Mkutano wa TEDxDar una lengo la kuanzisha mchakato wa kushirikisha raia na kubadilishana mawazo kuhusiana na ubunifu, jumuiya, utamaduni, sanaa na masuala mbalimbali yanayohusiana na Tanzania katika kiwango cha nchi na kimataifa.


Mkutano huo unatokana ana imani katika kuendelea kwa mawasiliano na kuhusisha raia kwa kuitikia vikwazo vya kitaasisi katika maendeleo ya ubunifu. Lengo ni kukusanya kundi kubwa la watu wenye mitizamo mbalimbali na utaalamu kutoa mada za dakika ishirini za kanuni za TED ambazo zitaunda msingi wa mazungumzo mapana."


TEDxDAR imepangwa kuwa jukwaa litakalokuwa mwanzo wa kuunda kundi kubwa la wabunifu na wapenda mabadiliko katika jamii. Tunahisi kuwa mkutano wa TEDx utakuwa kianzio cha kukifikia kizazi kipya cha Watanzania ambao wanahitaji fora ya kuwajumuisha pamoja na waundaji wa mamlaka ya kijamii na kisiasa.


Kama wewe au mtu unayemfahamu ni mtu mwenye ubinifu, mpenda kufanya vitu, mwundaji na kadhalika na umo katika kundi hili tuarifu, Tanzania imejaa watu wanaofanya mambo makubwa, wenye mawazo makubwa lakini hawana uwezo kimapato na hawajatambuliwa kwa muda mrefu.
Ni wakati wa kubadilika na TEDxDar itaiteka BONGO kwa mawazo ya kimapinduzi.


Tafadhali tembelea


kupendekeza mtu anayefaa kutoa mada, au tuwasiliene

TEDxDar@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...