Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Private Yusuph Haji Hussein juzitarehe 23/11/2009 aliwapiga risasi na kuwasababishia kifo askari wenzake wawili.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya JWTZ imewataja waliouawakuwa ni Private Hildiphonce Burunja Masanja mwenyeji wa Shinyanga na Praiveti Rashid Hasani Nawawi kutoka Zanzibar.
Tukio hilo lilitokea katika eneo la Manyovu wilayani Kasulu mkoani Kigoma kwenyekiteule cha kitambuka ambapo askari hao wapo kulinda mkapa kati ya Tanzania naBurundi.
Taarifa hiyo imesema kuwa siku ya tukio, Priveti Huseein alipewa ruhusa kwenda benkmjini Kasulu kuchukua mshahara wake. Aliporejea majira ya saa moja jioni na kuwakuta askari wenzake wane wakiwa wanakula chakula akawaambia, “maskini anaishi muda mrefu kwa tabu nyingi na tajiri anaishi muda mfupi kwa raha nyingi.”
Baada ya maneno hayoo aliingia katika chumba cha silaha na kuchukua bunduki aina yaSMG moja yenye nambari 6760 na risasi 30 na kumpiga Private Masanja risasi mbili kichwani, na risasi nyingine katika mkono wa kushoto. Masanja alifariki palepale.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya tukio hilo, askari wenzake walikimbilia porini. Priveti Hussein kwa mara nyingine aliingia katika chumba cha silaha na kuchukuarisasi 120 na kisha kuchoma moto chumba chake na vyumba vya wenzake, kisha akaelekea makao makuu ya Kiteule hicho.
Akiwa njiani kiasi cha kilometa mbili, askari huyo aliyeajiliwa mwaka 2002,alikutana na askari mwenzake Private Nawawi na kumpiga risasi zilizomsababishia kifo. Private Nawawi alikuwa akitokea mjini Kigoma ambako naye aliruhusiwa kwenda kuchukua mshahara wake.
Baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitelekeza silaha hiyo pamoja na risasi 92 na kutokomea kusikojulikana. Risasi nyingine 51 hazijulikani mahali zilipo. Chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana. Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa JWTZ wanaendelea kumtafuta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. MICHUZI EEH, UWE UNA PROOF READ VITU KABLA YA KUVIANIKA....KULINDA mkapa AU mpaka...TAFADHALI BWANA!!

    ReplyDelete
  2. huyo mjeshi si mzima atakuwa amerukwa na akilini tu punguzeni mjani ohoo watu mnakata network na kufanya dizasta lol

    ReplyDelete
  3. “maskini anaishi muda mrefu kwa tabu nyingi na tajiri anaishi muda mfupi kwa raha nyingi.” Maneno ya Kifalsafa haya. Inaonekana maisha yalikuwa magumu kwa huyu afande ingawa mimi nadhani kwamba wanajeshi ni moja kati wa wafanyakazi wanaolipwa vizuri na kutunzwa na serikali.

    Pole kwa waliouawa, pamoja na familia zao. Mambo haya tumeyazoea huku Marekani ambako kutokana na visasi, msongo wa mawazo, matatizo ya kiakili, ugumu wa maisha na upatikanaji huria wa silaha mfanyakazi mwenzako anaweza kuja na pisto kazini na kuanza kumimina risasi. Natumaini kwamba uchunguzi utafanyika kujua sababu zilizomfanya achukue uamuzi huu. Hii itasaidia kuzuia visa vingine vya aina hii visitokee. RIP

    ReplyDelete
  4. HUYU INAELEKEA ANAFUATILIA SANA HABARI ZA MAREKANI. HIVYO AMEAMUA KUIGA YULE MJESHI WA MAREKANI ALIYEPIGA RISASI WENZAKE KAMBINI HIVI KARIBUNI.

    VIONGOZI BONGO HATARI HIYO MNAFIKIRI WANAJESHI WANAWALINDA SIO WAKATI WANA MATATIZO KIBAO. WATU WAMESHACHANYWA NA MAISHA MAGUMU SASA. KAZI SASA KUTUMIA SILAHA TU.

    ReplyDelete
  5. Mim kwa maoni yangu naona kuna kauzembe hapo,huyu jamaa wenzake walimwona akifanya mauaji wakakimbia porin,kweli MWANAJESH wa jeshi unakimbia porin?hao waliokimbia porin wanatakiwa wawajibishwe.Manake walipoona mwenzao naanza kufanya mauaji wangejibu mashambuliz kwa namna ya kuzuia mauaji zaidi yasitokee na sio kukimbia sasa kama wanajeshi watavamiwa tena na mjesh mmoja wakimbie na raia itakuaje?Halafu ukizingatia walikuwa wanalinda mpaka kati ya TZ na Burundi jee wangevamiwa na waas kutoka burundi si wangeruka kabisa?

    ReplyDelete
  6. Kwani na yeye alikuwa kwenye listi ya kwenda Afgani?

    Hawa jamaa wenye majina haya msiwape kazi hizi.

    ReplyDelete
  7. "maskini anaishi muda mrefu kwa tabu nyingi na tajiri anaishi muda mfupi kwa raha nyingi.” I like that quote.

    ReplyDelete
  8. Huyo Anony wa mwanzo asilete udini hapa, Jeshi halina dini wala kabila. Huyo Mjeshi ni hasira na msongo wa mawazo ya maisha magumu aliyonayo mwenyewe ndio yaliyomsababisha kuuwa na sio sababu ya jina lake!

    ReplyDelete
  9. INGEFAA PICHA ZA HAWA WATU ZIWEKWE HADHARANI WATU WAWAONE NA KUWATAMBUA KWA SABABU MAMBO YA POLISI HUWEZI AMINI UNAWEZA SIKIA HAWA WATU WAMEACHIWA KIAJABU NA WAKIWA NJE WANAENDELEZA UTAPELI KAMA KAZI

    ReplyDelete
  10. Anon wa Thu Nov 26, 10:29:00 AM, bado una kazi ngumu.

    Watu woote saba wamekubaliana na anon wa mwanzo ila wewe tuu, au nawe ni miongoni mwa wenye majina hayo?

    Actually, aliyoandika anon wa mwanzo kila mtu ayasema wazi na nyuma ya pazia, kwa hiyo kama huwezi mezea utajiju (badili jina).

    ReplyDelete
  11. ...annony wa Wed Nov 25, 06:04:00 PM....uzembe?? u must b kiddin aisee....yan mtu ana SMG+ RISASI 120 afu ubaki mbele yake unauza sura?? apo ata ''SHOZNIGA'' lazima angeeenda kutafuta chimbo PORINI!!

    ReplyDelete
  12. We Anony Wed Nov 25, 06:04:00 PM
    Usijifanye mchapakazi ama mwanaume. Mwenye SMG na asiyenayo wanapambanaje?
    Kichwa tope
    Kukimbia ni mbinu ya kikomandoo kuokoa maisha na ku-estimate threat
    Acha kujifanya wajua
    Wape pole wafiwa na kaa kimya

    ReplyDelete
  13. Dunia inaelekea mwishoni hamna zaidi.maana unaweza kushtuka vita ya wanajeshi wa kambi moja wanatwangana. Duh! Hii noma Tumwombe Mungu Daima

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...