hayati hemedi maneti wa vijana jazz alipamba moto sana enzi hizo na kibao chake cha 'Bujumbura' kiasi hata ikawa wengi wangependa kupaona mahali hapo walipokula wali na nsambe....
katikati ya buja
bango linaeleza kila kitu
mtaani
pembeni mwa mji
taswira ya mji wa bujumbura toka kwenyevilima vya kiriri ambako ndio kama ostabei ama masaki ya dar
mikirismasi ishamea kila mahali katika mji wa bujumbura ambao ni wa kijani kila mahali,
mfano wake kama kigoma ama kyela vile yaani joto lakini unyevunyevu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AFADHALI MTANDAO UPUMUE!! KWANI KUNA NCHI FULANI WATU WANA TAAMBIKA SANA KWA UMEME KWA HIVI SASA!!

    ReplyDelete
  2. mhhh pazuri kuliko dar pia ni wasafi kuliko dar sisi jiji kubwaaaa lakini hamna kitu!!!

    ReplyDelete
  3. Natafuta mfuko wa Marlboro kwenye picha sioni! Aibu!

    ReplyDelete
  4. Sio wali na nsambe bwana,ni wali na SOMBE. we vipi wewe?

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi, yaani umeenda kila kona ya Nchi kuliko hata Mheshimiwa Raisi! Kweli nakuaminia!

    Hapo Buju panafanana na Tanga maeneo ya Bombo na Nguvumali!

    Mdau wa siku teleee!

    ReplyDelete
  6. Bro Michuzi, marehemu Maneti alikula "kuku na mayai yake" akiwa Buja. Wewe je?

    ReplyDelete
  7. Bahati RugunaNovember 05, 2009

    Thomas acha kupayuka na kushabikia vya wengine.Sasa hizi picha mbili,tatu zinathibitishaje uzuri wa Buyumburaah? Kamji kanaonekana kama upo Sumbawanga kadooogo.Mimi nilishafika Buju miaka kibao iliyopita si lolote si chochote.Dar ni bomba kuliko Bujumbura.kwanza magari yanahesabika.

    ReplyDelete
  8. Mbona hakuna mabinti mtaani

    ReplyDelete
  9. Bro michu,ungeenda mitaa ya Buyenzi na Bwiza ili kuwafurahisha wadau wanaotakana kuona mifuko ya rambo na vilabu vya gongo.

    Mdau
    -Uzumbura

    ReplyDelete
  10. UNAJUA BAHATI MBAYA MOJA WATZ ILIYOTUKUMBA, NI KUFUKUZA MKOLONI KABLA HATUJAJIWEZA!!
    MIMI NILIKUWA UZUMBURA MWAKA 90, NI KITAMBO SASA. NILIPIGWA NA BUMBUWAZI NILIPOTUA TU NA KUANZA KUKATA MITAA, JAMAA WAMEFUNZIKA HASA, NI WATU WA MIPANGO VIBAYA MNO!
    NIKAJA KUGUNDUA KWA MUDA NILIOKAA PALE CHUO KIKUU KAMPASI YA KIRIRI KUWA KUMBE WENZETU WAKO BEGA KWA BEGA NA WAFARANSA NA WABELEJI KATIKA NYANJA NYINGI TU NA WAMENUFAIKA SANA KWA HILO.
    NA MKUU UKITAKA KUFAIDI, USIACHE KUTEMBELEA NA MIKOA YA KANDO YA UZUMBURA ILI UJIONEE MAENDELEO YA HUKO NAKO. FIKA GITEGA, TEZA, RUMONGE. NENDA KAJIONEE KISHA UWAPEPERUSHIE WADAU NAO WAJIONEE.
    SISI BAADA YA UHURU TU WATAWALA WETU WAKAFUKUZA WAKOLONI WOTE, ETI NCHI IMILIKIWE NA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI. UBINAFSISHAJI.
    NA MATOKEO YAKE NDIO HAYO, NIMERUDI NYUMBANI MWAKA JANA, HUWEZI AMINI JINSI NCHI ILIVYORUDI NYUMA, INFRASTRUCTURE YOTE IMEVURUGIKA KABISA.
    ILE KARIAKOO NILIYOICHA SIYO NILIYOIKUTA.
    VURUGU TUPU. HATA HUKO KUNAKOSIFIWA, SIJUI MIKOCHENI, SIJUI SINZA, NAKO SHOMBO LINANUKA VIBAYA MNO.
    WAKULIMA NA WAFANYAKAZI WAMESHINDWA KUJIONGOZA, WANAHITAJI WA KUWAONGOZA AMBAE KWA BAHATI MBAYA AMEKUMBWA NA AZIMIO LA ARUSHA, HATAKIWI TENA.
    NA TUNAKOELEKEA NI KUBAYA ZAIDI. TUMETOROKEA HUKU TUKIWEKA MATUMAINI YA SIKU MOJA KURUDI NYUMBANI ILI KUANZA UKURASA MPYA, LAKINI UKWELI NI KUWA WADAU MNATUKATISHA TAMAA. NA SIWALAUMU SANA, SABABU SI KOSA LENU. LAITI TUNGEENDELEA KUCHANGIA MAWAZO NA MKOLONI, KAMA WENZETU WA MSUMBIJI, KAMA WENZETU WA NAMIBI, KAMA WENZETU WA BOTSWANA, NA BURUNDI, NA KENYA, NA RWANDA, HALI LABDA INGEBADILIKA NA KUWA BORA, WANGETUSAIDIA KATIKA KUJENGA MENTALITI. LAKINI KWA SASA NDIO TUMESHACHELEWA TENA, TUBAKI KUMEZEA MATE MAFANIKIO YA WENZETU.
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  11. Mh! asante sana kwa kutuwekea huo mji,tuwekee na buyenzi sijui inaonekana vipi.Sikujua kama ni kuzuri,picha niliyonayo kichwani kuhusu burundi ni mbaya sana,lakini nashuru imenipa makaratasi ya ulaya.

    ReplyDelete
  12. Mkuu hebu ulizia kama Havana Night Club bado ipo. Tulitembelea club hiyo mwaka 2004 na kufurahia sana.

    Henry

    ReplyDelete
  13. Et wanasema binti wa Kirundi sio mchezo! namna gani hamna hata picha zao.........????

    ReplyDelete
  14. nimefurahi sana kuona bujumbura inanikumbusha mbali sana 2003-2005 kaka michuzi hebu tuoneshe basi cety cetre avenue de la mission, maana hapo ndio kama posta ya bongo, nakumbuka sisi tulukuwa tunaishi lohero kidogo ni kwa vigogo kama vile mbezi beach, hujafika petit basam?

    ReplyDelete
  15. duu home natamani kurudi lakini kimbali niliusika

    Mdau uk

    ReplyDelete
  16. mbona kama mwanza hapa wadau hebu mpacheki vizuri ....

    ReplyDelete
  17. Miaka ya 80 wakati wa ukata Bongo Burundi ilikuwa Ulaya yetu .. kwani kila kitu kilipatikana hapo , nguo , mashati ya ndege ;magari , saa za Disco hata dola ziliuzwa sokoni kama nyanya wakati huo, Bongo ukikamatwa na dolla unakwenda kunyea debe,

    ReplyDelete
  18. Mimi wadau nimefurahishwa na hiyo hali ya hewa ya Bujumbura maana si ya kawaida. ''Joto na unyevunyevu'' kaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  19. ...joto lakini unyevunyevu...it reminds me of one of the night stories during the good old days at boarding school. A story of the Kigoma-Tabora train trip by Kalimanzila and a friend...jaso gani bwana mbona murendemurende?

    ReplyDelete
  20. hawa jamaa wawe watutsi,wahutu,congolese wanadharau sana waswahili, wanaona waswahili hawana mipango wala maendeleo, ni kweli angalia kainchi kadogo haka kanapendeza kama nini sijui? sisi nyerere katufunika macho mpaka leo, tunaringia amani!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...