Ni baada ya mapumziko sasa na bado Simba inawaongoza yanga goli lililofungwa na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi katika dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza.
Mgosi aliunganisha majalo moja bomba sana ya dan mrwanda ambaye aliwazuga mabeki wa yanga na kutoa pande. hata hivyo dan mrwanda alitolewa kwa kadi ya njano ya kuchupa ndani ya 18 akisaka penati. refa oden mbaga akamchapa nyekundu
picha na habari zaidi vyaja punde
Jangwani kama kawaida yao na mbeleko. Kwanza TFF wamewafungulia wachezaji wao wenye utovu wa nidhamu. Halafu refa kampiga mtu kadi nyekundu kwa kupiga krosi iliyozaa bao. Shida ya mbeleko haivuki mipaka ya nchi!
ReplyDeletesi mbaya mrwanda keshamaliza kazi yake.
ReplyDeletemambo yatakuwa safi tu.
watani leo mnatakiwa kuwa wapole sana maana hii ni ngoma nzito mwaka huu, simba imekamilika.
Mungu Mkubwa, Inshallah leo Simba mtakula kipunga cha magadi--- Nasi watoto wa Mburahati "Wembe hule hule, Yanga Imara" tutaimba kwa furaha. Yanga jamani zima makelele mtaani wa kuku tetele simba! Hii ndiyo sala yangu leo
ReplyDeleteBro Michu, post hilo libeneke chapuchapu manake sisi huku mashariki ya mbali hatujalala mpaka kieleweke. Presha inapanda na inasuka taratiibu, red card(s) hiyo (hizo) isijekuwa ni kupigana tafu kama walivyosema ndugu zangu hapo. Mwaka huu, aah... mwendo mdundo.
ReplyDeletemwaka huu jangwani kazi tunayo,mi naona hawa makocha wote tuwafukuze tu na timu apewe Ken Mkapa na Sekilojo Chambua,huu ni ujinga!
ReplyDeleteHii habari mbona imekaa kushoto,
ReplyDeleteSimba wamepata goli dk 26 kwa kross ya Dan Mrwanda na mrwanda alitolewa ya DK YA 18? kwa kadi ya njano?
MHHHH.MWAKA HUU SIMBA IKO JUU KI UKWELI.WAONYESHE PIA MAKALI KWENYE KOMBE LA AFRIKA.KAKA MICHUZI OMBI.ITAPENDEZA KAMA UKIWA UNATULETEA MATOKEO YA LIGI YA TZ.KAMA ILIVYO MAMBO YA BWAWA LA MAINI.CHEERS
ReplyDelete