
Exim Tower ni kikwangua anga kipya ambacho kimeshakamilika na mabati ya uzio wa ujenzi kuondolewa hivi karibuni. Kwa wageni wa Dar ama wale walioondoka siku nyingi kikwangua anga hiki kipo jirani na makao makuu ya polisi na uhamiaji ama kanisa la St. Alban na YWCA. mabati yaliyoziba njia hiyo ya kuelekea Gymkhana sasa hayapo tena. hii picha nimepiga usiku huu
duh safi sana sasa DAR ES SALAAM inazidi kupendeza kwa kuwa na majengo mazuri na ya kuvutia, lakini pia tuwakumbushe mamlaka zinazousika pia wajaribu kuboresha miundo mbinu inayoelekea katikati ya mji maana majengo makumbwa kama haya maana yake kuwa idadi ya watu na magari katikati ya mji itazidi kuongezeka,au majengo kama haya yajengwe pembeni ya mji kupunguza msongamano katikati ya jiji,Mdau NGAMANYA
ReplyDeleteNaungana na mdau Ngamanya; majengo haya ingekuwa vema yakajengwa nje ya mji kupunguza msongamano wa watu na magari.
ReplyDeletehongera Tanzania, vikwangua anga vinaongezeka kwa kasi sana, mimi sio mtaalamu wa uchumi ila sidhani kama ndio utambulisho wa ukuaji wa uchumi wa nchi.
ReplyDeleteHOFU YANGU KUBWA NI MSONGAMANO WA MAGARI KATIKATI YA JIJI, HAPO LILIPO HILI JENGO JIRANI KNA MAJENGO MENGINE KAMA, MAFUTA HOUSE, PPF TOWER, BILA KUSAHAU KUNA MAJENGO MAWILI YANAJENGA (UHURU HEIGTHS NA VIVA TOWER) ACHILIA MBALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI NA MENGINEYO. HEBU JARIBU KUPATA PICHA YA HARAKA HARAKA ITAKUWAJE BAADA YA MIAKA MIWILI IJAYO, ITAKUWA BORA KUTEMBEA KWA MIGUU KULIKO KUPANDA GARI.
HIYO NI CHA MTOTO HEBU TUENDE MBALI KIDOGO, MOTO! MOTO! MOTO!, TUNAJENGA MAJENGO MAREFU WAKATI UWEZO WETU WA KUZIMA MOTO TUNATAMBAA. KILA SIKU NIMEKUWA NAJIULIZA ITAKUWAJE MOTO UKITOKEA? MIUNDOMBINU YA KUZIMIA MOTO NI DUNI HATA KWA KAMPUNI BINAFSI ZINAZODAI KUTOA HUDUMA HIYO. OFISI NYINGI HATA ZA SERIKALI HAZINA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO, HATA OFISI ZILIZO NA HIVYO VIFAA VIMEACHWA KAMA UREMBO HAKUNA ANAYEJUA KUVITUMIA.KUMBUKA MOTO IKULU TULIAMBIWA ULITEKETEZA OFISI YOTE YA RAIS,KUMBUKA MOTO AMBAO ULIKUWA UNATOKEA JENGO LA KITEGA UCHUMI, HAPO UTAPATA PICHA YA HARAKA ITAKUWAJE MOTO UKITOKEA KWENYE ULE MSITU WA GHOROFA KARIAKOO. MUNGU TUSAIODIE TANZANIA MAANAKE KUNA MAJANGA UKIYAFIKIRIA UNAONA AHERI YA EL-NINO. \
HEBU TUAMKE WATAALAMU TANZANIA TUWE TUNAWAZA KWANZA KABLA YA KURUHUSU UJENZI WA HIVI VIGOROFA(VIKWANGUA ANGA). TUSIWE TUMEKALIA KUTI KAVU.
haya majengo mbona kama styles zimewapitia kushoto! Majengo ya sasa ni glass na steel sio zege kama hilo!
ReplyDeletemajengo makubwaaaa umeme wa mgao mji mzima umejaa makelele ya genereta,kila kitu posta hayo majengo yangekuwa yanajengwa nje ya mji kupunguza foleni za magari kwenda mjini hivi hawa viongozi wa tanzania huwa hawaoni mifano wakienda nchi za wenzao?
ReplyDeleteyaani haya majengo mapya yooote yaliyojengwa yangejengwa kigamboni kwa mpangilio mzuuuri mbona pangekuwa patamu. Huku dar wangekuwacha na kukawa Old Dar es Salaam. Kuna Uhuru heights, Viva, PSPF 30 flrs, TPA 36flrs, NSSF pale Haidery, CBA pale pembeni ya Barclays, Nyerere Conference Centre 18flrs, TBA kule Ocean Road, Manji/ Quality pale 19 flrs Salamander, Paradise pale Topaz na majengo mengine kama 10 ambayp yako kwenye mchakato wa kujengwa, sasa wote hawa wangejenga mji mpya na kukawa na tax incetives ya wafanya biashara, miundo mbinu ya kisasa, parks, schools, hospitals, shopping malls etc mbona in five years pangependeza!
ReplyDeleteBlaza Michu salama?
ReplyDeleteJuzi nilikuandikia kukuomba maendeleo ya vikwangua anga vinavyoendelea hapo mjini.Napata faraja sana nikiona mambo yanaenda hivi,hii ni kutokana na uzalendo nilionao.
Naomba utumie mwongozo wa anony wa "Fri Oct 30,12:49:00 PM" kutuletea maendeleo ya vikwangua anga vyote alivyovianisha.Naomba kumpongeza kwa kutung'ata sikio,maana vingine alivyovianisha sikua nafahamu kabisa.
Haya ingia kazini kaka.
Ndimi,
Mzawa.
Anonym 12.42, we ndo unajidai unaenda na wakati kumbe ndo uko nyuma kabisa, hayo majengo ya glass and steel kwenye nchi zilizoendelea ni kwa sababu nchi hizo gharama za ujenzi kwa kutumia concrete na cement ni kubwa mno,
ReplyDeletematerials hizo zenyewe hazipatikani tena, ujenzi wa concrete na cement bado ni ujenzi madhubuti kuliko glass na steel,
mi sisemi sana, yaliyotokea September 11 si yameonekana! ndio ujenzi wa steel and glass huo,
structurally, ujenzi huu ndio muafaka kwetu
Mgogoro wa Loliondo watua mikononi mwa Mwangunga
ReplyDeleteNa Mashaka Mgeta
Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, amekabidhiwa taarifa ya mgogoro wa wafugaji na mwekezaji Kampuni ya Ortelo Business Corporation (OBC) katika pori tengefu la Loliondo.
Mgogoro huo pamoja na mambo mengine, unagusia madai ya kuchomwa moto kwa makazi ya wafugaji wa Kimasai maarufu kama maboma katika baadhi ya vijiji vilivyopo Loliondo Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ezekiel Maige, aliliambia Bunge mjini hapa jana kuwa Mwangunga alikabidhiwa taarifa hiyo jana kutoka kwa timu aliyoituma kushughulikia mgogoro huo.
Alisema Mwangunga ataiwasilisha taarifa hiyo kwa Kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Mazingira, inaoyoongozwa na Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai, Novemba 2, mwaka huu mjini hapa.
Maige alisema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka.
Ole Sendeka alitaka kujua ikiwa mgogoro wa wafugaji na mwekezaji ambaye ni kampuni ya OBC, unaweza kuchangia uvamizi wa wafugaji katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro.
Maige alisema suala la Loliondo linatofautiana na changamoto zilizopo katika hifadhi ya Ngorongoro na kwamba ufafanuzi zaidi kuhusu mgogoro huo utajulikana katika taarifa ya Waziri Mwangunga.
Pia, Maige alisema wizara hiyo haijapata taarifa rasmi kuhusu mpango wa kuliondolea eneo la Ngorongoro hadhi ya maajabu saba ya dunia.
Lakini, Maige alisema taarifa ya wakaguzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (Unesco), iliionya serikali ichukue hatua za kulinda sifa za eneo hilo, ili lisiingizwe kwenye orodha ya maeneo hatari.
Kwa mujibu wa Maige aliyekuwa akijibu swali la Mbunge wa Kwela (CCM), Chrisant Mzindakaya, onyo la Unesco lilitokana na wakaguzi hao kubaini ongezeko la shughuli za kwenye eneo hilo.
Miongoni mwa shughuli hizo ni kilimo, ufugaji wa mifugo, magari, uchimbaji wa mashimo na mchanga kwa ajili ya ujenzi wa barabara hasa ndani ya kreta.
Maige alisema serikali inachukua hatua kadhaa kukabiliana na changamoto hizo, ikiwemo kupata eneo la ekari 13,000 huko Oldonyosambu kwa ajili ya kuweka makazi ya wafugaji kutoka ndani ya kreta.
Nyingine ni kuchimba mabwawa ya mifugo huko Sendui, Olbalba na Bulati, ununuzi wa chumvi kwa ajili ya mifugo, kusitisha kilimo, kudhibiti uingiaji magari kwenye kreta na kuzuia ujenzi wa lorge.
nani mmliki wa hili jengo
ReplyDelete