Na Woinde Shizza, Arusha
Bendera ya taifa iliyokimbizwa kwa miguu na wanariadha nyota kwa muda wa siku tano mfululizo hatimaye Novemba 7(jumamosi)imefikishwa sehemu ambapo ilikuwa imethamiriwa na wanariadha kufikishwa ambapo ni kwenye kilele cha mlima mrefu kuliko yote barani Afrika mlima Kilimanjaro.
Bendera hiyo ambayo ilipokelewa Novemba mbili na wanariadha maarufu 18 wa mkoa wa Arusha utoka kwa wenzao wa mkoani Dar es salaam ikiwqa ni sehemu ya ushiriki wao wa kufikisha bendera hiyyo katika kilele cha Uhuru kilichopo umbali wa futi 5,895 kutoka usawa wa bahari.
Mwanariadha maarufu ambayeni mzawa wa mkoani Kilimanjaro pia ni mzoefu wa kupanda mlima huo Elly Gerald Minja ndie aliyefanikiwa kuifikisha bendera hiyo ya taifa katika kilele cha uhuru mapema jumamosi asubuhi.
Mbali na mwanariadha huyu pia kulikuwa na wanariadha wengine ambao nao pia wamesha andikia historia ya kuzindua mbio hizi za aina yake nchini walikimbiza bendera huku wakipokezana kila baada ya kilometa kumi na kumi na tano kutoka Dar es salaam mpaka Marangu kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.
Wanariadha nyota ambao walikimbiza bendera hiyo ni pamoja na Samweli Mwera ,Sarah Maja, Nada Saya, Pius Sulle, John Rogert, Francis Naali na Mery Naali.
Mbio hizi zilishirikisha zaidi ya wanariadha 70 nchiniwengine wakiwa wa kimataifa na walikimbiza bendera hiyo zaidiya kilometa 567 waliifikisha Marangu Ijumaa jioni na baadhi yao waliipokea na kuanza kuipandisha bendera hiyo hadi kileleni.
Mbio hizo za kukimbiza bendera ya taifazilianza jijini Dar es salaam October25 na zilizinduliwa na mwanariadha wa kimataifa Samweli Mwera kwa kukata utepe na kukimbia na zimemalizika Novemba saba katika kilele cha Uhuru katika mlima Kilimanjaro.
Mbio hizi zilidhaminiwa TBL kupitia bia yao ya Kilimanjaro na kwa upande wa meneja wa bia hii ya Kilimanjaro George Kavishe alipozungumza na gazeti hili mara baada ya mbio hizo kuisha alisema kuwa amefurahia sana na kitendohichi cha wanaridha kupandisha bendera katika mlima Kilimanjaro na anashukuru kwani wamepata mafanikio makubwa kupitia mbio hizi.
kilele cha mlima kilimanjaro:
ReplyDeleteivi maana Gilman's ni nini?imetokana na nini?
na mengineyo yanayofanana na ayo