Kwa mara nyingine tena sisi ndugu zenu wa LEEDS SWAHILI COMMUNITY tunawapa mkono wa EID wasomaji wote wa globo hii popote pale walipo, zaidi ya salamu hizi tunachukua nafasi kumuomba Allah atujalie sote kwa ujumla siku kuu yenye furaha, amani, utulivu na upendo.
Sisi ndugu zenu wa hapa LEEDS tumeshaanza kusherekea EID AL-HAJJ kwa swala maalum iliyofanyika muda sio mrefu hapa "Grand Mosque" LEEDS. Ibada hii maalum ilihudhuliwa na masheirk kadhaa waalikwa akiwemo Sheik Lidhuwani Ubishi, Sheirk Omary Mahalua, Sheirk Lunde Kulakula Othman, Sheik Amadi Mazishi na Muft .
Tunawashukuru kwa dhati kabisa wote walihudhulia Ibada hii na wale wote waliohudhulia swala kama hii popote pale dunia na hata ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuli ibada kama tunawaombea baraka nyingi na kila lenye kheri na Inshaallah tusherekee vyema siku kuu hii tukufu.
Na pia tunawaombea Mahujaji wote walioko Macca hivi sasa wakimalizia Hijja zao Inshaallah Allah awapokelee dua zao na hija zao ziwe zenye kukamilika.
Kaka Issa Michuzi Inshaallah, Allah akujalie afya njema, akuzidishie hekima, busara na akudhurumu kiburi ili vyote hivi uweze kuvitumia vyema katika kuendeleza na kupanua mawasiliano ya globo hii.
Hivi basi tafadhali tujumuishe na wenzetu kupitia picha hizi tulizopiga tukifurahia Eid baada tu ya Swala
Asalaam Aleykum
Mwenyekiti Amran Rashid,
Asalaam Aleykum
Mwenyekiti Amran Rashid,
Dr. Khassim Mwintonde na Sheirk Dokta Mahil Mazishi
HAPPY EID DAY
HAPPY EID DAY
hivi huko leeds hakunaga mademu?? kila siku ni nyinyi tuu acheni ubaguzi bin umimi
ReplyDeleteminalfaizin tunashukuru sana ndugu zetu waislam wa leeds inshallah mwenyezi mungu atujaalie uhai na afya njema na atufikishe kwenye eid ya mwaka ujao ameen.
ReplyDeletemwenyezi mungu ni mkubwa na ashukuriwe sana kwa kweli mmependeza sana mnaonekana nadhifu na wenye furaha alhamdulilah hivyo ndivyo tunavyotakiwa ndugu wa kiislam kuishi
kuishi kwa upendo na umoja ushirikiano na inshallah kwa wale amabao sio waislam mungu atawapa nafasi siku moja ya kukaa na kugundua njia ya kweli ya kufatwa na watajiunga katika njia hiyo inshallah
wabillah tawfiq
hivi nyie ni wabongo au wasomali?,maana ninavyojua mimi hapa uk wabongo ni wale tu waliokuja kwa masomo,lakini wengine wote mlishabadilisha uraia na kuwa wasomali
ReplyDeletesina mengi nawatakia idd njema wadau wote
ni sisi wasomali wa leeds
siku zote katika watu wenye maana lazima atatokea mtu mmoja mjinga,maswali ya kihuni yasiyo na maana mjomba michuzi naomba usiyape nafasi ni kero kusoma comments za kiwazimu kama za hawa jamaa zetu mdau wa sat nov 28, 06.45pm na mwenziwe wa 02.02.00,kama huna neno la kusema bora ukae kimya, this is not the way to wind up someone, thanks
ReplyDeletewewe tatizo lako hasa nini?uraia si uraia tu msomali mbongo wote si waafrica tu?is not a BIG ISSUE wenzako wanatafuta maisha sio kukaa umebungaa kufatilia yawatu ndo maana mtu unakosa maendeleo coz hujui jinsi yakutafuta maisha yako jaribu kubadili mwenendo wako wa maisha naimani utafanikiwa GOD BLESS U LUV
ReplyDeleteati tusipewe nafasi ya kutoa hoja hii ni blog ya jamii kila mtu ana uhuru wa kusema inaelekea we mdau una mabavu sana kwenye familia yako we ndo mwenye sauti pole saana usilete ubaguzi wako humu blog ya jamii ndiyo ninauliza tena hivi huko leeds hakuna wanawake ?? manake idd zote ni picha za wanaume tuu sioni kasoro yoyote kuuliza hili swali au wao hawasaligi?
ReplyDeleteNiungane na ndugu yangu hapo juu Nov 30,02;39, jamani hii blong ya jamii kila mtu anatoa mawazo yake na tujaribu siku zote ktk maisha yetu tuwe na tabia ya kuvumilina
ReplyDeletekimawazo ,ili mradi si matusi wala lugha chafu,lakini ooo msiweke mawazo ya wengine kwanini?,kama unapinga jenga hoja siyo "UDIKTETA"mdau kauliza swali zuri tu je huko leeds hakuna wanawake mbona kila siku nyie?,sasa hapo kakosea nini jamani?,mie nikasema huku leeds,miltokeynes,reading na slough,huko koooote watanzania walishaukataa utanzania wao kweli si kweli?,nimekosea nini hapo maana hata mimi niko ktk kundi hilo ,sasa mnaanza sijui mjinga sijui uhuni,msipende kila siku msikie mambo ya kuwafurahisha mkubali kupokea na changamoto mbalimbali,mkuu wa wilaya ya nanii mara nyingi sana anakutana na maoni ya kukera ,hata jirani zake pale (jamiiforum)wanampiga madongo kila siku ,lakini hizo ndiyo changamoto ambazo unatakiwa uzikubali,mwisho namuomba mdau hapo juu nimwabie hukukosea hao WASOMALI umimi na ubanafsi umewazidi ndiyo maana dada zetu hawawapi nafasi ya kutolewa kwenye picha,na hao wakina dada ndiyo waswalihina wazuri sana ,hao unawaona utawaona mwakani tena kwenye idd
mwisho nawatakia xmass njema mkuu wa wilaya ya nanii,watanzania wote popote walipo,na WASOMALI wote wa leeds,miltonkenes,na slough