Picha zote na mdau Freddy Maro wa Ikulu
JK akanusha kuwapo
mgawanyiko ndani ya CCM
Na Mwandishi Maalum, Musoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa hakuna mgawanyiko ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), bali kuna makundi mawili ya wanachama wa chama hicho yanayovutana Bungeni.
Aidha, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Serikali yake haitasita kumfikisha kortini Mtanzania yoyote atakayethibitisha kuwa ameshiriki vitendo vya rushwa, bali kazi hiyo haitafanyika kwa kuongozwa na misingi ya hisia tu za watu.
Rais Kikwete ameyasema hayo jioni ya leo, Jumatatu, Oktoba 12, 2009, wakati anazungumza na viongozi wa CCM wa Mkoa wa Mara nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa huo, wakati alipokutana nao, ili kubadilishana mawazo juu ya hali ya chama hicho.
“CCM haina mgawanyiko. Hivi hapa Mara kuna mgawanyiko? Mwanza kuna mgawanyiko? Hivi Tanga kuna mgawanyiko? Singida umesikia kuna mgawanyiko? Mgawanyiko uko kwenye magazetini na ndani ya Bunge,” Rais Kikwete amewaambia wanachama hao.
Amesisitiza Rais Kikwete: “Ukweli ni kwamba wale wanachama wetu tuliowapeleka pale Bungeni kutuwakilisha, wanagombana. Ugomvi uko pale pale Bungeni. Wakiondoka wanauacha pale, wakirudi Bungeni wanaendelea nao. Mgawanyiko huu tunaoambiwa hauko Musoma wala Bagamoyo”
Rais Kikwete amesema kuwa wabunge hao wa CCM “wanagombana wao kwa wao na wakati mwingine wanaonyesha kuwa na ugomvi na Serikali yao. Mimi nimekaa Bungeni pale kwa vipindi vinne kama mbunge na wala sijapata kuona hali ya namna ile.”
“Watu wa chama kimoja hawawezi hata kukaa meza moja na kunywa maji. Kila wakikutana ni mti na macho. Lakini tutayamaliza haya. Lile jopo la wazee wetu linafanya kazi na tuna hakika kuwa hili nalo tutaondokana nalo,” amewahakikishia wanachama hao Rais Kikwete.
Katika kikao chake cha karibuni, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliteua Kamati Maalum ya Wazee wa Busara ikiongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kutafakari hali hiyo ya mvutano kati ya makundi hayo mawili na kutafuta mwafaka.
Kuhusu madai ya rushwa, Rais Kikwete amewaambia viongozi hao kuwaeleza wananchi ukweli kuwa kama kuna Serikali ya CCM imepata kuchukua hatua kubwa zaidi za kupambana na rushwa, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha kortini viongozi waandamizi, basi ni Serikali ya Awamu ya Nne.
“Mkiulizwa kwenye kampeni za sasa za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, waambie kuwa haijapata kutokea katika historia ya nchi yetu zikachukuliwa hatua kubwa zaidi za kupambana na rushwa kuliko katika kipindi cha miaka minne iliyopita.”
Amesisitiza kuwa Serikali yake itaendelea kukamata na kumfikisha kortini yoyote ambaye ushahidi utathibitisha anahusika na tuhuma za rushwa, lakini Serikali haitakamata watu tu kwa sababu ya matakwa na hisia za watu tu mitaani.
“Kwenye mazingira ya sasa ya Utawala Bora, hatuwezi kukamata watu kwa hisia na mapenzi tu ya watu. Ni lazima tufanye hivyo kama upo ushahidi wa kuiwezesha Serikali kuwafikisha kortini watu wanaotuhumiwa kwa rushwa.”
Kuhusu kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Rais Kikwete amewaambia viongozi hao wa CCM: “Fanyeni kampeni kifua mbele. Tumefanya mengi. Tuliahidi na tumetekeleza, na tunaendelea kutekeleza. Ni kweli shida za binadamu haziishi, lakini ukweli ni kwamba yaliyoahidiwa yametelezwa kwa kiasi kikubwa.”
Viongozi hao wa CCM wa Mkoa wa Mara wamemwiambia Rais Kikwete kuhusu jinsi kampeni za uchaguzi huo zinavyokwenda.
Katika vitongoji vyote 2,417 vya mkoa huo, CCM haikupingwa katika vitongoji 1, 029.
Katika vijiji 445, CCM haikupingwa katika vijiji 160 na katika mitaa 71, CCM ina wapinzani katika mitaa 69.


Mambo aliyoyafanya JK huko kwa mfano kuzindua mradi wa umeme na kufungua shule yana sura ya kiserikali. Vipi anaongea mambo ya kichamachama tuuu? JK akumbuke ni rais wa Watanzania wote, sio wa chama.
ReplyDelete"Mgawanyiko" maana yake ni nini?
"CCM haina mgawanyiko..."
"Watu wa chama kimoja hawawezi hata kukaa meza moja na kunywa maji...".
Kama sio kugawanyika huko ni nini? Watu bwana.
HIVI AFYA YA JK INAHITAJI MAELEZO KIASI HICHO? JK HUYU ANAYETOLEWA UFAFANUZI WA AFYA YAKE NI TOFAUTI NA YULE ALIYEJITOLEA UFAFANUZI KUHUSU AFYA YAKE WAKATI WA KAMPENI ZA URAISI KWA KILICHO SABABISHA AANGUKE PALE JANGWANI? HA BM TULIAMBIWA ALITEGUKA MGUU AKIWA MTOTO. UFAFANUZI WA MARAMBILIMBILI HULETA MASWALI MENGI.
ReplyDeleteni kweli kabisa mkuu ulivyongea nathan ni sahihi,hotuba haikuwa na malengo hasa katika kuchochea nguvu kazi na maslahi ya nchi na wananchi wake has hususani hapo mara.nachoweza kusema unajua kila mtu anahaha kutafuta kura ndo maana kila sehemu raisi au wabunge watakapoenda ni kuongelea vyama vyao na nini wamefikia.
ReplyDeletenatoa pongezi kwa huyo mzee aliyejenga shule,katika mkoa huo.nathani ni jambo jema la kujivunia na kuigwa kwa watu wote wenye uwezo.tunahitaji watu kama mkono.
Mungu akubariki mzee.
huyo rais nimemchoka mimi hamna ktu hapo..
Nampongeza Mkono kwa kujenga shule ambayo watoto wa masikini wataweza kusoma na kujipatia elimu ambao itawapa msingi mzuri wa maendeleo.
ReplyDeleteHela kapata wapi hilo ni swala lingine.Watu watasema ahaa mihela ya kesi za bioti hiyo.
Sisi tunafurahi tumeona shule.
mbona wanafunzi ni wakubwa??au ni a level?
ReplyDelete