nafuu wakati ule? wanasubuli mpaka serikali imepoteza mamilioni ya pesa kuwatunza harafu leo ndio kiongozi mzima wa nchi anadiliki kusema wagawiwe bure kwa nini wasiuzwe pesa itakayopatikana angalau ichangie kupata mitambo ya umeme watu waondokane na mgao wa umeme? hii serikali inajifanya tajiri wakati nchi yetu ni moja kati ya nchi masikini za kutupwa duniani,kazi kununua majengo ya ubarozi ya gharama nje ya nchi wakatu wananchi wake wanaishi kwa usd 2 pengine 1 kwa siku..lo ni aibu sana mungu tunusuru watanzania iko siku kitaeleweka na patakuwa hapatoshi hapo tz
ReplyDeleteYule jamaa aliyekua anawaifadhi ameshatajirika...Na Magufuli amechukua 10% yake, huo ndio ukweli!!!
ReplyDeletedu, natamani kulia usanii nchi hii kila mahali, eti anasema nchi haifanyi biashara, sasa mbona walitoa kwenye gazeti tenda ya wanaotaka kununua samaki , hakuna aliyetokea kwasabbu wameoza yeye anasema wanagawa bure. poa namshauri atayarishe na dawa za kuhara maana nchi nzima tutaharisha.
ReplyDeleteJe budget ya milioni 700 zilizotumika kuwatunza samaki kwenye cold facilities zilitoka wapi kama sio kodi zetu wananchi? Inakuwaje leo mmnafikia uamuzi wa kugawa bure wakati siku zote mlikuwa wapi au fungu la kuwatunza limeisha?
ReplyDeleteNi muhimu wauzwe hata kwa bei ndogo kufidia hasara, labda mseme hawanunuliki.
"There is no free lunch", there must be a reason behind this vague decision.
Hapa watu hawajiuliza maswala muhimu,unafikiri gharama za kuhifadhi hao samaki toka walivyokamatwa alikuwa analipa nani? Jibu....WALIPA KODI! Je,haijazidi hiyo thamani ya samaki wenyewe?
ReplyDeleteKwakuwa samaki hao wanahifadhiwa kwenye baridi, hivyo umeme ni swala muhimu mno tena bila kukosa. NAMGAO HUU WA TANESCO....INAONEKANA GHARAMA ZA KUNUNUA DIESEL YA GENERATOR NA HATA BILLS ZA TANESCO NDIYO IMEWASHINDA SERIKALI NA KUJIFANYA KUTOA BURE!
JE,HILILINAHITAJI MSOMI WA DGREE KUFIKIRIA KABLA HATA HAWAJAANZA KESI AU SIKU CHACHE BAADA YA KUANZA KUHIFADHI SAMKI HAO?
Nani atalipia hizo gharama?
Jamani, jamani, jamani tusijidanganye kuwa hao samaki watagawiwa bure ni uongo mtupu. Samaki hao wana "quid pro quo" Kwanza watapelekwa sehemu zenye watu wanaovaa kijani na njano kwa wingi. Halafu sehemu zingine, viongozi watakuwa wanawauza kwa bei ya chee kutunisha mifuko yao.
ReplyDeleteHivi kama serikali ingemua kuwauza kidogokidogo kwa bei Tanzania (I mean bei ya kusaidia wananchi) si wangekuwa wameisha?
Wameona mgao wa umeme umefika nia kuwatunza kwa majenerator ni gharama wanaona bora wawatupie wananchi samaki waliochina nusu kuliko kuja kuwafukia wakiisha china wote.
Kwa wale wa zamani kuchina (ni kuoza kwa kitoweo ambacho unaweza kula tu, ila ukisema wameoza huwezi kula utasikia unyanyapaa ndiyo maana tunatumia Tafisida)
Jamani wengine kwa taaluma zetu tunamajukumu ya kuonesha angalau tulishiriki vipi katika kuzuia Foodborne illness itakayo sababishwa na kitoweo hicho kilicho hifadhiwa kwenye mafriji kwa zaidi ya miezi 3! Naomba mungu uwe shahidi katika hili, mimi nanawa mikono damu ya watakao pata maradhi ya matumbo kwa sababu ya samaki hao naiwe juu ya kichwa waziri husika na watako shiriki...!
ReplyDeleteNashauri wafanyiwe uchunguzi (Microbiological test) kuona kama wale bacteria hatari wanaoweza hata ku survive low temperature (0 centigrade) kama Listeria monocytogen. Naomba hatua za makusudi zichukuliwe katika hili, ukichukulia kwamba samaki wenyewe wamevuliwa kwenye ziwa ambalo uchafuzi wake ni wa hali ya juu.
Magufuli usije sababisha wanafunzi wetu kukosa masomo kwa kuwapa waalimu magonjwa ya kuhara!
Hakuna seriousness
ReplyDeleteMuda wote huu leo ndio wamejua kwamba kuwahifadhi kwa mamilioni is nonsense!!!
Nchi imekosa leadership hii!!
LOL!! Hii nchi!!! kweli ina wenyewe. Yaani baada ya kulipa $236,800 kwa mwezi kwa ajili ya kuwahifadhi kwa muda wote wa takriban miezi nane wameamua kuwagawa baada ya kutengeneza Takriban $1,894,400 (Zaidi ya Tshs bilioni 2) sawa na iliyokuwa bei ya kuwauza hao samaki.
ReplyDeleteKila mtu analia kwenye kamba yake
Ni mapema mno kumlaumu Bwana Pombe kwa hili. Yeye amefanya harakati kukamata wavuvi haramu. Hatua inayofuata inahusisha mahakama na vyombo vingine vya dola, sio yeye. Kadri hatua zinavyochelewa ndivyo gharama za storage zinavyoongezeka (na mgao wa umeme tena ndio usiseme). Sasa imefika hatua wakiendelea kuhifadhiwa basi wanahifadhiwa kwa hasara.
ReplyDeleteKwa upande mwingine wakiwagawa bure kwanza hawaingii gharama za storage na yaelekea nia ni kugawia taasisi za serikali kama mashule. Shule hizo hupewa fungu kwa ajili ya msosi kwa hiyo ni kama serikali imejiuzia hao samaki kwa bei ya hasara.
Uzoefu ni makosa uliyowahi kufanya na kujifunza kwayo. Meli nyingine ikidakwa tumeshajua cha kufanya.
Microbiologist vipi unatupiga fiksi, samaki hawakuvuliwa ziwani hao, walivuliwa baharini.
ReplyDeleteAta hao samaki si bure tu, kuna tatizo, kweli hao samaki ni wazima, within 7 mornths? Tanzania bado atujafika atua hiyo kweli ukweli tuseme ukweli.......?????????????????????????????????????????????????????????????????????
ReplyDeleteMdau, Malaysia
kuna swali moja la kujiuliza,ok hao samaki wanagawiwa bure hapo dar essalaam tu au hadi mikoani ? maana tanzania sio dar es salaam peke yake sasa ina maana hao watakaopewa bure ina bidi watumie pesa tena kwa ajili ya kukodi maroli yenye kuhifadhi baridi hadi mikoani? au serikali itatumia tena pesa za usafiri wa magari yenye jokofu kuzipelekea hao samaki taasisi zilizo mikoani mfano mwanza, kagera, sumbawanga? mhhh kweli kuna wasomi wa economy hapa tanzania? mimi sina elimu yoyote wala sina degree yoyote lakini nimeshaliona hili..
ReplyDeleteJamaniiiiiiiiiiiiiiiii, ya wapi hii tena. Makubwa serikali yetu hii, hao samki hivi kweli ni suitable for human health au ni mambo ya kutest na kuua watu. Siamini kabisa kama bado hao samaki wako salama kabisa kuliwa na binadamu. Mimi sijui manake nchi yetu hii kuwapa watu mizoga sio news!!!
ReplyDeleteHivi hawa samaki si walishafanya tenda ya kuwachukua, sielewi, ni poor planning, or poor implementation or poor decisions? Ila Magufuli ninavyomfahamu hii issue atakuwa ameishikilia bango kwa muda mrefu sana, hadi kufikia huu uamuzi.
Bravo, Pombe
Kweli watanzania ni Wadanganyika kweli huwa tuna tapeliwa na maneno matamu ya uongo ya wanasiasa na kuishia kukubali.
ReplyDeleteHao samaki walitaka kuuzwa mwanzo hadi wakachagua YONO auction mart kuwauza na wakatangaza mpaka magazetini kwa taama zao wakataka kuwauza kwa bei juuu....eti leo wanasema serikali haifanyi biashara LOL uongo gani huuu......Wamefanya makosa kinachotakiwa waombe msamaha kwakuliingizia taifa hasara na si vinginenyo
Magufuli awe kwanza kuwala hao samaki.
ReplyDeletekweli huyu pombe
ReplyDeleteTunapimwa viatu Jamani. mmesahau kama mwakani 2010... mjomba oyeeeeeeeeeeeee
ReplyDeletePombe kweli!!!
ReplyDelete