Wahitimu wa shahada mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA) wametakiwa kutambua kuwa watapimwa na jamii, siyo kwa idadi ama uzito wa shahada walizojikusanyia , bali kwa vigezo vya matumizi vya elimu na ujuzi wao katika kuzalisha mali na kutoa huduma bora zitakazochangia kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Changamoto hiyo imetolewa jana ( Nov 27) na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Gerald Monela , katika hotuba yake kwenye sherehe ya mahafali ya 25 ya Chuo hicho ambapo Mkuu wa Chuo hicho Al -Noor Kassam akiwatunikiwa shahada mbalimbli kwa wahitimu wapatao 848 kwa mwaka huu wa 2008/2009.
Makamu wa Mkuu huyo wa Chuo Kikuu hicho aliwataka wahitimu hayo kuepuka mambo yasiyofaa katika jamii na kujihadhari na ukimwi sambamba na kuwataka kutumia fursa nyingine za kutafua elimu kwa vile njia za kujiendeleza bazo zipo.
Hata hivyo alisema kuwa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na Chuo Kikuu hicho imeongezeka kutoka 3,619 mwaka jana na kufikia 4,628 kati ya hao 3,492 ni wa shahada yaa kwanza na 1,036 ni wa shahada za juu kufuatia kudahili wanafunzi wengi zaidi mwaka huu.
Kwa mujibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, kuwa wanafunzi waliodahiliwa mwaka wa kwanza wameongezeka kutoka 1,933 mwaka jana na kufikia 1993 mwaka huu , ambapo shahada za juu wameongezeka kutoka 694 mwaka jana hadi 1,036 mwaka huu.
Makamu wa Mkuu huyo wa Chuo Kikuu alisema katika mahafali hayo , wahitimu wanawake walikuwa ni 297 sawa na asilimia 35 kati ya hao watunukiwa 252 ni washahada za kwanza na 44 ni wa shahada za uzamili wakati mmoja ni wa shahada ya uzamivu ( udaktari wa falsafa).
Alisema idadi ya wahitimu wanwake kwa mwaka huu wameongezeka kwa asilimia 3.8 kati ya wahitimu wote 893 waliomaliza mwaka 2007/2008 ambayo asilimia 32 walikuwa ni wanawake , hivyo bado juhudi kuwa zinahitajika ili kuongeza idadi ya wanawake.
Mbali na hayo Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu hicho alisema bado mikakati inahitajika ya kuendeleza kazi za utafiti hususani tafiti shirikishi zinazozingatia mahitaji ya mkulima na mfugaji katika kutatua matatizo yake na kuongeza kipato ili kuondokana na umasikini.
Hata hivyo alisema sherehe ya mwaka huu ni ya kihistoria nay a aina yake kwani mwaka huu , Chuo Kikuu hicho kimetimiza miaka 25 tangu kuanzishwa Julai mosi, mwaka 1984 na kuzinduliwa rasmi na Baba wa Taifa Mwalimu Juluis Kambarage Nyerere , Septemba 26, mwaka 1984.
Naye Mweyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Balozi Nicholas Kuhanga, alisema Serikali ya Norway imekubali SUA kuendesha mpango wa NUFU ilioanza mwaka 2008 ambapo uanzishwaji wa utatiti kuhusu mabadiliko ya taiba nchi kwa kushirikiana na Taasisi nyingine ndani na nje ya nchi umweanza kufanyika na kutarajia kufikia tamati mwaka 2013.
Home
Unlabelled
nondozzz SUA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
jamani siku kama ya leo ni ya furaha sasa wahitimu kwenye picha wamenunaa na kutumbua mijicho furahini kwani kusoma si mchezo hasa kwetu bongo mara migomo ya hapa na pale mitihani migumu sasa siku hi hii uso unatakiwa uwe na full smile tuu wakati wote ni hayo tu
ReplyDeleteWewe anonym wa 02:06 PM vipi, hapo wenzio ndo full shangwe. Wafany mchezo.
ReplyDeleteHizi sura jamani zilokula nondoz,zikiwepo ofisini tutakoma hakuna msaada hata kidogo,zinaonekana za kijeuri jeuri
ReplyDeleteUMEsema vema mwenzangu afu wanaonekana walikuwa wanadesedesa kinoko ila mhhh,usione wamenuna wengine si bure wana fikiria kutafta kazi na interview za ckuizi full unoko wa kizungu...
ReplyDeletewakijichanganya 2 full kuji-kanumba...
Wsalaam,mdau wenu...
Del.