Ni baada ya mapumziko sasa na bado Simba inawaongoza yanga goli lililofungwa na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi katika dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza.
Mgosi aliunganisha majalo moja bomba sana ya dan mrwanda ambaye aliwazuga mabeki wa yanga na kutoa pande. hata hivyo dan mrwanda alitolewa kwa kadi ya njano ya kuchupa ndani ya 18 akisaka penati. refa oden mbaga akamchapa nyekundu
picha na habari zaidi vyaja punde

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Jangwani kama kawaida yao na mbeleko. Kwanza TFF wamewafungulia wachezaji wao wenye utovu wa nidhamu. Halafu refa kampiga mtu kadi nyekundu kwa kupiga krosi iliyozaa bao. Shida ya mbeleko haivuki mipaka ya nchi!

    ReplyDelete
  2. si mbaya mrwanda keshamaliza kazi yake.
    mambo yatakuwa safi tu.
    watani leo mnatakiwa kuwa wapole sana maana hii ni ngoma nzito mwaka huu, simba imekamilika.

    ReplyDelete
  3. Mungu Mkubwa, Inshallah leo Simba mtakula kipunga cha magadi--- Nasi watoto wa Mburahati "Wembe hule hule, Yanga Imara" tutaimba kwa furaha. Yanga jamani zima makelele mtaani wa kuku tetele simba! Hii ndiyo sala yangu leo

    ReplyDelete
  4. Bro Michu, post hilo libeneke chapuchapu manake sisi huku mashariki ya mbali hatujalala mpaka kieleweke. Presha inapanda na inasuka taratiibu, red card(s) hiyo (hizo) isijekuwa ni kupigana tafu kama walivyosema ndugu zangu hapo. Mwaka huu, aah... mwendo mdundo.

    ReplyDelete
  5. mwaka huu jangwani kazi tunayo,mi naona hawa makocha wote tuwafukuze tu na timu apewe Ken Mkapa na Sekilojo Chambua,huu ni ujinga!

    ReplyDelete
  6. Hii habari mbona imekaa kushoto,
    Simba wamepata goli dk 26 kwa kross ya Dan Mrwanda na mrwanda alitolewa ya DK YA 18? kwa kadi ya njano?

    ReplyDelete
  7. MHHHH.MWAKA HUU SIMBA IKO JUU KI UKWELI.WAONYESHE PIA MAKALI KWENYE KOMBE LA AFRIKA.KAKA MICHUZI OMBI.ITAPENDEZA KAMA UKIWA UNATULETEA MATOKEO YA LIGI YA TZ.KAMA ILIVYO MAMBO YA BWAWA LA MAINI.CHEERS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...