
Flashback January 3, 2008: Mama Lucy Mwandosya akiwa na yatima wa Lufilyo anaowasaidia. Ujumbe wake ulikuwa huu chini...
Happy New year.Check hayo maisha ya watoto wengi huko Lufilyo, Tukuyu, Wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Ndio maisha taharishi! Naomba wadau wako wanisaidie niweze kuwajengea angalau nymba ya matofali mabichi masikini yatima hawa.
LUCY' S HOPE CENTRE FOR ORPHANS
P.O.BOX 5511,
DAR ES SALAAM
ama P.O.BOX 260,
TUKUYU
Na Mwandishi Maalum,
LUCY' S HOPE CENTRE FOR ORPHANS
P.O.BOX 5511,
DAR ES SALAAM
ama P.O.BOX 260,
TUKUYU
Na Mwandishi Maalum,
Rungwe, Mbeya
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amekemea tabia ya baadhi ya wananchi wadanganyifu wanaotumia matatizo ya watu wengine, kama vile yatima na watu wanaoishi na virusi kwa ukimwi, kujinufaisha binafsi na fedha za wafadhili zinatolewa kuwahudumia watu hao.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amekemea tabia ya baadhi ya wananchi wadanganyifu wanaotumia matatizo ya watu wengine, kama vile yatima na watu wanaoishi na virusi kwa ukimwi, kujinufaisha binafsi na fedha za wafadhili zinatolewa kuwahudumia watu hao.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake kwa sasa inawasomesha bure katika shule mbali mbali za sekondari nchini watoto yatima zaidi ya 32,700.
Akizungumza baada ya kuwa ameweka jiwe la msingi la maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Matumaini cha Lucy (Lucy Hope Centre) katika kijiji cha Lufilyo, Wilaya ya Rungwe, katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku nne Mkoani Mbeya, Rais Kikwete amekemea tabia hiyo ya watu wadanganyifu.
Rais amewaambia mamia kwa mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji jiwe hilo la msingi: “Huu ulaji wa raslimali za yatima, za watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, unakera sana.”
Ameongeza: “Watu wanaanzisha NGO’s, wanaitisha michango, wanapata fedha za wafadhili lakini wanatumia fedha zinazopatikana kujinufaisha binafsi. Wanajaza matumbo yao tu. Nimeambiwa habari ile pale Wilayani Makete, Mkoa wa Iringa na inakera sana.”
Kituo hicho cha Lucy Hope Centre kimeanzishwa na kinaendeshwa na Mama Lucy Mwandosya, mke wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark James Mwandosya, na kimejengwa karibu na nyumbani kwa familia hiyo katika eneo la ukoo wa Profesa Mwandosya.
Shabaha kubwa ya kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2003 ni kutumikia na kutunza watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.
Rais Kikwete katika hotuba yake fupi kwa wananchi hao baada ya kuwa ameweka jiwe hilo la msingi ameeleza pia kuwa utunzaji wa watoto yatima na walioko katika mazingira magumu ni Sera ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Amesema kuwa chini ya Sera hiyo, Serikali yake inawasomesha bure wanafunzi yatima zaidi ya 32, 700 katika shule mbali mbali za sekondari
nchini.
Rais Kikwete vile vile amesema kuwa katika kujali watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu, Serikali yake imeanzisha Sera ya Watoto ambayo inatambua umuhimu wa kuhudumia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.
Ameongeza vile vile kuwa Muswada wa Sheria ya Watoto unatambua umuhimu wa kuhudumia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.
Rais Kikwete amemwagia sifa Mama Mwandosya na Profesa Mwandosya kwa juhudi za kuanzisha kituo hicho ambacho kwa sasa kimehudumia na kusaidia zaidi ya watoto 300, ambao baadhi yao sasa wanasomeshwa katika shule za sekondari nchini.
AMINI USIAMINI KIJIJINI KWA MAMA HUYU NI SEHEMU MOJA NCHINI AMBAYO INA RUTUBA NYINGI NA MVUA NYINGI KIASI KUWA HAKUNA SABABU YA KUWEPO UMASIKINI KAMA KWERI SERIKALI YETU INGEKUWA INATEKELEZA INAYOYASEMA, HUKO HAWAHITAJI KILIMO KWANZA KWANI WAO TAYARI WANALIMA MWAKA MZIMA NA WANALIMA MAZAO YOTE UNAYOYAFAHAMU, MKUNGU MKUBWA HUUZWA KWA SHILINGI ELFU MBILI! NYUMBA HIYO INAYOONEKANA HAISTAHILI KUWEPO HAPO LABDA TU KAMA HAYO NI MATUNDA YA MKUKUTA AMBAO PIA UMEZAA MZEE WA VIJISENTI.
ReplyDeleteHayo ndio maisha ya watoto wetu vijijini! Halafu mdau anaomba mfandhili wa kumpeleka mtoto wake kutembea Hong Kong!!!
ReplyDelete